Nongo mwilini: Uhalisia wa mazoea uliopotoshwa

Nongo mwilini: Uhalisia wa mazoea uliopotoshwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,652
Reaction score
860,938
Nongo ninini?

Taka za mwilini: Huu ni uchafu unaojikusanya mwilini, mara nyingi kutokana na jasho lililokauka na vumbi kwenye ngozi.

Wengi wamekulia kwenye mazoea ya kwamba mwili huwa hautakati kwa asilimia 100 kwakuwa una nongo ya asili ...

Na kwa kuthibitisha madai yao ni matumizi ya taulo baada ya kuoga na uchafu unaobaki kwenye taulo baada ya kujifuta.. Haya ni mazoea potofu na kukosa elimu sahihi

Hakuna kinaitwa nongo ya asili mwilini bali uchafu kwenye taulo unatokana na sababu hizi

1. Kutokuoga kwa usahihi.. Wengi wetu hawajui kuoga kwa usahihi hivyo hawatakati..kuna maeneo nongo imegandiana lakini maji yanapita shwaa

2. Uchafu wa maji: Ni vigumu Tanganyika na pengine Africa kujivunia tuna maji safi achana na salama..

Maji yetu mengi tunayotumia hayajafanyiwa 'treatment ya kutosha.. Sasa imagine mwili wenye nongo uoge maji machafu😀 hapo hata kama unajua kuoga hutatakata

3. Matumizi potofu ya taulo. Taulo ni kwa ajili ya kukausha maji mwilini sio kitendea kazi cha kuondoa nongo zilizoachwa kusafishishwa

4. Taulo nalo ni kitu kinachohitaji usafi wa mara kwa mara! At least lifue mara 2 kwa wiki.. Wewe nara ya mwisho kufua taulo ni lini?😀

Mwili hauna nongo ya asili ndio maana kuna mataulo meupe
Mazingira yakiwa safi .. Hakuna vumbi
Ukioga maji safi
Ukioga kwa usahihi na kutakata
Ukalitumia taulo kwa usahihi , utaachana na dhana potofu za nongo za asili mwilini
Zingatia: hupaswi kuwa na taulo moja tu ndani ya nyumba.. At least mawili au matatu rangi tofauti tofauti
152d3a49-1e15-49b3-b714-6a6220542ab9.jpeg
 
Tazama mataulo ya hotel za gharama ya juu kidogo ambapo kuna maji safi na mataulo ya gesti za uswazi ambayo asubuhi hutumika mpaka kusafisha fangasi miguuni na kugeuzwa kikanyagio kabla ya kuvaa viatu 😁
 
Nongo ninini?
Taka za mwilini: Huu ni uchafu unaojikusanya mwilini, mara nyingi kutokana na jasho lililokauka na vumbi kwenye ngozi.

Wengi wamekulia kwenye mazoea ya kwamba mwili huwa hautakati kwa asilimia 100 kwakuwa una nongo ya asili ...
Na kwa kuthibitisha madai yao ni matumizi ya taulo baada ya kuoga na uchafu unaobaki kwenye taulo baada ya kujifuta.. Haya ni mazoea potofu na kukosa elimu sahihi

Hakuna kinaitwa nongo ya asili mwilini bali uchafu kwenye taulo unatokana na sababu hizi
1. Kutokuoga kwa usahihi.. Wengi wetu hawajui kuoga kwa usahihi hivyo hawatakati..kuna maeneo nongo imegandiana lakini maji yanapita shwaa

2. Uchafu wa maji: Ni vigumu Tanganyika na pengine Africa kujivunia tuna maji safi achana na salama.. Maji yetu mengi tunayotumia hayajafanyiwa 'treatment ya kutosha.. Sasa imagine mwili wenye nongo uoge maji machafu😀 hapo hata kama unajua kuoga hutatakata

3. Matumizi potofu ya taulo. Taulo ni kwa ajili ya kukausha maji mwilini sio kitendea kazi cha kuondoa nongo zilizoachwa kusafishishwa

4. Taulo nalo ni kitu kinachohitaji usafi wa mara kwa mara! At least lifue mara 2 kwa wiki.. Wewe nara ya mwisho kufua taulo ni lini?😀

Mwili hauna nongo ya asili ndio maana kuna mataulo meupe
Mazingira yakiwa safi .. Hakuna vumbi
Ukioga maji safi
Ukioga kwa usahihi na kutakata
Ukalitumia taulo kwa usahihi , utaachana na dhana potofu za nongo za asili mwilini
Zingatia: hupaswi kuwa na taulo moja tu ndani ya nyumba.. At least mawili au matatu rangi tofauti tofautiView attachment 3578904
Shukran kwa somo murua! Hivi Tanganyika, tunaishi viwango sahihi vya Utu, au ubinadamu? Naona kimtazamo, kila jambo tunachakachua katika hali ambayo hata miili yetu hatuiui, hatuijali. Inatisha!
 
Tazama mataulo ya hotel za gharama ya juu kidogo ambapo kuna maji safi na mataulo ya gesti za uswazi ambayo asubuhi hutumika mpaka kusafisha fangasi miguuni na kugeuzwa kikanyagio kabla ya kuvaa viatu 😁
Kuna taulo , ndogo sana za kujisugulia, mwili ukiwa na sabuni, au kwa mazingira yetu tungetumia dodoki, kutoa nongo katika mwili. Kwa wengi hatutumii, na bado tunashangaa kwa nini taulo linachafuka!
 
Kuna taulo , ndogo sana za kujisugulia, mwili ukiwa na sabuni, au kwa mazingira yetu tungetumia dodoki, kutoa nongo katika mwili. Kwa wengi hatutumii, na bado tunashangaa kwa nini taulo linachafuka!
Inategemea umetoka kufanya kazi gani.. Kama huna usafiri binafsi na hujashinda ndani kwenye kiyoyozi ni busara zaidi kutumia dodoki
Lakini pia kuna sabuni/shampoo.. Zaidi kuna nywele za aina zote! Hakuna maeneo yanahifadhi nongo nyingi kama shingoni kwapani na kwenye pachupachu za siri
 
Kumbe ni alternative nzuri ya kuondoa nongo, hivi nongo ndio ukurutu? ama ukurutu ni tatizo/ugonjwa wa ngozi?
Ukurutu ni ugonjwa wa ngozi
Ukurutu (kitaalamu eczema au atopic dermatitis) ni ugonjwa wa ngozi wa muda mrefu unaosababisha ngozi kuwasha, kuwa nyekundu, kukauka, na wakati mwingine kupasuka au kutoa majimaji.
 
View attachment 3578907
Shower gell zipo aina tofauti tofauti na brand tofauti..ukiogea hizii hakuna NONGO ITAKAYO BAKIA MWILINI..

😊 Asante brother mshana kwa kunipa msamiati mpya ambao ndio nimeujua Leo NONGO
😀 ujue na kuitumia pia.. Wengi wanaoga bila kujisafisha.. Bafuni dakika 5 mtu keshamaliza😁
 
View attachment 3578907
Shower gell zipo aina tofauti tofauti na brand tofauti..ukiogea hizii hakuna NONGO ITAKAYO BAKIA MWILINI..

😊 Asante brother mshana kwa kunipa msamiati mpya ambao ndio nimeujua Leo NONGO
Njia bora ya kutoa nongo (seli za ngozi zilizokufa na uchafu) mwilini ni kusafisha ngozi kwa kina kupitia michakato ya kiasili inayosaidia kulainisha na kuondoa uchafu huo bila kuchubua ngozi.

1. Kutumia Maji ya Vuguvugu
Kuoga au kushinda kwenye maji ya vuguvugu kwa dakika 10–15 husaidia kulainisha nongo na kufungua vitundu vya ngozi, jambo linalofanya nongo kutoka kwa urahisi zaidi unaposugua.

2. Kutumia Dodoki au Sifongo (Exfoliation)
Tumia dodoki la asili, sifongo, au glovu maalumu za kuogea kusugua mwili kwa mzunguko. Hii husaidia kukwangua nongo iliyolainika.
Kidokezo: Usisugue kwa nguvu sana ili kuepuka kuumiza ngozi.

3. "Scrub" za Kiasili za Nyumbani
Unaweza kutengeneza scrub yako mwenyewe kwa kutumia vitu vinavyopatikana jikoni:
Sukari na Mafuta ya Nazi: Changanya sukari na mafuta kidogo ya nazi au mzeituni. Sugua mwili wote kabla ya kuoga. Sukari husaidia kuondoa nongo na mafuta hulainisha ngozi.
Kahawa na Asali: Mchanganyiko huu ni mzuri kwa kutoa nongo na kuuacha mwili ukiwa na harufu nzuri na mng'ao.
Chumvi ya Bahari: Inafaa zaidi kwa sehemu zenye ngozi ngumu kama magoti na viwiko.

4. Matumizi ya Sabuni na Mafuta ya Kulainisha
Tumia sabuni zenye asidi ya kiasili kama salicylic acid au sabuni za asili (kama sabuni ya mkaa au limao) ambazo husaidia kuvunja mafuta yanayonata na nongo.
Hakikisha unapaka mafuta mazuri ya kulainisha (moisturizer) mara baada ya kuoga ili kuzuia ngozi isikauke na kutengeneza nongo mpya haraka.

5. Kunywa Maji ya Kutosha na Detox
Afya ya ngozi huanzia ndani. Kunywa maji mengi husaidia seli za ngozi kuwa na unyevu, jambo linalopunguza kuteleza kwa nongo kavu mwilini. Njia nyingine za kutoa sumu zinazoweza kusaidia afya ya ngozi ni pamoja na:

Kunywa maji ya limau asubuhi.
Kufanya mazoezi ili kutoa jasho linalosaidia kusafisha vitundu vya ngozi.

CC: kitalembwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom