Mkuu mbona unazunguka tu wakati mimi nimeenda straight to the point? Mimi siungi mkono mapenzi ya jinsia moja bali nawacrush wale mnaowarushia mawe wanaofanya mapenzi ya jinsia moja ilihali na ninyi ni wazinzi, majambazi, wakana Mungu nk na ndiyo maana nikakuuliza utofauti wa hizo dhambi uko wapi ikiwa adhabu ya mzinzi na shoga ni moja wote wataenda kuchomwa moto wa milele wasipotubu?
Wengi mmeng'ang'ania huo mfano wa Sodoma na Gomora ila hamtaki mfano wa Mungu kuangamiza dunia kwa gharika sababu ya dhambi nyinginezo! Haya je tangu Mungu aangamize hiyo Sodoma na Gomora mbona mashoga wamezidi kuongezeka je kuna adhabu nyingine ya hapa duniani ambayo mmeona amewapa hawa mashoga wanaozidi kuongezeka mbona kuna wengine ndiyo kwanza maisha yao yanazidi kuwanyookea mmebaki ninyi ndiyo mnateseka?
Mkuu narudia kwa sisi wakristo maandiko yako wazi kwamba baada ya Yesu mwana wa Mungu kutufia msalabani dhambi zote zikawa sawa kasoro dhambi moja tu ya KUMDHIHAKI ROHO MTAKATIFU! Kwamba mtu yeyote mwenye dhambi yoyote ile isipokuwa hiyo tajwa basi akitubu kwa roho na kweli atasamehewa na asipotubu hatasamehewa na ataenda kuface hukumu na moto wa milele!
Mbona mnajifanya mnajisahaulisha kwamba kwenye agano jipya baada ya Yesu kupaa mbinguni sheria nyingi za agano la kale zilibadilishwa? Kwa taarifa yako hayo mambo ya kupimiana ukubwa wa dhambi yalikuwa kwenye agano la kale enzi ambapo torati au sheria ya Musa ilikuwa inafuatwa ila kwenye agano jipya hakuna hayo mambo!
Na Yesu alishasema mtu hataenda mbinguni kwa matendo yake tu bali pia anatakiwa amuamini yeye kama njia ya kwenda mbinguni kwa Baba yake na hayo maneno yamekuwa yakihubiriwa hadi wa leo! Hivyo watu kutokujua uwepo wa Mungu hapo zamani siyo excuse ya kwamba hata ulimwengu wa sasa ambao umeshaijua injili nao usiamini eti kisa tu babu zetu hawakuijua dini!
Nilikupa andiko linalosema kwamba mtu ambaye anatoa boriti kwenye jicho la mwenzie ilihali hajatoa kibanzi kilichopo kwenye jicho lake mwenyewe biblia inamuita mnafiki! Kwa sababu kazi ya kuhukumu Mungu alishaitoa mikononi kwa wanadamu akaiweka mikononi mwake ndiyo maana hayo mambo ya kupigana mawe na kunyongana kwenye dunia ya leo hayapo kwa wanaoamini Mungu!
Hakuna kitu kibaya kama kujihesabia haki yaani Mungu anachukia sana mtu anayejihesabia haki na kujiona yeye mtakatifu na wengine wana dhambi kuliko yeye na hicho ndicho ambacho wazinzi mnafanya kwa mashoga! Hata Musa pamoja na kwamba Mungu alimpenda hadi alikubali amuone!
Lakini kosa lake kubwa lillilomfanya Mungu amnyime neema ya kuingia Kanaani ni kujihesabia haki akaishia tu kuoneshwa Kanaani ile na akafia kule kule! My point from the beginning is acheni kujihesabia haki na kujiona ninyi ni watakatifu sana binafsi nachukia sana uzinzi na sipendi kuona mijitu inajisifia uzinzi eti ni kawaida hivyo kwangu (na kwa Mungu ofcourse) wazinzi na mashoga wote wana dhambi na watahukumiwa!
Usijifiche kwenye kichaka cha sijui eti "hiyo hoja yako ni mfu" bila kutoa ufafanuzi ukidhani kwamba tunashindania hoja mimi siko hapa kushindana ila inabidi tukubali tu kwamba tuache unafiki kuhukumu watu kama biblia inavyotuita! Wewe unavyowaona na kuwachukulia mashoga ndivyo mimi ninavyowaona na kuwachukulia wazinzi na wakana Mungu na kiuhalisia wote hao ni threat kwa dunia ya sasa hakuna mwenye afadhali kama unavyotaka kuniaminisha hapa!