Ukweli mchungu kuhusu Maisha ya Mwanadamu

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Maisha wakati mwingine huonekana kutokuwa na maana, lakini ni mwalimu bora kwa mwanadamu uwe jeuri na mkaidi ila Maisha ndo yatakufunza vyema. Kila uzoefu na hali mbaya tunayokabiliana nayo ukitazama ndani yake basi kuna somo kubwa ndani limejificha kwake, ajabu ni kwamba wachache sana wanaweza kuliona jambo hilo. Ninaamini katika fundisho kwa kila kitu ambacho tunakipitia katika harakati za Maisha.
1702468314688.png

Mtu akikutukana fahamu ndani yake kuna somo kubwa anakufundisha kuhusu yeye na jamii yake. Kwa wale wenye ukaidi ndo unakuta hujifunza masomo kwa njia ngumu, maumivu na majut makubwa ndo hufuata kwenye mkakati wa kufahamu msingi wa Maisha yako, na ukishindwa kabsa kuelewa basi mwishoni huingia kwenye mtego wa kurudia makosa yale yale mara kwa mara, na kwa akika hiyo sio njia bora ya kuishi.

Muda
Tuko hapa kwa muda mfupi sana kwenye sayari hii ya dunia, haijalishi utafanya nini, saa ikifika tutakufa mmoja mmoja, hatuishi milele Tunalielekea kaburi moja moja na huwezi kupinga hilo. Hili ni gumu kukubali kwa sababu mpaka sasa unafanya vyema, wewe ni mzma na huna ugonjwa wowote. Ni vyema kujikumbusha juu ya ukweli kwamba hatuishi hapa milele kutakusaidia kuishi kwa uangalifu zaidi kwa kuweka kipaumbele kile ambacho ni muhimu kwako na kile ambacho sio.
1702468428429.png

Muda haumsubirii mtu yeyote, na ukiisha, huwezi kuupata tena. Maria Branyas Morera ndo mwanadamu aliye na umri mrefu zaidi mpaka sasa kwa mujibu wa Kitabu cha Guinness World Records akiwa na miaka yake 116 lakini Maria anajua kuwa ipo siku atakufa tu ndo ukweli wa Maisha hapa duniani. Weka mipango yako ukitambua hili suala.
1702468564094.png

Upendo
Kila mtu ni tofauti na wa kipekee kwa njia yao wenyewe. Haijalishi uko wapi, unafanya nini, na unamfanyia nani. Kila mahala kila wakati lazma kutakuwa na mtu ambaye hatakubaliana nawe, mtapishana tu kwa kauli, matendo na kadhalika, kitu ambacho ni sawa katika maisha. Kadiri unavyokutana na watu wa sampuli hii ndivyo inavyokuwa bora zaidi maishani mwako.
1702468706540.png

Nakumbuka Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu aliwahi kusema kuwa utofauti wake wa mawazo bungeni na aliyekuwa Spika wa Bunge, Mama Anna Anne Semamba Makinda ulikuwa ukimpa nafsi ya kufikiria zaidi hoja za kuleta bungeni, wanabishana bungeni ila wakitoka nje wanasakata dansi hatari sana.

Pambana
Ni wewe tu unaweza kujiondoa kwenye giza na kufanya kitu kutoka kwa maisha haya. Kumbuka maisha haya ni 100% jukumu lako hakuna anayekuja kukuokoa na usitegemee kupata msaada kama hauoneshi juhudi yoyote mtu wangu.
1702469068260.png
Sio marafiki zako, na baada ya umri fulani hata wazazi wako, ila tu usifuate mkumbo wa kuiga watu wengine, pambana kwa uwezo wako bila kutazama mtu mwingine. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha chochote katika maisha yako mpaka wewe uwe radhi na jambo hilo. Ni juu yako kabisa rafiki yangu. unataka kuyapeleka wapi maisha yako, wewe ndo mwenye remote control.

Afya
Najua naendelea kurudia hii. lakini siwezi kusisitiza vya kutosha juu ya suala hili, Tunza sana mwili na akili yako, hivi ndo dhahabu na almasi ya Maisha yako. Ukweli ni kwamba tukiwa Watoto tunakuwa na maendeleo mazuri ya kiafya kwa kuwa tunatazamwa na watu haswa wazazi na walezi wetu, kuna nyakati Maisha yanatufanya tuishi katika hali nzuri sana huwa tunachukulia afya zetu kuwa za kawaida. tunakula chochote tunachotaka, na kulala wakati wowote tunapotaka.
1702469193288.png
Usipuuze afya yako kwa gharama yoyote, kumbuka kuna matibabu yanachukua muda na gharama kubwa sana. Usiweke uzembe katika afya yako jilinde na magonjwa yote sio tu Ukimwi au Gono hata Malaria inaweza kukupeleka kaburi chap tu, achana kabsa kuchezea afya ulio nayo. Kuna watu wapo mahospitalini wanatamani wapate hata siku moja watembea kwenye flyover ya Ubungo ila wapo wamelala kitandani. Heshimu sana afya yako Mkuu.
1702469275770.png

Dalai Lama aliwahi kusema “We sacrifice our health in order to make wealth, then we sacrifice our wealth in order to get back our health.”.

Maisha
Hauko mbele au nyuma ya mtu yeyote katika harakati za Maisha yako. Maisha ya kila mtu ni ya kipekee na tofauti sana hakuna ufanano wowote ule seemu yoyote ile duniani. Kila mtu ana muda wake wa kuteseka na kufanikiwa, usije kusema kuwa mbona Fulani ana pesa nyingi na magari ya kifahara bila kufahamu historia yake ya upambanaji, wapo wanaotumia njia chafu za kupata Maisha mazuri na wengine hutumia njia sahihi.
1702469464550.png
Chaguo ni lako Mkuu, duniani hakuna ratiba ya kitu chochote kuwa kifanyike wakati Fulani, wakati UVIKO-19 imeingia kuna wafanyabiashara wengi walipata faida sana kwenye kuuza bidhaa kama Ndoo, Barakoa pamoja na kutoka huduma kwa umma. Binfasi una haki ya kufanya kila kitu na kitu chochote kwa kasi yako mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yoyote, jiamini utafanya vizuri na acha kabsa papara usiwe na haraka.
1702469591405.png

Kuna shinikizo kubwa kwa sisi sote kuwa na furaha kutokana na vile tunavyojichukulia. Lakini maisha wakati mwingine ni magumu na yenye uchungu sana, yanatunyima hata sekunde ya kuweka tabasamu katika nyuso zetu, lakini hii isiwe kikwazo cha kuturudisha nyuma na kuacha kupambana kila siku.

Jiandae kukutana na watu wasiokukubali hata kidogo, kwa sababu kukataliwa ni sehemu ya maisha, na sio kila mtu atakukubali au kukupenda, wewe sio chupa ya asali ama ukwaju! Wewe ni mwanadamu na wanadamu watakuvuruga na kukuchukia bila sababu yoyote vivyo hivyo na wewe utawachukia wenzako bila sababu yoyote, kitu cha msingi ni kuwa huwezi kudhibiti mambo hayo lakini unaweza kudhibiti jinsi unavyojibu. Jambo pekee la msingi ni kuwa unaweza kudhibiti kila wakati–na hilo ni wewe mwenyewe, miitikio na mawazo yako.

Maisha hayatawahi kuwa bora kwa 100% katika fikra zako futa hiyo Mkuu. Kutakuwa na siku ambazo utahisi kukata tamaa. sote tuko hapa kujifunza sehemu yetu ya masomo na kubadilika kulingana na wakati. maisha ni 10% kile kinachotokea kwako na 90% jinsi unavyoitikia wewe binafsi.

Hakuna mtu mmoja, narudia hakuna mtu kwenye sayari hii ambaye hana mateso na shida hata walimbwende wazuri kutoka Ufilipino ama Mexico bado wana shida zao nyingi tu. Ni mtazamo wako kuelekea ugumu ndio utakaoamua ubora wa maisha yako. kabili changamoto, jifunze somo linalohusiana nayo, na uendelee kupambana.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom