Sophia Simba, Anne Kilango nusura wazichape

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,401
UHASAMA wa kisiasa kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, umevuka mipaka na sasa ni uadui wa wazi wazi. Hali hiyo ilidhihirika wiki iliyopita mjini Dodoma, wakati wawili hao walipokutana katika Benki ya CRDB iliyopo bungeni na badala ya kusalimiana, waliishia kutofautiana. Shuhuda wa tukio hilo, aliiambia MTANZANIA, kuwa tukio hilo lilitokea saa 6 mchana, baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha Bunge kutokana na vurugu zilizosababishwa na wabunge wa upinzani, wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Shuhuda huyo alisema kuwa, kabla ya tukio hilo, Anne Kilango pamoja na wabunge wengine wa CCM, walikuwa ndani ya benki hiyo wakibadilishana mawazo.



Wakati wakiendelea kuzungumza, Sophia Simba aliingia ndani na kuanza kuwasalimia kila mmoja kama ilivyo kawaida.


“Sisi tulikuwa hapa ndani ya benki pamoja na Diana Chilolo (Mbunge wa Viti Maalum CCM), Turky, Mbunge wa Mpendae (Salim Abdallah Turky) pamoja na wahudumu wa benki.


“Sofia Simba alipofika, alitusalimia lakini Anne Kilango hakuitikia salamu yake na hapo Sofia akasema, mheshimiwa Anne Kilango nakusalimia.


“Aliposema hivyo tu, Anne Kilango akahamaki na kusema usinisalimie, mimi sitaki salamu yako. Kauli hiyo ilionekana kutushangaza na wakati tunashangaa, Sofia Simba akasema, mheshimiwa Anne Kilango mimi ni shoga yako na tumetoka mbali, kwa nini tusisalimiane?


“Aliposema hivyo, Anne Kilango akasema sitaki kusikia salamu yako, ‘shut up’ kisha akaondoka,” alisema shuhuda huyo akinukuu maneno ya Anne Kilango.


Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Simba alisema kwa kifupi, kwamba, “nina ngozi ngumu, sizungumzi mambo haya kwa sababu mimi ni kiongozi,” alisema na kukata simu.


Naye, Anne Kilango alipoulizwa naye alisema yeye hawezi kuzungumzia masuala hayo, kisha akakata simu.



Chanzo - Mtanzania
 
Angalau wanawake hawa wameonyesha ukomavu kuzidi wanaume wa kiswahili! Sasa ili kulinda heshima ya nchi, naombaai mama Makinda atafute muda wake binafsi awapatanishe ili washiiriki kwa moyo mmoja katika mazoezi yakupulizia oksijeni chama chao ambacho kiko ICU. Na ukiona hivi ujue hakuna tena maadili ndani ya ccm.
 
Wangepasuana tuone gagulu za waheshimiwa zinatofauti gani na wapiga kura.
 
Huyu mama mara apandishiane na lissu, sasa tena mwanamke mwenzake. Kwanini ni yeye tu? atakuwa chanzo cha matatizo huyu!
 
Huyu mama mara apandishiane na lissu, sasa tena mwanamke mwenzake. Kwanini ni yeye tu? atakuwa chanzo cha matatizo huyu!

nakusapoti mkuu,uyu mama ni mkorofi sana,cjui anaringa nini,au ni sababu ya ndoa za uzeeni
 
Mbona sioni sehemu inayoonesha kuwa nusura wazichape? Ni mimi sielewi maana ya kuzichapa au mwandishi ni kanjanja?
 
Anna Kilango ni kama mwanamke wa mnanda... she is surrounded by stupid drama na kugombana na watu

ana A ya kupayuka
 
Wazipige wakalale polisi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Haya mambo ya mvuto ndiyo yanamaliza nchi...mkuu hustuki..!? Wangapi wameingia madarakani kwa mvuto na waka'deliver' ?

Sina majibu ya swali lako. Angalia hiyo clip ya hotuba yake utapata majibu
.
Sijui tunawezaje kuwa na waziri wa aina hiyo na mwenye uelewa mdogo kiasi hicho.
Kwanza unajiuliza alipataje uwaziri?
CCM ni alpha and Omega!
 
Back
Top Bottom