Yerusalemu: Kikombe Kinachowalevya Mataifa

Green Beret

JF-Expert Member
Apr 22, 2022
624
986
Jerusalemu Katika Siku za Mwisho
Zekaria 12:2 Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.

3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.

World-Data-Locator-Map-Israel.jpg

Siku ya Jumamosi 7/10/2023 taifa la Israel na dunia nzima kwa ujumla iliamka na Habari za kuwa Israel imevamiwa na magaidi wa Hamas, mpaka leo hii Zaidi ya waisrael elfu 1 wameripotiwa kuuwawa kikatili na wengine Zaidi ya 100 (ikiwamo na wananchi wa mataifa mengine) kuchukuliwa mateka na magaidi wa Hamas na kuwaficha Gaza.

Israel kama nchi nyingine yoyote, kuwa na haki ya kujilinda, imeapa kulitokomeza kundi hilo la kigaidi kwa kuanzisha operesheni ya kulipua miundombinu ya Hamas huko Gaza Pamoja na kujiandaa kuvamia mji wa Gaza kuwatafuta magaidi na kuwatokomeza kabisa.

Kama ilivyo kawaida unapoongelea Israel basi kuna hisia nyingi zinaibuka hasa za kiimani na saa nyingine za kishabiki Zaidi.

Ni ukweli usiopingika kuwa mgogoro wa Israel na Palestina una pande mbili. Ya kimwili na kiroho.

Ndo maana unasikia Operesheni ya Hamas inaitwa ‘Al-Aqsa Floods’ au mafuriko ya Al-aqsa. Al-aqsa ni msikiti uliopo Yerusalem, ni eneo la tatu la utakatifu katika uislamu baada ya eneo la pili la Msikiti wa Al-Masjid an-Nabawi ilipokuwa nyumba ya Mtume Muhammad na eneo la kwanza la Mecca ilipo Kaaba.

Msikiti huu wa Al-aqsa upo eneo ambalo hekalu la Wayahudi lilikuwapo zamani. Pia lipo inaposemekana ndio Mlima Moria ulipo, pale Abrahamu alipotaka kumtoa Isaka sadaka kama wanavoamini wayahudi au Abrahamu alipotaka kumtoa sadaka Ishmael.

Hapa ndipo ilipo siri ya kugombaniwa nchi hii.

Kwa nini Jerusalem?

Endelea kunywa mtori na nyama utazikuta chini!

TAHADHARI:
Moja
- Ujumbe huu sio wa kishabiki bali ni wa kimtazamo wa hali halisi tu kuhusu yanayoendelea sasa na hata huko mbeleni. Ujumbe huu haupo kwa madhumuni ya kumvamia yeyote kihisia au kiimani na endapo hayo yatatokea basi iwe radhi kwani hilo sio dhumuni la andiko hili.

Mbili- Madini yaliyopo katika andiko hili sio ya Watoto wanaokunywa maziwa bali ni ya watu wazima (thabiti) wanaoweza kutafuna nyama, mifupa na hata kula chapati kavu jangwani bila maji!

Tatu: Vyanzo tutakavotumia ni Historia, Biblia, Quran na akili ya kawaida.

Nne: Kuna mambo mengi sana inabidi kuyaongea ili kupata uelewa mzima wa mgogoro huu wa karne hadi karne. Lakini hapa tutaongea machache maana muda na nafasi haitoshi kuyaongea yote.

HISTORIA
Sio mara ya kwanza Israel na Palestina kupigana vita!

images (11).jpeg

Toka tukiwa wadogo tumekuwa tukisikia vita kati ya jamii hizi mbili.

Ila vita hii ya 2023 ni tofauti. Kama unavoona kwenye picha apo juu. Vita za zamani Israel walikua wakipoteza watu wachache sana. Tofauti na sasa wameshapoteza zaidi ya watu 1200+ ukijumuisha na wanajeshi watakaofariki kama wakivamia Gaza kwa majeshi ya ardhi!

Kutokana na Vita za mara kwa mara imepelekea hadi baadhi ya watu kuzoea na kuota sugu za masikio na hisia kila wanaposikia Habari hizi za mashariki ya kati baina ya Israel na Palestina.

Ile hadithi ya kijana mchungi wa kondoo mtukutu aliekua akilia "mbweha, mbweha, mbweha!!!" Na kisha wanakijiji walikuja haraka kumuokoa na kukuta alikua akitania. Siku ilipofika ikawa kweli mbweha kaja alipolia apate msaada wanakijiji walijua anazingua kama siku zote hawakwenda kumsaidia na aliangamia. Usugu huu sio mzuri.

Basi kwa nini imekuwa hivyo?
Kujua sababu ni vizuri kurudi nyuma hadi mwaka 1948 ambako ndipo Taifa la Israel kama unavolijua sasa lilipoundwa.
Ilikuwa 14 Mei 1948,

Tarehe 14 Mei 1948, siku moja kabla ya muda wa Uingereza kumalizika, David Ben-Gurion, kiongozi wa Shirika la Kiyahudi, alitangaza "kuundwa kwa nchi ya Kiyahudi katika Eretz-Israel, itakayojulikana kama Nchi ya Israel." Marejeo pekee katika maandishi ya Tamko kuhusu mipaka ya nchi mpya ni matumizi ya neno Eretz-Israel ("Nchi ya Israel"). Siku inayofuata, majeshi ya nchi nne za Kiarabu - Misri, Syria, Jordan na Iraq - yaliingia sehemu za eneo la Palestina lililokuwa chini ya Uingereza, na kuzindua Vita vya Kiarabu-Kiyahudi vya mwaka 1948; vikosi kutoka Yemen, Morocco, Saudi Arabia na Sudan walijiunga na vita hivyo. Madhumuni ya wazi ya uvamizi huo ilikuwa kuzuia kuundwa kwa nchi ya Kiyahudi mwanzoni, na baadhi ya viongozi wa Kiarabu walizungumza kuhusu "kuwafukuzia Wayahudi baharini".
Baada ya mwaka wa mapigano, kusitishwa kwa mapigano kilitangazwa na mipaka ya muda, inayojulikana kama Mstari wa Kijani, ilianzishwa. Jordan ilijumuisha eneo linalojulikana kama Ukingo wa Magharibi (West Bank), pamoja na Jerusalem Mashariki, na Misri iliiteka Ukanda wa Gaza.

Hapa tunaona kuwa Israel ilizaliwa na vita. Ni kama mtoto wa swala nyikani, huzaliwa na hapo hapo simba humtafuta kumuangamiza,

images (12).jpeg

kwa maana hio basi unakuja msemo kuwa ‘unapoishi nyikani basi haijalishi wewe ni simba au swala kama ukitaka kuishi basi ujue kukimbia Zaidi ya adui yako”

Je, ilikuwaje hadi Israel ikaundwa 1948? Kwani walikuwa wapi siku zote hizo??
Miaka ya 1940 wayahudi wengi walianza kurudi eneo hilo lililokuwa likiitwa Palestine na sababu kubwa ni kuwa wengi walikua wakiishi Ulaya walikua wakitafutwa kuuliwa na Ujerumani ya Hitler (alifanikiwa kuwauwa milioni 6).

Wakati huo Hitler na kundi lake la Nazi Germany walikuwa wakipiga Ulaya nzima.

images (13).jpeg
Walikua wakiipeleka Ulaya mputa mputa kwa kutumia ‘tactics’ zao za kuvamia kwa spidi kubwa, maarufu kama Blitzkrieg , mashambikizi ya ghafla ya ndege za kivita zilizoitwa Luftwaffe na vifaru vya Tiger chini ya jeshi mahiri na katili la Werhmacht na baadae vikosi katili Zaidi yaani kikosi cha SS kilikuwa kikipita kuendeleza unyama ambao Hamas wanaeza wasiwe wamefikia bado!

download.jpeg

Waisrael wengi waliingia nchi ya apo Palestina kama wakimbizi.
Na hapo walipofikia walikua wakiishi hao wapalestina na mataifa mengine.

Lakini kabla ya Vita Ya Pili ya dunia kulikua na Vita ya Kwanza ya dunia ambayo baada ya kuisha Uingereza ilitengeneza mkataba wa Balfour baada ya vita ya 1 ya dunia walipoishinda Ottoman empire iliyokuwa ikitawala
Palestina wakati huo.

Balfour_declaration_unmarked.jpg

Mkataba huo ulikua na nia ya kutengeneza taifa la wayahudi na wapelestina. Kwa maana ya Tangazo la Balfour iliahidi kwamba hakutafanywa jambo lolote linaloweza kudhuru haki za raia na haki za kidini za watu ambao tayari walikuwa wanaishi Palestina na ambao hawakuwa Wayahudi.

Lengo lilikuwa kulinda haki za raia na dini za jamii hizi zisizo za Kiyahudi, hasa Wapalestina.

Kutokana na kutokua wazi hasa tangazo hili halikuweza kufanikiwa kipindi hiko hadi WW2 ilipokwisha.

Na baada ya vita ya 2 ya dunia iliyoanza 1939-1945 na kufikia 1948 ndipo walipogawa Palestina maeneo matatu:

🇮🇱Israel- chini ya waisrael
🇯🇴Gaza- chini ya Misri
West bank - Chini ya Jordan
Jerusalem iligawanya mara mbili. Sehemu moja chini ya Israel na nyingine chini ya Jordan.

israel49.gif
Hapa ndipo picha la mambo yaliyopo sasa linaanza kupata taswira.
Jordan ilibaki na ule msikiti wa Al-aqsa ambao ni sehemu ya tatu takatifu inaaminika kuwa ni mahali ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni kuona maono.

images (14).jpeg
Hapa ndipo lilipokua hekalu la Solomon na baadae la Herode ambalo Waroma waliliharibu mwaka 70AD.

Sasa hivi kumebaki ukuta wa nje ambao wayahudi hawakuruhusiwa kutembelea wakati ipo chini ya Jordan.

images (15).jpeg

Ni hapa hapa mahali ndipo wayahudi wanatarajia kujenga hekalu la III la kuabudu ambalo litakua na nafasi kubwa siku za mwisho wa dunia hii tunayoijua!

Tukirudi katika historia
waarabu wanaozunguka Israel hawakukubali taifa la Israel liwepo na siku moja tu baada ya Israel kuzaliwa waliivamia ilia Israel ilishinda na vita zilitokea zingine.

Vita nyingine iliyo na uhusiaono na hii ya sasa ni ya 1967 au 6 day war ambayo waarabu Misri, Syria na Jordan walipigana na Israel.

Israel alishinda na hivyo kuinganisha kwa mara ya kwanza Jerusalem.
images (16).jpeg
Pia walichukua mamlaka ya Gaza na West bank na Golan Heights yaliyokua chini ya Misri, Jordan na Syria. Na toka siku hiyo hawajayarudisha tena.

Ndio maana mpaka sasa unasikia Hamas na washirika wake Pamoja na mataifa ya kiarabu yote yanataka Israel irudishe maeneo iliyochukua kurudi mipaka ya 1967.

Israel wamekuwa wakituhumiwa kujenga majengo ya makazi sehemu hizo walizochukua na hii inaleta hasira sana kwa waarabu na wapalestina kwa ujumla maana huhisi ardhi yao inachukuliwa. Japo utakumbuka yaliyotokea hapo nyuma mpaka Israel akayamiliki.

Pia kuna wapalestina waliokua wakiishi Israel wakati huo na walikimbilia Gaza na mpaka wa leo wengi bado wapo Gaza.

-------------
Lakini pia Hamas wamevamia sasa hivi maana Israel wanafanya kampeni kuingia mikataba na waarabu ya amani na mashirikiano. Hata wiki chache zilizopita Netanyahu alisifu sana huo mkakati alipokua akitoa hotuba yake UN.

Sasa Wako kwenye mchakato wa kuingia mkataba na Saudi Arabia lakini Iran ambaye anaapa siku zote kuitokomeza Israel kwenye uso wa dunia hataki hilo litokee na Iran ndo wanadaiwa kusapoti Hamas ndo maana wamevamia sasa.

Maana jinsi Israel anavojibu mapigo ndipo hio oparesheni yao na Saudia na wengine zitafeli.
Inaezekana kwa unyama waliokua nao Hamas walitaka haya yote yatokee.

Kadiri Israel anavoshambulia Gaza ndivyo wananchi watakufa wengi nan do jinsi Israel anavoeza kuonekana mbaya hasa kwa mataifa ya waarabu ambao watalazimika kumvamia ili kuokoa wenzao wapalestina. Iwapo jambo hili litatokea basi hakika, hakika, hakika tambua kuwa utakua unaona unabii ukitimia mbele ya macho yako. Na uonapo hivyo basi fanya hima uweke mambo yako saw ana Aliyekuumba.

Mahmoud Abbas ambaye ndo alikuwa rais wa Palestina alikua akifanya mazungumzo na Saudi Arabia na Israel pia katika hio mikataba lakini hawapatani na Hamas pia. Ndo maaana Hamas wameamua kutumia nguvu ili ajenda yao ibakie kutokua na ushirikiano wowote na Israel.

Mpaka sasa Hamas wamefanikiwa lengo lao la kusitisha normalization Israel iliyokua iktafuta na Saudi Arabia kwani mazungumzo yamekwama.

Hamas ni kina nani?
Katiba ya Hamas inasema

"Katiba inasema kwamba 'mapambano yetu dhidi ya Wayahudi ni makubwa sana na ya kutiliwa maanani sana' na inaita kwa hatimaye kuundwa kwa Dola la Kiislamu katika Palestina, badala ya Israeli na maeneo ya Palestina, na kufuta au kuvunja Israel. Inasisitiza umuhimu wa jihad, ikisema katika kifungu cha 13,

'Hakuna suluhisho la swali la Kipalestina isipokuwa kupitia Jihad. Mashauri, mapendekezo, na mikutano ya kimataifa ni muda na jitihada zisizo na maana."

Hizo ni sehemu za katiba yao. Hivyo wana mrengo wa bunduki na ugaidi tu.

Kupigana na watu kama hao ni ngumu sana.

Kama Israel itaingia Gaza basi tunaeza kushuhudia another battle of Stalingrad. Yaan mapigano ya Stalingrad

battle-stalingrad-gettyimages-107759352.jpg
Hii ni vita ngumu na ya kinyama iliyopiganwa na warusi na wanazi wa ujerumani katika ardhi ya urusi kwenye vita ya pili ya dunia. Ilipiganwa wakati wa barudi kali la Urusi. Na ilikua mara ya kwanza Ujerumani ilishindwa battle WW2.

images (19).jpeg

Ni urban warfare. Vita vya mjini. Unaingia jengo baada ya jengo. Kupigana mkono kwa mkono na hapo kuna wadunguaji yaani snipers na mitego ya mabomu kama IFDs na mengineyo ambayo yatamfanya mtu legelege aite mmaa

images (18).jpeg
-------------

Pia jambo kushangaza ni kuwa Israel wana sera ya 'We dont negotiate with terrorists' ila Hamas wameteka zaidi ya waisrael 100 na wanaeza kudai waachiliwe kwa kupewa wafungwa wao zaidi ya elfu na waliopo magereza ya Israel.

Sasa wanadai kuwauwa kila Israel inaposhambulia Gaza.
Kama Hamas wakifanya haya, na endapo watafanya basi watafanya kwa kurekodi na kutangaza kukata vichwa watu kama ilivokuwa ISIS.

Basi Israel atapata presha kubwa sana kwani ndugu wa mateka watakua na lawama kwa serikali ya Netanyahu kushindwa kuwaokoa wapendwa wao.

Hio inaitwa double-whammy. Hakika Hamas ni wahuni lakini mpango huu waliusuka kiufundi japo kwa uharamia mkubwa kupitiliza.

Pia Benjamin Netanyahu PM wa Israel ana historia mbaya na magaidi maana miaka ya 70 magaidi waliteka ndege iliyokuwa na Waisrael na kuipeleka Uganda ya Idd Amin.

Walitaka Palestina iwe ‘huru’ na pia kutaka fedha na wafungwa kuachiliwa.

Israel walifanya oparesheni ya kikomando na komando mmojawapo alikua ni kaka yake Benjamin Netanyahu alikuwa akiitwa Yonatan Netanyahu na ndie mwanajeshi pekee alikufa kwenye hio oparesheni ya Uganda. Kuna muvi moja kali sana ‘Raid in Entebbe’, wakongwe wanaijua hii, ilielezea oparesheni Nightfall kama ilivoitwa na jeshi la Israel.

images (20).jpeg
Katika vita ya sasa Israel wanaoenakana kuchukua msimamo tofauti kwani wanasema wataendelea kshambulia targets za Hamas hata kama mateka wataumia hawataacha.

Hii inaonyesha hasira kali aliyonayo muisrael na siku za mbele hali inaeza kuwa ngumu sana kwa watu wa Israel, Palestina na hata dunia nzima kwa ujumla.
---------
Ukitaka kutawala dunia (kiroho na hata kimwili) unaanzia Jerusalem. (Kama unabisha jiulize why US yupo bega kwa bega na Israel??!!)

Hakuna katika historia mji uliowahi kupiganiwa Zaidi ya Jerusalem, sio Washington, sio London, sio Moscow, sio Paris (hakuna anayehitaji kunguni!), sio Beijing, Sio Tehran.

Jerusalem imekuwa ikipiganiwa toka enzi na enzi n ahata sasa vita yote hii ni kuhusu Jerusalem.

Jaribu kusikiliza matakwa ya pande zote mbili.
Israel: Anataka taifa la Israel, ikiwa Jerusalem ndio mji wake mkuu.
Palestina: Anataka taifa la Palestina ikiwa Jerusalem ndio mji wake mkuu.
Ndo maana ni ngumu sana hawa jamaa wawili kupatana maana wanachotaka kila mtu ndio anachotaka. Na sababu ya kutaka mji huu ni huo mlima wa hekalu na msikiti wa Al-aqsa. Kuna nguvu ya kiroho imejificha hapo. Ila kwa mwenye macho ipo wazi!
Waromani Catholic wenyewe wana sehemu yao hapo Jerusalem. Japo hili ni jambo la kujadili siku nyingine.

Kiroho
Israel ni taifa la Mungu. Alilichagua toka siku zile za Babeli. Wapo watakaobisha na ni sawa kubisha ila hapa tutangalia Biblia inasemaje. Kwa wasioamini Biblia haitashangaza kukataa. Ila kama unaamini Biblia basi endelea kunywa mtori.

Mungu alilichagua taifa la Israel toka siku zile za Babeli.
images (21).jpeg

Utakumbuka pale ndipo Mungu aliwatawanya mataifa.

Sasa wanazuoni wa Biblia wanasema kuna mengi yalitokea zaidi ya lugha kugawanywa. Yaliyotokea ni kuwa mataifa mengine yote walipewa malaika au waangalizi “Watchers” kuyasimamia ila Mungu aliichagua Israel iwe ya kwake mwenyewe.

Hawa watchers waliopewa mataifa mengine waliasi na kuanza kutaka kuabudiwa wao badal ya Mungu wa kweli, nan do maana unaona dunia nzima ya zamani kasoro Israel walikuwa wanaabudu miungu, ni Israel pekee ilikuwa na Mungu mmoja.

Ukitaka kupata picha kidogo yah ii issue kumbuka Malaika Gabriel alimuambiaje Daniel tunasoma Daniel 10: 12 Ndipo akaniambia, Usiogope, Danielii; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

Watchers hawa bado wapo duniani na wanashikilia maeneo mbalimbali duniani na kufanya maovu yao.

Ndo maana hata katika Agano Jipya, Paulo anatungata sikio na kutupa mbinu za kivita kama Roho Mtakatiu alivomuonyesha ya kuwa;

Waefeso 6:10
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake.

11Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

images (2).png
Hao wakuu wa giza ndio wanatakiwa kupigwa pia kabla ya kudili na mapepo wabaya. Hao ndio maadui zetu!

(Hii issue ya watchers ni mada ndefu pia inayohitaji muda na nafasi kuijadili kwa kina, ila kwa sasa dokezo hilo latosha)

Turudi kwenye mada kuu
Kumbukumbu la Torati 32:8-9
Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake, kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake.

Na kuanzia hapo alipanga kupitia Israel awapate watu wote duniani kuwaleta kwake. Kuwaleta kwake kivipi?

Kupitia Yesu Kristo, dunia nzima inabarikiwa kwani kila amuaminiye basi hasira na adhabu ya Mungu juu ya dhambi inaondoka na huyu muamini anabarikiwa haijalishi ni myahudi au mtu wa mataifa yaani mimi na wewe.

Wote tuna uwezo sasa wa kuongea na Mungu mwenyewe na kuwa na uhusiano naye.

Waisrael kama binadamu wengine ni watu wabishi walimkataa Yesu Kristo kama Masihi wa Bwana na mwishowe walitawanyika.

Hata sasa hivi waisrael wengi sio wakristo. Wengi ni wayahudi (dini ya Judaism ambayo wanaamini Zaidi agano la kale na traditions nyingine za kiyahudi) na wengine ni atheists.

Lakini Mungu yupo nao bado.

Lakini kama kipindi walipokua watumwa Misri miaka 400, Mungu aliwakumbuka huko kwenye mataifa na aliwarudisha Kanani au nchi ya ahadi, Palestina au Israel.

Lakini 'adui' alishaweka mikakati yake.

Ukitaka kujua kuwa Mungu yupo nao bado. Kuna tabiri ziliandikwa Biblia kuhusu kurudi kwa Israel miaka ya baadae ambayo ndio hio 1948

Isaya 11:12
Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa, kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa, kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa, na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.

Utakumbuka kuanzia mwaka 70AD waroma walipoteketeza Israel na kuvunja hekalu waisrael waliishi utumwani na ugenini na wengi walikua Ulaya.

Mpaka WW2 Hitler na wenzake wakaawalaumu kuwa ndo chanzo cha mabaya na kuleta Final Solution yaani kuwauwa wote na ndiyo iliyopelekea Holocaust.
Hivyo kila mahali Ujerumani ilipofika Ulaya walikua na kikosi chao cha SS chenye kazi ya kuwakusanya wayahudi na kuwauwa kimkakati aidha kwa kuwauwa kwa sumu ya gesi au kuwanyima chakula kuwafanyisha kazi au majaribio ya kisayansi kwenye concentration camps nk. Kama ulishawai kuona picha linaitwa ‘Escape form Sobibo” utakuwa unaelewe hizi codes.
images (22).jpeg

. Hivyo ilikua ni mateso makubwa sana na wajanja na wenye bahati walikimbia ujerumani na ulaya kuanzia miaka ya 30s (maana Hitler na wanazi walishaanza kuonyesha dalili za kudondosha ute kama simba anavotamani swala mawindoni) na wengi zaidi miaka 40s wakati na baada ya WW2 maelfu kwa maelfu walikimbilia Israel na wengine US kama kina Einstein na wengineo.

Hivyo walikusanywa kutoka pembe za dunia kama nabii Isaya alivyotabiri.

Mstari mwingine unasema

Isaya 66:8
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.

Unavoona apo katika uchungu mwingi wa Israel kuteswa na kuuliwa watu milioni 6 walizaliwa siku moja hiyo ya 14, Mei 1948. Kuanzia hapo ndo Israel tunayoijua sasa.

Jambo lingine kushangaza na la kufahamu ni kuwa Gaza imekua mwiba kwa Israel toka miaka ya kale. Ndipo Samson alipotobolewa macho na kutumikishwa na Wafilisti wa zama hizo.

Mwisho wa siku alijiua na kufa nao zaidi ya 3000 lakini mpaka leo ni kikwazo kikubwa.

_____________
Okay, Mwanzo hio ardhi hawakuwa wanakaa wayahudi au Israel. Ilikua ikiitwa Kanani.

Kwa nini Mungu aliwapa Kanani waisrael?

Utakumbuka Israel alikua Yakobo. Yakobo alitoka kwa Isaka na Isaka alitoka kwa Ibrahim.

Ibrahim alitokea Ur ya wakaldayo. Ambayo wanasema ni Iraq ya leo.
Uzao wa Ibrahim unaendelea nyuma hadi kwa Adam.

Lakini Mungu alimuita Ibrahim ampe ardhi ya Kanani kwa sababu waliokaa pale walikua waasi kupitiliza na ardhi ile iliwakataa!

Walawi 18:24-28
“Msijitie najisi kwa kufanya mambo hayo kwani kwa sababu ya mambo hayo nayafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile wao hufanya hayo na kujitia najisi. Nchi yao ilitiwa unajisi nami nikaiadhibu, nayo ikawakataa wakazi wake. Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. Machukizo hayo waliyafanya watu waliokaa katika nchi ya Kanaani kabla yenu, nao wakaitia nchi unajisi. Basi, nyinyi msifanye mambo hayo, la sivyo nchi hiyo itawatapika kama ilivyolitapika taifa lililokuwa kabla yenu.

Walifanya mambo gani hadi nchi ikawatapika?

Ukisoma hio chapter utaona jamaa walikua wakilala na wazazi wao, wajukuu zao, ndugu zao, shangazi, mkwe, shemeji, dada wa mke, walikua wakitoa watoto wao sadaka ya kuchomwa kwa mungu Moleki, mahusiano ya jinsia moja yaani usagaji na ushoga. Haya mambo hayakuanza leo. Jambo moja la kushangaza ni kuwa leo hii kuna baadhi ya watu hasa wanaume wanapenda sana kutumia neno ‘msenge’ katika maongezi ya kawaida au kutukana wengine.

Ni neno maarufu sana katika vinywa vya ‘wasela’ jambo hili ni la kushangaza sana hasa ukizingatia vitendo hivi vinashamiri huko duniani na kuleta taharuki hata katika jamii za kiafrika popote linapotokea. Basi watu na wachunge midomo yao!

Hayo ndo mambo yaliyofanya nchi iwatapike wakaanani na Mungu kuwapa nchi Israel.

Kuna wakati Israel ilifanya mambo kama hayo na wao waliondolewa pia.

------------
Mungu alishaamua hakuna anayeeza kuingamiiza Israel.
Maana alishaapa haya👇 (pia kumbuka kuwa kama ni Taifa la Mungu sio kuwa wao ndo hawapigwi hawafanyi makosa au ni wa kutetea pale wanapokesea. Kama ilivyo katika historia Israel imemkosea Mungu mara nyingi na mara nyingi walipigwa na kuipeleka utumwani na wameteseka vilivyo. Shida ni kuwa wengi walikua na kiburinkwa nafasi hio na kushindwa kuelewa kuwa Mungu aliwachagua wao ili baadaye wote watakaomuamini wawe sehemu ya Taifa lake pia. Japo ipo siku watakuja kuamini yote hayo)

*Mwanzo 12:2-3 *
Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka. Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani. Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Ndo maana unaona Haman alitaka kuwaangamiza enzi za Farao alitaka kuwaangamiza akaishia kumezwa na bahari, Haman alisuka mpango wa kuwaua wayahudi wote, Esther alitumiwa na Mungu kuwaokoa, Ilikuja kipindi cha Tauni au Black death Ulaya na walilaumiwa Waisrael wakauwawa wengi sana, Hitler na wanazi hawapo sasa ila Israel ipo na wengine wengi walijaribu ila walishindwa.

Hata Mpinga Kristo (,antichrist,) atajaribu na itabaki kidogo afanikiwe ila Mungu mwenyewe ataingilia kati wakati huo sio US+washirika tena?

Kama ukiona picha na video za leo ndivyo itakavokua hizo siku za mpingakristo.

Kwa jinsi vita hii inavoendelea sio ajabu ikasambaa Kwenda nchi nyingine pia:

Scenario kama hii inaeza kutokea:
Kadiri Israel anavoshambulia Gaza, watu watafariki Hezbollah wanaeza kuanza kushambulia upande wa pili, Hezbollah wanaadhiliwa na Iran. Iran anatuhumiwa kufadhili uvamizi wa Hamas. Iran alishaapa ataiondoa Israel kwenye uso wa dunia. Israel anaeza kuamua kumvamia Iran na Hezbollah.

Akipigwa sana (maana inasemekana Hezbollah kajipanga vilivyo) anaeza kuomba msaada kwa Marekani. Bwana US akiingia ni lipua lipua mpaka Lebanon na sehemu kadhaa. Waarabu wengine wanaeza kasirika na kumshukia Israel.

Lakini pia rafiki yake Iran ni Russia, na China ambao wanaeza kulazimika kumsaidia kama akianza kupigwa na Israel na Marekani na washirika wake. Kinachofuata hapo ni WW3 na mwishowe mpinga Kristo.

Anyway haya yote ni speculations lakini ni muhimu kufatilia kwa ukaribu mambo yanayotokea Israel kwani hio ndio saa ya Mungu.

Utabiri huu unaeza kutokea endapo hayo hapo juu yatakuwa hivyo.

Zekaria 14:1-4
Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Mwenyezi-Mungu atayakusanya mataifa yote ili kuushambulia mji wa Yerusalemu. Mji utatekwa, nyumba zenu zitatekwa nyara, na wanawake wenu watanajisiwa. Nusu ya wakazi wa mji watapelekwa uhamishoni, lakini nusu itakayosalia haitachukuliwa nje ya mji. Kisha Mwenyezi-Mungu atatoka na kuyapiga vita mataifa hayo, kama afanyavyo daima siku za vita.
------
Kuna vita nyingi zinatokea kati ya Israel na Palestina. Hii nayo ni ya kuangalia kwa makini.
Kama wewe ni mkristo basi kumbuka haya:

Mathayo 24:4
Yesu akawajibu, “Angalieni, mtu asiwadanganye. 5Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo, nao watawadanganya wengi. 6Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita,angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 7Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu. 11Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. 12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 13Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.

Luka 21: “Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni
utakuwa kama wanawali kumi waliochukua
taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano
wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa
wenye busara. 3Wale wapumbavu walichukua
taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,
4
lakini wale wenye busara walichukua taa zao na
mafuta ya akiba kwenye vyombo. 5Bwana arusi
alipokawia
kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
6
“Usiku wa manane pakawa na kelele:
‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje
mkamlaki!’
7
“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na
kuzitengeneza taa zao. 8Wale wapumbavu
wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni
mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika.’
9
“Lakini wale wenye busara wakawajibu,
‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali
mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.
10“Nao walipokuwa wakienda kununua
mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali
waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye
kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
11“Baadaye wale wanawali wengine nao
wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie
mlango!’
12“Lakini yeye bwana arusi akawajibu,
‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
13“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui
siku wala saa.’’

Ufunuo 22: 20Yeye anayeshuhudia mambo haya
asema, “Naam, naja upesi!’’
Amen. Njoo Bwana Yesu.
21Neema ya Bwana Yesu iwe na watakatifu
wote. Amen.
 
Tumezoea kufundishwa kuhusu Watoto wa Ibrahim.

Mara nyingi historia inazungumzia Isaka na Ismahili. Tunaambiwa Isaka ndo baba wa Wayahudi. Ismaili baba wa Waarabu.

Biblia imetuambia kuwa Baada ya mke wa Ibrahimu kufariki (Sarah) Ibrahim alioa mwanamke mwengine anayeitwa Ketura na akazaa naye Watoto 6 Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Hatujaambiwa historia ya Hawa Watoto wake wengine.

Je, unajua hawa Watoto wake wengine ndo baba wa mataifa haya?

Zimradi baba wa taifa la Warusi
Medani baba wa taifa la Wachina
Ishbaki baba wa taifa la Wahindi
Yokshani: baba wa taifa la Wajerumani
Shua baba wa wa taifa la Waingereza
Midiani baba wa taifa la Waethiopia
 
Kwa utaalamu wangu wa migogoro, naamini taifa bandia la israel liliundwa baada ya kugunduliwa mafuta uarabuni ili kulipa nguvu na kuwatisha waarabu na kuwalazimisha ima kununua silaha toka magharibi au kutafuta ulinzi toka kule kama ilivyotokea. Zaidi ya hapo, sijui kwanini mataifa yanachachawa na kugeuka vipofu hata kwenye mambo ambayo hata ndege anaweza kusuluhisha. Je zaidi ya biashara ya mafuta na silaha kunani? Je hawa akina Niite nyau wazungu wanaojiita waarabu ndiyo wanaohangaisha wazungu wenzao wasimalizwe na waarabu?
 
Hii inakusaidia nini wewe kabla ya sisi? Mataifa ya kisasa na ngano wapi na wapi au unatafuta jinsi ya kuyahalalisha au uonekana umepiga skuli isiyo na msaada kwako?
 
Kuna mmoja hayupo hapo baba wa Taifa la USA.
 
Jerusalemu Katika Siku za Mwisho
Zekaria 12:2 Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.

3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.

Siku ya Jumamosi 7/10/2023 taifa la Israel na dunia nzima kwa ujumla iliamka na Habari za kuwa Israel imevamiwa na magaidi wa Hamas, mpaka leo hii Zaidi ya waisrael elfu 1 wameripotiwa kuuwawa kikatili na wengine Zaidi ya 100 (ikiwamo na wananchi wa mataifa mengine) kuchukuliwa mateka na magaidi wa Hamas na kuwaficha Gaza.

Israel kama nchi nyingine yoyote, kuwa na haki ya kujilinda, imeapa kulitokomeza kundi hilo la kigaidi kwa kuanzisha operesheni ya kulipua miundombinu ya Hamas huko Gaza Pamoja na kujiandaa kuvamia mji wa Gaza kuwatafuta magaidi na kuwatokomeza kabisa.

Kama ilivyo kawaida unapoongelea Israel basi kuna hisia nyingi zinaibuka hasa za kiimani na saa nyingine za kishabiki Zaidi.

Ni ukweli usiopingika kuwa mgogoro wa Israel na Palestina una pande mbili. Ya kimwili na kiroho.

Ndo maana unasikia Operesheni ya Hamas inaitwa ‘Al-Aqsa Floods’ au mafuriko ya Al-aqsa. Al-aqsa ni msikiti uliopo Yerusalem, ni eneo la tatu la utakatifu katika uislamu baada ya eneo la pili la Msikiti wa Al-Masjid an-Nabawi ilipokuwa nyumba ya Mtume Muhammad na eneo la kwanza la Mecca ilipo Kaaba.

Msikiti huu wa Al-aqsa upo eneo ambalo hekalu la Wayahudi lilikuwapo zamani. Pia lipo inaposemekana ndio Mlima Moria ulipo, pale Abrahamu alipotaka kumtoa Isaka sadaka kama wanavoamini wayahudi au Abrahamu alipotaka kumtoa sadaka Ishmael.

Hapa ndipo ilipo siri ya kugombaniwa nchi hii.

Kwa nini Jerusalem?

Endelea kunywa mtori na nyama utazikuta chini!

TAHADHARI:
Moja
- Ujumbe huu sio wa kishabiki bali ni wa kimtazamo wa hali halisi tu kuhusu yanayoendelea sasa na hata huko mbeleni. Ujumbe huu haupo kwa madhumuni ya kumvamia yeyote kihisia au kiimani na endapo hayo yatatokea basi iwe radhi kwani hilo sio dhumuni la andiko hili.

Mbili- Madini yaliyopo katika andiko hili sio ya Watoto wanaokunywa maziwa bali ni ya watu wazima (thabiti) wanaoweza kutafuna nyama, mifupa na hata bumunda lililo kavu na kula chapati kavu jangwani bila maji!

Tatu: Vyanzo tutakavotumia ni Historia, Biblia, Quran na akili ya kawaida.

Nne: Kuna mambo mengi sana inabidi kuyaongea ili kupata uelewa mzima wa mgogoro huu wa karne hadi karne. Lakini hapa tutaongea machache maana muda na nafasi haitoshi kuyaongea yote.

HISTORIA
Sio mara ya kwanza Israel na Palestina kupigana vita!

Toka tukiwa wadogo tumekuwa tukisikia vita kati ya jamii hizi mbili.

Ila vita hii ya 2023 ni tofauti. Kama unavoona kwenye picha apo juu. Vita za zamani Israel walikua wakipoteza watu wachache sana. Tofauti na sasa wameshapoteza zaidi ya watu 1200+ ukijumuisha na wanajeshi watakaofariki kama wakivamia Gaza kwa majeshi ya ardhi!

Kutokana na Vita za mara kwa mara imepelekea hadi baadhi ya watu kuzoea na kuota sugu za masikio na hisia kila wanaposikia Habari hizi za mashariki ya kati baina ya Israel na Palestina.

Ile hadithi ya kijana mchungi wa kondoo mtukutu aliekua akilia "mbweha, mbweha, mbweha!!!" Na kisha wanakijiji walikuja haraka kumuokoa na kukuta alikua akitania. Siku ilipofika ikawa kweli mbweha kaja alipolia apate msaada wanakijiji walijua anazingua kama siku zote hawakwenda kumsaidia na aliangamia. Usugu huu sio mzuri.

Basi kwa nini imekuwa hivyo?
Kujua sababu ni vizuri kurudi nyuma hadi mwaka 1948 ambako ndipo Taifa la Israel kama unavolijua sasa lilipoundwa.
Ilikuwa 14 Mei 1948,

Tarehe 14 Mei 1948, siku moja kabla ya muda wa Uingereza kumalizika, David Ben-Gurion, kiongozi wa Shirika la Kiyahudi, alitangaza "kuundwa kwa nchi ya Kiyahudi katika Eretz-Israel, itakayojulikana kama Nchi ya Israel." Marejeo pekee katika maandishi ya Tamko kuhusu mipaka ya nchi mpya ni matumizi ya neno Eretz-Israel ("Nchi ya Israel"). Siku inayofuata, majeshi ya nchi nne za Kiarabu - Misri, Syria, Jordan na Iraq - yaliingia sehemu za eneo la Palestina lililokuwa chini ya Uingereza, na kuzindua Vita vya Kiarabu-Kiyahudi vya mwaka 1948; vikosi kutoka Yemen, Morocco, Saudi Arabia na Sudan walijiunga na vita hivyo. Madhumuni ya wazi ya uvamizi huo ilikuwa kuzuia kuundwa kwa nchi ya Kiyahudi mwanzoni, na baadhi ya viongozi wa Kiarabu walizungumza kuhusu "kuwafukuzia Wayahudi baharini".
Baada ya mwaka wa mapigano, kusitishwa kwa mapigano kilitangazwa na mipaka ya muda, inayojulikana kama Mstari wa Kijani, ilianzishwa. Jordan ilijumuisha eneo linalojulikana kama Ukingo wa Magharibi (West Bank), pamoja na Jerusalem Mashariki, na Misri iliiteka Ukanda wa Gaza.

Hapa tunaona kuwa Israel ilizaliwa na vita. Ni kama mtoto wa swala nyikani, huzaliwa na hapo hapo simba humtafuta kumuangamiza,

kwa maana hio basi unakuja msemo kuwa ‘unapoishi nyikani basi haijalishi wewe ni simba au swala kama ukitaka kuishi basi ujue kukimbia Zaidi ya adui yako”

Je, ilikuwaje hadi Israel ikaundwa 1948? Kwani walikuwa wapi siku zote hizo??
Miaka ya 1940 wayahudi wengi walianza kurudi eneo hilo lililokuwa likiitwa Palestine na sababu kubwa ni kuwa wengi walikua wakiishi Ulaya walikua wakitafutwa kuuliwa na Ujerumani ya Hitler (alifanikiwa kuwauwa milioni 6).

Wakati huo Hitler na kundi lake la Nazi Germany walikuwa wakipiga Ulaya nzima.

Walikua wakiipeleka Ulaya mputa mputa kwa kutumia ‘tactics’ zao za kuvamia kwa spidi kubwa, maarufu kama Blitzkrieg , mashambikizi ya ghafla ya ndege za kivita zilizoitwa Luftwaffe na vifaru vya Tiger chini ya jeshi mahiri na katili la Werhmacht na baadae vikosi katili Zaidi yaani kikosi cha SS kilikuwa kikipita kuendeleza unyama ambao Hamas wanaeza wasiwe wamefikia bado!

Waisrael wengi waliingia nchi ya apo Palestina kama wakimbizi.
Na hapo walipofikia walikua wakiishi hao wapalestina na mataifa mengine.

Lakini kabla ya Vita Ya Pili ya dunia kulikua na Vita ya Kwanza ya dunia ambayo baada ya kuisha Uingereza ilitengeneza mkataba wa Balfour baada ya vita ya 1 ya dunia walipoishinda Ottoman empire iliyokuwa ikitawala
Palestina wakati huo.

Mkataba huo ulikua na nia ya kutengeneza taifa la wayahudi na wapelestina. Kwa maana ya Tangazo la Balfour iliahidi kwamba hakutafanywa jambo lolote linaloweza kudhuru haki za raia na haki za kidini za watu ambao tayari walikuwa wanaishi Palestina na ambao hawakuwa Wayahudi.

Lengo lilikuwa kulinda haki za raia na dini za jamii hizi zisizo za Kiyahudi, hasa Wapalestina.

Kutokana na kutokua wazi hasa tangazo hili halikuweza kufanikiwa kipindi hiko hadi WW2 ilipokwisha.

Na baada ya vita ya 2 ya dunia iliyoanza 1939-1945 na kufikia 1948 ndipo walipogawa Palestina maeneo matatu:

🇮🇱Israel- chini ya waisrael
🇯🇴Gaza- chini ya Misri
West bank - Chini ya Jordan
Jerusalem iligawanya mara mbili. Sehemu moja chini ya Israel na nyingine chini ya Jordan.

Hapa ndipo picha la mambo yaliyopo sasa linaanza kupata taswira.
Jordan ilibaki na ule msikiti wa Al-aqsa ambao ni sehemu ya tatu takatifu inaaminika kuwa ni mahali ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni kuona maono.

Hapa ndipo lilipokua hekalu la Solomon na baadae la Herode ambalo Waroma waliliharibu mwaka 70AD.

Sasa hivi kumebaki ukuta wa nje ambao wayahudi hawakuruhusiwa kutembelea wakati ipo chini ya Jordan.

Ni hapa hapa mahali ndipo wayahudi wanatarajia kujenga hekalu la III la kuabudu ambalo litakua na nafasi kubwa siku za mwisho wa dunia hii tunayoijua!

Tukirudi katika historia
waarabu wanaozunguka Israel hawakukubali taifa la Israel liwepo na siku moja tu baada ya Israel kuzaliwa waliivamia ilia Israel ilishinda na vita zilitokea zingine.

Vita nyingine iliyo na uhusiaono na hii ya sasa ni ya 1967 au 6 day war ambayo waarabu Misri, Syria na Jordan walipigana na Israel.

Israel alishinda na hivyo kuinganisha kwa mara ya kwanza Jerusalem.
Pia walichukua mamlaka ya Gaza na West bank na Golan Heights yaliyokua chini ya Misri, Jordan na Syria. Na toka siku hiyo hawajayarudisha tena.

Ndio maana mpaka sasa unasikia Hamas na washirika wake Pamoja na mataifa ya kiarabu yote yanataka Israel irudishe maeneo iliyochukua kurudi mipaka ya 1967.

Israel wamekuwa wakituhumiwa kujenga majengo ya makazi sehemu hizo walizochukua na hii inaleta hasira sana kwa waarabu na wapalestina kwa ujumla maana huhisi ardhi yao inachukuliwa. Japo utakumbuka yaliyotokea hapo nyuma mpaka Israel akayamiliki.

Pia kuna wapalestina waliokua wakiishi Israel wakati huo na walikimbilia Gaza na mpaka wa leo wengi bado wapo Gaza.

-------------
Lakini pia Hamas wamevamia sasa hivi maana Israel wanafanya kampeni kuingia mikataba na waarabu ya amani na mashirikiano. Hata wiki chache zilizopita Netanyahu alisifu sana huo mkakati alipokua akitoa hotuba yake UN.

Sasa Wako kwenye mchakato wa kuingia mkataba na Saudi Arabia lakini Iran ambaye anaapa siku zote kuitokomeza Israel kwenye uso wa dunia hataki hilo litokee na Iran ndo wanadaiwa kusapoti Hamas ndo maana wamevamia sasa.

Maana jinsi Israel anavojibu mapigo ndipo hio oparesheni yao na Saudia na wengine zitafeli.
Inaezekana kwa unyama waliokua nao Hamas walitaka haya yote yatokee.

Kadiri Israel anavoshambulia Gaza ndivyo wananchi watakufa wengi nan do jinsi Israel anavoeza kuonekana mbaya hasa kwa mataifa ya waarabu ambao watalazimika kumvamia ili kuokoa wenzao wapalestina. Iwapo jambo hili litatokea basi hakika, hakika, hakika tambua kuwa utakua unaona unabii ukitimia mbele ya macho yako. Na uonapo hivyo basi fanya hima uweke mambo yako saw ana Aliyekuumba.

Mahmoud Abbas ambaye ndo alikuwa rais wa Palestina alikua akifanya mazungumzo na Saudi Arabia na Israel pia katika hio mikataba lakini hawapatani na Hamas pia. Ndo maaana Hamas wameamua kutumia nguvu ili ajenda yao ibakie kutokua na ushirikiano wowote na Israel.

Mpaka sasa Hamas wamefanikiwa lengo lao la kusitisha normalization Israel iliyokua iktafuta na Saudi Arabia kwani mazungumzo yamekwama.

Hamas ni kina nani?
Katiba ya Hamas inasema

"Katiba inasema kwamba 'mapambano yetu dhidi ya Wayahudi ni makubwa sana na ya kutiliwa maanani sana' na inaita kwa hatimaye kuundwa kwa Dola la Kiislamu katika Palestina, badala ya Israeli na maeneo ya Palestina, na kufuta au kuvunja Israel. Inasisitiza umuhimu wa jihad, ikisema katika kifungu cha 13,

'Hakuna suluhisho la swali la Kipalestina isipokuwa kupitia Jihad. Mashauri, mapendekezo, na mikutano ya kimataifa ni muda na jitihada zisizo na maana."

Hizo ni sehemu za katiba yao. Hivyo wana mrengo wa bunduki na ugaidi tu.

Kupigana na watu kama hao ni ngumu sana.

Kama Israel itaingia Gaza basi tunaeza kushuhudia another battle of Stalingrad. Yaan mapigano ya Stalingrad

Hii ni vita ngumu na ya kinyama iliyopiganwa na warusi na wanazi wa ujerumani katika ardhi ya urusi kwenye vita ya pili ya dunia. Ilipiganwa wakati wa barudi kali la Urusi. Na ilikua mara ya kwanza Ujerumani ilishindwa battle WW2.

Ni urban warfare. Vita vya mjini. Unaingia jengo baada ya jengo. Kupigana mkono kwa mkono na hapo kuna wadunguaji yaani snipers na mitego ya mabomu kama IFDs na mengineyo ambayo yatamfanya mtu legelege aite mmaa

-------------

Pia jambo kushangaza ni kuwa Israel wana sera ya 'We dont negotiate with terrorists' ila Hamas wameteka zaidi ya waisrael 100 na wanaeza kudai waachiliwe kwa kupewa wafungwa wao zaidi ya elfu na waliopo magereza ya Israel.

Sasa wanadai kuwauwa kila Israel inaposhambulia Gaza.
Kama Hamas wakifanya haya, na endapo watafanya basi watafanya kwa kurekodi na kutangaza kukata vichwa watu kama ilivokuwa ISIS.

Basi Israel atapata presha kubwa sana kwani ndugu wa mateka watakua na lawama kwa serikali ya Netanyahu kushindwa kuwaokoa wapendwa wao.

Hio inaitwa double-whammy. Hakika Hamas ni wahuni lakini mpango huu waliusuka kiufundi japo kwa uharamia mkubwa kupitiliza.

Pia Benjamin Netanyahu PM wa Israel ana historia mbaya na magaidi maana miaka ya 70 magaidi waliteka ndege iliyokuwa na Waisrael na kuipeleka Uganda ya Idd Amin.

Walitaka Palestina iwe ‘huru’ na pia kutaka fedha na wafungwa kuachiliwa.

Israel walifanya oparesheni ya kikomando na komando mmojawapo alikua ni kaka yake Benjamin Netanyahu alikuwa akiitwa Yonatan Netanyahu na ndie mwanajeshi pekee alikufa kwenye hio oparesheni ya Uganda. Kuna muvi moja kali sana ‘Raid in Entebbe’, wakongwe wanaijua hii, ilielezea oparesheni Nightfall kama ilivoitwa na jeshi la Israel.

Katika vita ya sasa Israel wanaoenakana kuchukua msimamo tofauti kwani wanasema wataendelea kshambulia targets za Hamas hata kama mateka wataumia hawataacha.

Hii inaonyesha hasira kali aliyonayo muisrael na siku za mbele hali inaeza kuwa ngumu sana kwa watu wa Israel, Palestina na hata dunia nzima kwa ujumla.
---------
Ukitaka kutawala dunia (kiroho na hata kimwili) unaanzia Jerusalem. (Kama unabisha jiulize why US yupo bega kwa bega na Israel??!!)

Hakuna katika historia mji uliowahi kupiganiwa Zaidi ya Jerusalem, sio Washington, sio London, sio Moscow, sio Paris (hakuna anayehitaji kunguni!), sio Beijing, Sio Tehran.

Jerusalem imekuwa ikipiganiwa toka enzi na enzi n ahata sasa vita yote hii ni kuhusu Jerusalem.

Jaribu kusikiliza matakwa ya pande zote mbili.
Israel: Anataka taifa la Israel, ikiwa Jerusalem ndio mji wake mkuu.
Palestina: Anataka taifa la Palestina ikiwa Jerusalem ndio mji wake mkuu.
Ndo maana ni ngumu sana hawa jamaa wawili kupatana maana wanachotaka kila mtu ndio anachotaka. Na sababu ya kutaka mji huu ni huo mlima wa hekalu na msikiti wa Al-aqsa. Kuna nguvu ya kiroho imejificha hapo. Ila kwa mwenye macho ipo wazi!
Waromani Catholic wenyewe wana sehemu yao hapo Jerusalem. Japo hili ni jambo la kujadili siku nyingine.

Kiroho
Israel ni taifa la Mungu. Alilichagua toka siku zile za Babeli. Wapo watakaobisha na ni sawa kubisha ila hapa tutangalia Biblia inasemaje. Kwa wasioamini Biblia haitashangaza kukataa. Ila kama unaamini Biblia basi endelea kunywa mtori.

Mungu alilichagua taifa la Israel toka siku zile za Babeli.
View attachment 2779382
Utakumbuka pale ndipo Mungu aliwatawanya mataifa.

Sasa wanazuoni wa Biblia wanasema kuna mengi yalitokea zaidi ya lugha kugawanywa. Yaliyotokea ni kuwa mataifa mengine yote walipewa malaika au waangalizi “Watchers” kuyasimamia ila Mungu aliichagua Israel iwe ya kwake mwenyewe.

Hawa watchers waliopewa mataifa mengine waliasi na kuanza kutaka kuabudiwa wao badal ya Mungu wa kweli, nan do maana unaona dunia nzima ya zamani kasoro Israel walikuwa wanaabudu miungu, ni Israel pekee ilikuwa na Mungu mmoja.

Ukitaka kupata picha kidogo yah ii issue kumbuka Malaika Gabriel alimuambiaje Daniel tunasoma Daniel 10: 12 Ndipo akaniambia, Usiogope, Danielii; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

Watchers hawa bado wapo duniani na wanashikilia maeneo mbalimbali duniani na kufanya maovu yao.

Ndo maana hata katika Agano Jipya, Paulo anatungata sikio na kutupa mbinu za kivita kama Roho Mtakatiu alivomuonyesha ya kuwa;

Waefeso 6:10
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake.

11Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Hao wakuu wa giza ndio wanatakiwa kupigwa pia kabla ya kudili na mapepo wabaya. Hao ndio maadui zetu!

(Hii issue ya watchers ni mada ndefu pia inayohitaji muda na nafasi kuijadili kwa kina, ila kwa sasa dokezo hilo latosha)

Turudi kwenye mada kuu
Kumbukumbu la Torati 32:8-9
Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake, kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake.

Na kuanzia hapo alipanga kupitia Israel awapate watu wote duniani kuwaleta kwake. Kuwaleta kwake kivipi?

Kupitia Yesu Kristo, dunia nzima inabarikiwa kwani kila amuaminiye basi hasira na adhabu ya Mungu juu ya dhambi inaondoka na huyu muamini anabarikiwa haijalishi ni myahudi au mtu wa mataifa yaani mimi na wewe.

Wote tuna uwezo sasa wa kuongea na Mungu mwenyewe na kuwa na uhusiano naye.

Waisrael kama binadamu wengine ni watu wabishi walimkataa Yesu Kristo kama Masihi wa Bwana na mwishowe walitawanyika.

Hata sasa hivi waisrael wengi sio wakristo. Wengi ni wayahudi (dini ya Judaism ambayo wanaamini Zaidi agano la kale na traditions nyingine za kiyahudi) na wengine ni atheists.

Lakini Mungu yupo nao bado.

Lakini kama kipindi walipokua watumwa Misri miaka 400, Mungu aliwakumbuka huko kwenye mataifa na aliwarudisha Kanani au nchi ya ahadi, Palestina au Israel.

Lakini 'adui' alishaweka mikakati yake.

Ukitaka kujua kuwa Mungu yupo nao bado. Kuna tabiri ziliandikwa Biblia kuhusu kurudi kwa Israel miaka ya baadae ambayo ndio hio 1948

Isaya 11:12
Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa, kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa, kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa, na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.

Utakumbuka kuanzia mwaka 70AD waroma walipoteketeza Israel na kuvunja hekalu waisrael waliishi utumwani na ugenini na wengi walikua Ulaya.

Mpaka WW2 Hitler na wenzake wakaawalaumu kuwa ndo chanzo cha mabaya na kuleta Final Solution yaani kuwauwa wote na ndiyo iliyopelekea Holocaust.
Hivyo kila mahali Ujerumani ilipofika Ulaya walikua na kikosi chao cha SS chenye kazi ya kuwakusanya wayahudi na kuwauwa kimkakati aidha kwa kuwauwa kwa sumu ya gesi au kuwanyima chakula kuwafanyisha kazi au majaribio ya kisayansi kwenye concentration camps nk. Kama ulishawai kuona picha linaitwa ‘Escape form Sobibo” utakuwa unaelewe hizi codes.

. Hivyo ilikua ni mateso makubwa sana na wajanja na wenye bahati walikimbia ujerumani na ulaya kuanzia miaka ya 30s (maana Hitler na wanazi walishaanza kuonyesha dalili za kudondosha ute kama simba anavotamani swala mawindoni) na wengi zaidi miaka 40s wakati na baada ya WW2 maelfu kwa maelfu walikimbilia Israel na wengine US kama kina Einstein na wengineo.

Hivyo walikusanywa kutoka pembe za dunia kama nabii Isaya alivyotabiri.

Mstari mwingine unasema

Isaya 66:8
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.

Unavoona apo katika uchungu mwingi wa Israel kuteswa na kuuliwa watu milioni 6 walizaliwa siku moja hiyo ya 14, Mei 1948. Kuanzia hapo ndo Israel tunayoijua sasa.

Jambo lingine kushangaza na la kufahamu ni kuwa Gaza imekua mwiba kwa Israel toka miaka ya kale. Ndipo Samson alipotobolewa macho na kutumikishwa na Wafilisti wa zama hizo.

Mwisho wa siku alijiua na kufa nao zaidi ya 3000 lakini mpaka leo ni kikwazo kikubwa.

_____________
Okay, Mwanzo hio ardhi hawakuwa wanakaa wayahudi au Israel. Ilikua ikiitwa Kanani.

Kwa nini Mungu aliwapa Kanani waisrael?

Utakumbuka Israel alikua Yakobo. Yakobo alitoka kwa Isaka na Isaka alitoka kwa Ibrahim.

Ibrahim alitokea Ur ya wakaldayo. Ambayo wanasema ni Iraq ya leo.
Uzao wa Ibrahim unaendelea nyuma hadi kwa Adam.

Lakini Mungu alimuita Ibrahim ampe ardhi ya Kanani kwa sababu waliokaa pale walikua waasi kupitiliza na ardhi ile iliwakataa!

Walawi 18:24-28
“Msijitie najisi kwa kufanya mambo hayo kwani kwa sababu ya mambo hayo nayafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile wao hufanya hayo na kujitia najisi. Nchi yao ilitiwa unajisi nami nikaiadhibu, nayo ikawakataa wakazi wake. Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. Machukizo hayo waliyafanya watu waliokaa katika nchi ya Kanaani kabla yenu, nao wakaitia nchi unajisi. Basi, nyinyi msifanye mambo hayo, la sivyo nchi hiyo itawatapika kama ilivyolitapika taifa lililokuwa kabla yenu.

Walifanya mambo gani hadi nchi ikawatapika?

Ukisoma hio chapter utaona jamaa walikua wakilala na wazazi wao, wajukuu zao, ndugu zao, shangazi, mkwe, shemeji, dada wa mke, walikua wakitoa watoto wao sadaka ya kuchomwa kwa mungu Moleki, mahusiano ya jinsia moja yaani usagaji na ushoga. Haya mambo hayakuanza leo. Jambo moja la kushangaza ni kuwa leo hii kuna baadhi ya watu hasa wanaume wanapenda sana kutumia neno ‘msenge’ katika maongezi ya kawaida au kutukana wengine.

Ni neno maarufu sana katika vinywa vya ‘wasela’ jambo hili ni la kushangaza sana hasa ukizingatia vitendo hivi vinashamiri huko duniani na kuleta taharuki hata katika jamii za kiafrika popote linapotokea. Basi watu na wachunge midomo yao!

Hayo ndo mambo yaliyofanya nchi iwatapike wakaanani na Mungu kuwapa nchi Israel.

Kuna wakati Israel ilifanya mambo kama hayo na wao waliondolewa pia.

------------
Mungu alishaamua hakuna anayeeza kuingamiiza Israel.
Maana alishaapa haya👇 (pia kumbuka kuwa kama ni Taifa la Mungu sio kuwa wao ndo hawapigwi hawafanyi makosa au ni wa kutetea pale wanapokesea. Kama ilivyo katika historia Israel imemkosea Mungu mara nyingi na mara nyingi walipigwa na kuipeleka utumwani na wameteseka vilivyo. Shida ni kuwa wengi walikua na kiburinkwa nafasi hio na kushindwa kuelewa kuwa Mungu aliwachagua wao ili baadaye wote watakaomuamini wawe sehemu ya Taifa lake pia. Japo ipo siku watakuja kuamini yote hayo)

*Mwanzo 12:2-3 *
Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka. Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani. Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Ndo maana unaona Haman alitaka kuwaangamiza enzi za Farao alitaka kuwaangamiza akaishia kumezwa na bahari, Haman alisuka mpango wa kuwaua wayahudi wote, Esther alitumiwa na Mungu kuwaokoa, Ilikuja kipindi cha Tauni au Black death Ulaya na walilaumiwa Waisrael wakauwawa wengi sana, Hitler na wanazi hawapo sasa ila Israel ipo na wengine wengi walijaribu ila walishindwa.

Hata Mpinga Kristo (,antichrist,) atajaribu na itabaki kidogo afanikiwe ila Mungu mwenyewe ataingilia kati wakati huo sio US+washirika tena?

Kama ukiona picha na video za leo ndivyo itakavokua hizo siku za mpingakristo.

Kwa jinsi vita hii inavoendelea sio ajabu ikasambaa Kwenda nchi nyingine pia:

Scenario kama hii inaeza kutokea:
Kadiri Israel anavoshambulia Gaza, watu watafariki Hezbollah wanaeza kuanza kushambulia upande wa pili, Hezbollah wanaadhiliwa na Iran. Iran anatuhumiwa kufadhili uvamizi wa Hamas. Iran alishaapa ataiondoa Israel kwenye uso wa dunia. Israel anaeza kuamua kumvamia Iran na Hezbollah.

Akipigwa sana (maana inasemekana Hezbollah kajipanga vilivyo) anaeza kuomba msaada kwa Marekani. Bwana US akiingia ni lipua lipua mpaka Lebanon na sehemu kadhaa. Waarabu wengine wanaeza kasirika na kumshukia Israel.

Lakini pia rafiki yake Iran ni Russia, na China ambao wanaeza kulazimika kumsaidia kama akianza kupigwa na Israel na Marekani na washirika wake. Kinachofuata hapo ni WW3 na mwishowe mpinga Kristo.

Anyway haya yote ni speculations lakini ni muhimu kufatilia kwa ukaribu mambo yanayotokea Israel kwani hio ndio saa ya Mungu.

Utabiri huu unaeza kutokea endapo hayo hapo juu yatakuwa hivyo.

Zekaria 14:1-4
Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Mwenyezi-Mungu atayakusanya mataifa yote ili kuushambulia mji wa Yerusalemu. Mji utatekwa, nyumba zenu zitatekwa nyara, na wanawake wenu watanajisiwa. Nusu ya wakazi wa mji watapelekwa uhamishoni, lakini nusu itakayosalia haitachukuliwa nje ya mji. Kisha Mwenyezi-Mungu atatoka na kuyapiga vita mataifa hayo, kama afanyavyo daima siku za vita.
------
Kuna vita nyingi zinatokea kati ya Israel na Palestina. Hii nayo ni ya kuangalia kwa makini.
Kama wewe ni mkristo basi kumbuka haya:

Mathayo 24:4
Yesu akawajibu, “Angalieni, mtu asiwadanganye. 5Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo, nao watawadanganya wengi. 6Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita,angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 7Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu. 11Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. 12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 13Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.

Luka 21: “Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni
utakuwa kama wanawali kumi waliochukua
taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano
wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa
wenye busara. 3Wale wapumbavu walichukua
taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,
4
lakini wale wenye busara walichukua taa zao na
mafuta ya akiba kwenye vyombo. 5Bwana arusi
alipokawia
kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
6
“Usiku wa manane pakawa na kelele:
‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje
mkamlaki!’
7
“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na
kuzitengeneza taa zao. 8Wale wapumbavu
wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni
mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika.’
9
“Lakini wale wenye busara wakawajibu,
‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali
mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.
10“Nao walipokuwa wakienda kununua
mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali
waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye
kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
11“Baadaye wale wanawali wengine nao
wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie
mlango!’
12“Lakini yeye bwana arusi akawajibu,
‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
13“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui
siku wala saa.’’

Ufunuo 22: 20Yeye anayeshuhudia mambo haya
asema, “Naam, naja upesi!’’
Amen. Njoo Bwana Yesu.
21Neema ya Bwana Yesu iwe na watakatifu
wote. Amen.
Wacha tuone itakavyokuwa.
 
Kwa utaalamu wangu wa migogoro, naamini taifa bandia la israel liliundwa baada ya kugunduliwa mafuta uarabuni ili kulipa nguvu na kuwatisha waarabu na kuwalazimisha ima kununua silaha toka magharibi au kutafuta ulinzi toka kule kama ilivyotokea. Zaidi ya hapo, sijui kwanini mataifa yanachachawa na kugeuka vipofu hata kwenye mambo ambayo hata ndege anaweza kusuluhisha. Je zaidi ya biashara ya mafuta na silaha kunani? Je hawa akina Niite nyau wazungu wanaojiita waarabu ndiyo wanaohangaisha wazungu wenzao wasimalizwe na waarabu?
Soma andiko langu mwanzo linasema "Yerusalemu itakua kikombe cha kuwalevya wote wanaoizunguka" ukijua maana na historia ya Yerusalemu utaelewa kwanini huo mgogoro haujasuluhishwa mpaka leo hii

Ila kaa macho. Kuna kiongozi wa dunia atakuja kama sio siku za usoni basi siku za baadae sana. Huyo ndio ataweza kusuluhisha huo mgogoro na waisrael na wapelestina watakaa kwa amani kwa mara ya kwanza. Ila baadae atawageuka na DHIKI kuu itasambaa duniani

Utakapoona hayo yanatokea basi jua unabii unatimia na inakubidi ufanye likupasalo!
 
Hii inakusaidia nini wewe kabla ya sisi? Mataifa ya kisasa na ngano wapi na wapi au unatafuta jinsi ya kuyahalalisha au uonekana umepiga skuli isiyo na msaada kwako?
Ndo maana nilisema mwanzo andiko hili linahitaji watu wazima wanaokula nyama na sio watoto wanaokunywa maziwa maana yake inahitaji utulivu wa akili na kungamua mambo bila kuhamaki au kuwa na 'prejudices' zozote kabla ya kusemea jambo hili

Huu mchezo hauhitaji hasira, ukweli uko wazi. Israel ni taifa. Majirani zake wamejaribu kuliangamiza tokea siku limeundwa. Imeshindikana. Juhudi zinaendelea kama unavoona sasa.

Sio kuhalalisha. Bali ni mchanganuo wa facts.

La muhimu wewe fatilia yanayotokea mashariki ya kati. Huko ndipo dunia ilianzia na ndipo itakapoishia. Unaeza usiamini au ukaamini. Ila kumbuka mwenye macho haambiwi tazama na asiyeona nafsi yake mwenyewe hata akionyeshwa hataona!
 
Umeandika vzr sana kwakweli ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya utawala wa Kristo hapa duniani, dunia itaingia kwenye vita na mapigano makali.

Lakini tusisahau unyakuo utaanza.

Luka 17:28-36
[28]Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
[29]lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
[30]Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
[31]Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
[32]Mkumbukeni mkewe Lutu.
[33]Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.
[34]Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
[35]Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. [
[36]Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]

Lutu ni tulio mwamini Kristo, tutatoweka gafla.
Huo ni Unyakuo Utaanza.

Kisha waliobaki wataongozwa na mpinga kristo na kuwa Jeshi moja.

Mathayo 24:5-8,11-14
[5]Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.
[6]Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
[7]Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.
[8]Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.
[11]Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
[12]Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
[13]Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
[14]Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Ndipo Kristo Atashuka sasa na Jeshi lake kuja kusimika ufalme wake hapa Duniani.
Watakuwepo wayahudi 144,000.

Ufunuo wa Yohana 19:11-16
[11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
[12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
[13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
[14]Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
[15]Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
[16]Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Unyakuo umekaribia watu wa Mungu, ukipitwa na unyakuo kuna mateso ya hatari ya mpinga kristo na Mapigo ya Bwana. mimi sipo Mtakoma mtakao kutwa mmezubaha. 😂😂

Ufunuo wa Yohana 8:7,11,13
[7]Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.
[11]Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
[13]Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.
 
Back
Top Bottom