BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,779
Dawa inayodaiwa kuongeza nguvu za kiume maarufu 'Akayabangu' pamoja na vumbi la Kongo zimepigwa marufuku kutumika nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa hazijathibitishwa ubora wake.
Hayo yamesemwa jana Ijumaa, Juni 23, 2023 na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Hamis Malebo kupitia taarifa kwa umma.
"Baraza limepata taarifa ya uwepo wa dawa asili inayotumika kama kinywaji na jamii kubwa hasa wanaume ijulikanayo kwa jina la Akayabagu, hivyo liliamua kufanya uchunguzi wa uingizwaji, usambazwaji, ubora na usalama wa kinywaji hicho," amesema.