Maghorofa mazuri, picha nzuri, shukurani kwa kuziweka.
Dar inakua vizuri. Upanga yangu (ambayo sijakanyaga miaka 14 sasa) naangalia picha mpaka nashindwa kujua hapa wapi.
Oysterbay na Masaki nilizozijua miaka ile na za leo tofauti sana.
Napenda kuona real estate ya Dar na Tanzania inapanda kifikia viwango vya kimataifa.
Jambo moja nataka kusema, na hii si crticism wala upinzani kwa maendeleo haya, ni angalizo la common sense tu.
Ujenzi wa mji uendane na realistic demand za kiuchumi, watu wasijenge kwa fashion kutaka majengo makubwa ambayo hayana economic demand na hayataleta faida. That is not sustainabke.
Kama kuna demand, kama kuna business case, au hata kama kuna realistic projected demand, ni vizuri.
Mji wa Dar unakua kwa kasi sana, umepanua sana. Tunatakiwa kupunguza urban sprawl kwa kujenga kuelekea juu. Hili linatakiwa si hapo katikati mjini na Upanga tu, bali hata kwenye vitongoji vya nje kidogo ya mji.
Traxtion