Skyline ya jiji la Dar es Salaam imepanuka sana

Naomba hii mada ispark kiu ya jamii nzima kubadilika na tujitafakari kama nchi , tubadilike Tanzania inatia aibu .Si majiji ,miji midogo hata vijijini aiisee ni takataka..Kifupi Tanzania ni kama wanaishi panya au mende na si watu
 
Wengine tunaweza ku multitask na kufanya system thinking mkuu.
Huoni kama unajadili mada nyingine ambayo hakuna anayeipinga na unalazimisha hapa ionekane thread inapinga kuwa unayosema hayapo. Umetengeneza imaginary topic, ambayo unabishia wewe mwenyewe against nothing, sijui ni nani ulie imagine kuwa anapingana na hizi hoja zako.
Unajua wewe mwenyewe ulikotolea hiyo mada na huyo imaginary person unayebishana nae na kudai anahusudu vitu ambavyo havijui undani wake
 
Kuna namna fulani wabongo huwa tunahusudu vitu bila kuelewa undani wake, Skyscrapers/maghorofa haipaswi kuwa kitu cha maana sana kwa raia wa kawaida anayezurura Kariakoo ambako njia za watembea kwa miguu na usafiri wa umma ni tatizo kubwa, watu wanasongamana muda wote kama siafu kwa sababu njia za magari ndizo hizo za watembea kwa miguu, parking za kushushia na kupakia mizigo na wamachinga waliozagaa kila kona.

Ukweli ni kwamba kwa watu wengi wa kipato cha kawaida wanaotegemea usafiri wa umma, hospitali, na shule za umma inahitaji moyo sana kuishi Dar.

Wanaofurahia kidogo labda ni hao wamiliki wa hizo skyscrapers, top 1% na middle class wenye vigari kimoja viwili, wengine wote wanaishi kwa matumaini tu kwa sababu imebidi tu wawepo Dar.

Hembu fikiria soko kubwa zaidi la chakula la Jiji la Mabibo halina hata sakafu au pavements, watu wanaishi na kufanyia biashara kama wako zizini.
Exactly mkuu ,huwa naumia sana na kupata hasira niikaa na kufikiri ujinga wa nchi yangu Tanzania, na picha iliyojengwa hadi kwa wananchi wa kawaida ni kuona kwamba hawastahili quality ya maisha ya kuwa na miji yenye miundombinu ya kueleweka atleast yenye kutimiza mahitaji ,miji misafi na iliyopangika na yenye amenities za muhimu kufanya binadamu ajione ni binadamu .
Ni kama nchi nzima imejaa mazuzu na misukule
 
Naomba hii mada ispark kiu ya jamii nzima kubadilika na tujitafakari kama nchi , tubadilike Tanzania inatia aibu .Si majiji ,miji midogo hata vijijini aiisee ni takataka..Kifupi Tanzania ni kama wanaishi panya au mende na si watu
Sasa kwa nini usingeanzisha mada special ambayo wananchi watakuwa wanatoa changamoto zao juu ya miji na majiji yetu Tanzania
Itakuwa ni jambo zuri zaidi kuliko kujadili mambo mabaya kwenye mada iliyojikita kwenye upande mzuri wa Dar es Salaam
 
Exactly mkuu ,huwa naumia sana na kupata hasira niikaa na kufikiri ujinga wa nchi yangu Tanzania, na picha iliyojengwa hadi kwa wananchi wa kawaida ni kuona kwamba hawastahili quality ya maisha ya kuwa na miji yenye miundombinu ya kueleweka atleast yenye kutimiza mahitaji ,miji misafi na iliyopangika na yenye amenities za muhimu kufanya binadamu ajione ni binadamu .
Huu ni uongo mkubwa
Watanzania wamekuwa wakilalamika miaka na miaka kuhusu miundombinu mibovu, mafuriko, mipango miji nk
Ni uongo mkubwa kusema Watanzania wamejijengea picha kwamba hawastahili quality ya maisha. Umeingia Jamii Forums na kuona mada ngapi humu tumekuwa tukiongelea changamoto za miji yetu?

Watanzania wote wanataka maendeleo. Ni kama wewe tu ila tofauti yetu na wewe sisi hatuioni Tanzania kama takataka. Na tunaona maeneo mazuri na mabaya ya Tanzania, wewe unaona mabaya pekee
 
Huoni kama unajadili mada nyingine ambayo hakuna anayeipinga na unalazimisha hapa ionekane thread inapinga kuwa unayosema hayapo. Umetengeneza imaginary topic, ambayo unabishia wewe mwenyewe against nothing, sijui ni nani ulie imagine kuwa anapingana na hizi hoja zako.
Unajua wewe mwenyewe ulikotolea hiyo mada na huyo imaginary person unayebishana nae na kudai anahusudu vitu ambavyo havijui undani wake
Uzi wako umechangamka vizuri zaidi kwa sababu watu wamejiongeza wakachangia mambo ya maana zaidi yanayohusiana au kwenda pamoja na skylines au skyscrapers zako pendwa.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Huoni kama unajadili mada nyingine ambayo hakuna anayeipinga na unalazimisha hapa ionekane thread inapinga kuwa unayosema hayapo. Umetengeneza imaginary topic, ambayo unabishia wewe mwenyewe against nothing, sijui ni nani ulie imagine kuwa anapingana na hizi hoja zako.
Unajua wewe mwenyewe ulikotolea hiyo mada na huyo imaginary person unayebishana nae na kudai anahusudu vitu ambavyo havijui undani wake
Huu ni uongo mkubwa
Watanzania wamekuwa wakilalamika miaka na miaka kuhusu miundombinu mibovu, mafuriko, mipango miji nk
Ni uongo mkubwa kusema Watanzania wamejijengea picha kwamba hawastahili quality ya maisha. Umeingia Jamii Forums na kuona mada ngapi humu tumekuwa tukiongelea changamoto za miji yetu?

Watanzania wote wanataka maendeleo. Ni kama wewe tu ila tofauti yetu na wewe sisi hatuioni Tanzania kama takataka. Na tunaona maeneo mazuri na mabaya ya Tanzania, wewe unaona mabaya pekee
Criticism yangu ni valid ,sorry kama unaziona ni matusi kwa nchi ,If that is the case then let it be .
Tanzania miji ,majiji feki na vijiji ni takataka na havifai kwa watu kuishi kwa ustawi wao .Huu ni ukweli kubali ukatae picha ya nchi yako hiyo unayo unajua hali ilivyo kijijini kwenu ,hapo mtaani kwako unajua kilivyo haina haja ya kubishana na kujilisha upepo kwamba tupo vizuri ,tupo ovyo sana ,denialism Tu ndio umeikubatia

Na kama watu milioni 60 tumeshindwa kubadilisha hii ,basi hatuna haki ya kujiita raia wa Tanzania,ni bora iuzwe kwa walowezi tu ,tûtakuwa hatuna tofauti na maiti
 
Kwa Skyline Dar imejitahidi sana kwa mtu ambaye aliondoka Tz miaka mingi akirudi Dar lazima atashangaa jinsi kulivyo pendeza.

Kuna sehemu Dar ukikanyaga utaacha kupachukulia poa bongo jinsi kulivyo pendeza na kupangika . Kuna siku niliamua kutembea kwa miguu mitaa ya Masaki , O bey , Msasani nk ndani ndani nikasema Kuna sehemu Dar pana hadhi kubwa sana jinsi kulivyopangika na kupendeza.
 
Hiyo mitaa unayosemea ndio inayoongelewa kwenye mada?
 
Naomba hii mada ispark kiu ya jamii nzima kubadilika na tujitafakari kama nchi , tubadilike Tanzania inatia aibu .Si majiji ,miji midogo hata vijijini aiisee ni takataka..Kifupi Tanzania ni kama wanaishi panya au mende na si watu
Tanzania ni NCHI Masikini.

Unapokuwa unajadili MADA kwa KUKAZA fuvu, ujue HILO.
 
Traxtion Dar es Salaam ni nzuri achana na hawa washamba akina Yoda maana wao walishajikataa kinafsi. Kila utakacholeta watabisha.

Dar hii hapa:-

20260506_222750.jpg
 
Dar Salaam bado ya hovyo, chafu sana na yenye mabanda mengi tu ya kutu na nyumba kama magofu.
Ukianzia Ubungo, Mwenge na Tazara kuelekea upande wa mikoani ni aibu tupu. Zaidi sana tatizo hata sio ukosefu wa maghorofa bali mpango mji mbovu, makazi yako shaghalabagala.
Tanzania ni nchi masikini..

Na watu wake bado ni masikini.

Hayo unayoita mabanda ndio nyumba za watanzania hizo, kwa vipato vyao.
 
Traxtion Dar es Salaam ni nzuri achana na hawa washamba akina Yoda maana wao walishajikataa kinafsi. Kila utakacholeta watabisha.

Dar hii hapa:-

View attachment 3585324
Dar es Salaam ndio my favorite city in East Africa
So hata watu wakisema Dar ni pabaya, binafsi najua sio pabaya, coz huwezi kuignore all the good parts na kufocus kwenye bad parts pekee
 
Dar ni nzuri kiasi kwa watu wenye kipato kizuri kiasi wanaoweza afford angalau ka gari kamoja binafsi mfano IST, ni nzuri sana kwa matajiri na watawala walio nafasi za juu. Dar sio liveable city kwa watu wenye kipato cha kawaida na majority ya wafanyakazi wanaotegemea huduma za umma zaidi.
 
Traxtion Dar es Salaam ni nzuri achana na hawa washamba akina Yoda maana wao walishajikataa kinafsi. Kila utakacholeta watabisha.

Dar hii hapa:-

View attachment 3585324
Hayo maghorofa mnayoringia yaliyo ya maana ambao wana enjoy ni chini ya 5% ya wakazi wa Dar. Tengenezeni mfumo wa usafiri wa umma wa kueleweka, hospitali zote za serikali ziwe bora ziikaribie Agha Khan, Kairuki au Regency, Hakikisheni Wanafunzi wasitangatange kwenye dalaladala
 
Tanzania ni nchi masikini..

Na watu wake bado ni masikini.

Hayo unayoita mabanda ndio nyumba za watanzania hizo, kwa vipato vyao.
Hayo mabanda serikali ilipaswa kuhakikisha yanawekwa kwenye mpangilio wa kueleweka, kunakuwa na njia za kupitika, mifereji ya maji, mifumo ya maji taka n.k Hata ukiwa na nguo zilizochakaa tu ni vizuri ukajitahidi kuzifua na kuzipiga pasi.
 
Ujenzi wa skyline una reflect attitude na maisha ya watu katika jiji/ mji directly

Mtu aliyekulia Mbeya akija Dar es Salaam in his/her twenties lazima ataipa Dar benchmark ya juu kutokana na kule alipotoka na ataona the best place ever

Mtu aliyekulia Dar na akaishi zaidi ya miaka 30 ataona tofauti na kufikiri kwamba ni maendeleo kwa hayo majengo mapya ambayo kwa kiasi kikubwa hata yeye yanaweza asinufaike nayo zaidi ya kuongeza misongamano ya watu due to overpopulation, kuondoa public places and spaces kua accommodate hayo magorofa, noise pollution ya magari, pikipiki na makumbi ya starehe na hata lack of basic social service kama huduma ya maji ya uhakika na overlow ya sewage na sewerage systems

Mzaliwa wa Dar akienda nje ya nchi kuanzia hapo Nairobi, Kigali na mbali kidogo kama Johannesburg au Addis kidogo ndiyo ataona backwardness ya Dar
Sasa ukipata bahati/nafasi ya kwenda nje zaidi kama hapo Middle East, Far East huko Japan, Singapore mpaka Western Europe na US ndio utajua hata hiyo miji mingine ya Afrika kama Cairo hata Joburg bado iko nyuma ambao kwa mtu wa Dar kwake ni benchmark

Kwa experience yangu, kwa mtu aliyeondoka Dar akawa nje ya nchi miaka mingi excitement ya kurudi Dar inaishia unapoanza kuona zile kutu za Kipawa na Vingunguti kabla hata hujatua JNIA tofauti na ukiwa unatua airport nyingi duniani unapoona miji imepangika na skyline za kuvutia na hapo hujakutana na madimbwi ya maji machafu mitaani na misongamano na lawlessness ya bodaboda na waywardness na jaywalking watu kujivukia barabara hovyo sehemu zisizoruhusiwa
Cultural changes zinahitajika kubadilisha mindset kwani hata miji ikijengwa vipi attitude za wakazi zitafanya hivyo vitu kuwa superficial mf Magorofa ya Magomeni taka hazizolewi, hawataki kulipa, lift zinanuka mikojo wanajisaidia humo na maji juu hayatoki watu wanachota maji chini wanapanda nayo mpaka juu
Huwezi kuwa na skyline nzuri ambayo utashindaa kui maintain
 
Kwa Skyline Dar imejitahidi sana kwa mtu ambaye aliondoka Tz miaka mingi akirudi Dar lazima atashangaa jinsi kulivyo pendeza.

Kuna sehemu Dar ukikanyaga utaacha kupachukulia poa bongo jinsi kulivyo pendeza na kupangika . Kuna siku niliamua kutembea kwa miguu mitaa ya Masaki , O bey , Msasani nk ndani ndani nikasema Kuna sehemu Dar pana hadhi kubwa sana jinsi kulivyopangika na kupendeza.
Umeiona skyline ya Mogadishu, Somalia iliyo vitani muda wote?? Kuna mambo huwa yanatokea tu mahali kadri ya muda ili mradi binadamu wapo hapo halafu kuna mambo yanafanyika kwa sababu binadamu wamejiongeza, wana ufanisi na merits.
 
Ujenzi wa skyline una reflect attitude na maisha ya watu katika jiji/ mji directly

Mtu aliyekulia Mbeya akija Dar es Salaam in his/her twenties lazima ataipa Dar benchmark ya juu kutokana na kule alipotoka na ataona the best place ever

Mtu aliyekulia Dar na akaishi zaidi ya miaka 30 ataona tofauti na kufikiri kwamba ni maendeleo kwa hayo majengo mapya ambayo kwa kiasi kikubwa hata yeye yanaweza asinufaike nayo zaidi ya kuongeza misongamano ya watu due to overpopulation, kuondoa public places and spaces kua accommodate hayo magorofa, noise pollution ya magari, pikipiki na makumbi ya starehe na hata lack of basic social service kama huduma ya maji ya uhakika na overlow ya sewage na sewerage systems

Mzaliwa wa Dar akienda nje ya nchi kuanzia hapo Nairobi, Kigali na mbali kidogo kama Johannesburg au Addis kidogo ndiyo ataona backwardness ya Dar
Sasa ukipata bahati/nafasi ya kwenda nje zaidi kama hapo Middle East, Far East huko Japan, Singapore mpaka Western Europe na US ndio utajua hata hiyo miji mingine ya Afrika kama Cairo hata Joburg bado iko nyuma ambao kwa mtu wa Dar kwake ni benchmark

Kwa experience yangu, kwa mtu aliyeondoka Dar akawa nje ya nchi miaka mingi excitement ya kurudi Dar inaishia unapoanza kuona zile kutu za Kipawa na Vingunguti kabla hata hujatua tofauti na ukiwa unatua airport nyingi duniani unapoona miji imepangika na skyline za kuvutia na hapo hujakutana na madimbwi ya maji machafu mitaani na misongamano na lawlessness ya bodaboda na waywardness watu kujivukia barabara hovyo sehemu zisizoruhusiwa
Cultural changes zinahitajika kubadilisha mindset kwani hata miji ikijengwa vipi attitude za wakazi zitafanya hivyo vitu kuwa superficial mf Magorofa ya Magomeni taka hazizolewi, hawataki kulipa, lift zinanuka mikojo wanajisaidia humo na maji juu hayatoki watu wanachota maji chini wanapanda nayo mpaka juu
Tatizo ni kwamba mada haikufanya comparison na miji ya Middle East
Halafu yote haya hayabadilishi kitu kuwa skyline ya Dar imepanuka
Sio kila kitu kinahusu exposure. Tunajua kuhusu Dubai, tunajua kuhusu miji ya China, Marekani, Japan etc. Hauna haja ya kwenda huko kujua kuwa imezidi Dar
 
Back
Top Bottom