Serikali itwambie ukweli kuhusu inflation na thamani halisi ya pesa. Gharama za maisha zimepanda sana

Sasa subirini, miaka michache ijayo watapiga hodi IMF kuomba mkopo wa kufufulia uchumi ndipo hili la thamani halisi ya shilingi itakapofichuka.

Wataambiwa sarafu iwe floated ili ijitafutie thamani yake yenyewe ndipo hili ninalolisema hapa litakapo dhihiri na serikali italazimishwa kupunguza matumizi yake ya (Recurrent Expenditure) na ndipo itabidi wapunguze mikoa na wilaya kwani ndio chanzo cha gharama ya uendeshaji kuongezeka.

Lazima watalazimishwa kufanya (Restructuring characterized by reducing the bloated civil service), pia watatakiwa kuacha kutoa ruzuku kwa mashirika mizigo kama Atcl nk. It will be a bitter pill to swallow.
 
Au ndo pesa imemwagika mitaani kufuatia yale madai ya ''mama rudisha pesa mtaani''

Nafikiri haya yatakuwa mazao yake.

mtoa mada umeniduwaza kdg kuutaja mchele kama moja ya bidhaa ghali.

Niliko huku ni elf 1 @ kg
 
Kwani Nchi inaongozwa na Chadema?
Mbona mlisema wapinzani walituchelewesha Sana kupata maendeleo Sasa kelele za nini?
CHADEMA ndoo mtaa gani ? Hatujadili habari za marehemu aliyejifia siku mwenyekiti wao alipobadili gia angani mwaka 2015.
 
Huu ndiyo wakati mzuri wa kukumbuka Yale mazuri ya JPM likiwemo na hili la ku hold inflation kwa miaka 5, hata kama hakupandisha mishahara angalau hiyo 10,000 ilikuwa na thamani

Mwezi March mwaka huu petrol na diesel zilikuwa chini ya shilingi 1,650 hapa dar. Sasa mchwa umeingia kazini Cha moto tutakiona.
Eti...'mazuri ya JPM"...!😝😝😝😝😝
 
Kwani IMF wanasemaje mkuu ina maana wanaweza kuachia mtu afanye manipulation mchana kweupe
Wapo wanaoshusha thamani ya fedha yao kwa makusudi kama China na wapo wanaopandisha pia kwa makusudi kama Tanzania tatizo litakuja pale utakapohitaji mkopo.
 
Kumbe ndio maana Jiwe alikuwa ameshindwa kupata mikopo nafuu mpaka akaanza kukopa Bayport & Finca
 
Here we go, maisha ni magumu mno
Quality ya maisha inazidi kushuka maana watu hawaafford tena vitu walivyokuwa wakiviafford zamani
 
Wamtoe yule anaejisifia mchumi wa Taifa kila kukicha huku Nchi ikienda shimoni kwa mbinu zake za hovyo za kuongeza gharama kwenye kipindi kigumu cha Covid...
 
Siku hizi ukiwa na shilingi elfu 10, inayoyoma kama upepo, thsmani ya pesa haipo kabisa
Maisha ya wananchi yanazidi kuwa juu na magumu.
Wakati serikali haikuongeza stahiki za wafanyakazi kwa miaka Sita sasa, lakini imewazunguuka na kuwaongezea TOZO lukuki na kodi Lukuki na hivyo kuifanya Quality ya maisha yao izidi kushuka.

Wakati huohuo bidhaa muhimu zinaendelea kupanda bei, Mafuta, Mchele, Sukari, Mkate vyote viko juu

Tunataka serikali ije na takwimu halisi kuhusu thamani ya shilingi yetu, mbona hela inayoyoma sana na pia inakuwa ngumu sana kupata inayokidhi maisha ya kila siku?

Serikali inaweza kudhani kuwa hizi TOZO ndiyo suluhisho kwa yenyewe kupata hela za kufanya mambo yske ikiwemo miradi mikubwa lakini mimi naona kuwa hii solution ya muda mfupi tu, na itajikuta kila mwaka hata hizo tozo zinapungua maana maisha ya wananchi yanazidi. kuwa magumu, na wananchi wengi wanarudi katika umasikini uliotopea

Kibaya zaidi, Serikali haibani matumizi, kutwa kucha watu wako barabarani Dar-Dodom, Dodoma-Dar. Hata Spika Ndugai amehoji shughuli za serikali kuwa Dar

Serikali itueleze, Hali ya inflation nchini ikoje, maana this is too much, Hela zinapukutika kama chuma ulete
Ngoja tathmini ya ugaidi wa Mbowe ifanyike utapata jibu.
 
Sasa subirini, miaka michache ijayo watapiga hodi IMF kuomba mkopo wa kufufulia uchumi ndipo hili la thamani halisi ya shilingi itakapofichuka.

Wataambiwa sarafu iwe floated ili ijitafutie thamani yake yenyewe ndipo hili ninalolisema hapa litakapo dhihiri na serikali italazimishwa kupunguza matumizi yake ya (Recurrent Expenditure) na ndipo itabidi wapunguze mikoa na wilaya kwani ndio chanzo cha gharama ya uendeshaji kuongezeka.

Lazima watalazimishwa kufanya (Restructuring characterized by reducing the bloated civil service), pia watatakiwa kuacha kutoa ruzuku kwa mashirika mizigo kama Atcl nk. It will be a bitter pill to swallow.
Hii Kweli Mkuu Ilowa
Sijui Itakauka Lini
 
Siku hizi ukiwa na shilingi elfu 10, inayoyoma kama upepo, thsmani ya pesa haipo kabisa
Maisha ya wananchi yanazidi kuwa juu na magumu.
Wakati serikali haikuongeza stahiki za wafanyakazi kwa miaka Sita sasa, lakini imewazunguuka na kuwaongezea TOZO lukuki na kodi Lukuki na hivyo kuifanya Quality ya maisha yao izidi kushuka.

Wakati huohuo bidhaa muhimu zinaendelea kupanda bei, Mafuta, Mchele, Sukari, Mkate vyote viko juu

Tunataka serikali ije na takwimu halisi kuhusu thamani ya shilingi yetu, mbona hela inayoyoma sana na pia inakuwa ngumu sana kupata inayokidhi maisha ya kila siku?

Serikali inaweza kudhani kuwa hizi TOZO ndiyo suluhisho kwa yenyewe kupata hela za kufanya mambo yske ikiwemo miradi mikubwa lakini mimi naona kuwa hii solution ya muda mfupi tu, na itajikuta kila mwaka hata hizo tozo zinapungua maana maisha ya wananchi yanazidi. kuwa magumu, na wananchi wengi wanarudi katika umasikini uliotopea

Kibaya zaidi, Serikali haibani matumizi, kutwa kucha watu wako barabarani Dar-Dodom, Dodoma-Dar. Hata Spika Ndugai amehoji shughuli za serikali kuwa Dar

Serikali itueleze, Hali ya inflation nchini ikoje, maana this is too much, Hela zinapukutika kama chuma ulete
Haya nilishaliona muda nimebuni mchanganuo ambao unaweza ng'amua tatizo linaloweza kutokea kwenye biashara ama taasisi "IPYANA analysis' bado sijapata alama ya utambulisho(patent)
 
Hali ni mbaya sana
Mafuta ya kula, Bidhaa za vyakula kama vile mchele , unga na nyinginezo kama gesi vimepanda bei sana.
Hapo hujazungumzia kuadimika kwa vitu vya msingi kama vile maji etc
 
Back
Top Bottom