Siasa za Mbeya 2005-2010

Mwingine ajimwaga kuwania Kyela.

Na Israel Mwaisaka,Kyela Mbeya
MFANYABIASHARA maarufu hapa nchini Bw,Elias Mwanjala ametangaza rasmi nia yake ya kutaka kugombea nafasi ya kiti cha ubunge katika jimbo la Kyela na kutaka kupambana na mbunge wa sasa Dkt,Harrison Mwakyembe katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu

Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya Kyela ameitangaza azma yake hiyo mbele ya mkutano mkubwa wa wananchi wanaotoka katika kata mbalimbali za wilaya Kyela wakiwemo na waandishi na wa habari kwenye ukumbi wa hotel ya Kyela resort

Akizungumza kwenye mkutano huo alisema kuwa yeye kama mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatangaza rasmi kugombea nafasi ya ubu nge na ana imani kubwa ya kumkabili Dkt,Mwakyembe na kumwangusha kwa kishindo kutokana na mapungufu kadhaa aliyoyaonyesha Dkt,Mwakyembe katika kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano

Alisema kuwa kuna mambo mengi yaliyomsukuma yeye binafsi kutaka kuwania nafasi hiyo na kubwa ni kutaka kuyaua makundi ambayo ambayo yamejengeka ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuhatarisha uvunjifu wa amani miongoni mwa wana Kyela kiasi kwamba hivi sasa hakuna umoja na kuaminiana kumepotea na kufanya maendeleo ya wilaya kusimama

Alifafanua kuwa yeye katika uchaguzi uliuopita alikuwa ni meneja kampeni wa Dkt,Mwakyembe hadi akashinda na kuchukua jimbola Kyela na alifanya hivyo akiwa na imani kuwa Dkt,Mwakyembe angeweza kuwaondolea kero ambazo zimewakabiri watu wa Kyela kwa muda mrefu lakini kinyume chake Dkt,Mwakyembe amekuwa kinara wa kusababisha makundi na kutengeneza chuki miongoni mwa wakazi wa Kyela

Alidai kuwa toka mbunge huyo achaguliwe wilaya Kyela imekuwa katika historia mbaya sana hususani ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kumekuwepo na malumbano yasiyokwisha na kutupiana vijembe vya hapa na pale na kupenda kuitukana serikali hata pasipo na msingi na watu kuishangaa wilaya Kyela kana kwamba wanaishi watu wa aja bu

Bw,Mwanjala alidai kuwa kwa kuwa sasa si wakati wa kampeni si vizuri kuelezea mabaya ya Dkt,Mwakyembe bali watu wajue kuwa yeye ataingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge wakati ukifika kwani kutangaza nia ya kugombea si kosa ila kupiga kampeni na wakati ukifika wa kampeni wataelezana ukweli.

Pia katika mkutano huo Bw,Mwanjala aliitaja mikakati mbalimbali kama vipaumbele atakavyoanza navyo atakapopata ubunge na pia aliitumia nafasi hiyo kujibu maswali mbalimbali aliyokuwa ameulizwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
 
Kwani umelazimishwa kusoma kuhusu mambo ya Kyela?

Buchanan,
Achana na mbabaishaji huyo Masanilo, anafikiri atatengeneza CV yake kwa kumshambulia mtanzania hapa JF.

Hao ndio wasomi wetu walio bobea wanaofikiri personal attacks zitasaidia kuliokoa taifa letu.
 
Alifafanua kuwa yeye katika uchaguzi uliuopita alikuwa ni meneja kampeni wa Dkt,Mwakyembe hadi akashinda na kuchukua jimbola Kyela na alifanya hivyo akiwa na imani kuwa Dkt,Mwakyembe angeweza kuwaondolea kero ambazo zimewakabiri watu wa Kyela kwa muda mrefu lakini kinyume chake Dkt,Mwakyembe amekuwa kinara wa kusababisha makundi na kutengeneza chuki miongoni mwa wakazi wa Kyela

Ni haki yako ya kikatiba Bwana Mwanjala, kama ilivyo kwa wengine wanaotaka kugombea hapo Kyela ama majimbo mengine. Manake jimbo halina hati miliki ya mtu. Lakini hofu yangu ni kuwa nawe waweza ambiwa umetumwa na mafisadi, jamaa hawapambani kwa hoja bali wanatumia ufsadi ili waonekane wapambanaji na pia kupata huruma.
 
Have a nice weekend Wakuu

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=TjiOCLol0qY[/ame]
 
Buchanan,
Achana na mbabaishaji huyo Masanilo, anafikiri atatengeneza CV yake kwa kumshambulia mtanzania hapa JF.

Hao ndio wasomi wetu walio bobea wanaofikiri personal attacks zitasaidia kuliokoa taifa letu.

Kama Mwakalinga anavyotengeneza CV yake kwa kupost upupu wa Kyela
 
Kama Mwakalinga anavyotengeneza CV yake kwa kupost upupu wa Kyela

Masanilo,

Kama ya Kyela ni upupu basi tuletee ya Scotland, ya Edinburgh.

Naona posts zako nyingi hapa JF ni kumtukana Mwakalinga; ni kama kelele za chura tu ambazo hazimzuii ng'ombe kunywa maji.
 
Mtanzania tumekuchoka bwana huwezi post kitu kingine huko kwenu?

Buchanan,
Achana na mbabaishaji huyo Masanilo, anafikiri atatengeneza CV yake kwa kumshambulia mtanzania hapa JF.

Hao ndio wasomi wetu walio bobea wanaofikiri personal attacks zitasaidia kuliokoa taifa letu.

Kama Mwakalinga anavyotengeneza CV yake kwa kupost upupu wa Kyela

Masanilo,

Kama ya Kyela ni upupu basi tuletee ya Scotland, ya Edinburgh.

Naona posts zako nyingi hapa JF ni kumtukana Mwakalinga; ni kama kelele za chura tu ambazo hazimzuii ng'ombe kunywa maji.

Nyie ndugu zangu, acheni huu UGOMVI.

Kama mngelielewana, nina imani kuwa Watanzania kadhaa wangelifadi na mawazo/michango yenu. Ngoja nisubiri uchaguzi uishe labda na ugomvi utaisha. All in all, MNANIANGUSHA ndugu yenu.
 
mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wanajitegemea kimawazo hivyo c kwamba jk hapendi kuenda hapana anaogopa kuulizwa, unajua ni rahisi kuwambia wajinga kuwa maisha bora kwa kila mtanzania na wakakupigia makofi mengi tu,,,,Lakini waelevu ukiwambia hivyo watakuhoji yata kujaje? so mbeya si mahali pa kwenda tu bila mpango ujiandae vizuri tena vizuri
 
Back
Top Bottom