Siasa za Mbeya 2005-2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Mbeya 2005-2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keil, Dec 3, 2007.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kikwete azuliwa jambo Mbeya

  * Mulla asema ni kukaribisha laana ya Mungu
  * Akemea tabia ya wanaoendekeza majungu
  * Aorodhesha mafanikio lukuki ya mkoa huo


  Na Charles Mwakipesile, Mbeya

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoani Mbeya, Bw. Nawab Mulla amesema wanadai kwamba Rais Jakaya Kikwete haupendi mkoa huo wamefilisika kiroho na kisiasa na kauli hizo zinakaribisha laana.

  Bw. Mulla aliwataka watu hao kuona fahari na kuthamini uamuzi wa Rais Kikwete kuteua mawaziri kadhaa na mkuu wa mkoa, kutoka mkoa huu.

  "Wana wa Israel walipozidi kumlaumu Mungu wakati amewapa chakula na neema tele alichukia na kuwapa adhabu ya kula mawe, sasa wana Mbeya nanyi mnataka nini Mungu awape zaidi ya upendeleo mliopewa na Rais wetu ?"Alihoji Bw. Mulla.

  Akihutubia wananchi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Utengule Usongwe katika kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Elimu kwa Watu Wazima cha Kanisa la Pentekoste Holiness Ministry ,Bw. Mulla alisema kuna watu mkoani hapa wamekuwa wakizuia viongozi wakuu wasije kutokana na maneno yao ya uongo.

  Alisema watu hao wachochezi wamekuwa wakitoa maneno ya uongo huku baadhi wakidai kuwa Rais Kikwete haupendi mkoa wa Mbeya,jambo ambalo alisema ni upuuzi na kutafuta laana ya Mungu.

  Bw.Mulla ambaye alichaguliwa kushika wadhifa huo kwenye uchaguzi Mkuu wa CCM uliomalizika hivi karibuni karibuni, alisema wakati huu si wa kuzungumza maneno ya uongo kwa ajili ya Mbeya bali kinachotakiwa ni kuzungumzia mshikamano wa dhati na kuijenga Mbeya upya.

  "Kipindi kilichopita maneno yalikuwa mengi yenye kukera kwa sisi tunaopenda amani na ninawambia ndugu zangu yamefanya mkoa uonekane kama kisiwa kutokana na ukweli kuwa yaliyokuwa yanazungumzwa hayakuwa na ukweli kabisa na waliokuwa wanafanya hivyo ilikuwa ni kwa manufaa yao na si ya wana Mbeya,"alisema Bw. Mulla.

  Akifafanua, alisema uthibitisho kwamba Mkoa wa Mbeya unapendwa na Rais Kikwete ni kitendo cha mkoa huo pekee kupewa Mkuu wa Mkoa wa ambaye ni mzaliwa wa hapo.

  "Hii inaonesha ni kwa namna gani Rais ana imani kubwa na wasomi wa Mkoa wa Mbeya,"alisema Bw. Mulla.

  Alisema mbali na Mkuu huyo wa Mkoa, Rais aliteua wabunge ambao ni Bw. Thomas Mwang'onda na Bi.Frorence Kyendesya ambaye aliteuliwa kuziba nafasi ya Dkt. Rose Migiro, mbali ya mawaziri wawili na naibu waziri mmoja.

  Mbali na hao mkoa huo unajivunia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Magreth Sitta ambaye ni mzaliwa wa Mbeya na na Naibu Waziri wa Maji Bi.Shamsa Mwangunga ambaye ameolewa na Kyela ambapo alisema wote hao wanaonesha jinsi ambavyo Mbeya imepewa kipaumbele.

  "Sasa ndio maana nawauliza kuwa ninyi wana Mbeya mnataka nini mnaposema, Rais hawapendi, mnataka hasira ya Mungu ishuke kisha awavue uongozi hawa aliotupa, ninyi mtapata nini? Watumieni vema viongozi hawa waliopo kwa ajili ya kuiunganisha Mbeya ninyi ndio kwanza mnasema mnatengwa na Rais acheni mambo hayo ! Alikemea Bw. Mulla.

  Akionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kama wakazi wa Mbeya watashindwa kumtumia Mkuu wao wa Mkoa ambaye wanayemfahamu hadi wazazi wake kuleta maendele, itakuwa ni hasara kubwa kwao.

  Katika mkutano huo ambao ulikuwa ni wa kuchangia ujenzi wa jengo la kusomea na kulala yatima ,mwenyekiti huyo baada ya kusomewa risala na mahitaji aliahidi kupaua jengo hilo lote lenye vyumba zaidi ya 10 kwa gharama zake.

  Alisema kinachotakiwa ni kwa wahusika hao kuhakikisha wanafikisha hatua fulani kisha kumpa taarifa ili afanye kazi hiyo ili watoto yatima na waliokosa elimu wapate nafasi ya masomo.


  Source: Majira
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 3, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Juzi kwenye sherehe ya Kagera day, yule kiongozi, mahiri, shujaa aliyetamba Bungeni alisimama na kutukuza watu wa Kagera, miezi michache iliyopita mbunge wa Tarime Chacha Wangwe alisimama na kutukuza Wakurya na watu wa Mara; Leo hii anasimama huyu na kuanza kutukuza watu wa Mbeya.. what on earth is going on?
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2007
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo Mula anatakiwa kuelewa kuwa uteuzi wa watu hao ni based on their capabilities na si kwama jk anapenda watu wa mbeya na kama ni kwa mapenzi basi JK is not a leader. Mkuu huyo toka ameshika madaraka (2 yrs) hajafika Mbeya lakini ameenda Shinyanga mara 11, Mwanza kama 8 times, Serengeti kama 5t times. Je haoni umuhimu wa kwenda kuwashukuru waliompigia kura????????? Au hazikutosha kutoka tht side. Haoni umuhimu wa kutembeea eneo linalolisha nchi yake? au mpaka itokee njaaaa??

  Kwa kifupi ni kwamba Mula anataka kutuambia kwamba JK naipendelea Mbeya, lakini je Mbeya imeanza kuwa na viongozi serikalini mara tu baada ya JK kuingia madarakani?????, sounds ridiculous eeeh!!!!!!. Anyway nipo hapa MB kwa wiki hivi ntamtafuta huyu Mula nimsikie hoja yake as some first hand info, and then will give the feedback
   
 4. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2007
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MULLA? Sounds "TALIBAN" Mulla Tunasema tatizo la kisiasa Mbeya lipo na Tunasema Kingwendu na Prof. lazima wamalize vitina vyao kwa faida ya Mkoa.Kweli nyie Vingwendu ni mazuzu..Mbeya hakuna nini?
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Such a stupid comment. Kweli ni jambo la kushangaza kwa mtu mwenye wadhifa kama huo kutoa maoni ya kijinga kama hayo. Kada uko wapi utuambie kama hili ni kweli, au ni uongo wa magazeti, mimi siamni kama kweli kiongozi mkubwa wa CCM anaweza kusema ujinga huo.
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Mulla anafikiri anamsaidia raisi kumbe ndio anamchuuza kabisaaaa! Sasa kudai kwamba Mwandosya, Mwangunga, Mama Sita, Mwakyusa na wengine wameteuliwa nafasi zao kutokana na kuheshimiwa kwa wasomi wazawa wa Mbeya ni umbumbumbu uliopitiliza mipaka. Hiyo mikoa mingine isiyo hata na mkuu wa wilaya katika utawala, wenyei wake watajisikiaje?

  Tunachosisitiza hapa ni kwamba, huu mgogoro wa Profesa Mwandosya na mkuu wa Kaya upo na inabidi umalizwe, hata kama wao wanakana kuwa hawana bifu yoyote. Haiwezekani mkuu akae miaka miwili madarakani bila kwenda kuwashukuru watu wa Mbeya kwa kumpatia kura mwaka 2005, haiingii akilini! Kaenda Iringa, Kaenda Rukwa,na sasa yuko mkoani Pwani, huku kote kuna umbali gani kutoka Mbeya? Wanasisiemu wa Mbeya wamemkosea nini raisi wao?

  Nahisi anaogopa kuzomewa, kwa sababu wananchi wa Mbeya hawakopeshi,
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mbeya chapeni kazi na acheni ujinga huu wa siasa kila sehemu.

  Badala ya kuhimiza maendeleo ya mkoa yeye bado anaendelea na siasa za wakati wa uchaguzi.

  Mbeya msipoangalia mtakuwa mabingwa wa siasa huku maendeleo yanashuka chini. Matendo yana nguvu zaidi ya maneno.

  JK kateuliwa na Watanzania na mupende au musipende ataendelea kuwa raia.
   
 8. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  Je kuna mkono wa mafisadi kumpunguzia umaarufu wake?

  Je Mwakipesile bado anadonge kooni kwa kushindwa kwa ktk kura za maoni?

  Rais JK yuko upande upi ktk hili?

  CCM mbeya hawakufurahishwa na ripoti ya kamati.

  Mwakyembe azua jambo Mbeya

  na Christopher Nyenyembe

  MAPOKEZI makubwa yaliyoandaliwa kwa ajili ya kumpokea Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, inadaiwa kuwa yameanza kuhujumiwa kutokana na chuki za kisiasa.

  Hujuma hizo zinatoka kwa baadhi ya watendaji wa serikali na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawakuwa kwenye kambi ya mbunge huyo katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.

  Wakati hali hiyo ikiwa imejidhihirisha hivyo, viongozi wa serikali na CCM wilayani humo wamekana kujihusisha na njama za kuzuia mapokezi hayo licha ya kutokuwa tayari kuelezea kama wameyaunga mkono au kutoa baraka za kuruhusu kufanyika kama wananchi walivyokusudia.

  Habari kutoka kwa baadhi ya wananchi na wajumbe wa kamati ndogo ya mapokezi ya mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, zimeeleza kuwa tangu kuanza kwa maandalizi hayo, wahusika wamekuwa wakikumbana na vikwazo na vitisho katika ushiriki wao.

  Wananchi hao waliozungumza na Tanzania Daima jana, walisema walikuwa wakiitwa mmoja mmoja na baadhi ya vigogo wa serikali na chama na kuwatolea vitisho huku wakionywa kuacha mara moja kuendesha mikakati ya mapokezi ya mbunge huyo bila kutolewa sababu za msingi.

  Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutowekwa wazi, walisema maandalizi yaliyopangwa kufanyika Machi 2, mwaka huu yana lengo la kumpongeza kwa niaba ya wajumbe wote wa kamati hiyo teule ya Bunge kwa kazi nzuri na ujasiri waliouonyesha katika kuchunguza suala hilo.

  Walidai uamuzi wa kuandaa maandamano hayo umeibua upya uhasama na chuki za awali za kisiasa zilizokuwa zimeliandama jimbo hilo mwaka 2005 na kuligawa makundi mawili -
  lile lililokuwa likimuunga mkono Dk. Mwakyembe aliyeibuka mshindi na la John Mwakipesile, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

  Aidha, imebainika kuwa wakati wananchi wakiendelea na mikakati ya kumpokea mbunge huyo,
  kundi la pili limedaiwa kuwatumia viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhakikisha wanazuia kufanyika kwa mapokezi hayo.

  Mwenyekiti wa kamati ya mapokezi hayo, Christopher Mullemwa, alikiri kuwepo kwa vitisho vinavyodaiwa kufanywa kwa baadhi ya wananchi wanaojitolea kuandaa mapokezi ya Dk. Mwakyembe, na kusema hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi kuacha kuhudhuria vikao vya maandalizi.

  Alisema pamoja na jitihada za kutaka kukwamishwa kwa maandalizi hayo, kwa upande wao wamekamilisha maandalizi yote ya awali, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za kimaandishi serikalini za kuomba kibali kwa Jeshi la Polisi, ambalo alidai limekubali.

  Alieleza kushangazwa na baadhi ya wananchi wanaoogopa kushiriki katika maandalizi hayo, na kusema mapokezi hayo yamefanywa bila kujali itikadi za vyama.

  Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela, Japhet Mwakasumi, alikana chama hicho kujihusisha na mapokezi hayo.


  Source: Tanzania daima
   
 9. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2008
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,005
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  NABII HAHESHIMIKI KWAO. ILA SISI WATZ TUNAUTHAMINI MCHANGO WAKE KWA TAIFA HILI NA TUNAMPA BIG UP SAAANA
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Unajua kamati ya uyu mbunge wengi wameumia as a result maadui ni wengi.

  Kama fisadi alipokewa kwo kwa kishindo why not shujaa kama huyu asipokelewe kwa kishindo apo ndo utakapoona ni jinsi gani watu wazima na akili zao wanavyouukumbatia ufisadi,ni aibu kabisa?

  Ningeona watu wa maana kama wangewazuia wana Monduli na sio wanakyela ambao wanataka mpongeza shujaa wao?

  Nimeamini common sense sometimes is not common.

  Apo lazima kuna mkono wa RC bse Dr ni hasimu wake mkubwa kisiasa.

  Ila wanakyela aminia am sure watapush through na mapokezi regardless na izo hila za watu.

  Shujaa hapongezwi alafu fisadi anapongezwa angekuwa Nyerere am sure angesema ni Upumbavu huu na ni signs za kuukumbatia Ufisadi.
   
 11. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Haya ndio mauzauza ya Tanzania. Wakati FISADI anapokelewa 'kishujaa'na Askofu anahubiri kwenye mapokezi hayo_On the other scene, everyone distant himself from an innocent person, this is a big shame, sio kwa Wakyela tu, bali kwa taifa zima. Yaani kila mtu anamkimbia mtu ambaye ameweza kujaribu kulinda kinachoitwa maslahi ya taifa. Honestly speaking, naanza kuona aibu kuitwa Mtanzania. Siamini kuwa wakati viongozi wanaoheshimika wanajitoa kimasomaso kumuosha FISADI, viongozi wanaogopa hata kujihusisha na Mwakyembe kwa karibu.
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hayo mambo ya Mbeya yananishinda. Habari ni kwamba wananchi wanataka kumpokea mbunge wao kwa mbwembwe zote na wameshachanga zaidi ya milioni 6 kwa ajili ya siku hiyo.

  Mkuu wa mkoa kaagiza wilayani wasiruhusu kitu kama hicho. Bahati mbaya kwao hakuna sheria inayokataza watu kuandamana kwahiyo hata mkuu wa wilaya hana nguvu na badala yake wanatumia vitisho. Pia CCM wilaya nao wanatoa vitisho vya chinichini.

  Kamati ya mapokezi wamepanga iwe tarehe 2 March ili iwe weekend kwasababu weekends zote Mwakipesile anakuwa Kyela. Wanataka warushe vijembe na nderemo mpaka Mwakipesile aipate.

  Mimi sipendi mapokezi ya viongozi lakini kama wananchi wanataka kwa hiari yao, wacha waandamane. Kuwapinga ni kuwanyima uhuru wao. Pia kwa kazi aliyofanya Mwakyembe na kamati yao wanastahili pongezi nyingi ingawaje sio lazima iwe kwa mapokezi makubwa. Kama Lowassa kapokelewa kwa mapokezi makubwa kwanini wakatae wananchi kumpokea Mwakyembe kwa mapokezi?

  Pia kutumia pesa nyingi hivyo kwenye ulaji tu wakati shule nyingi kule wilayani hazina vitabu, zahanati zina hali mbaya naona ni wastage of resources kwa mambo ambayo hayaongezi tija zaidi ya kuwafurahisha wanasiasa.

  Naona pale fahari wawili wanapigana na Kyela ndio inaumia.
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ugomvi wa Mwakyembe na Mwakipesile sijui kama utaisha ... halafu JK alifanya kosa kubwa sana kumuweka Mwakipesile kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Aidha inaweza kuwa ni makusudi kwamba Mwakipesile awe karibu na Kyela kwa ajili ya 2010 ili ashinde ama ni kumkomoa Mwakyembe kwa kuwa alikuwa pro-Prof!

  CCM watamalizana wao kwa wao!
   
 14. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  word on d street (reliable source) ni kwamba EL alitoa motisha ya fedha na mafuta ya gari kwa wananchi wa Monduli kuput on a show. Nashangaa kwanini na wao hawaku'mfisadi' kidogo kwa kutoshow up baada ya mshiko! Ask T Laizer ni rafiki mkubwa wa EL...go figure.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Waangalie, wote wanaweza kuwa panzi. Wana concentrate kwenye kugombana kumbe mwewe anakuja na kuwanyakua wote. Wasipoangalia watu wengine wanaweza kwenda na kuchukua jimbo kirahisi 2010.
   
 16. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Yaaap, huyu Mwakipesile asipoangalia anaweza kulipa ng'ombe kwa mbuzi aliyepewa na JK na EL. Ushauri wangu kwake ni kuwa wenzio wanachagua marafiki lakini hawachagui ndugu. Mmasai na Mkwere wakishamaliza term zao watakutosa wakati ambapo utakosa hata jirani hapo kwenu Kyela.
   
 17. RR

  RR JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Ishu za mapokezi hazina maana kwa Tanzania yetu.
  Ukiwa fisadi waweza kununua watu na ukiwa na mapokezi ya kufa mtu.

  Mwakyembe should not entertain this, tunajua yeye ni mtu mwema na inatosha.
   
 18. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwizi anapokelewa kwa shangwe halafu aliyemkamata wanataka kumzuia, hama kweli mbeya. Mbeya asiwababaishe mtu , ni shujaa yule Mwakyembe, mpokeeni kwa heshima yote.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Feb 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Hivi mkoa gani mwingine ambapo mkuu wa mkoa ni mzaliwa wa mkoa huo?
   
 20. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa Mtanzania, ila huyu Mwakipesile naona amezidi hapa na sasa inabidi yeye awe bangusilo hapa ili wana Kyela wapone!
   
Loading...