Serikali ya CCM imeshindwa kuleta suluhisho la Maji kwa zaidi ya nusu Karne Madarakani....Shame!

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,520
86,072
Yaani ukiwakuta wamevaa zile uniform za Kijani wanavyoonekana kama Spinach utadhani ni Watu innocent na wenye maono makubwa kwenye Maendeleo ya nchi. Subutuuuuu!!

Ni aibu unapita mikoani eti Kuna Watu wanachota maji kwenye madimbwi, juzi nilikua safarini huko, Kuna vijiji viko barabarani kabisa unawakuta Watu wanachimba vidimbwi vya Maji wanachota.....miaka 50 ya Uhuru?

Yaani Wizara ya Maji Ina kazi gani? Gharama za kuchimba visima kwa Bei ya kawaida inaanzia 10,000,000 na kuendelea, tuna maeneo mengi saaana Tanzania water table iko juu sana. Tunashindwaje kuchimba visima tukasambaza Maji Kwenye vijiji?

Nimepita Manyoni mjini Kuna lile Windmill liko Mjini kabisa, limeharibika na limeachwa as if hakuna mtu analiona.

Ukienda barabara ya Tabora only 15-20km kutoka Manyoni Mjini Kuna Windmill jingine liko barabarani, limeharibika Zaidi ya mwaka, hakuna anayehangaika nalo.

Eti Kasulu na Kibondo nao Wana uhaba wa Maji?! Eti Chalinze Karibu na Mizani nyuma pale Kuna tuta (road hump) kubwa kwa kando Kuna wananchi wanachota maji kwenye kashimo!

Kati ya Moro na Dodoma Kuna kijiji Kiko njiani pale, nimesahau jina, wanachota maji kwenye vidimbwi. Eti Lushoto Tanga na wenyewe wanakosa Maji?!

Nimepita Ile barabara ya vumbi ya Kagongwa kutokea Nzega, Kuna wananchi wanachota maji kwenye vidimbwi...

Nini kifanyike?
1. Tuweke Siasa kando kwenye issue ya Maji.

2. Tuitumie Force account au pesa yoyote kwenye halmashauri kuchimba visima vya kisasa ambavyo pump zitaendeshwa na solar Panels kama ilivyo pale Kibondo.

3. Tuwajengee Uwezo wananchi waweze kusimamia hii miradi, Ile feeling ya ownership.

4. Usimamizi uwe kwenye ngazi ya Kijiji. Hii itasaidia usimamizi uwe mzuri, vile vya Kibondo baadhi yake vipo vipo tu.

5. Visima visizinduliwe na Wana siasa Ili kukwepa Ile hali ya Siasa kutumika ambayo itapunguza Ile ownership.

6. Pesa ya Maendeleo ya Jimbo itumike kujengea visima kwa nguvu.

7. Wananchi waruhusiwe kuratibu upatikanaji wa Wachimba visima (free market) Ili mradi awe amesajaliwa.

8. Wananchi wachangishwe kama tulivyofanya kwenye madawati na madarasa.

9. Tozo ya Maendeleo ya Reli (railway Development Levy) iliyowekwa kwenye Mafuta ifutwe na iwe replaced na Water levy.

10. Kufuta mara moja ule ujinga ulioanzishwa hapo juzikati wa mmiliki wa kisima binafsi kuilipa SERIKALI.

11. Family zenye kumiliki kisima iwe LAZIMA kuwachangisha Majirani pesa Kati ya 50-100 kwa Majirani Ili wachote Maji, hii itasaidia mwenye kisima at family level kufanya matengenezo ya pump.

12. Tuondoe URASIMU kwenye biashara ya Maji, iwe biashara huru.
 
Back
Top Bottom