Dr. ni mkweli, Mungu atamsaidia. Mwakalinga ana future nzuri, ni mtu ambaye namfahamu na tuko jirani sana. Kinachoniudhi hapa ni mlango aliopitia Mwakalinga. Otherwise he is a very polite and wise man. Kama angepita njia tofauti , anafaa tu kama ilivyo kwa Dr. Watu wa Kyela hawana tabia ya kujikomba kwa watu wenye hela chafu. Ni watu wanaojiamini kama walivyo. Hivi inakuwaje mtu ambaye amekuwa msitari wa mbele kupinga ufisadi anatumiwa na hao watu waliohujumu maendeleo ya Kyela? Mwakipesile ni kibaraka wa hao wanaomchukia Mwakyembe. Heri Mwakyembe hata kama wanasema hajaleta maendeleo, kuliko mtu ambaye anatumiwa. Please , Please George jiengue na hao watu na nitakupigia debe! Tena utakuwa umeweka Historia kwenye kata ya Katumba Songwe. One word " JIENGUE NA HAO MAFISADI" come clean we will be on your back. Hujachelewa......
Nyumbu,
Sasa unataka Mwakalinga afanye nini?
Ndio maana muda wote Dr. anahangaika kumwunganisha Mwakalinga na Mwakipesile au RA au Lowassa, kwasababu anajua kuna watu kama nyie mtaamini hizo story na kuzidi kueneza.
Kwa taarifa yako tu, Mwakalinga kwa mara ya kwanza aliongea na baadhi ya viongozi wa CCM kuhusu nia yake ya kugombea March 2007. Hiyo ilikuwa kabla ya RICHMOND na pia kabla hata ya Mwakipesile kutangaza kwamba hatagombea. Kama ni mtu wa Kyela na unataka ukweli basi mwulize hata huyo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ambaye alikuwa mmoja wapo. Huyo Mwenyekiti anamwunga mkono Dr. lakini naamini ni mzee mzima hawezi kuongopa kwenye hili la lini aliambiwa mara ya kwanza. Ukitaka niandikie PM na nitakuambia huo mkutano ulifanyika wapi na nani alikuwepo.
Kwa ujumla ni kwamba Mwakalinga hajatumwa na mtu, hana mawasiliano na akina Lowasa na RA au mafisadi wengine.
Sio siri wapambe wa Mwakipesile sasa wanamuunga mkono Mwakalinga. Hicho kitu ni cha kutegemea maana adui wa adui wako ni rafiki yako na hao watu wako Kyela wala hawahitaji kufuatwa.
Hayo yote wanayoandika IPPMEDIA ni mwendelezo huo huo wa kutumia vyombo vyao ili ionekane Mwakalinga anasaidiwa na akina Lowassa, katumwa na akina Lowassa. Yote hiyo ni kwasababu hawawezi kushindana kwa hoja za maendeleo na wamekimbilia kwenye mambo ya kuzua.
Kwa anayeamini tunayosema anaweza kutuunga mkono, kwa wale wanaoamini ya ya Mwakyembe sawa pia only time will tell kama kweli hayo mnayosema yana ukweli.
Kwa watu wa Kyela wengi wanajua ukweli maana huwezi kusema mtu kapewa mamilioni wakati hata kampeni yake inaendeshwa kwa kujitolea zaidi kuliko pesa. Vijana wanaomsaidia Mwakalinga hata hawana vitendea kazi tofauti na wale wa Mwakyembe ambao wamepewa mpaka pikipiki.