Barabara za TASAF ni kuwatesa wananchi halafu mbona hazina usimamizi mzuri kutoka kwa wataalamu wa barabara?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Habari...
Kuna ule utaratibu wa serikali kutoa fedha kwa kaya zisizojiweza maarufu kama fedha za TASAF. Sasa pesa hizo kuanzia mwaka jana nimeona serikali imekuja na utaratibu mzuri ila usimamizi wake utaratibu huu si mzuri kabisa

Nimeona vijijini wananchi kuanzia mwaka jana waliambiwa wachimbe visima ili kupunguza kero ya maji kwa maeneo yenye adha ya maji. Visima vile kwa eneo nilipo vilichimbwa mwaka jana mapema tu ila mpaka naandika hapa wananchi wanasubiri viongozi waje wafungue rasmi na kutoa mwongozo. Sidhani kama walikuja kufungua na hivi mvua zimekuwa nyingi ndo kabisa ni kama vimetelekezwa vile

Mara nikaona tena hao "wanyonge" wapo barabarani wanalima barabara na hili ndilo lililonisukuma kuandika humu!

Jamaa hao (wananchi) wana kipimo chao cha upana wa barabara (nadhani wamepewa na viongozi wao huko) basi wanapima wanalima barabara haijalishi kuna nini wala nini (eti wanaiga ujinga wa TANESCO)

Wanalima barabara hizo kwa vifaa vya mkono na nimeona wakigawana kazi kwa kukatiana viplot.

Wanalima barabara leo kesho mvua inapiga ya hatari barabara ile haipitiki hata Kwa miguu kutokana na tope lililopo (hii ni kwa sababu hakuhashindiliwa. Yaani barabara hizo zimeshamiri kulimwa msimu huu wa mvua

Wakifika kwenye majengo sasa ndo kabisa wanahatarisha usalama maana hiko kipimo kitakapokomea hata iwe ni inchi 5 kutoka ukuta wa nyumba yako utachimbiwa limtaro hapo ushangae (wanatengeneza mitaru kwenye kingo za barabara wanazolima)

Binafsi ningetaka kujua kwa undani kwamba;

1. Je, wanachofanya hawa wananchi ndiyo maelekezo ya TASAF? Hayo ya kung'oa mazao na miti ya watu hovyo na kuwaundia njia za maji karibu na nyumba zao ambapo kwa mvua hizi maji yanakula mpaka yanaongeza njia kuukaribia ukuta?

2. Mfano kukitokea uharibifu wowote kutokana na shughuli hizi je TASAF na mainjinia wa halmashauri watawajibika au wataachwa wananchi wenyewe? Maana kwa mfano shuleni kwangu wamechimba hiyo barabara mpaka karibu kabisa na pembe ya darasa sasa sijui siku maji yakidondosha upande wa darasa itakuwaje? Vipi wale wananchi wakishitakiwa?

3. Hizi barabara vijijini nyingi zilikuwa vinjia tu kwahiyo habari ya barabara imeibuka baadae, sijui maswala ya sheria za barabara yapoje lakini unapolima barabara mpaka mlangoni kwa mtu maana yake si ni kwamba amezidi vipi sasa akitaka kusogeza jengo hilo na eneo likawa limebana/limekwisha? Au vipi kuhusu yule ambaye ardhi yake ya shughuli ndogondogo binafsi imemegwa kwa kiasi kikubwa na barabara hizo?

4. Je tathmini yenu (serikali kupitia TASAF) ilibaini barabara za mitaa kama kipaumbele cha wananchi kwa maeneo yao husika?

5. Je swala hili ni endelevu na kwenye mambo mengine au linaishia kwenye visima na barabara na kufanya usafi zahanati? Kwa nini wale wananchi wapo wao kama wao tu siwaoni wakiwa na mtaalamu hata mmoja wa halmashauri wala mtendaji wala nani, sanasana nimemwona mwenyekiti wa kijiji tu mara kadhaa
 
Back
Top Bottom