Ngara: Bilioni 41 Kujenga Mradi Mkubwa wa Maji Utakaohudumia Wakazi Zaidi ya 170,678.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Wizara ya Maji inatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa Maji Ngara Mjini kwa gharama ya Shilingi Bilioni 41. Usanifu wa mradi umekamilika na unatarajia kuhudumia wananchi 170,678 waishio katika Kata ya Ngara Mjini, Kanazi, Kidimba, Nyamiaga na Murukurazo" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri Maji

"Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili Utekelezaji wa mradi wa Maji Ngara uanze. Kwa mpango wa muda mfupi wa kupunguza kero ya Maji katika Mji wa Ngara na viunga vyake Serikali katika mwaka wa fedha 2023-2024 imetenga Shilingi Milioni 600 na kazi zitakazofanyika ni pamoja na uchimbaji wa Visima viwili ambapo kisima kimoja kimekamilika, ujenzi wa tenki la ujazo wa Lita 250,000 na ulazaji wa mtandao Umbali wa kilomita 12 na ufungaji wa Pampu 2 za kusukuma Maji" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri Maji

"Je, Serikali iko tayari kuanza kujenga mradi huu mkubwa wa Shilingi Bilioni 41 kwa kutumia mapato ya ndani yanayotoka Serikalini wakati ikiendelea kutafuta fedha kutoka nje" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Ni lini Serikali italipa fedha ya Bwana Baraka Makobwe Shilingi Milioni 104 ambaye Ardhi yake imechukuliwa na Wizara ya Maji na eneo limejengwa tenki kubwa la Maji na hajalipwa kwa muda mrefu sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

Mhe. Marypriscas Mahundi amesema kuwa ushauri wa kutumia mapato ya ndani kwenye mradi wa Maji umepokelewa na pia Mwananchi ambaye Ardhi yake ilichukuliwa na Wizara ya Maji fidia yake atalipwa kadiri inavyitakiwa.

sddefaultsawq.jpg
FDNS5gSWEAQBmZ9.jpg
 
Back
Top Bottom