Single momz tunashida sana katika mahusiano

Single momz tunashida sana katika mahusiano

Status
Not open for further replies.
Mkuu pata picha ifuatayo... mkeo ana mtoto na mwanaume mwingine nanyi mna watoto wawili pamoja. Mnakaa nao wote. Mtoto wa kambo anasomeshwa shule na baba mtoto ya million 6 kwa mwaka, wewe mume ukijipiga sana unaweza kuwasomesha watoto hawa wawili government na vi tuition kidogo. Aisee noma sana kidume lazima uwe mpole tu ukisikia wife anaenda kuchukua matunzo ya mtoto! Ndo maana kwangu mimi naona its more than money, kuna jealously, kujisikia inferior mbele ya kidume mwenzio nk.

Noma sana mzee!!unaweza kufa....single moms waende zao hukooo!!
 
Daah!! Noma sana halafu utakuwa mnyonge sana!! Kuna uzi jamaa alikuwa anaomba ushauri humu, mkewe kawa close sana na mzazi mwenzie na kila akihoji jibu ni nafuata matumizi na kujadili malezi ya mtoto.

Huyo nae hata Kama kusoma hajui...picha inaonekana clear!!!!anakung'utiwa hapo!!
 
Jamani nafuu kuwa single mama, ulee mtoto peke yako, kuliko kuishi na baba mtoto asiyejua majukumu.
Utakuta mdada aliolewa, ameshazaa ila ndoa imemshinda sababu ya mume aliyekuwa naye ni mzigo.

Mume yupo yupo tu, hatoi penzi kwa mkewe. Kila siku sababu kibao ilimradi akwepe wajibu wake.
Hivi mwanamke wa aina hii, akiamua kuwa single mama kuna ubaya gani? Cha muhimu ni kuweza kulea mtoto wako mwenyewe tu. Hata kama hutakuja kuolewa tena ni bora, mie kwangu ndoa haina umuhimu wowote. Mtoto ndio kila kitu kwangu, kama mwanaume hataamua kunioa kwa ajili ya mwanangu na ajiendee tu.

Kuna single mama, hawakutaka kuwa single mama ila ilibidi kutokana na mazingira. Na watu tunajifunza kwa makosa.
Wengine walipata wrong husband, hivyo hata baadaye wakija olewa tena ni wazuri sana.
 
Tatizo kubwa ni, kujifanya unafuatilia matumizi ya mtoto kwa uliyezaa nae!! Wanaume huwa hatulipendi hilo na ni chanzo cha kurudisha mahusiano yenu yaliyovunjika. Sasa ukute bahati mbaya uliyezaa nae amekuja kuwa na mafanikio zaidi yangu, huduma na caring ni moja ya sumaku ya kumnasa mwanamke yeyote. Inawezekana ni kweli alikutenda vibaya but akianza kujifanya anakujali na kukuhudumia wewe na mwanao kinachofuata ni kushindwa kuelewana na mumeo uliye nae sasa, kisingizio ni matumizi ya mtoto au ni mzazi mwenzangu.

Wanaume tunapolikumbuka hilo, tunaumia sana coz tunahisi ni moja ya vijidharau katika mahusiano

Absolutely true ! Ikumbukwe pia kuwa MTALAKA HATONGOZWI ukienda kufuata sijui ada ya mtoto, mara hela ya tuisheni, ni kiasi cha kuangalia mazingira kama panaruhusu kupasha kiporo jamaa linagonga tu
 
Kwa kweli single moms n dads wanna mtihani. Ila si vizuri kuficha, japo changamoto zitokanazo na hali hii ni nyingi. Ila kwanini single moms wengi hawajali mahusiano ya wengine? Ni desperation ya ndoa au? Nimeona wengi wanavamia watu wenye mahusiano Vila kujali unamuumizaje mwanamke mwenzako. Na mara nyingi mnaumia wenyewe na kubaki na guilty.
 
ukiona wanakukimbia, tatizo si mtoto peke yake, kuna jingine ...

umeona eeh! halaf anasema eti bora tuliozaa tunajijua tuna kizazi sijui kuliko hao ambao hawajazaa. anashangaza! anataka aonekane yeye ni bora zaidi kwa kuponda wengne!! wanaume siku hizi hawakimbii mtoto, ukikimbiwa ni ww mwenyewe kwa kauli chafu chafu kama hizo.
 
Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..
wewe ndo maana unakimbiwa maana una kauli chafu sana.
 
Sijapenda ulivyosema eti aliyeza atleast yeye ana kizazi kuliko huyo ambae hajazaa!! Ya mungu ni mengi dada yangu huwezi jua labda na wewe ndo umebarikiwa uzao wa huyo tu mtoto mmoja,na hata kama akikuoa unaweza usizae tena!! Jitetee kwa jambo lingine lakini swala la uzazi hilo achana nalo kabisa.
 
Mimi kama una mtoto ambae si wangu sikuoi. Kama nikigundua ulikuwa na mtoto nakuacha. Ila nikikupa mimba nitakuoa
 
Sijapenda ulivyosema eti aliyeza atleast yeye ana kizazi kuliko huyo ambae hajazaa!! Ya mungu ni mengi dada yangu huwezi jua labda na wewe ndo umebarikiwa uzao wa huyo tu mtoto mmoja,na hata kama akikuoa unaweza usizae tena!! Jitetee kwa jambo lingine lakini swala la uzazi hilo achana nalo kabisa.

yaani kaharibu hapo tu atakuwa ni mtu wa kujikweza sana huyu
 
Absolutely true ! Ikumbukwe pia kuwa MTALAKA HATONGOZWI ukienda kufuata sijui ada ya mtoto, mara hela ya tuisheni, ni kiasi cha kuangalia mazingira kama panaruhusu kupasha kiporo jamaa linagonga tu

Kiporo hakihitaji moto mwingi
 
Sijapenda ulivyosema eti aliyeza atleast yeye ana kizazi kuliko huyo ambae hajazaa!! Ya mungu ni mengi dada yangu huwezi jua labda na wewe ndo umebarikiwa uzao wa huyo tu mtoto mmoja,na hata kama akikuoa unaweza usizae tena!! Jitetee kwa jambo lingine lakini swala la uzazi hilo achana nalo kabisa.

kweli kabisa halafu anaongea kwa kujiamin kuzaa ni mipango ya Mungu kwahyo asiyezaa ndio asiolewe?! Amegalagazwa huko mpaka amezalishwa halafu leo anataka mwingne ndio aoe wakat kachoka
 
Watu wengi wanachukulia single momz kama hawana umuhimu tena na hawafai katika mahusiano. Siku hizi wanaume wengi ambao hawajakuwa na watoto utasikia wakisema "Mimi mwanamke wenye mtoto simtaki amechoka na amekongoroka kabisa huyo"

Kumbuka hapa kuna wanawake wengine hata ukikutana nae na asipokuambia ana mtoto huwezi jua, anajipenda na ni mrembo wa kuvutia na mwenye maendeleo.

Wanaume wengi sana wanaona hana thamani, na wengine kusema ni wameshindikana walikotoka yaani na jaamaa aliyezaa nae.Tukumbuke NOT EVERYMAN MEANT TO BE A DADY, kuna wengine ni waharibifu tu, pengine pia tofauti za maisha zinazotokea zinapelekea yote hayo kutokea, Watu hawaelewi...

Single moms haimaanishi hawatakiwi kuwa na mahusano mengine mapya labda na mwanaume ambaye hana mtoto, wengi hudhani ukijitumbukiza hapo basi utalea mtoto.

Jamani kuna watu wanauwezo wa kutake care ya watoto wao bila msaada, jiulize kabla yako nani alikuwa anamsaidia kama sie mwenyewe. Ni faraja na upendo tu anahitaji kutoka sehemu nyingne.

Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?

Mwenye mawazo hayo wewe ni katili na mbinafsi kabisa. Na ndo maana inafikia hatua wanaume mnafichwa mnakuja kutambua kwamba ana mtoto imepita hata miaka 10, halafu unalaumu oooh hakuniambia. Hakukuambia kwasababu anajua mtazamo wenu kwao...

Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..

Mimi mwenyewe ni mfano mzuri, nimepata unyanyasaji sana na wanaume, pale nilipokuwa nawaambia nina mtoto, wengine walishia kimya kimya, wakidai eti tuna kawaida ya kupasha kiporo na mzazi mwenza HIYO NI UONGO NA FIKRA MBOVU ZA WATU
Na kamwe sikuweza kuficha kama sina mtoto kwasababu najua nini maana ya mtoto. Mtoto ni zaidi ya thamani ya vitu ulivyonavyo ndani...
Tena wanawake ambao mmekutana na haya wala msifiche ukweli, Mwanaume akikimbia ujue mungu kakuepushia jambo.

WANAUME HEBU TOENI NA MBADILIKE NA HIZO IMANI AMBAZO SIO...

Swali lolote linakaribishwa... Asanteni

ww hata ujitetee vp single mom nenden zenu hatutaki kuoa used sisi.
Labda kwa kugegedwa tu ila kuoa hakuna
 
Unatakiwa kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuishi na single parent. Kulea mtoto wa mwenzako sidhani Kama Ni issue, tatizo Ni bond iliyopo baina ya wazazi hawa. Ni lazima wawasiliane, wasaidiane katika malezi ya mtoto wao na huwezi kuwazuia kufanya hivyo.

Tatizo kubwa ni wivu wa kibinadamu, Kama unampenda mwenzako, then kila siku simu haziishi toka kwa mzazi mwenzake, hakika kidogo kitadunda tu..

Pia wengi wao mapenzi yao yapo kwa watoto zaidi, hawezi kukupa upendo wakati Kuna mtoto ambaye ni kila kitu kwake, hata mkikwaruzana anamchukua mtoto wanaenda kulia wote, kwa kweli Kuna hatari ya kutoonyeshwa upendo wa kutosha.

Swala la pesa sidhani kama ni issue, nadhani single parents waoane wenyewe kwani wanashare interests moja...watoto, hata wakiwa kwenye zile dates za mwanzo ni rahisi kuenjoy vile watakuwa huru kuzungumzia watoto wao..
 
Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?

Hapo kwenye red ndio jibu au tatizo zima lilipo... jamii. Ukiwalaumu wanaume unawaonea, nadhani mind set ianze kubadilika kwa jamii nzima.
Wanaume wengi wanasita kuoa wanawake wenye watoto sio kwa sababu wao wanawaona hawana thamani, bali kwa kuhofia jamii, hasa ndugu, jamaa na marafiki watawachukuliaje. Mimi na wewe ni sehemu ya tatizo. Siku wewe ukiwa free happy kumuona kaka yako ameoa mwanamke mwenye m/watoto, na mimi na mtu mwingine, then hili tatizo litapungua sana...
 
Daah!! Noma sana halafu utakuwa mnyonge sana!! Kuna uzi jamaa alikuwa anaomba ushauri humu, mkewe kawa close sana na mzazi mwenzie na kila akihoji jibu ni nafuata matumizi na kujadili malezi ya mtoto.

!
!
bonge la topic...... nina mtoto na x wangu. Wakati nahaha kumrudisha tulee familia akawa ana hasira zaidi na mimi hivyo akawa anatoka na rafiki yangu wa utotoni ambae alisoma nae na nilishawahi kuwatoa out mara kadhaa kabla hawajaanza kudate. So wakati nahaha kwa simu of coz almost a year kuweka mambo sawa wao wakawa wanafanya yao. Mie nikabonyezwa na mtu kuwa ana mimba ya jamaa nikapewa hadi tarehe tarajiwa, nikampandia hewani nikamchana nikabadili namba ya simu. Yule mchizi akamwaga demu. Baadae nikawa napeleka matunzo kwa mtoto wangu miksa shule kali ya nursery nini pamba na matumizi bwena, akaanza kujirudisha rudisha,nisiendelee sana ila kuingia mahusiano na mtu mwenye mtoto iko complex sana. Umakini unatakiwa kabla kufanya maamuzi.
 
umeona eeh! halaf anasema eti bora tuliozaa tunajijua tuna kizazi sijui kuliko hao ambao hawajazaa. anashangaza! anataka aonekane yeye ni bora zaidi kwa kuponda wengne!! wanaume siku hizi hawakimbii mtoto, ukikimbiwa ni ww mwenyewe kwa kauli chafu chafu kama hizo.

inapendeza taratibu tu mtaanza kuwaelewa wanaume vyema.

mwanaume yeyote kamili kama umezaa bila kujali why hamjaoana na mwanamke husika hawezi kukubali wala kujisikia amani mtoto wake apate tabu yeye akiwa hai atafanya kila awezalo mtoto apate matunzo anayostahili.

nina experience unaweza kukuta wazazi mna beef zenu na mwanamke ni mama minyodo huku akimtumia mtoto kama weapon ya kumpanish mwanaume maana anaamini ukiambiwa mtoto anaumwa tu utakuja mbio kama kifaru au m-pesa faster itahusika.

lakini naomba niwape angalizo wanawake wote msidhani kila mwanamke aliyetelekezwa na mtoto ni kwamba mwanaume hana uwezo wa kutunza au ni mkatili, hapana bali kuna point of no return mwanaume yuko tayari kujiambia kimoyomoyo mtoto atakapopata akili atamtafuta baba yake na hapo sahau kitu kinaitwa mawasiliano tena na mwanaume huyo.

maana ninao ushshidi wanawake huwa hawawapi watoto baba zao hata baada ya umri wa kisheria kufika ili wawatumie watoto kuwatesa baba zao.
 
pole aisee ila jichunguze nawe ukute kuna mahali una tatizo......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom