Siwezi kulala njaa inauma, nipo ugenini

Siwezi kulala njaa inauma, nipo ugenini

Guys nipo mkoa fulani sasa mchana nilikula ugali nikaleta zile mbwembwe za Dar za sili usiku zaidi ya matunda tu,

Sielewi nini kimetokea ila njaa inaniuma siwezi kulala na siwezi kutoka kutafuta chakula wala sina mtu ninayemjua nimuagize,

Tumbo linaunguruma, baridi kali kuna vibiscuti wala havitoshi, tumbo lataka chips kuku paja au ndizi choma mishikaki,

Nyie kumbe njaa inauma namna hii🙌🏻
Kujeni basi tupige story, i can't sleep😭
Kujiendekeza tu
Kula usiku ni anasa
 
We mvumilivu umefika hadi asubuhi Dr.

Mi njaa ya usiku siwezi vumilia hata kidogo, bora mchana naweza nisile siku nzima sio usiku. Akili yangu huwa inatumika sana usiku lazima nile nishibe, huwa nakula hata saa 7 usiku fully meal.
Hata mimi siwezi kuvumilia njaa usiku naweza kuamka nikakaanga mayai au kupika tambi ila sasa kuna mazingira uvumilivu ndio the only choice, jana hapana kwa kweli nimeandika hadi kwenye diary halafu sasa kila nikiwapigia watu ninaowajua wanipe kampani ya kuongea kwenye simu wote hawakupokea wamelala, nilitiaje huruma
 
Back
Top Bottom