Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Masanilo,
Ningekujua unaishi wapi basi nisingeumiza kichwa changu.
Lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, mtu mzima hatishwi ny'au, sasa huyo Mwakyembe wenu kama anapika habari ambazo hazipo basi ni mtu wa hatari sana.
Anateka nyara wapiga kura wake huku akiwaomba wamsaidie 2010, nani atampa kura?
Anataka kuharalisha uongo na kuingilia utalaamu wa police, lakini watu wa Kyela sasa watajua uongo wake wa kila siku anaoimba.
Iweje kijana mdogo apenyeze kisu kikubwa kwenye mkutano na asipigwe na wapambe? Unampeleka nyumbani kwako kumdhalilisha kana kwamba yeye ndiye police sasa.
Mwakyembe hana jipya, ameshindwa kuliendeleza jimbo lake na huku anatapatapa tu.

Gwamaka,

Huyo Masanilo asikubabaishe, mimi namfahamu maana nimewahi kuishi naye karibu huko Norway.

Sitaki kusema mengi ya kwake maana asije akaumbuka bure hapa.
 
Gwamaka,

Huyo Masanilo asikubabaishe, mimi namfahamu maana nimewahi kuishi naye karibu huko Norway.

Sitaki kusema mengi ya kwake maana asije akaumbuka bure hapa.

Bapumbile

Nimekuruhusu sema chochote juu yangu, na karibu Kyela ila kesho nitakuwa kijijini Njisi! Nitarudi Kyela Mjini J5 nitalala Pattaya Hotel ama pale jirani Makete half London Guest House.
 
Bapumbile

Nimekuruhusu sema chochote juu yangu, na karibu Kyela ila kesho nitakuwa kijijini Njisi! Niatrudi Kyela Mjini J5 nitalala Pattaya Hotel ama pale jirani Makete half London Guest House.

Wewe sio wa Kyela angalia hata guests unazoongelea, ni zile za miaka ya 90. Siku hizi Kyela ina nyumba za maana hasa.

Vipi mitaa ya Oslo hapo mnaendeleaje? Hilo baridi litakuua mkuu, tuachie Kyela yetu tujidai. heri wengine tuliwahi kurudi nyumbani baada ya shule.
 
Hujui kama za Kale dhahabu! umeshindwa kusema uliyonuia unaleta hadithi za alinacha.....Oslo wee nitafute Njisi kesho ama J5 nitakuwa mjini,

10441430.jpg

Unapajua hapa?
 
Engineer,

Nimefuatilia post zako nyingi humu mara nyingi unaegemea upande mmoja na unaelekeza upinzani/mashambulizi moja kwa moja kwa mtu unayemtuhumu na kuwaaminisha wote watakaosoma waamini unaloliandika kuwa ni sawa.

Unalalamikia magazeti ya IPPmedia siyo kweli, siku ya Ijumaa magazeti yote yaliandika kuhusu hili la Mwakyembe siyo Nipashe pekee! Hizi habari hatujazisoma nipashe.

Engineer, kama unakuja humu JF basi jaribu kuvaa ngozi ya kuhabalisha ukweli usije kishabikishabiki na kuelekeza mashambulizi kwa mtu ambaye haumshabikii. Jiulize wote humu tukiwa kama wewe kwenye hii forum patatosha?

Margreth,

Soma habari hii nyingine hapa chini ya huyo Mwandishi wenu Mwanakatwe, halafu niambie kama huyu ana report habari au anapika habari. Huyo huyo ndiye kaandika habari mbili tunazozijadili katika thread hii.

Na Thobias Mwanakatwe
7th September 2009
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk.Harrison Mwakyembe, amewaweka katika wakati mgumu viongozi wa kijiji cha Kingila na Kapwili, Kata ya Kajunjumele pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kuwatuhumu kuwa walikwamisha jitihada za kushughulikia mgogoro wa mashamba yanadaiwa kuporwa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kambi ya Kyela.

Akizungumza na wananchi wa Kata Kajunjumele mwishoni mwa wiki, alisema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba Hussein Mashimba kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji hivyo, walimgeuka (Mwakyembe) baada ya kuchukua uamuzi wa kuandika barua kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuelezea suala la mashamba hayo.

Alisema Mkuu wa Wilaya na viongozi wa vijiji hivyo, walisema madai hayo hayana msingi bali mbunge anataka kujipatia umaarufu.

Dk. Mwakyembe, alikuwa akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Agrayson Mwakalekela.

Alisema baada ya kuchukua hatua ya kwenda kufuatilia kwa Waziri mwenye dhamana, alishangaa kukuta umeandikwa muhtasari unaoelezea kuwa mbunge ni mzushi na kwamba hakuna mgogoro wowote.

"Kero yenu ya mashamba nilikwenda kuonana na Waziri wa Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa wa wakati huo, Profesa Philemon Sarungi akanieleza mbona Kamati ya Maendeleo ya Kata imeleta muhtasari unaoonyesha kuwa mbunge ni mzushi hakuna mgogoro wowote,'' alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema kutokana maelezo hayo ya Waziri, aliacha kufuatilia suala hilo.

Hata hivyo, mbunge huyo alisema kama wananchi na viongozi wa vijiji hivyo wanataka suala hilo alishughulikie tena, wakae kikao na kuandika muhtasari mwingine wa kukanusha ule wa awali.
Mkuu wa Wilaya Kyela, Abdallah Kihato, aliiambia Nipashe kwa simu kuwa atalifuatilia suala hilo kwa kuwa halifahamu kwa kipindi hicho hakuwepo wilayani humo.

Kwa upande wao, wananchi hao walisikitishwa na hatua ya viongozi wao kukwamisha suala hilo na kuahidi kuwaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi mkuu ujao.
 
Duh! hii vita ya Mwakyembe na mwakalingan bado tu inaendelea!... ama kweli hawa jamaa hawapendani na mwisho wa yote tutasema hawaitendei haki Kyela!
 
Haya mambo ya siasa za Kyela yanakwamisha hata Maendeleo ya wananchi wa Kyela...Ugomvi wa mashamba ya Kajunjumele ndio chanzo cha kuondolewa Ukuu wa wilaya kwa Ndg Mashimba Hussein Mashimba.Mkuu wa Wilaya huyo alitofautiana mawazo na Mbunge wake matokeo yake ikawa ni kutunishiana misuli na kuonyeshana nani zaidi ya mwingine na matokeo yake ni kwamba Mkuu wa Wilaya akaondolewa kazi katika mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya.Wananchi wengi wa Kyela ikiwa ni pamoja na Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo walijaribu kufuatilia bila mafanikio kujua nini chanzo cha Mkuu wa wilaya hiyo kuondolewa..Mkuu wa Mkoa pamoja na baadhi ya watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu pia walishangazwa,kwani Mashimba alikuwa kijana na ni mmoja kati ya Wakuu wa Wilaya wachache waliokuwa makini katika kazi zao...Sio alibadilishwa kituo...Ndg Mashimba aliondolewa kabisa katika orodha ya Wakuu wa Wilaya.

Ndugu zangu wana-kyela tuwe waangalifu hizi siasa za mashambulizi ya watu binafsi hazitotufikisha mbali....Tujiunge katika umoja wetu na tuangalie maendeleo ya Jimbo kwanza.Yule mtu wa Ipinda asiwe na shaka kwenda Itope na yule wa Kajunjumele awe huru kutembelea Ndandalo,hiyo ndiyo Kyela tunayoitaka na tuliyoizoea!
 
Mkuu Mwawado,

Asante kwa ujumbe wako maana hata mimi umenifungua macho kwenye fumbo lililokuwa linanisumbua muda mrefu.

Nilikuwa katika waliomtetea Mashimba muda mfupi baada ya kuondolewa na sababu kubwa ilikuwa kwa muda mfupi nilomfahamu jamaa alikuwa mchapa kazi. Ndio pia alikuwa na udhaifu wake mdodo mdogo lakini huwezi kubeza utendaji wa Mashimba kwa Kyela hasa upande wa maendeleo.

Bahati mbaya Watanzania tunapenda blaah! blaah! na mara nyingi watu kama akina Mashimba tunawaona wabaya kwasababu wanafuatilia kila kitu.

Mwandishi wa hii makala anongelea prof Sarungi na wakati huo huo anamtuhumu Mashimba. Hawa ni viongozi ambao walikuwa madarakani wakati tofauti. Sarungi alikuwa waziri kabla ya 2006 wakati Mashimba alikuwa mkuu wa wilaya kuanzia katikati ya 2006.

Mengine yote uliyoysema ndio ukweli mtupu. Kyela inahitaji umoja na sio haya mambo ya magazetini kila siku na vijembe. Ifike mahali tuwape nafasi wananchi kuhangaika na shida za kila siku badala ya kila siku kujikusanya vijiweni kujadili kijembe gani kimetokea leo.

Mkuu wa Majeshi ni kaka yetu kutoka Kyela; hili tatizo la mashamba lingeweza kushughulikiwa kwa njia bora kabisa badala ya kulaumiana sisi wenyewe kupitia magazetini. Naamini kila jambo lina solution hata kama ni gumu kiasi gani. Jeshi wana haki na hayo mashamba ila pia kunaweza kutumika busara ili kwa wakati huu ambao jeshi hawayatumii kwa mambo ya maana basi wananchi waazimishwe na kulima mazao ya muda mfupi kama mpunga. Kuwaambia wananchi hayo ni mashamba yenu, kayachukueni, haikuwa busara kabisa. Hapo wanamponza hata kaka yetu Mwamunyange maana inaanza kuonekana ni yeye against wana Kyela wenzake wakati sio kweli kabisa.
 
Wewe sio wa Kyela angalia hata guests unazoongelea, ni zile za miaka ya 90. Siku hizi Kyela ina nyumba za maana hasa.

Vipi mitaa ya Oslo hapo mnaendeleaje? Hilo baridi litakuua mkuu, tuachie Kyela yetu tujidai. heri wengine tuliwahi kurudi nyumbani baada ya shule.

Bambumbile,

Mbona nilishaandika hapa? Huyo sio kwa Kyela ila yuko Marekani. Na matatizo ya wivu kama ndugu yake Shalom na ndio maana mimi nawaita
masanilo aka Shalom aka Ze Comedy.

Jamaa kazi yake ni kujifanya anajuana na watu kwenye system wakati hakuna lolote. Ni msanii tu.

Mawivu yamemjaa kuona wenzake wanafanya yale ambayo yeye yamemshinda.

Watu kama hao niachie mimi au hata Sikonge naye anamweza.
 
Engineer

Habari yako bwana, nisaidie nilipo, ni Olso ama US, Texas! Unaninyima hata uraia wa jamhuri ya Kyela!!!....Kesho nitakuwa mjini hapo njoo Makete Half London unaweza pata beer za buree hahahaha!
 
TAHADHARI KWA WANAKYELA!
Umasiki na ujinga ndio mambo amabayo waliobahatika ama kupata elimu au kuwa matajiri wanayatumia kwa manufaa yao kasiasa au kiuchumi.Wanakyela wanaweza kufikiri wanampinga mwakyembe au wanampinga mwakalinga kumbe kuna matajili jambo nyuma yao mwalinga anatumiwa na masadi ili kumdhoofisha na hatimae kumwondoa dr.mwakyembe hili halina ubishi na kama hamuamini wanakyela mtajikuta mnagombanishwa na watu kutoka arusha,kilimanjaro,tabora n.k bila kujua.Kitakacho wauwa ni ushabiki wa kisiasa msikubali,pesa chukueni kaneni maana wanarudisha walichowaibia.Msikubali kudharirishwa kiasi hiki kwamba kati ya watanzania wote wanakyela tu mnaweza kununuliwa kwa gharama ndogo kiasa hiki na kusahau utu wenu.Nawaheshimu sana ila nawaomba msikubali kurubuniwa imepitwa na wakati kwa pamoja tuseme sasa basi imetosha............
Inawezekana msiamini lakini huo ndio ukweli...............
 
TAHADHARI KWA WANAKYELA![/COLOR]

Inawezekana msiamini lakini huo ndio ukweli.

Toa ujinga wako hapa,Huo ushauri wako kawape watu wa kijiji chako ambao hawajuhi nini maana ya demokrasi...Hawa wachunga ngombe naona wameanza kujaa hapa
 
TAHADHARI KWA WANAKYELA!
Umasiki na ujinga ndio mambo amabayo waliobahatika ama kupata elimu au kuwa matajiri wanayatumia kwa manufaa yao kasiasa au kiuchumi.Wanakyela wanaweza kufikiri wanampinga mwakyembe au wanampinga mwakalinga kumbe kuna matajili jambo nyuma yao mwalinga anatumiwa na masadi ili kumdhoofisha na hatimae kumwondoa dr.mwakyembe hili halina ubishi na kama hamuamini wanakyela mtajikuta mnagombanishwa na watu kutoka arusha,kilimanjaro,tabora n.k bila kujua.Kitakacho wauwa ni ushabiki wa kisiasa msikubali,pesa chukueni kaneni maana wanarudisha walichowaibia.Msikubali kudharirishwa kiasi hiki kwamba kati ya watanzania wote wanakyela tu mnaweza kununuliwa kwa gharama ndogo kiasa hiki na kusahau utu wenu.Nawaheshimu sana ila nawaomba msikubali kurubuniwa imepitwa na wakati kwa pamoja tuseme sasa basi imetosha............
Inawezekana msiamini lakini huo ndio ukweli...............

Mkuu Jile,
Fungua macho kijana. Kwa taarifa yako wanaosoma humu JF, nusu yao wako nje ya Tanzania. Katika hiyo nusu iliyobaki 4/5 wako miji mikubwa kama Dar, Arusha, Dodoma, Mwanza na Mbeya. Na hiyo 1/5 ni miji midogomidogo kama Sikonge na Kyela. Sasa uwezekano wa watu wa Kyela kusoma au kusikia haya maneno yako ni mdogo saana.

Lazima nikusifu kwa habari yako nzuri saana na iliyojaa busara za hali ya juu. Nakubaliana na wewe kabisa kuwa MWAKALINGA ANATUMIWA NA MAFISADI. Ila kuna jambo moja sijui kama ulishawahi kulisikia. Wote humu ndani ya JF wanafahamu kuwa "Mamvi alimchoresha mama yako 7". Kwa hiyo Mkuu, Mama yako na Mwakalinga wote mwaajiri wao ni mmoja, huu wivu wa nini? Mama yako apata mgawo wake na Mwakalinga apata mgawo wako. Kama hazitoshi, nenda na wewe ukajiandikishe.

NB: Milele ukumbuke kuwa majina ya miji yanaanza kwa herufi kubwa.
 
TAHADHARI KWA WANAKYELA!
Umasiki na ujinga ndio mambo amabayo waliobahatika ama kupata elimu au kuwa matajiri wanayatumia kwa manufaa yao kasiasa au kiuchumi.Wanakyela wanaweza kufikiri wanampinga mwakyembe au wanampinga mwakalinga kumbe kuna matajili jambo nyuma yao mwalinga anatumiwa na masadi ili kumdhoofisha na hatimae kumwondoa dr.mwakyembe hili halina ubishi na kama hamuamini wanakyela mtajikuta mnagombanishwa na watu kutoka arusha,kilimanjaro,tabora n.k bila kujua.Kitakacho wauwa ni ushabiki wa kisiasa msikubali,pesa chukueni kaneni maana wanarudisha walichowaibia.Msikubali kudharirishwa kiasi hiki kwamba kati ya watanzania wote wanakyela tu mnaweza kununuliwa kwa gharama ndogo kiasa hiki na kusahau utu wenu.Nawaheshimu sana ila nawaomba msikubali kurubuniwa imepitwa na wakati kwa pamoja tuseme sasa basi imetosha............
Inawezekana msiamini lakini huo ndio ukweli...............

Jifunze kuandika kwanza ndio uje hapa
 
Bambumbile,

Mbona nilishaandika hapa? Huyo sio kwa Kyela ila yuko Marekani. Na matatizo ya wivu kama ndugu yake Shalom na ndio maana mimi nawaita
masanilo aka Shalom aka Ze Comedy.

Jamaa kazi yake ni kujifanya anajuana na watu kwenye system wakati hakuna lolote. Ni msanii tu.

Mawivu yamemjaa kuona wenzake wanafanya yale ambayo yeye yamemshinda.
Watu kama hao niachie mimi au hata Sikonge naye anamweza.

Mhandisi,
Na heshima zote lazima nikuambie kuwa Shalom na Masanilo ni watu wawili tofauti. Shalom ni Mnyakyusa na Masanilo ni Msukuma. Mengine yote nawaachieni wenyewe ila nilitaka kukusaidia kwa hilo tu.
 
Sahihisho, mimi ni Msukuma mazee! wanyakyusa ni shemeji zangu

Masa
Kumbe wewe ni shemeji yetu? Please Masa mbona wewe unapendelea shemeji mmoja tu?Mwakalinga naye si shemeji yako.Mbona unamwandama sana ,Mwakalinga naye ana ndugu zake wengi wako Mwanza.
 
Masa
Kumbe wewe ni shemeji yetu? Please Masa mbona wewe unapendelea shemeji mmoja tu?Mwakalinga naye si shemeji yako.Mbona unamwandama sana ,Mwakalinga naye ana ndugu zake wengi wako Mwanza.

Hahaha

Jamani ni mambo ya siasa haya msisabaishe nikose kipenzi changu Sekelaga! hahahaha nimecheka sana mkuu......simwandami wala nini nasikitika hujanisoma ndugu yangu. Mbona GAM yeye amenielewa! Vita imetangazwa Masanilo na Engineer, huyu rafiki yangu mhandisi wa Kyela mimi huwa namwita boga yeye anapenda aendelee kuwa kiazi tu kwa nia nzuri wala si kumtusi hahahaha!
 
engineer wa majungu ya ukweli mkuu,wanakyela wamesha mstukia kuwa ni mamluki katumwa na mafisadi na kapewa minoti kufa mtu.......
Engineer wa majungu!

Kuwa mtu mzima kidogo basi, stop lamenting and crying like a little high school girl.....wengine sisi tunakujua wewe kama ni kishoka tu huna mbele wala nyuma...uko kama saa mbovu, either utakuwa mbele ya muda ama nyuma.
 
jamani bado tu mnae mamluki?? hamumwachii hata kidogo...kazi kweli hapo.
 
Afadhali hata wengine wameanza kuona ukweli:
TAZAMA TANZANIA TOLEO Na. 356 JUMANNE SEPTEMBA 8-15, 2009

DK. MWAKYEMBE AANDAMWA NA MAFISADI
Na mwandishi wetu- KYELA.

Nguvu ya kisiasa ya Mbunge wa Kyela wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. Harrison Mwakyembe ameanza kupungua baada kubainika kuwa tukio la kutaka kumchoma kisu mbunge huyo ni la kupangwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa Dk. Mwakyembe na washirika wake, wameonekana kujiandalia tukio hilo ili ionekane kuwa mbunge huyo anaandamwa na mafisadi hewa;
Baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi, walisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha uwepo wa tukio hilo, isipokuwa limetengenezwa ili kuonyesha umma kuwa mbunge huyo anawindwa na watu anaowaita maadui wake kisiasa.
Awali lilifanyika tukio linalofanana na hilo, lililohusisha na ajali ya gari la mbunge huyo lililodaiwa kugongwa na roli la mizigo, lakini uchunguzi wa polisi ulipofanyika ulibaini kuwa ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa Dk. Mwakyembe.
Tukio hilo la Dk. Mwakyembe kupata ajali lilitafsiriwa kuwa liliandaliwa na kundi aliloliita la maadui zake kutaka kuumaliza kwa lengo la kufifisha juhudi zake za kupambana na ufisadi na mafisadi.
Kuibuka kwa tukio la kutaka kushambuliwa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana ni muendelezo wa mbunge huyo kutaka umaarufu hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchanguzi mkuu mwakani (2010).
Martha Mwakasole (45) mkazi wa kata ya Kajunjumele alidai aamini kama tukio hilo lilitokea kutokana na ukweli kuwa alihudhuria mikutano karibu yote inayofanywa na mbunge huyo katika jimbo hilo, lakini hakusikia wala kuona kufanyika kwa tukio hilo.
Mwana mama huyo alidai uenda vijana hao wanaodaiwa kutaka kumdhuru Dk. Mwakyembe waliandaliwa na wapambe wa mbunge huyo ili kunogesha mambo katika ziara hiyo.
Unajua Dk. Mwakyembe amekuwa akizungumza maneno yale yale ya kila siku ya ufisadi, ufisadi tu, lakini hakuna kipya ambacho anakiibua katika kuleta maendeleo ya jimbo. Kwa hali hii wananchi wengi hawahudhurii mikutano yake, sasa inatengenezwa tukio hilo ili kuamsha ari ya wananchi kumshabikia alidai.
Lucas Mwakatobe ambaye pia ni mkazi wa kata ya Kajunjumele alidai hata kama tukio hilo lilitokea basi hizo ni dalili za wazi kuwa Dk. Mwakyembe ameanza kuchokwa kisiasa. Hakuna anayemwinda Dk. Mwakyembe kwa lipi hasa?
Alidai hatua yake ya kuwaambia wakazi Kyela kukaa mkao wa kuhongwa na mafisadi kumewachukiza wananchi kwani kauli hiyo inaonyesha kuwadhalilisha wao na viongozi wao wa dini.
Kauli hiyo ya Mwakatobe inafuatia maneno ya Dk. Mwakyembe aliyoyatoa katika mkutano hadhara uliofanyika Jumamosi ya Agosti 29 katika daraja la Lufilyo kata ya Lusungo ambapo alidai mafisadi wametenga fedha chafu shilling milioni 400 kuwahonga wananchi ili wamchukie.
Mbunge huyo alidai fedha hizo zimeandaliwa mahususi ili kuwatengeneza watu waliojitokeza katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwakyembe akawataka wakazi wa jimbo lake kutoogopa kuzitwaa fedha hizo ambazo alidai kuwa zimepitishwa kupitia madhehebu ya dini.
Mbunge anapotoa madai mazito kama hayo kwa viongozi wetu wa madhehebu ya dini na kuwatisha watu wengine wasijitokeze kuchuana naye katika ubunge anamanisha nini si kama kuleta mgawanyo miongoni mwa jamii na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi? Alihoji Mwakatobe.
Akaongeza kudai kuwa miundombinu ya jimbo letu imechoka, mbunge wetu ameshindwa kutafuta wafadhili kutusaidia badala yake amekuwa akihubiri wimbo wa ufisadi na mafisadi wasioonekana, wimbo huo utatusaidia nini katika mazingira magumu kama haya?
Tumekuwa tukitembea umbali mrefu kutafuta maji, zahanati hazina dawa, sasa leo mbunge anapokuja na ajenda ya kutukutaza tusichangie maendeleo yetu anataka tumkomoe nani maana hatujawahi mkumuona Mwakyembe akitibiwa katika zahanati hizi za vijijini, mara nyingi yupo Dar es Salaam ambako huko kuna hospitali kubwa kubwa, alidai.
Daminan Mwakibinga mkazi wa Lusungo alidai Dk. Mwakyembe akiulizwa ni fisadi gani ambaye anamjua kwamba baado yumo ndani ya CCM na akitoka huyo basi CCM ndipo itabaki haina fisadi? Mbona hatutajii? Sijui Mwakyembe anaweza kumtaja nani? Lakini kinachoonekana ni namna Fulani ya kampeni za kutaka kutushawishi tumpigie kura za huruma.
Kinachoonekana kwa Dk. Mwakyembe badala ya kuwahubiria watu maandiko ya CCM kwamba rushwa ni adui wa haki, yeye anaifagilia kwa kututaka wananchi tuchangamkie pesa hizo, alidai Mwakibinga.
Akaongeza kudai kuwa mbunge wetu anawataka mafisadi watoke ndani ya CCM, lakini wakati huo huo mpinga rushwa na mchukia hongo ameshikamana na wapiga kura ambao wamelengwa kuhongwa milioni 400, ili kumngoa kwenye ubunge kwa hili tutashindwa kumuelewa.
Naye mmoja wa wachungaji wa kanisa la Pentekoste, ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alimtaka Dk. Mwakyembe kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya madhehebu ya dini.
Mchungaji huyo alisema kuwa ipo sababu ya Dk. Mwakyembe kuthibitisha hizo shilingi 400 na nani na wapi. Akishindwa kuthibitisha madai yake basi tutaamini kuwa hizo ni propaganda za kutaka kujikweza kisiasa na kutuhadaa ihali pesa hizo zimetolewa na wapambe kutoka kwenye kundi lake, alidai mchungaji huyo.
Pia Mchungaji huyo aliwataka wananchi wenye sifa za kutaka kugombea jimboni humo wajitokeze bila kuhofia propaganda za Dk. Mwakyembe kwa sababu ni haki ya kila raia kuchangua na kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Hakuna mwenye hati miliki ya jimbo la Kyela wala hakuna mwenye mamlaka ya kuwazuia wengine wasijitokeze kuwania ubunge kutokana na hira ya choyo, hivyo yeyote mwenye sifa na aje kugombea Kyela bila wasiwasi wowote kwani hili ni jimbo la wote, alibainisha.
Akasema tumechoshwa na ngonjera na mashaihiri ya kupambana na ufisadi barabarani, kama wanaona wana ushahidi na wale wanaowatuhumu kuwa ni mafisadi milango ipo wazi kwenda mahakamani au kupeleka suala hilo kwenye vyombo vya dola. Hatuwezi kukubali kuona katiba ikipindishwa na wachache kwa kuwazuia wengine wasiwanie uongozi, kwa madai kwamba wakithubutu kuwania madaraka basi ionekane wametumwa na mafisadi.
Naye Christina Masangula (89) alihoji kwa nini CCM hivi sasa vikao vyake vingi vya ngazi ya juu vinapofanyika maamuzi mengi yayotolewa na kwa kipindi cha muda mfupi yanakuwa yameisha samba mitaani tofauti na miaka ya nyuma hali inayotia mashaka uadilifu wa viongozi wa chama hicho.
Haiwezekani kikao cha kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM kinaazimia mambo ya msingi kwa chama hicho lakini cha ajabu na chakushangaza utakuta kwa kipindi kifupi maneno hayo yameenea kwenye vilabu vya pombe. Hali hii inawafanya wananchi kutafsiri kuwa CCM imekuwa sasa kama sawa vyama vya upinzani, mbona enzi za mwalimu Nyerere mambo hayo hayakuwepo? Masangula alihoji huku akionekana mwenye kukereka.

Back
Top Bottom