Sio lazima kuoga kila siku.

Sio lazima kuoga kila siku.

Kunuka ni nnje nnje , bila kuoga mara mbili kwa siku siwezi jisikia vizuri , na ubaya wa harufu mtoaji hauwezi isikia , ila kiukweli watu wengi wananuka, sio masikio vikwapa na mapua , na wengi wanazunguka na chembechembe za mapupu bila kujua wanatema vibaya mno
Ptuu, adi nimejisikia kinyaa!

Siyo watu 'wengi wananuka', watu wote tunanuka, ila kila mmoja kivyake na jasho lake.

Eti mtu usioge kweli, nimeshangaa sana.
 
Yoda
Kuna faida sana kwenye kuoga
Kwangu mimi nikimaliza kuoga najihisi mwepesi sana nakua na amani sana
kuna hisia fulani napata wakati wa kuoga na hata nikimaliza

Zaidi nakua comfortable 👌
Kitu ukishakuwa na mazoea nacho kuna namna kinakutengeneza kisaikolojia, hata ukifika Njombe ukawa unashinda ndani unaweza kutaka kuoga kila siku
 
Kisayansi kila siku na kila muda cells za skin membrene zinakufa ujue!

Tunachokisugua na dodoki kukiondoa kwenye ngozi kama uchafu wakati wa kuoga %kubwa ni chembe chembe za ngozi mfu na jasho kwa %kidogo.

Hata usipotoa jasho kwa kazi lakini ni lazima mwili wako utachafuka tu.

Hivyo kuoga kila siku si hitaji la hiyari la mchafukoge, bali ni hitaji la lazima la binadamu ili kuuweka mwili wake katika hali ya siha.
elezea vizuri khs hizo chembechembe
 
Back
Top Bottom