Kipi ni bora, wanyama pori au watanzania wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi za Taifa. Hapa nitatoa mifano miwili.
(1) Wananchi wanaoishi pembe zoni wa Hifadhi ya Serengeti Wilayani Tarime.Ikumbukwe kuwa wananchi kila kukicha wanaongezeka na ardhi haiongezeki. Beacons ziliwekwa miaka 1962 kuonyesha mipaka halali ya Hifadhi ya Serengeti.
Ingekuwa ni busara Serikali ikaheshimu mpaka uliowekwa mwaka 1962 na wakashirikisha wananchi kwa kila hatua. Pili kama watu wameongezeka basi ni busara kwa Serikali kasogeza mpaka mpya ndani kabisa ya Hifadhi. Ukubwa Hifadhi ya Serengeti ni kama nchi ya Rwanda.
Sasa kipi ni bora kuheshimu wanyama pori kuliko binadamu. Jukumu nambari moja ni kuheshimu watu na siyo wanyama. Serikali yetu ni sikivu na mpaka uliopo basi usogezwe ndani kabisa ya Hifadhi ili wananchi wapate maeneo ya kulima. Tujali wananchi kwanza na siyo wanyama pori.
(2) Eneo la Nyatwali Wilayani Bunda. Serikali imeanza kufanya utaratibu wa kuwahamisha wananchi wa Kata ya Nyatwali ili wapishe wanyama pori. Kipi ni bora wanyama pori au binadamu. Wazo hili lilianza wakati wa utawala wa Magufuli na alipopelekewa wazo hili la kuwahamisha wananchi alikataa katakata na wananchi wakafurahi sana. Eneo hili linatambulika kama kata na ina vijiji vitatu vilivyoandikishwa kisheria.
Awamu ya sita ilipoingia madarakani ikabariki wazo hili na sasa ni dhahiri kabisa wananchi wanahamishwa bila kupenda. Kinachosikitisha ni malipo wanayopewa ili kuhama.
Kwanza waliwaeleza wananchi kuwa kwa ekari moja malipo yatakuwa shillingi milioni nne. Juzi wamekuja kusainisha watu malipo yao na kila ekari ni shillingi millioni mbili tu kinyume na makubaliano ya hapo awali. Ni masikitiko makubwa wananchi kuonewa na wanyama pori kuonekana wana thamani kuliko binadamu.
Hata kama wananchi watahama basi malipo yao yawe malipo ambayo ni mazuri. Mwisho kipi ni bora, binadamu au wanyama pori?.