Somo kutoka kwa Pauline Gekul, uasi uzaa uasi?

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kama mtu ninayeheshimu ile dhana ya kutokuwa na hatia mpaka sheria ithibitishe hivyo, ( pressumption of Innocence ), sitaki Moja kwa Moja kumhukumu paulin Gekul aliyekuwa naibu waziri wa Katiba na sheria kwa Yale yanayosemekana aliyafanya.

Na ndiyo maana kichwa Cha andiko langu ni swali. Ni swali kwa sababu tunasubiri vyombo vya kutoa haki kisheria vitoe uamuzi wa saga hilo ingawa tayari mheshimiwa Rais, ameshamvua madaraka ya unaibu waziri.

Hata hivyo, nilitaka kulijadili jambo hili kwa tahadhari, kumsema kidogo hapa mdogo wangu Paulina Gekul ,aliyewahi kuwa kada kindakindaki wa Chadema, mbunge kutoka chama hicho na baadae kuwaasi wenzake na kukimbilia CCM jinsi alivyodhirihisha dhahiri kwamba mbegu ya uasi ilikuwa ndani yake.

Najiuliza? Inawezekanaje mtu tena wa jinsia ya kike, ana madaraka makubwa serikalini, na ubunge, anawezaje kusimamia vitendo vya utesaji wa kijana yule ?

Sitaki kujenga hoja hapa kwamba " watu huwa hawabadilishi maisha, na kwa maana yake yeye ,kubadili vyama. La hasha. Watu hubadili mazingira na kutafuta mabadiliko inapobidi.

Kwa paulina Gekul, ckuwahi kuona hakika mtu aliyekuwa amebadilika kwa maana chanya.( Change for the better).

Wakati anaondoka Chadema nilimuona mtu ambaye ukweli usemwe alionyesha alama zote za disloyalty. ( kwa maana ya hapa niseme kutokuwa mtii na mwema).

Aliwasema vibaya Wana Chadema na kuwananga kana kwamba hawakuwahi kuwa mwenzake.

Nakumbuka alivyotoa kashfa kwamba alikuwa anashurutishwa kutoa pesa zake na wenzake kufanya Kila kitu Cha Chadema wakati huo.

Aliwananga Chadema na kuwa paint kwa jamii kama mazurumati na watu ambao hawakua na utu.

Leo ni kinyume, alichokifanya yeye, Sasa kimeonyesha dhahiri kwamba uasi huzaa uasi ( disloyalty breeds even greater disloyalty).

Tabia aliyoionyesha Gekul ya kuwageuka wenzake tena wakati ambao walikuwa katika misukosuko na mateso ya kisiasa ilionyesha kabisa disloyalty ya huyu dada.

Na hapa Kuna somo, "mtu yeyote anayegeuka wakati ambao ulikuwa unamhitaji, mtu anayekukimbia wakati wa mateso yako, mtu ambaye hata bila Soni anadharau wema uliowahi kumtendea, kirahisi mtu huyu utamuita muasi. ( Disloyal).

Najua uasi uendelea Kila mahali, lakini tujifunze namna ambayo tunawapokea watu waliotoka mahali wakiwa disloyal.

Tuwatenge kwanza kabla ya kuwaamini, tuwapogolee kama inawezekana zile element ambazo huwa tunaziona mapema kwamba siyo nzuri, dharau, kusema wandani wako wa awali vibaya, kutokumbuka wema hata kidogo.

Na hapa Leo nijifanye walau kidogo kuwa mwanazuoni wa dini, " ukiasi wema wowote kwa sababu zozote, Mungu wewe atakuaibisha zaidi na kukulipa Yale ulofanyia wengine.

Leo anatukanwa CCM kuwa chama kilicholea tabia mbaya. Lakini tujiulize ni kweli? Mimi naona hapana. " Hii tabia ilikuwepo tangu mwanzo, CCm walitakiwa kabla ya kumwamini pengine, wanempogolea, wangemtenga kwanza kwa maana ya kutomwamini mapema kwa mambo makubwa nk.

Tujifunze kuwa tunachunguza, anayetoka hapa Leo katukana na kukana hata mazuri ya wenzie, ni mzuri kweli?

Wasaalam. No
 
Ndio maana nchi hii inauhitaji mkubwa wa Katiba mpya na pia viongozi wote wawe wanaomba hizo.nafasi na kuwashindanishi pia kujieleza bungeni kwa nini anafaa kwenye hiyo nafasi pia elimu yake kuhojiwa. Hizi mambo za siasa kisa mtu tu ana kadi ya Chama basi mfano wa Daudi Albert Bashite Aka Makonda!!
 
Back
Top Bottom