Ni lini tataanza kuweka mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu?

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,679
Inakuwaje kwamba Kenya, kuanzia kati ya mwaka uliopita, ilishuhudia kuanguka vibaya kwa sarafu yake, Kenya Shilling, hadi kufikia mwisho wa 2023, ilipoteza asilimia 20% ya thamani yake.

Shilingi ya Kenya iliwahi kubadilishwa Sh.167 kwa dola moja, kutoka shilling 135 kabla rais Ruto kushika madaraka.

Lakini katika wiki mbili zilizopita, wataalamu wa uchumi Kenya, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, walifanya juhudi za ziada kuinua kima cha Shilingi, na hii leo shlingi inabadilishwa kwa sh. 137 kwa dola moja. Wataalamu hao wameapa kuirusha shillingi hadi kufikia sh.100 kwa dola 1 hadi Juni.

Baadhi ya faida za kupanda thamani ya sarafu ya nchi ni kupunguza mzigo wa deni, hivi kwamba serikali italipa kiasi hafifu. Pia bidhaa zinazotoka nje zinakuwa na bei hafifu, na la muhimu zaidi kuna uwezekano wa kupungua bei za bidhaa zinazoingizwa. Kama vile Kenya hivi sasa bei ya mafuta imeshuka kwa zaidi ya shilingi 27 kwa lita.

Ukitazama Tanzania, hali inazidi kuwa mbaya katika exchange rate na kana kwamba hakuna juhudi zozote zinazofanyika ili kuinua kima cha shilingi ya Tanzania. Twasikia maneno tu ya kejeli na ya kihuni yasiyoonesha taaluma, kwamba 'tunakopa kwa vile tuna uwezo wa kulipa' kana kwamba kukopa ni ibada ya faradhi!

Nashuku kwamba kuna uhaba wa elimu na uelewa wa masuala ya fedha katika ngazi za juu za wanaoongoza sera za fedha nchini humu. Kama ungekuwepo, suala la thamani ya fedha yetu lingekuwa lajadiliwa kila siku, kama ilivyo Kenya. Hili ni suala kubwa kabisa linaloathiri maisha ya watu, lakini halipewi umuhimu huo.

Swali langu kwa Dk Waziri: lini ataanza kuweka mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu? Aanze kwa kufanya dola moja iwe tu = 2,000 kutoka Tshs. 2,549.60 hivi sasa. Watanzania wangeona mabadiliko makubwa sana ya maisha yao.
 
Mimi naona hata hiyo dola moja kwa 2000 ni bado hakuna msaada kqa wananchi.

Naona serikali itafute wataalamu wa maswala ya fedha .
Walau dolla moka iuzwe kwa 100 sh .mpaka tufike 1-1
 
Huyu huyu Dokta wa TRAB na TRAT pale tuliingizwa Chaka hakuna kitu kabisaaaaaa namaanisha empty set according to John Venn
 
Moja ya njia ya kuipandisha ni kuongeza interest rate. Uko tayari riba iongezwe? Pia kuongeza thamani artificially siyo susutainable kabisa. Misri wanafanya hivyo na kinawaramba
No. Kwa Tanzania kwa kweli kupandisha shillingi kutatokana na kukata matumizi makubwa na yasiyo lazima ya serikali, kuongeza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na hiyo ni kwa kupungza vikwazo lukuki kwa wasafirishaji bidhaa, pia kuongeza akiba ya psa za kigeni nje badala ya kukopa ovyo ovyo......
Interest rates zenyewe hivi sasa si sustainable hivi kwamba ni mwendawazimu tu, au aliye desparate ndiyo atakopa benki!
Ikiwa Waziri wa Fedha ni huyo.......
 
Mimi naona hata hiyo dola moja kwa 2000 ni bado hakuna msaada kqa wananchi.

Naona serikali itafute wataalamu wa maswala ya fedha .
Walau dolla moka iuzwe kwa 100 sh .mpaka tufike 1-1
Hii haitatokea katika umri wako wala wangu!
 
Mimi naona hata hiyo dola moja kwa 2000 ni bado hakuna msaada kqa wananchi.

Naona serikali itafute wataalamu wa maswala ya fedha .
Walau dolla moka iuzwe kwa 100 sh .mpaka tufike 1-1
Tatizo dhahabu na madini yetu Mengi tunayatoa bure, hakuna mzunguko wa fedha nchini, hela inapopigwa au madini , Kesho yake kabla hamjawashika , pesa imetoka nje ya nchi, hivyo mahitaji ya dollar ni makubwa, Kwani hela inayopelekwa nje ni ya kigeni.mzigo unakuwa mdogo. Sio madafu yetu utakaza pick up
 
Inakuwaje kwamba Kenya, kuanzia kati ya mwaka uliopita, ilishuhudia kuanguka vibaya kwa sarafu yake, Kenya Shilling, hadi kufikia mwisho wa 2023, ilipoteza asilimia 20% ya thamani yake.
Shilingi ya Kenya iliwahi kubadilishwa Sh.167 kwa dola moja, kutoka shilling 135 kabla rais Ruto kushika madaraka.
Lakini katika wiki mbili zilizopita, wataalamu wa uchumi Kenya, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, walifanya juhudi za ziada kuinua kima cha Shilingi, na hii leo shlingi inabadilishwa kwa sh. 137 kwa dola moja. Wataalamu hao wameapa kuirusha shillingi hadi kufikia sh.100 kwa dola 1 hadi Juni.
Baadhi ya faida za kupanda thamani ya sarafu ya nchi ni kupunguza mzigo wa deni, hivi kwamba serikali italipa kiasi hafifu. Pia bidhaa zinazotoka nje zinakuwa na bei hafifu, na la muhimu zaidi kuna uwezekano wa kupungua bei za bidhaa zinazoingizwa. Kama vile Kenya hivi sasa bei ya mafuta imeshuka kwa zaidi ya shilingi 27 kwa lita.
Ukitazama Tanzania, hali inazidi kuwa mbaya katika exchange rate na kana kwamba hakuna juhudi zozote zinazofanyika ili kuinua kima cha shilingi ya Tanzania. Twasikia maneno tu ya kejeli na ya kihuni yasiyoonesha taaluma, kwamba 'tunakopa kwa vile tuna uwezo wa kulipa' kana kwamba kukopa ni ibada ya faradhi!
Nashuku kwamba kuna uhaba wa elimu na uelewa wa masuala ya fedha katika ngazi za juu za wanaoongoza sera za fedha nchini humu. Kama ungekuwepo, suala la thamani ya fedha yetu lingekuwa lajadiliwa kila siku, kama ilivyo Kenya. Hili ni suala kubwa kabisa linaloathiri maisha ya watu, lakini halipewi umuhimu huo.
Swali langu kwa Dk Waziri: lini ataanza kuweka mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu? Aanze kwa kufanya dola moja iwe tu = 2,000 kutoka Tshs. 2,549.60 hivi sasa. Watanzania wangeona mabadiliko makubwa sana ya maisha yao.
Wanaharibu kuongeza interest rates ambazo Kwao Ina make some.sense Kwa sababu Wana inflation kubwa.

Tanznaia hatihitaji huu upuuzi
 
Siku zote masuala ya muhimu na yanayotaka mjadala wa fikra hayapati mchango wa kutosha hapa. Watu wataka kujadili vitunguu, Yanga n Waziri amevaa nini.
Suala hili la exchange ya Shilingi ni kubwa sana katika maisha ya watu ya kila siku. Miaka ya sabini mkulima wa pama ilibidi auze magunia sita ya pamba anunue trekya. Leo, kwa trekta lile lile inabidi auze magunia 230! Hayo yote yamefanywa na hela zetu kugeuzwa madafu na Waziri mwenye dhamana ala hana mkakati wowote, aona sawa tu...
 
Back
Top Bottom