Somo kutoka Urusi: Ili Taifa lipate mafanikio lazima kuwe na "consistency" kwa viongozi wa wandamizi na nguli

Russia hakuna until wowote inatawaliwa na kikundi kidogo cha mafisadi wakiongozwa na Putin.Hawataki kuachia madaraka walijua wakiondoka tu Takukuru ya Urusi inao

Hao wote uliwataja mali zao za mabilioni na pesa mabilioni zimekuwa frozen nchi za Magharibi

Vikwazo wamewekewa wao na familia zao
Ile vita sio Kuwa anapigana na Ukraine la.Yeye kavamia Ukraine kisa aliota kuwa kuna siku Ukraine watakuja mvamia.Hivi mtu unaota tu halafu unaenda fanya uharibifu kama ule Ukraine kweli? Mtu hajakuvamia .

Alichofanya Urusi kinatakiwa kulaaniwa ns kila binadamu mwenye akili timamu si cha kufanya kwenye dunia ya kistaarabu ya sasa hivi
Halafu unakuta una familia kabisa
 
nyerere amekaa miaka 30 kuna nini jipya kafanya zaidi ya kutaifisha nyumba za watu na mgao wa dawa za mswaki na sukari
 
Umeiweka vizuri sana consistency na unguli wa viongozi lakini sio huyu bibi tunahitaji Raisi kama kiongozi sio ceremonial figure for which she fits very well yaan ni mweupe mpaka anatia huruma
 
Hili ni somo ambalo Urusi wamelitumia na likawapa mafanikio makubwa sana hasa ndani ya hii miongo miwili ya Rais Putin.

Ni somo ambalo China sasa wamelichukua na naona linaendelea kuwalipa. Hata jirani zetu Rwanda linawalipa.

Ni somo la kuwapa viongozi Nguli na waandamizi muda wa kutosha kusimamia mipango ya muda mrefu na kupanga mipya. Kwenye sakata linalogonga vichwa mwezi Sasa kati ya Urusi na Ukraine(NATO) Kuna miamba kadhaa upande wa Urusi inasikika mara kwa mara, matharani.

PUTIN.
1.Sergei Lovrov, Waziri wa mambo ya nje.
2. Dmitry Peskov, Msemaji wa Ikulu na na Deputy chief of staff.
3. Anatoly Antonov, Balozi wa Urusi Marekani.
4. Sergei Ivanov, Mkuu wa baraza la usalama.
5.Dmitry Medvedev, Naibu Mwnyekiti baraza la Taifa la usalama.
6. Sergei Shoigu. Waziri wa Ulinzi.

Ndugu zanguni hawa ni miamba wachache ambao nimeona angalau nitolee mfano.
Ukiwaangalia hawa watu kila mtu ni nguli wa eneo fulani na wapo kwenye serikali si chini ya miaka 10.
Miamba wanaweza wakawa wanahama kutoka eneo moja kwenda lingine lakini wapo.
Ukichukua serikali nyingi za sasa hata US ukawapambanisha na hawa Miamba ni kama unawaonea tu aise. Yaani Hawa maimba ni Galaticos.

Putin yupo hapo tangu 2000, amepambana na Bush, Obama na kisiki Trump. Amepitia mikiki mikiki anawajua US and Co in and out. Babu Biden kwake Hana jipya.

Sergei Lavrov yupo foreign ministry tangu 2004. Amepambana na Condi, amepambana na kina Pompeo and Co. Huyu Blinken anamuona mrembo tu aise.Kabla ya hapo alikuwa balozi umoja wa mataifa, anazijua Kona zote, diplomasia imekaa. Miaka 18 kwenye foreign ministry.

Mwamba Peskov yupo Klemrin tangu miaka ya 2006. Ni mwamba kweli kweli kwenye usemaji. Anawajua Westerners inje ndani hawampi kichwa hata kidogo kwenye propaganda aise. Jumlisha mwamba Anatoly Antonov, amewahi kuwa naibu waziri wa Ulinzi na mambo ya nje, Dmitry Medvedev, Sergei Ivanov.N.k.

Kwahiyo ukiona Urusi anawatoa watu kamasi, moja ya msingi ni huu, kuwa na Nguli, na veterans kwenye maeneo tofauti tofauti ambao wanajua uhuni wote wa dunia hii. Ambao wanajua chocho zote na wanaoweza kupanga Jambo likapangika.
Sisi huku kila baada ya miaka miwili sura mpya, hawajulikani wametoka wapi. Anayejitahidi anakaa miaka mitano na wale wanaodumu ni wale wenye sifa za uchawa, very unproffesionall.

Yaani kwetu ukimuangalia waziri huoni ule uzito kwenye nafasi aliyopo. Huoni kitu Cha maana alichokifanya hapo alipo.
Wizara ukiifanyia tathmini leo haina tofauti na ilivyokuwa 2004. Labda yamebadilika majengo, magari na watu. Huoni Wanaume wa shoka waliokaa pale wanaosimamia vitu vya maana. Ni watu wanakuja wanapiga salary ya waziri wanaondoka, anakuja mwingine anapiga Salary anaondoka.

Ndugu zanguni kwa mtindo huu ni k hatuwezi kupiga hatua.
Nadhani tufike mahali tuweke utaratibu tuwape viongozi waandamizi mda wa kutosha, wapange mipango, watafute wandani wao wa kuwasaidia kusimamia mipango. Miaka mitano ni mda wa kujifunza. Baada ya hapo aangalau wapewe miaka mingine 10 ili sasa wafanye kazi. Tuanze na Chifu, tumpe hadi 2035.

Baada ya miaka hii minne atakuwa amejifunza Sasa baada ya hapo ataanza kupanga na kusimamia mipango ya Inchi na atafafuta watu wa kumsaidia ambao ni nguli na ambao atawaamini kwa mda mrefu atakuwa ameilewa serikali na atakuwa amepata nafasi ya kuwajua vizuri watu wanaomfaa. Hatahadaika na vipara na miwani au skafu za kijani.

Ndugu zanguni hata hapa kwetu somo lipo. Hapo tu Ufipa, CHADEMA imekua taasisi imara kwakuwa yupo mwamba, ameaminiwa na akapewa mda wa kutosha karibia 18 sasa. Amejifunza akazielewaa siasa na sasa za bongo na anawatoa kamasi wanakijani, ameijenga CDM. Sasa ni Taasisi imara kiasi kwamba 2015 Watanzania walitaka kuipa dora. Kama tunaona Urusi mbali tuchukue basi hata hilo somo la hapo Ufipa.

Tunazidiwa akili hadi na Zito jamani. Mkuu wa Chama, Ayatola, mbona ameshaliona mapema hilo, akaazima pale Tehran.
Umeniangusha kwa kumsahahu waziri wa mambo ya nje na yulr binti secretary wake.
 
Kama viongozi wa Urusi unadhani wanauwezo mkubwa wa kuongoza na kutoa maamuzi mazuri kuliko hawa wa kwetu,basi wasingeingia mkenge wa kuivamia Ukraine,uvamizi ambao umepelekea nchi za magharibi kuiwekea Urusi vikwazo vya uchumi ambavyo vimeirudisha Urusi miaka 50 nyuma kimaendeleo.
Punguz kusoma na kusikiliz propaganda za west.
Tafuta habari, soma utajua ukweli ni upi.

Eti russia ilikuwa aichukue ukrain kwa siku mbili tatu, umesikia wapi ujinga huu?

By way wanasema leo na jana walitishia mbwa kiev kapital ili jamaa wakomae kule, kaxi iee rahisi huko donbas, na wamefanikiwa.

Kwanini hawakusimulii hiyo chenga ya mwili?
 
Babu Biden kwake Hana jipya.
Unajua amekuwa seneta toka lini?

Ungesema watu kama Bush (Jr), au Obama hapo ungekaribia uhalisia wa mifano sahihi unayotoa hapa.

Lakini usisahau mtindo wao wa ma-'think tank', talking heads, taasisi mbalimbali wanaowakusanyia taarifa kila sehemu za dunia. Hizi ni taasisi mbalimbali zinazotumiwa kukusanya taarifa, au ku-'analyze' jambo.

Wanapotaka kumpiga mtu, kama Gaddafi vile, kuna watu maalum wanapewa kazi ya kumpamba kama shetani kabla hajatwangwa. Media zao zote zinageuzwa kufanya kampeni, kama zinavyofanya sasa dhidi ya Putin, na kumpamba ZOLO.
 
Kama viongozi wa Urusi unadhani wanauwezo mkubwa wa kuongoza na kutoa maamuzi mazuri kuliko hawa wa kwetu,basi wasingeingia mkenge wa kuivamia Ukraine,uvamizi ambao umepelekea nchi za magharibi kuiwekea Urusi vikwazo vya uchumi ambavyo vimeirudisha Urusi miaka 50 nyuma kimaendeleo.
Duh, na wewe unaamini Urusi imerudishwa miaka hamsini nyuma?

Aiseee, nchi yetu hii tuna matatizo kwelikweli na ufahamu wa mambo yalivyo ya wananchi wetu. Hili ni tatizo kubwa sana, na hatuwezi kuendelea tukiwa na watu wa kiwango hiki cha kukosa ufahamu.
 
Hili ni somo ambalo Urusi wamelitumia na likawapa mafanikio makubwa sana hasa ndani ya hii miongo miwili ya Rais Putin.

Ni somo ambalo China sasa wamelichukua na naona linaendelea kuwalipa. Hata jirani zetu Rwanda linawalipa.

Ni somo la kuwapa viongozi Nguli na waandamizi muda wa kutosha kusimamia mipango ya muda mrefu na kupanga mipya. Kwenye sakata linalogonga vichwa mwezi Sasa kati ya Urusi na Ukraine(NATO) Kuna miamba kadhaa upande wa Urusi inasikika mara kwa mara, matharani.

PUTIN.
1.Sergei Lovrov, Waziri wa mambo ya nje.
2. Dmitry Peskov, Msemaji wa Ikulu na na Deputy chief of staff.
3. Anatoly Antonov, Balozi wa Urusi Marekani.
4. Sergei Ivanov, Mkuu wa baraza la usalama.
5.Dmitry Medvedev, Naibu Mwnyekiti baraza la Taifa la usalama.
6. Sergei Shoigu. Waziri wa Ulinzi.

Ndugu zanguni hawa ni miamba wachache ambao nimeona angalau nitolee mfano.
Ukiwaangalia hawa watu kila mtu ni nguli wa eneo fulani na wapo kwenye serikali si chini ya miaka 10.
Miamba wanaweza wakawa wanahama kutoka eneo moja kwenda lingine lakini wapo.
Ukichukua serikali nyingi za sasa hata US ukawapambanisha na hawa Miamba ni kama unawaonea tu aise. Yaani Hawa maimba ni Galaticos.

Putin yupo hapo tangu 2000, amepambana na Bush, Obama na kisiki Trump. Amepitia mikiki mikiki anawajua US and Co in and out. Babu Biden kwake Hana jipya.

Sergei Lavrov yupo foreign ministry tangu 2004. Amepambana na Condi, amepambana na kina Pompeo and Co. Huyu Blinken anamuona mrembo tu aise.Kabla ya hapo alikuwa balozi umoja wa mataifa, anazijua Kona zote, diplomasia imekaa. Miaka 18 kwenye foreign ministry.

Mwamba Peskov yupo Klemrin tangu miaka ya 2006. Ni mwamba kweli kweli kwenye usemaji. Anawajua Westerners inje ndani hawampi kichwa hata kidogo kwenye propaganda aise. Jumlisha mwamba Anatoly Antonov, amewahi kuwa naibu waziri wa Ulinzi na mambo ya nje, Dmitry Medvedev, Sergei Ivanov.N.k.

Kwahiyo ukiona Urusi anawatoa watu kamasi, moja ya msingi ni huu, kuwa na Nguli, na veterans kwenye maeneo tofauti tofauti ambao wanajua uhuni wote wa dunia hii. Ambao wanajua chocho zote na wanaoweza kupanga Jambo likapangika.
Sisi huku kila baada ya miaka miwili sura mpya, hawajulikani wametoka wapi. Anayejitahidi anakaa miaka mitano na wale wanaodumu ni wale wenye sifa za uchawa, very unproffesionall.

Yaani kwetu ukimuangalia waziri huoni ule uzito kwenye nafasi aliyopo. Huoni kitu Cha maana alichokifanya hapo alipo.
Wizara ukiifanyia tathmini leo haina tofauti na ilivyokuwa 2004. Labda yamebadilika majengo, magari na watu. Huoni Wanaume wa shoka waliokaa pale wanaosimamia vitu vya maana. Ni watu wanakuja wanapiga salary ya waziri wanaondoka, anakuja mwingine anapiga Salary anaondoka.

Ndugu zanguni kwa mtindo huu ni k hatuwezi kupiga hatua.
Nadhani tufike mahali tuweke utaratibu tuwape viongozi waandamizi mda wa kutosha, wapange mipango, watafute wandani wao wa kuwasaidia kusimamia mipango. Miaka mitano ni mda wa kujifunza. Baada ya hapo aangalau wapewe miaka mingine 10 ili sasa wafanye kazi. Tuanze na Chifu, tumpe hadi 2035.

Baada ya miaka hii minne atakuwa amejifunza Sasa baada ya hapo ataanza kupanga na kusimamia mipango ya Inchi na atafafuta watu wa kumsaidia ambao ni nguli na ambao atawaamini kwa mda mrefu atakuwa ameilewa serikali na atakuwa amepata nafasi ya kuwajua vizuri watu wanaomfaa. Hatahadaika na vipara na miwani au skafu za kijani.

Ndugu zanguni hata hapa kwetu somo lipo. Hapo tu Ufipa, CHADEMA imekua taasisi imara kwakuwa yupo mwamba, ameaminiwa na akapewa mda wa kutosha karibia 18 sasa. Amejifunza akazielewaa siasa na sasa za bongo na anawatoa kamasi wanakijani, ameijenga CDM. Sasa ni Taasisi imara kiasi kwamba 2015 Watanzania walitaka kuipa dora. Kama tunaona Urusi mbali tuchukue basi hata hilo somo la hapo Ufipa.

Tunazidiwa akili hadi na Zito jamani. Mkuu wa Chama, Ayatola, mbona ameshaliona mapema hilo, akaazima pale Tehran.
Tz KWa katiba Hii ,ni kutengenezea watu ufisadi
 
Umeiweka vizuri sana consistency na unguli wa viongozi lakini sio huyu bibi tunahitaji Raisi kama kiongozi sio ceremonial figure for which she fits very well yaan ni mweupe mpaka anatia huruma
Mbona JK alisema anaongoza vizuri
 
Nchi zilizofanikiwa ziliachana na utamaduni wakutegemea watu,wakawekeza kwenye mifumo imara inayosimamia kila sekta ndo maana mambo yao mengi yanaenda kwenye mtiririko miaka mingi ata kama viongozi watakua wanabadilika.Hayo mambo yakua na hao unaowaita nguli wakukaa muda mrefu wala sio msaada kwa nchi kama watakua hawajali kuboresha maisha ya wananchi wao.na mifano ipo mingi ,wengi wao wanaishia kua mafisadi.Hao nguli wa urusi wengi ni rafiki zake na putin nasio kwamba kuna chochote cha maana zaidi ya kikundi cha wachache kula mema ya nchi.
 
Back
Top Bottom