BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Dawa inayodaiwa kuongeza nguvu za kiume maarufu 'Akayabangu' pamoja na vumbi la Kongo zimepigwa marufuku kutumika nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa hazijathibitishwa ubora wake.

Hayo yamesemwa jana Ijumaa, Juni 23, 2023 na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Hamis Malebo kupitia taarifa kwa umma.
1687586570569.png


"Baraza limepata taarifa ya uwepo wa dawa asili inayotumika kama kinywaji na jamii kubwa hasa wanaume ijulikanayo kwa jina la Akayabagu, hivyo liliamua kufanya uchunguzi wa uingizwaji, usambazwaji, ubora na usalama wa kinywaji hicho," amesema.
1687586603521.png
 
Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala limepiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa kinywaji cha kuongeza nguvu kiitwacho AKAYABAGU baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa kinywaji hicho hakijawahi kusajiliwa na Baraza hilo Nchini.

Taarifa ya Baraza hilo imesema pia limegundua kuwa kimechanganywa na dawa ya kisasa aina ya sildenafil (Viagra majina mengine Erecto ama Vega) jambo ambalo ni kinyume cha sheria hivyo Watumiaji wamedanganywa na Wahusika ambapo kwa kitendo cha kuchanganywa na Sildenafil (Viagra) kinywaji hiko sio tena cha tiba asili bali ni kinywaji chenye viagra, millard Ayo- 24/06/2023
 
Mtanyweshwa masumu na madawa yasiyoeleweka mpaka mkome. TBS walikuwa hawajaifanyia uchunguzi au ni ile kawaida yao mpaka kitu kilalamikiwe kwa kuleta madhara ndiyo wanashtuka?

Screenshot_20230625_161713_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom