Dawa ya Vumbi la Kongo 'hensha' yapigwa marufuku Tanzania

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo kwa binadamu, na kwamba tayari limekwishaifutia usajili baada ya kubaini imechanganywa na dawa za kuongeza nguvu za kiume (Viagra).

VUMBI.JPG
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake, lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.

CHanzo: Habari Leo
 
Duuh...Maskini wale vijana a.k.a Marioo wanaotunzwa na Mashangazi kwasababu ya show za Vumbi la kongo....

Mbona maisha yanaenda kuwa magumu zaidi kwao? Na sasahv hakuna hiyo booster jogoo atainuka na kulala muda huohuo.
 
Msife moyo mliokuwa mnatumia. Tutaileta kwa jina jingine naona kuna boya ametutibulia biashara kisa mgao wake.

Awamu hii ya pili tutaiongezea nguvu kidogo Yaani nguvu ya kukufanya urudie tendo mara nyingi.
Tukutane mwezi "ujayo"
 
😂😂😂

Kuna ndoa zinaenda kuvunjika hapo, Kama katazo hili litashikiliwa kidete
Huyo labda aliidevelop kwa kuongeza mbwembwe zake.

Vumbi la Congo kasongo Mundende purutu lipo kibao mtaani.

Kuna Energy ya Lubumbashi.

Kuna asali ya kutoka Uturuki.

Kuna Vicks.

Kuna Konyagi na Red bull.

Kuna Jack Daniels mixer na Amarula, aisee list ni ndefu.
 
Tanzania inashika no . 5 kwa utumiaji wa bangi NA IMEPIGWA MARUFUKI NA SERIKALI, no wonder huo mkongo utaendelea kutapakaa mtaani hizi ni sheria za mdomoni Tu SI AJABU TANZANIA IKATANGAZWA KUWA NAMBA MOJA KWA MATUMIZI YA MKONGO
 
Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala limeifungia dawa ya Hensha maarufu ‘mkongo’ (usajili TZ17TM0027) baada ya kukutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume ya Sildenafil “Viagra” na kusisitiza Baraza kufungia wote wanaofanya kinyume na Sheria.
 
Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala limeifungia dawa ya Hensha maarufu ‘mkongo’ (usajili TZ17TM0027) baada ya kukutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume ya Sildenafil “Viagra” na kusisitiza Baraza kufungia wote wanaofanya kinyume na Sheria.
 
Back
Top Bottom