Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

5451_102491053097392_100000094936155_71976_3605114_n.jpg
 
Siku Mwakyembe alipoomba radhi baada kuonekana malalamiko yake dhidi ya mkuu wa mkoa yalikuwa ya uongo.

Mwakyembe amuomba radhi Mwakipesile

2007-06-05
Na MwThobias Mwanakatwe, PST Mbeya

Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, amemuomba radhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw.John Mwakipesile, kufuatia kuwepo na mgogoro wa kisiasa baina yao.

Dk. Mwakyembe, alimuomba radhi Mkuu huyo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kyela.

Mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja uliibuka wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, ambapo Dk. Mwakyembe na Mwakipesile walikuwa wakigombea Ubunge wa Jimbo la Kyela mwaka 2005.

Katika kinyang'anyiro hicho, kilichokuwa na ushindani mkali, Mwakipesile ambaye awali alikuwa mbunge wa jimbo hilo, alibwagwa na Dk. Mwakyembe katika kura za maoni na hatimaye kushinda ubunge.

Mgogoro huo umemalizika wiki iliyopita katika kikao cha Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo na tume iliyoundwa na Makao Makuu ya CCM, kuchunguza tuhuma zinazodaiwa kutolewa na Dk.Mwakyembe dhidi ya Bw. Mwakipesile na baadhi ya viongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Kyela.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kikao hicho kilifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo, chini ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bw.Abrahaman Kinana.

Zilisema kuwa Dk. Mwakyembe aliiomba kamati ya siasa kumaliza tofauti zake na Mkuu wa Mkoa, baada ya tume iliyoundwa na CCM Makao Makuu kubaini tuhuma alizozitoa dhidi ya Mkuu wa Mkoa kuwa siyo za kweli.

Akizungumza jana na gazeti hili kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kyela, Bw. Glasswel Mwakalukwa, alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho, kilichohudhuriwa na wajumbe wanane wa kamati ya siasa ya wilaya na wajumbe wanne wa tume, iliyokuwa ikichunguza madai hayo.

Alipohojiwa na PST kuhusu suala hilo, Mkuu wa Mkoa alithibitisha kuitwa katika kikao hicho cha ghafla cha usuluhishi na kukiri kumalizika kwa tofauti za kisiasa zilizokuwapo baina yake na Mbunge wa Kyela.

Juhudi za kumpata Dk. Mwakyembe kuzungumzia suala hilo, ziligonga mwamba.
 
Siku Mwakyembe alipoomba radhi baada kuonekana malalamiko yake dhidi ya mkuu wa mkoa yalikuwa ya uongo.

Bambubile

Habari hii ni ya zamani(mwaka 2007) sana na haina ukweli wowote na ilikanushwa vikali na Mbunge Mwakyembe!

Kuhusu Kyela;Bambubile tuletee habari mpya motomoto sio hizi ambazo hadi Mzee Glasswell Mwakalukwa akiwa bado yupo kundini;Mwakalukwa aliangushwa na Mzee Mwakasumi ktk uchaguzi mgumu uliojaa kila aina ya hila za rushwa, na hivi sasa yupo kijijini kwake Kafundo akilima!

Naama tunataka tuzipate habari za Kyela,lkn sio kama hizi za kale.
 
Malafyale,

Nilitaka tu kuonyesha kwamba kuna mtu alimuomba msamaha mwingine kwa uzushi.

Bahati nzuri nilikuwa mjumbe kwenye hicho kikao na mheshimiwa aliomba msamaha. Hilo la kwamba alikanusha labda ni kwa nyie wapambe.

Kuna sehemu leo nimesikia mheshimiwa anakanusha kwamba jaribio la kutaka kumwua halikuwepo. Labda kama nimesikia vibaya, kuna waandishi walikuwa wanamhoji, huenda magazeti ya kesho yakaandika. Sitashangaa akiwaruka wale vijana wake, labda yeye anajua upelelezi wamegundua nini.
 
Bambumbile

Pamoja na habari zzko nzuri unazotupa kuhusu Kyela hasa sakata hili la kijana wetu Dan Mwakalinga,lkn bado hamjatueleza lolote kinagaubaga ni vipi Mwakyembe kama Mbunge anahusika na huo utekaji nyara!Tafadhali tupeni ushahidi timilifu iweje Mwakyembe ahusishwe na kitu ambacho yeye binafsi hajafanya!

Maelezo yako na mwenzetu Engineer kuhusu sakata hili iwe kwa faida ya wana JF,mtueleze hasa ni nini kinamuunganisha Mwakyembe na jambo hili hata kufikia kuwa eti nafasi yake ya kushinda ubunge mwakani sasa ni finyu?

Anyways,leo nipo kijijini kwetu Ilopa,na week hii nitakuja Kyela mjini hasa pale ninapofikia Baling'onye;njoo pale Bambubile tuje badilishana mawazo hasa kuhusu mustakabali wa Wilaya yetu nzuri-Kyela!
 
Malafyale
Uko Ilopa wanasemaje kuhusu huo mpambano wa 2010.Baado Dr. anauzika?Vipi Kijana Mwakalinga uko kwenu Ilopa watu wanasemaje.Tukatie news za uko
 
Bambumbile

Pamoja na habari zzko nzuri unazotupa kuhusu Kyela hasa sakata hili la kijana wetu Dan Mwakalinga,lkn bado hamjatueleza lolote kinagaubaga ni vipi Mwakyembe kama Mbunge anahusika na huo utekaji nyara!Tafadhali tupeni ushahidi timilifu iweje Mwakyembe ahusishwe na kitu ambacho yeye binafsi hajafanya!

Maelezo yako na mwenzetu Engineer kuhusu sakata hili iwe kwa faida ya wana JF,mtueleze hasa ni nini kinamuunganisha Mwakyembe na jambo hili hata kufikia kuwa eti nafasi yake ya kushinda ubunge mwakani sasa ni finyu?

Anyways,leo nipo kijijini kwetu Ilopa,na week hii nitakuja Kyela mjini hasa pale ninapofikia Baling'onye;njoo pale Bambubile tuje badilishana mawazo hasa kuhusu mustakabali wa Wilaya yetu nzuri-Kyela!

Malafyale,

Unataka ushahidi gani zaidi ya uliopo?

1. Wapambe wake kumteka huyo kijana
2. Tendo kufanyika kwenye mkutano wake
3. Kwenda kufungiwa nyumbani kwa mbunge Ikolo
4. Mbunge mwenyewe kugeuka polisi kumhoji huyo kijana
5. Gari lake kutumika kumsafirisha huyo kijana kote huko walikomficha
6. Maelezo yake ya mwanzo polisi.

Ila sasa nasikia amegeuka na anasema hakuona na wala hilo tendo la kutaka kumwua yeye halikuwepo. Ni hatua nzuri kama ameona ukweli na kuamua kusema ukweli. Ila hao vijana kazi ndio imegeuka kwao.

Malafyale,

Hivi ungelikuwa mbunge kweli ungelikuwa unawatumia akina Kinanasi, Mwamlinge na Kilumbu? Sijui hata kwanini Dr. anawatumia watu kama hao kama wasaidizi wake kwa pale Kyela. Kwanini asiajiri kijana wa maana na mwenye uelewo badala ya waganga njaa?

Kwasasa sipo Kyela, ila tunaomba michapo ya huko vijijini. Waambieni watu wafanye kazi na waache hayo malumbano ya siasa. Mwakalinga anakula kuku zake Europe, Dr Mwakyembe anafaidi matunda ya ubunge Dar. Wanaoumia kwa kuendeleza siasa ni wao wenyewe.

Ningependa utujulisha ukikutana na Engineer.
 
Nimetimiza ahadi yangu ya jana, kazi kwenu wapambe wa Dr. Mwakyembe

UVCCM KYELA YATOA TAMKO JUU YA DKT MWAKYEMBE

Na Israel Mwaisaka,Kyela, Mbeya

UMOJA wa vijana (UVCCM) wilayani Kyela mkoani Mbeya umetoa tamko kali la kukitaka Chama Cha Mapinduzi wilayani Kyela kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge wa jimbo hilo Dkt,Harrison Mwakyembe dhidi ya uvumi aliouvumisha kuwa alitaka kuchomwa kisu kwenye mkutano wa hadhara kitu ambacho si cha kweli

Akizungumza jana mara baada ya kutoka kwenye kikao cha kamati ya utekelezaji ya wilaya ya vijana mwenyekiti UVCCM wilayani kyela Dkt,Hunter Mwakifuna alisema kuwa katika kikao chao hicho licha ya kuwa na ajenda nyingine pia walizungumzia suala la mbunge wao kutaka kuvamiwa na kubaini kuwa halikuwa ni jambo la kweli kitu ambacho waliamua kutoa tamko la kulaani na suala hilo kulipeleka kwenye baraza la vijana la wilaya

Alisema katika kikao chao cha kamati ya utekelezaji kilichoketi tarehe 8 mwezi huu walimtaka katibu wa vijana Bw,George Silindu aliyekuwa katika msafara na mbunge huyo kudhibitisha kama hilo lilitokea na ndipo katibu alipokataa kata kata kuwa kitu hicho hakikuwepo nay eye alishangazwa kuona jambo hilo likitangazwa kwenye vyombo vya habari kitu ambacho hata yeye kilimshitua na kubaki na bumbuwazi

Mwenyekiti huyo wa wilaya alidai kuwa wao kama vijana wakiwa kama ndiyo walinzi wa chama na viongozi wao waliamua kulifanyia uchunguzi wa kina suala hilo kwa lengo la kutaka kujiridhisha na ndipo walipobaini kuwa kitendo hicho hakikuwepo na kilikuwa na nia tu ya kutaka kujiongezea umaarufu wa kutaka jamii ione kana kwamba mbunge huyo anaandamwa kitu ambacho si cha kweli

Alifafanua kuwa kufuatia hari hiyo wao kama vijana na walinzi wa chama wameona kuwa suala hilo hawawezi wakalikalia kimya kwani athari yake ni kubwa kwani jambo kama hilo linaweza kuleta machafuko na kugawa wananchi wa Kyela katika makundi ambayo tukifikia hatua hiyo ni vigumu Kyela kupata maendeleo halisi

Dkt,Mwakifuna alidai kuwa kwa kuwa suala hilo ni la hatari wao watalisimamia ipasavyo kama chama hakitachukua hatua madhubuti dhidi ya mbunge huyo wao hawatakuwa tayari kufanya naye kazi kwani hari hiyo ikiachwa hivi kiholela hata ilani ya Chama Cha Mapinduzi itakua ngumu kutekelezeka na kukifanya chama hicho kuwa katika mazingira magumu katika chaguzi zijazo

Alidai kuwa wilaya kyela kwa sasa haitawaliki kutokana na siasa mbaya za uchochezi zinazotokana na mbunge huyo wakati wilaya kyela ina matatizo makubwa katika nyanja mbalimbali kama vile maji,Elimu,Afya,Miundo mbinu na mengine mengi sasa malumbano hayo yakiachwa yaendelee wakazi wa Kyela ndiyo watakaozidi kuumia huku jamii nyingine ikikaa na kuamini kuwa wilaya Kyela ina mbunge mahiri wakati wilaya yake inadoda

Alifafanua kuwa toka uvumi huo utangazwe na kijana Danny Mwakalinga aliyedaiwa kutaka kumchoma kisu Dkt,Mwakyembe kuwekwa mahabusu na kupata hadha ambayo akuitarajia wananchi wa Kyela sasa wapo katika makundi makundi ambayo yamewatenganisha katika umoja wao na kuacha kufanya shughuri nyinginezo za maendeleo

Kana kwamba hiyo aitoshi uongozi wa CCM kata ya ngusa wilayani Kyela ambako Mwakyembe alidai kuwa alitaka kuchomwa kisu wameandika mtasari wa kikao cha kamati ya siasa kilichokaa cha kueleza masikitiko yao ya taarifa iliyotolewa ya kuwa mbunge wao alitaka kuchomwa kisu na kuipeleka kwenye ofisi ya chama ya wilaya

Kwenye muhtasari huo uliosainiwa na katibu kata wa kata hiyo Bw,Karume Mwakipesile na ambao majira imefanikiwa kupata nakala yake imeelezea kukerwa na uzushi huo kwani kata yao inakaliwa na watu wasitaarabu na kwa hilo tu pekee chama katika ngazi hiyo ya wilaya kimechafuliwa na kudhalilishwa kitu ambacho hata akikutokea

Katika muhtasari huo wamekitaka chama wilaya kielewe hari hiyo na kama kuna lolote chama ngazi ya wilaya kitajua nini cha kufanya lakini walichokifanya wao ngazi ya kata ni kutaka kukielezea chama ngazi ya wilaya kuwa jambo hilo halikufanyika kwenye kata yao na hawajui nini malengo ya uzushi huo

Pia majira ilifika eneo la tukio katika kijiji cha Tenende ambapo Dkt,Mwakyembe alidai kutaka kuchomwa kisu watu waliokuwepo kwenye mkutano huo walikataa kata kata kuwa katika eneo hilo la mkutano hakukutokea vurugu wala vurumai za aina yoyote ile

Mmoja wa wananchi waliokuwepo eneo hilo Bw,Nice Mwakibinga alisema kuwa mpaka mkutano wao ulipofungwa kulikuwa hakuna vurugu za namna yoyote ile bali kulikuwa na shamrashamra tu za vigelegele na ngoma tu.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw,Maclaud Mwambelo na afisa mtendaji wa kijiji Bw,Hollodin Mwakajila walidai kuwa wao kama walinzi wa amani wa kijiji hicho wamefadhaishwa mno na taarifa hizo kwani kulikua na ulinzi wa kutosha kiasi kwamba ilikua ni vigumu kwa mtu mwenye nia mbaya kuweza kutimiza hazima yake hiyo

Walisema kuwa hadi mkutano huo unamalizika serikali ilikuwepo na kama kuna kijana aliyekamatwa basi walimkuta njiani tu na kwa taratibu ilibidi wamkabidhi kwanza kwenye ofisi ya kijiji lakini kitendo cha wao kumchukua kijana huyo na kwenda naye nyumbani kwa mbunge na kukaa naye masaa kadhaa na kasha kumpeleka polisi kunawapa maswali mengi yasiyokuwa na majibu

Ndugu wa kijana aliyetuhumiwa kutaka kumchoma kisu mbunge Bw,Danny Mwakalinga wamefungua jalada polisi na kupewa RB No,KYL/RB/3241/09 faili No,KYL/IR/2350/09 ambalo bado wanasubiri uchunguzi wa jeshi la polisi ili waweze kwenda mahakamani .

Juhudi za kupata Dkt,Mwakyembe kwa njia ya simu ambaye yupo jijini Dar es salaamu ili aweze kuzungumzia sakata hilo ziligonga ukuta baada ya simu yake kuita bila ya kupokelewa.
 
Pole Dr. Mwkyembe, kama habari hii ni kweli basi we huwafai wananchi kabisa. Msomi mzima unafanya kampeni za kitoto, hatari na uonevu mkubwa. No way, you must pay for it.
 
Nimetimiza ahadi yangu ya jana, kazi kwenu wapambe wa Dr. Mwakyembe

Tunashukuru sana kwa habari hii nzuri na ya kufundisha Mkuu Engineer,na inatupa picha halisi sisi wana Kyela nini kilitokea ktk Mkutano huo!

Lkn kwenye habari hii kuna sehemu yeyote inayoeleza kuhusika kwa Dr Mwakyembe moja kw amoja na ujasusi huu?

Tupe zaidi maelezo kama yapo,yanayomsukuma Dr Mwakyembe kwenye sakata hili kama mtuhumiwa namba moja!
 
Mbona iko wazi sana kwamba Dr. Mwakyembe alihusika? Labda hutaki kuelewa tu.

Alishapiga hata simu kwa IGP kulalamikia kwanini kijana Daniel kaachiwa wakati alitaka kumuua.

Kwa mtu anayemfahamu Dr. Mwakyembe kwa karibu hawezi kushangaa hili. Dr. pamoja na uwezo wake mkubwa pia ana matatizo makubwa sana kwenye baadhi ya maamuzi yake.

Hizo ndio siasa za Kyela; muda wote amekuwa akimlundikia kila aina ya upuzi mkuu wa mkoa. Sasa kahamishia uongo huo huo kwa Mwakalinga. Kitu ambacho ameshindwa kuelewa ni kwamba watu walimchoka Mwakipesile na hivyo uongo wowote wanauchukulia kama ukweli. Mwakalinga hajawafanyia Kyela ubaya wowote, sana sana ana mazuri mengi tu ambayo watu wengi wanamshukuru. Kumuundia scandals Mwakalinga ni lazima ziwe credible vinginevyo ataishia kujichafua mwenyewe.

Huyo kijana asingelikuwa na ndugu wenye uwezo huenda mpaka leo angekuwa bado yuko ndani.
 
Last edited:

Duu
Mbunge wa taifa kumbe Jasusi basi taifa hilo choka mbaya ,kama jasusi ndiye anaonekana mwandilifu, sipati picha.
 
tuliisha sema huyo bwana katumwa na mafisadi kumuangamiza mwakyembe......kazi iko kwa wana kyela wenyewe,kukubali kurubuniwa kwa vijisenti au kusema hapana imetosha na kujifunza kusema no kwa mafisadi
''usawa haupatutikani kwa mzani kuwa sawa......ila inategemea na mpimaji mwenyewe''
 
Mheshimiwa Mwawado,

Baada ya ujumbe huu nitaacha kutumia lugha mbaya maana wewe ni katika waungwana na wenye busara kwenye ukumbi huu.

Mtu ukiambiwa uache na wahuni wenzako unaweza kudharau lakini wazee wa maana kama wewe wakisema ni kweli inabidi niache.

Kuhusu somo, hapa tunaelemisha sana watu. Tuna uhakika mwana Kyela wa 2010 atafanya uchaguzi wa maana.

Pia tunasubiri Kyela FM radio ianze, nasikia mwezi kesho ili tuwaelemisha wananchi ipasavyo.

Tatizo ninaloliona ni vurugu kutokea. Kuna watu wa upande mmoja wako tayari hata kutumia mapanga ili kubaki madarakani.

Mwakalinga ni muungwana kama wewe tu. Hata vijana hapa juzi tulitaka kuwashughulikia hawa akina Kilumbu na Kinanasi ambao ndio mwanzo wa hili jungu lakini Mwakalinga akatuonya na kutuomba tusiwaguse wala kuwatukana. Badala yake alitushauri mkondo wa sheria utafanya kazi yake na kwamba yeye atasimamia kuhakikisha haki ya kijana Dan hainyang'anywi. Vijana hawakufurahi lakini tunamheshimu ila itafika siku hata yeye hatutamsikiliza kama wataendeleza hizi siasa zao za chuki.

Baada ya hii vurugu hata CCM wilaya wameamua kuingilia kati na wanaita kikao ili Dr. Mwakyembe athibitishe nani katoa hizo milioni 400 na kampa nani? Hii ya kutunga mauaji kwa kisu imewaamsha wana Kyela wengi kujua ukweli juu ya uropokaji wa mbunge wao.

- Ninaomba kumkumbusha Mkulu Mwakalinga, kwamba wakati ni huu akajitokeza mapema na kuwakataa wapambe wa namna hii, yaani kweli atapata ubunge wa Kyela na this kind of advisers? are you kidding me or what?

- Mwakalinga huyu mtu anakuongezea maadui wabure tu humu ndani, nenda uka-concetrate na jimbo, give JF a break mkuu watu washau kidogo kwanza! ni ushauri wa bure tu!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu FMES,

Wewe una uzoefu na JF, kweli kuna mtu hapa ana uwezo wa kumkataza mtu mwingine kuandika atakacho?

Kumbuka yale majadiliano juu ya Masha. Kuna watu wengi waliambiwa wanazidi kumharibia rafiki yao, je waliacha kuandika?

Naamini huyo Mwakalinga mwenyewe hamfahamu Engineer kwa sura na hata akimwambia aache sidhani kama atafuata.

Mimi mwenyewe nimewahi kumkataza engineer hapa na kuna siku anapunguza na siku anaongeza. Naamini hata Mwakalinga kesha fanya hivyo.

Uzuri tu siasa za Kyela zitapiganiwa Kyela; kinachofanyika hapa ni watu kujifurahisha. Zaidi ya 99% ya wapiga kura wa Kyela hawajawahi hata kugusa kompyuta.

Magazeti yenyewe yanafika siku ya pili na yanasomwa na wajanja wa pale mjini tu.

Wananchi wa Kyela hawataamua wamtakaye kwa kufuata propaganda za JF au magazeti ya watu wa Dar. Wataangalia nani anaweza kuwasaidia zaidi katika matatizo yao ya kila siku kama elimu, afya, maji, barabara, kilimo nk.

Vinginevyo wengine tunasoma hapa kwasababu baadhi ya hoja na propaganda zinazotolewa hapa ndio hizo hizo zitakazokuwa zinatolewa kule Kyela hapa mwakani.
 
- Ninaomba kumkumbusha Mkulu Mwakalinga, kwamba wakati ni huu akajitokeza mapema na kuwakataa wapambe wa namna hii, yaani kweli atapata ubunge wa Kyela na this kind of advisers? are you kidding me or what?

- Mwakalinga huyu mtu anakuongezea maadui wabure tu humu ndani, nenda uka-concetrate na jimbo, give JF a break mkuu watu washau kidogo kwanza! ni ushauri wa bure tu!

Respect.

FMEs!

Nyani haoni kundule, wewe umekatazwa mara ngapi hapa kwamba unaharibia unaowatetea na bado hukuacha.

Mimi ni mtu huru na kwa huku vijijini nina uwezo wangu. Siwezi kununuliwa au kuamrishwa na mtu.

Wewe unayemtaja Mwakalinga kwenye kila maandishi yako kuhusu mimi ndio unamharibia Mwakalinga. Huenda wakati umefika Mwakalinga ambaye ulishasema ni rafiki yako akakuambia wacha hiyo mizee!

Kwa Kyela hata asipokuwepo Mwakalinga mimi nitamuunga mtu mwingi dhidi ya huyu msanii wenu ambaye anaiba hata michango ya maskini huku anajifanya mpmbanaji wa ufisadi.

Wewe endelea na Ze Comdy yako kule kwenye kamati kuu. Tuna akina Hussein Yahaya wengi sana TZ.
 
Mkuu FMES,

1. Wewe una uzoefu na JF, kweli kuna mtu hapa ana uwezo wa kumkataza mtu mwingine kuandika atakacho?

2. Mimi mwenyewe nimewahi kumkataza engineer hapa na kuna siku anapunguza na siku anaongeza. Naamini hata Mwakalinga kesha fanya hivyo.

QUOTE]

- Mkuu Mtanzania, heshima yako mkuu siwezi hata siku moja kumkataza member yoyote wa JF kuandika anachotaka, nilichosema na ninachokisema ni kwamba mkataze kujihusisha na jina la Mwakalinga au kampeni za Mwakalinga na mfano nitauweka hapa chini,

- Ya kuhusu Masha, ni kwamba ni rafiki yangu wa karibu sana tena sana, tena ni majuzi tu nilimuangushia hafla nzito sana mdogo wake ambaye ni ofisa wa juu sana huko JWTZ, ambaye tulikua hatujaonana for the last six years, tofauti ya Mwakalinga na Masha ni moja kwamba Masha ni mbunge na waziri tayari, kwa hiyo kumlinganisha na Mwakalinga kama ninavyoona hapa na ile thread nyingine kule, politically ni suicide,

- Huwa ni tabia yangu kusimamia ninachokijua, ndio maana huwa ninatetea background ya Masha ninayoijua sana, infact nimekwua offered hela nyingi sana kusema mengi zaidi ninayoyajua lakini nimekataa, Mwakalinga alipokuwa Kyela niemsimamia sana hapa pamoja na kuambiwa sana kwamba ninamharibia, na aliporudi alinipa ahsante nzito sikusikia akilalamiaka kuwa nilikuwa ninamharibia, kwa hiyo hii hoja ya Masha kama mlivyoileta kati yako na Engineer ni batili mkuu!

Lakini uamuzi wa kusuka au kunyoa ni wenu mkuu, sio wangu, wangu ulikuwa ni ushauri wa bure tu!

Respect.

FMEs!
 
1. Tatizo ninaloliona ni vurugu kutokea. Kuna watu wa upande mmoja wako tayari hata kutumia mapanga ili kubaki madarakani.

2. Mwakalinga ni muungwana kama wewe tu. Hata vijana hapa juzi tulitaka kuwashughulikia hawa akina Kilumbu na Kinanasi ambao ndio mwanzo wa hili jungu lakini Mwakalinga akatuonya na kutuomba tusiwaguse wala kuwatukana.

3. Badala yake alitushauri mkondo wa sheria utafanya kazi yake na kwamba yeye atasimamia kuhakikisha haki ya kijana Dan hainyang'anywi. Vijana hawakufurahi lakini tunamheshimu

.

- Mkuu Mtanzania, ninaongelea maneno kama haya, ya Engineer kujiunganisha na Mwakalinga, ndio maana ninasema hivi ni vyema Mwakalinga akaiokoa kampeni yake mapema kwa kum-denounce huyu Great Thinker Engineer kwamba hahusiki naye,

- Sijamkataza Engineer wala wewe kusema mnayotaka hapa JF, sina huo ubavu na wala sio tabia yangu, maana ninaiheshimu sana demokrasia ya watu kutoa maoni yao huru,

- Isipokuwa ninarudia hivi ni vyema na wakati ni sasa, Mwakalinga akamkana huyu mtu kua hahusiki naye, tena mbele ya huu umma.

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom