Scholarships mbona zipo kibao? Na hawa jamaa hakuna cha nepotism mambo ya shangazi wala mjomba. Kila kitu kiko online ukitimiza masharti yao basi huna shida wanakufanyia kila kitu.
Elimu yao ni nzuri sana kwa kweli na mavyuo mashuhuri kama Harvard, Princeton, Columbia, Yale na Stanford wana program maalum za kusomesha vijana kutoka Afrika. Cha muhimu tu uwahakikishie kuwa utarudi home baada ya kumaliza masomo yako. Ukiwa kwenye mambo ya afya (MD, Public Health, Microbiology...) na Uchumi na nyanja zingine zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja mbona inawezekana kabisa?
Ila kama ni postgraduate hakikisha una angalau first class kwenye Bachelor yako na uwe na barua zako za recommendation ziandikwe vizuri.
Nilishawahi kukaa kwenye selection committees za baadhi ya hawa sponsors naweza kukupa mwongozo wa kiundani kama uko siriazi mjukuu.