Ukifatilia haya mambo ya muhimu unaitwa mzee yaani vijana wa nchi hii ni bongofleva tu akilini mwao na wasanii ndio hivyo tena wanaipigia promo ccm so painful.
 
Urithi kwa namna gani? Wanyama wanazaliana kila mwaka.

Mimi nimekuwa positive kwasababu unless kufanyike utafiti utakaotoa majibu negative, sioni ubaya wa kuuza na kutengeneza fedha za kuboresha huduma kwa jamii.
Zamani mikumi nakumbuka nimewahi kuwaona faru na mbuni sasa unawaona mara nyingi kwenye zoo tu na huko nako wanauzwa!
 
Huu mjadala niliamua kuuacha kwasababu exposure yangu nadhani iko juu kidogo kuliko watanzania wa kawaida.

Utalii sio maliasili wala wanyama. Utalii ni hospitality industry na ndio maana nchi zinazoongoza kwa utalii duniani hazina hivyo mnavyoita maliasili.

Ukijaliwa fika Spain, Bahamas, Mauritius nk then utakuwa na mtazamo mpana kuhusu hii sector.

Hawa wanyama tulionao Tanzania nimewahi kuwaona kwenye zoo kule Switzerland, France, Thailand, US, Dubai, Qatar etc hivyo kama ni kuwaona wanyama tàyari wapo kule.

Hii mitazamo general na ya kijamaa ndio inafanya hii nchi wakenya wananufaika nayo. Watanzania wanalima halafu wanauza kwa bei ya kutupa kwa wakenya ambao wanafanya packaging na kuuza masoko ya dunia ya kwanza.

Hii mitazamo isipobadilika tukajua nini hasa ni tourism leo hii fukwe tu za bahari ya hindi zingeweza kuleta watalii milioni 20 kwa mwaka kama tungewekeza kwenye huduma zinazofanya mtalii aje.

Naishia hapa.
Ulitaka kutupia watanzania lawama za export utakuwa mjinga wa halo ya juu. Wakenya serikali yao kwenye suala la ku add value na kutafuta masoko imewajengea mazingira mazuri kulinganisha na hapa kwetu mbali watu tukio wapa shamans ya kutuongoza wamekuwa ni wachumia tumbo.

Huwezi kusema eti utalii ni hospitality. Ndugu kubali kuwa hapa wewe ni mweupe. Kwa kukusaidia utalii na hospitality ni vitu viwili tofauti japo vinashabihiana. Kwahiyo msitake kuhalalisha wizi wa wanyama kwa sababu zisizo na mashiko.

Watalii hufuata vivutio na si hospitality kama unavyodai na kwa taarifa yako hizo nchi ulizo zitaja kuongoza kwa kupokea watalii wengi ni kwa sababu ya gharama kuwa chini ukilinganisha na Africa kwahiyo ni rahisi watu kwenda kutoka nchi za jirani kwenda kula bata spain, france n.k.

Hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini asilimia kubwa ya watalii kutoka America wanapokuja Tanzania wanaokwenda mbugani na si Zanzibar?
 
View attachment 2250921Hali iko hivyo, tunaelekea kule 7kule tulipotoka, sasa ni rasmi twiga wetu wataanza kupandishwa ndege tena kwenda Ughaibuni.



_______________


Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Hawa Bihoga
Tupe jina la Kamishnaa ....TAWRI EIA??
 
Back
Top Bottom