Single momz tunashida sana katika mahusiano

Single momz tunashida sana katika mahusiano

Status
Not open for further replies.
single mom or not, heshima yako ni utu wako na tabia yako. Waoaji ni wengi mno, tena hawa hawa wasio na watoto.

Kikubwa jitambue, punguza utegemezi, usijinyanyapae na kujiona hufai tena. Jithamini wewe kwanza, jamii inayokuzunguka itakuthamini pia.

Ila kama unaweza, date single dads too

Kamata LIKE!
 
Watu wengi wanachukulia single momz kama hawana umuhimu tena na hawafai katika mahusiano. Siku hizi wanaume wengi ambao hawajakuwa na watoto utasikia wakisema "Mimi mwanamke wenye mtoto simtaki amechoka na amekongoroka kabisa huyo"

Kumbuka hapa kuna wanawake wengine hata ukikutana nae na asipokuambia ana mtoto huwezi jua, anajipenda na ni mrembo wa kuvutia na mwenye maendeleo.

Wanaume wengi sana wanaona hana thamani, na wengine kusema ni wameshindikana walikotoka yaani na jaamaa aliyezaa nae.Tukumbuke NOT EVERYMAN MEANT TO BE A DADY, kuna wengine ni waharibifu tu, pengine pia tofauti za maisha zinazotokea zinapelekea yote hayo kutokea, Watu hawaelewi...

Single moms haimaanishi hawatakiwi kuwa na mahusano mengine mapya labda na mwanaume ambaye hana mtoto, wengi hudhani ukijitumbukiza hapo basi utalea mtoto.

Jamani kuna watu wanauwezo wa kutake care ya watoto wao bila msaada, jiulize kabla yako nani alikuwa anamsaidia kama sie mwenyewe. Ni faraja na upendo tu anahitaji kutoka sehemu nyingne.

Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?

Mwenye mawazo hayo wewe ni katili na mbinafsi kabisa. Na ndo maana inafikia hatua wanaume mnafichwa mnakuja kutambua kwamba ana mtoto imepita hata miaka 10, halafu unalaumu oooh hakuniambia. Hakukuambia kwasababu anajua mtazamo wenu kwao...

Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..

Mimi mwenyewe ni mfano mzuri, nimepata unyanyasaji sana na wanaume, pale nilipokuwa nawaambia nina mtoto, wengine walishia kimya kimya, wakidai eti tuna kawaida ya kupasha kiporo na mzazi mwenza HIYO NI UONGO NA FIKRA MBOVU ZA WATU
Na kamwe sikuweza kuficha kama sina mtoto kwasababu najua nini maana ya mtoto. Mtoto ni zaidi ya thamani ya vitu ulivyonavyo ndani...
Tena wanawake ambao mmekutana na haya wala msifiche ukweli, Mwanaume akikimbia ujue mungu kakuepushia jambo.

WANAUME HEBU TOENI NA MBADILIKE NA HIZO IMANI AMBAZO SIO...

Swali lolote linakaribishwa... Asanteni

Mimi naamini Hivi : Kama kuna wanaume ambao hawawezi kuoa Single Mom, basi tujue vilevile wapo wanaume wanaoweza kuoa single Mom ivyo TULIA LEA MWANAO mume atakuja tu, binadamu tuko tofauti, Hatuko sawa!ILA kwa upande wangu sio siri SIWEZI ilo lilinishinda, ilishatoka nilikua na date binti wa kichaga mzuri vibaya mno, alikua hajawahi niambia kua alishazaa huko uchagani, tulieeenda mwsho wakati nataka kutangaza nia ananiambia ana watoto tena wawili dah, nikasema ngoja nijaribu niendelee siwezi kumuacha. Aisee kwa wivu wangu, maisha yalikua magumu sana nikakubali kuachia ngazi, Kingine nachopenda kuongeza usiwaze upande wa uyu muoaji TU kua yukoje, Kuna tabia za wanaume kama alizaa na binti basi akijua binti ameolewa na wanae wanalelewa nyumba ya mtu mwingine hutaka kuonesha kua nae alishamfaidi sana uliyemuoa hata akazaa nae tena anaweza fanya lolote,unakuta ataanza kutaka kuonana na mkeo hata muda ambao wewe upendezwi nao, Simu kila muda kwa mkeo ili kukughasi tu muoaji na kukuonesha nae ni wa umuhimu kwa mkeo, sasa pale wewe uliyeoa unajikuta una mawazo kibao wala huna amani. Hivyo inategemea na jamaa aliyezaa na uyu single mom yukoje pia
 
ww ndio upewe ufahamu kuwa kuzini nje ya ndoa ni dhambi.
Ww mwanamke hatari sana unajifariji wakat ww ni mzinzi!
Kipindi cha sheria ya Mussa ulistahili upigwe mawe hadi kufa.

Who are you to judge her jamani? Ivi we hujawahi kuzini achilia mbali dhambi nyingine! Nakushauri tu acha kuhukumu mana hata bibilia imekataza
 
Tatizo kubwa ni, kujifanya unafuatilia matumizi ya mtoto kwa uliyezaa nae!! Wanaume huwa hatulipendi hilo na ni chanzo cha kurudisha mahusiano yenu yaliyovunjika. Sasa ukute bahati mbaya uliyezaa nae amekuja kuwa na mafanikio zaidi yangu, huduma na caring ni moja ya sumaku ya kumnasa mwanamke yeyote. Inawezekana ni kweli alikutenda vibaya but akianza kujifanya anakujali na kukuhudumia wewe na mwanao kinachofuata ni kushindwa kuelewana na mumeo uliye nae sasa, kisingizio ni matumizi ya mtoto au ni mzazi mwenzangu.

Wanaume tunapolikumbuka hilo, tunaumia sana coz tunahisi ni moja ya vijidharau katika mahusiano

Hilo tatizo nilianza kuliona TZ na sehemu mbalimbali za dunia. Baby daddy wake akiwa hai, halafu awe na mambo mazuri kuliko wewe, mara nyingi huendelea kupiga mashine na anaona kama amewaweka ndani wote wewe na mkeo. Halafu itokee bahati mbaya umetetereka kifedha, hakuna rangi utaacha ona.
 
Absolutely true ! Ikumbukwe pia kuwa MTALAKA HATONGOZWI ukienda kufuata sijui ada ya mtoto, mara hela ya tuisheni, ni kiasi cha kuangalia mazingira kama panaruhusu kupasha kiporo jamaa linagonga tu

yah, ni kuangalia kushoto na kulia, kama vile unavuka barabara
 
Mwisho wasiku munaolewa wote,ebu chukulia mekeo ana mtoto wa jamaa na wewe una mtoto inatokea jamaa kampeleka mwanae kwenye shule kubwa alafu akamtuma mkeo aje akwambie kuwa kama inawezekana na mtoto wako ampeleke kwenye shule aliyo mpeleka mtoto wake mahitaji yote juu yake.je utakubali au na ukicheki uwezo wako wa chini mtoto ana soma shule ya kata, utafanya je?
 
Is not the same
Ukimwambia mwanamke una mtoto hakuna ugumu sana kama mwanamke akikuambia ana mtoto let's be honest bro we have to stop being selfish

Ugumu ni sawasawa. Ni wewe unadhani hakuna tofauti.

Mwanaume huwa anafanya maamuzi kwa kuangalia mbali na kutumia logic kadha wa kadha na kuangalia hali halisi ya wakati ujao. Hivyo hukataa tatizo kabla halijatokea (kwa kifupi wao wapo kwenye kinga zaidi sio kutibu)

Mwanamke atakwambia sasa hivi kwamba mtoto sio tatizo halafu akishaingia ndani ya nyumba ndio utaanza kuona kwamba mtoto wako ni tatizo.

Ni mara mia mwanaume anayemkubali mwanamke mwenye mtoto huwa anampenda mke na mtoto wake na huwa anamjali sana mtoto wa mke. Kwa wanawake ni kinyume mkuu. Hili nimeliona sehemu nyingi sana.

Wanawake huwa wanafanya maamuzi ambayo wanaona yatawanasua kwa wakati huo tu, hawaangalii mbeleni itakuwaje, wanaamini kesho itaji-take care yenyewe halafu baadae wanaanza kuleta sokomoko(kwa kifupi wao hawajali kinga, wapo tayari kuingia kwenye tatizo na kutafuta tiba mbele kwa mbele).

Angalizo: hapa naongelea majority, sio wote.
 
Pia uombe usizae nje ya ndoa/usichepuke na kusababisha mtoto kulelewa na mama pekee. Hali upendi watu waliolelewa na mama pekee.

inategemea na mwanamke utakaezaa nae huko mchepukoni, kawaida mama wa kawaida hawezi kumuacha mwanae afe njaa, nikimtumia pesa kila mwezi atalea mwanangu kwa uhakika.

Labda kama mama mwenyewe ni wale wakurukaruka viwanja tofauti, huyu unaweza ukamtumia hela ya matumizi ya mtoto yeye akaenda kununua mkufu wa dhahabu akamuacha mtoto taabani.
 
Dad died when I was 2...my mom became a single mom.... but she got married to my step dad and I'm enjoying staying with my super super step dad
step daddy mara nyingi wanakuwaga supper. Tatizo ni step mom. Ndio maana naona hoja ya mleta mada haina mashiko, imelalia upande mmoja, bila kuangalia ukweli wa upande wa pili pia.
 
hapo ninaowaonea huruma na kuwaombea kwa Mungu ni namba 1 tu.
Kwasababu hawajapenda yaliyowakuta na hata mm binafsi naweza kuoa mwanamke wa aina hyo.
Lakn hayo makundi mawili ni chipsi kuku,soseji na bagga ndio zmewaponza

"Ni kiherehere chao" by JK.
 
single mom or not, heshima yako ni utu wako na tabia yako. Waoaji ni wengi mno, tena hawa hawa wasio na watoto.

Kikubwa jitambue, punguza utegemezi, usijinyanyapae na kujiona hufai tena. Jithamini wewe kwanza, jamii inayokuzunguka itakuthamini pia.

Ila kama unaweza, date single dads too

A word brother much respect
 
Kwann ulimuacha kama bado unampenda?
Ujinga huo badala ya kumuheshim jamaa anafanya kazi uliyoishindwa unaleta hzo dharau
Trust me nikioa mwanamke ana mtoto
Mwanae atatibiwa kama wanangu
Atasoma kama wanangu
Hataki ataishi nje ya nyumba yangu
Hzo tiba zako za India sijui japan zilikua wp wakat una kana/unamuacha?
Mkuu, duniani kuna mambo ya ajabu.
Kuna wanawake ambao kulala au kuzaa na mwanaume fulani anaona yeye ndio anapewa favor. Yupo tayari kukubali kuzalishwa bila kuolewa na mtu ambae pengine ni rais, mkurugenzi fulani, mwenye pesa za ukweli, n.k na anakuwa ashajulishwa in advance kwamba ndoa hakuna, hivyo anatafuta mwanaume mwingine wa kujibanza kwake. kwa hiyo ikitokea mtoto anaumwa wanaweza kweli kusafiri kwenda nje ya nchi kumtibu, kwa sababu hawa watu hawajagombana na hawajaachana kama ulivyoambiwa.
Kuna mambo ya ajabu, Nilishafuatwa na mke wa mtu ambaye alikuwa demu wangu kabla hajaolewa anataka azae na mimi mtoto moja akiwa ndani ya ndoa yake na amlee humohumo kwenye ndoa yake.

Mkuu kuna mambo ya ajabu humu duniani kuliko unavyoweza kufikiri.
 
Unajua wanawake mnatupasua kichwa sana, hivi unamuongeleaje Mwanamke ambae alipendwa, tena kwa dhat na Mwanaume wa mtaani kwao, Ofisin ama hata college, kisha kwa sababu tuu ya hali duni ya mshkaji, mdada akamkataa kata kata, na badala yake akatanua miguu kwa Mwanaume mwingine kisa tuu huyo yy anapesa za kumzidi jamaa, kufika huko baada ya kutumika, dhaman yake ikashuka, akapata Mimba, jamaa akaikataa, kisha mama kajifungua mwana. Technically huyu ni single Mama, nae akirudi kwa Yule jamaa wa zamani, afu mshkaj akamchukulia kama Mfa Maji anaetapa tapa kutafuta baba wa pili, Utamlaumu Mwanaume?

Kwa ishu hii ni kama vile BigG aka chewing gum, imetafunwa wee imekuwa nyeupee imeisha sukari, sasa ndio watemewa na wewe ule, wakati ulishanyimwa kabla.
I m just Joking.
 
Huu uzi ni somo kubwa kwa ambao bado hawajaitwa mama kama huu ndo msimamo wa wanaume wengi katika jamii mabinti tujitunze sana kusubiri mtu sahihi atakayekufanya uitwe mama ndani ya ndoa kwa heshima zote
single momz nawaheshim sana msikatishwe tamaaa na kina makomana mnayo second chance

Mtu sahihi inategemea na usahihi wa kichwa chako katika ku-muaprove.
Mtu sahihi kwa binti Uwoya hawezi kuonekana sahihi kwa binti Shusho, na kinyume chake.

Omba Mungu akupe akili sahihi katika kuchagua mtu.
 
ni heri nichukiwe na wengi lakin lazma niseme ukweli ambao upo kwa wanaume dhid ya single mums.......
Tusilee ujinga yaani sku hiz kila kischana cha miaka 22-25 kina mtoto.
Tunasifia watu waendekeze uzinzi shiiiit!
Comments zako humu zitawaamsha na kuwaepushia hili janga mabinti kadhaa ambao wamezisoma.

Watu wanakwenda Misikitini/Makanisani kwa sababu wanajua kesho kuna moto. Kama binadamu wangeambiwa hakuna adhabu siku ya mwisho, nadhani unajua ingekuaje.

..............
 
Akili yako imejionesha uko level gani wala usitumie nguvu nyingi sana kulazimisha upo bright

ww bwana usitake kila mwanaume awe na mawazo kama yako na mtazamo kama wako, ndio maana mwingne huanza na gari na mwingne huanza na nyumba.
Sasa ww usiilazmishe akili yangu ikubali mawazo ya kishenzi kama yako.
Kwa mtazamo wako ww inaonesha upo tayar hata kulelewa familia yako na mwanaume mwenzako wakat ww upo hai bado.
:::::::::::: kila mtu na aonavyo yeye, ndio maana kuna watu wanajiita wanaume wakat huo wanapigania na kulilia kuolewa na wanaume wenzao lakin nao ni wanaume na wanajiona wako sahihi kabisa hata ww siwez kukushangaa ukisifia upuuzi kama huo siwez kujua upo kundi gan la wanaume:::....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom