Mto Songwe unatajwa katika kuweza kuinua kipato cha wakaazi wa Jimbo la Songwe iwapo mto huo utatumika katika kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo mto huo ambao unamwaga maji yake katika Ziwa Rukwa una umuhimu kwa nchi mbili, Tanzania na Malawi. Kwani unamwaga maji yake ndani ya Ziwa Malawi/Nyasa vilevile.
Kabla ya kuendelea kujadili hili kuna memba yoyote mwenye ufahamu wa mto huu, unaanzia wapi?
Iwapo una manufaa kwa nchi mbili, je kuna mpango wowote wa kuwa na kamisheni ya pamoja kati ya Tz na Malawi ili kuona kuwa mto huo unatumika kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili pasipo kuwepo na ugomvi?
Kibunango,
Hiyo makala imenifungua kichwa. Mimi nilikuwa najua mto Songwe unaanzia huko mlimani na kuishia lake Nyasa, kumbe upande mwingine unaishia lake Rukwa?
Hapo imenichanganya zaidi, naomba wenye ujuzi na hayo maeneo tuelemisheni. Je mto Songwe unaanzia wapi na kuishia wapi?
Kule Malawi wakati wa Banda kulikuwa na kilimo cha kumwagilia maji, sisi Watanzania mpakani tukashindwa hata kuiga na badala yake tulikuwa tunaenda kule kuhemea chakula.
Inasikitisha kwamba huwa hatujifunzi kutokana na mafanikio ya mtu mwingine labda ndio maana tunaweka fitina badala ya kujifunza ili nasi tufanye yaliyo bora zaidi.