Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

I am just few years older than you right now.

fine, then behave. Huu sio wakati wa malumbano. Huu ni wakati wa kutoa confidance kwa wananchi. Malumbano yanasaidia nini? Taifa linapata faida gani? lets subordinate our individual interests to the interests of our beloved nation which is in testing moments!
 
Ngoja nikujibu hili ambalo umeng'ang'ania nalo sana.

Mosi. Katika kama hali hii ya CCM na CHADEMA bado hatujaongelea CUF, ni kipi hicho ch kunifanya nijunge na yeyote. Kwangu mimi muhimu ni Tanzania. Na kama uanachama mimi ni Mwanachama wa Tanzania mwenye kuamini ndoto za umajumuyi wa Uafrika na siasa ya ujamaa na kujitegemea....Yote haya yalikuwepo wakati wa TANU lakini sasa hakuna.....Niende wapi ndugu yangu...

Uanachma sio swala la oppurtunity kama muonavyo wengi. Uanachama ni imani thabiti katika ajenda, misingi, ndoto na falsafa.......

Kwa hali tuyonayo, na machaguo tuliyonayo...nachelea kusema kama kujiunga katika chama kimojawapo labda nitakapofika mahala naamini kuwa ninahitaji kuwa na nafasi ya kuchaguliwa kisiasa ili kufanikisha ndoto na dira ya yangu ambayo ni kuwa na Tanzanianjema yenye kuwa mchango mkubwa katika kufanikisha kujenga Africanjema yenye kujengwa katika misingi ya demokrasia ya kweli, uongozi wa kinidhamu na maadili, umoja wa kibara na maendeleo ya binadamu.

Hadi sasa naamini kuwa naweza kufanikisha ama hata kujengea misingi imara ya kufanikisha hiyo ndoto na dira yangu bila ya kuwa mwanachama wa chama chochote. Hadi sasa naamini kuwa hakuna chama ambacho kinaonyesha kwa vitendo kuwa angalao kina dira inayofanana kidogo na dira yangu. Mpaka sasa naamini kuwa ni UTANZANIA pekee ndio unaoweza kuniwezesha kujenga misingi hiyo ya kujenga Tanzanianjema na Africanjema....

Ndugu yangu, kwangu mimi what matters ni nini nafanya na sio nafasi gani ninakuwa nayo ama ukada gani ninauvaa....

omarilyas

Na hii inathibitisha kuwa, wewe hujaona bado (au kukubali) kuwa chadema au chama chochote cha upinzani Tanzania kina nafasi (au kinatakiwa kuwa na nafasi) sawa na ccm ya kuongoza nchi.

Inawezekana wewe unaamini kuwa chadema itakuja kuwa bora only when Zitto amekuwa mwenyekiti au mgombea uraisi. Katika hili, nafasi yoyote ya kuijenga chadema wakati hili halijawezekana, haijapewa msukumo mkubwa katika imani na matazamio yako kuhusu chadema. Bado naamini kuwa wewe hujawahi kuwa na malengo mema na chadema.
 
Haya wewe unayejua sana na mwenye malengo mema sana na CHADEMA. Mungu akuongezee ujuvi wako na nia yako njema.....

Nilidhani ulitaka kuelewa kumbe unatka kulumbana....

omarilyas
 
fine, then behave. Huu sio wakati wa malumbano. Huu ni wakati wa kutoa confidance kwa wananchi. Malumbano yanasaidia nini? Taifa linapata faida gani? lets subordinate our individual interests to the interests of our beloved nation which is in testing moments!

Zitto,

As far as I can feel it, I am behaving. I am on top of my well behaving mannered (sic) behavior right now.

NOTE - I am (and will always) taking bs as they come. I am not the one to take a high road when my opponent is taking out all my bridges.

You can stay away if you dont like this.

Thanks!
 
Haya wewe unayejua sana na mwenye malengo mema sana na CHADEMA. Mungu akuongezee ujuvi wako na nia yako njema.....

Nilidhani ulitaka kuelewa kumbe unatka kulumbana....

omarilyas

Ukitaka kuyaita malumbano, fine. But as far as I am concerned, huu ndio mtizamo wangu binafsi kukuhusu wewe.
 
Kwi kwi kwi....!I truly miss Mwafrika wa kike with mijadala moto moto!
 
Mwenyekiti wa chama chochote anafanya kazi yake kwa kukutana na Sekretariati ya chama. Dk. Slaa ndiye mkuu wa sekretariati na Mbowe alipokuwa Dodoma alikuwa na wajibu pamoja na mamlaka ya kuita kikao kama alihisi kuna jambo la kujadili.

Ubaya uliotokea ni kwamba mmoja wa hao maofisa wa Sekretariat alitoa siri ya mazungumzo kwa gazeti. Hakuna chama kinachoweza kuendeshwa bila kujadili dukuduku za wanachama, hasa viongozi.

Kama kuna ofisa katika Sekretariat ambaye mienendo yake haina tija kwa chama, hatua ni lazima zichukuliwe kusahihisha. Ni choko choko za wahasimu wa Chadema, hasa wakati huu tunapoelekea Uchaguzi wa 2010, zitatuvuruga kama hatuwi makini katika kushughulikia matatizo ya kila siku.

Viongozi na wanachama wa Chadema tujihadhari. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.
 
Sawa kiongozi umesikika!
 
Chadema sasa hali si shwari waendesha vikao vya siri kuwajadili wanachama

Na Fidelis Butahe

HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaonekana kuyumba baada ya Mwananchi kupata habari kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe juzi aliongoza kikao cha siri mjini Dodoma kilicholenga kuwajadili baadhi ya wanachama akiwemo mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum.

Habari hizo kutoka ndani ya chama hicho, zilieleza kuwa waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Hemed Sabula, John Mrema, Erasto Tumbo, Benison Kigaila, Halima Mdee, Lucy Owenya na Anna Komu.

Habari hizo zilifafanua kuwa Mbowe aliwasilisha ajenda ya kufukuzwa uanachama kwa afisa habari wa chama hicho, David Kafulila, mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Danda Juju ambaye ni afisa Mwandamizi kwa kuwa wanakichafua chama kwa kuchochea mgogoro kutokana na kuvujisha siri za chama kwenye vyombo vya habari.

Habari hizo, zilieleza kwamba baada ya Mbowe kuwasilisha hoja yake, ilipingwa na wajumbe wa kikao hicho kwa maelezo kuwa, Zitto Kabwe hatakubaliana na jambo hilo na kusisitiza kuwa linaweza kukipasua chama, lakini katika majumuisho Mbowe alisisitiza kuwa hataweza kufanya kazi na Kafulila hivyo alisisitiza kuwa Kafulila apewe barua ya kufutwa uanachama.
Kutokana na kusimamia uamuzi huo, ilidaiwa kuwa wajumbe wa mkutano huo walikubali kwa shingo upande umauzi huo.

Baada ya tarifa hizo Mwananchi liliwatafuta wahusika ambao walikiri kuwepo kwa taarifa za kikao hicho na kusisitiza kuwa wanasubiri kuona kama watapatiwa barua za kufutwa uanachama au la.

"Mimi hizo taarifa nimezisikia na nilikuwa najua kuwa kulikuwa na kikao kisicho rasmi kilichokaa Dodoma ila mpaka sasa sijapata barua yeyote, nasikia kuwa wanataka kunitimua uanachama, lakini ngoja tusubiri tuone wakinipatia barua kila kitu kitakuwa wazi," alisema Kafulila ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania Ubunge mwaka 2010 Kigoma Kusini

Kafulila pia aliwahi kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho, (Bavicha) katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa Agosti mwaka huu, lakini mshindi hakupatikana baada ya mpinzani wake, John Heche kupinga matokeo kwa madai kuwa kura 20 zilikuwa zimeongezeka.

Naye Danda Juju alisema taarifa hizo, amezisikia ingawa hana uhakika nazo na kusisitiza kuwa kwa kiasi fulani anaweza kuziamini kwa kuwa alikuwa na taarifa kuwa Mbowe anafanya kikao kisicho rasmi mkoani Dodoma. Mama mzazi wa Zitto, Shida Salum hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo.

Ha ha ha! Mna Hamu ya Kuona Wanafukuzana ili Mle Nji Vizuriee, Hawafukuzani Ng'o na watakula Sahani moja na Mafisadi nyinyi si Mmewashindwa Last week Dodoma ngoja Makamanda wa Ukweli wavae magwanda Muone moto wake
 
Chadema sasa hali si shwari waendesha vikao vya siri kuwajadili wanachamaNa Fidelis Butahe
HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaonekana kuyumba baada ya Mwananchi kupata habari kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe juzi aliongoza kikao cha siri mjini Dodoma kilicholenga kuwajadili baadhi ya wanachama akiwemo mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum.

Habari hizo kutoka ndani ya chama hicho, zilieleza kuwa waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Hemed Sabula, John Mrema, Erasto Tumbo, Benison Kigaila, Halima Mdee, Lucy Owenya na Anna Komu.

Habari hizo zilifafanua kuwa Mbowe aliwasilisha ajenda ya kufukuzwa uanachama kwa afisa habari wa chama hicho, David Kafulila, mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Danda Juju ambaye ni afisa Mwandamizi kwa kuwa wanakichafua chama kwa kuchochea mgogoro kutokana na kuvujisha siri za chama kwenye vyombo vya habari.

Habari hizo, zilieleza kwamba baada ya Mbowe kuwasilisha hoja yake, ilipingwa na wajumbe wa kikao hicho kwa maelezo kuwa, Zitto Kabwe hatakubaliana na jambo hilo na kusisitiza kuwa linaweza kukipasua chama, lakini katika majumuisho Mbowe alisisitiza kuwa hataweza kufanya kazi na Kafulila hivyo alisisitiza kuwa Kafulila apewe barua ya kufutwa uanachama.

Kutokana na kusimamia uamuzi huo, ilidaiwa kuwa wajumbe wa mkutano huo walikubali kwa shingo upande umauzi huo.

Baada ya tarifa hizo Mwananchi liliwatafuta wahusika ambao walikiri kuwepo kwa taarifa za kikao hicho na kusisitiza kuwa wanasubiri kuona kama watapatiwa barua za kufutwa uanachama au la.

Mimi hizo taarifa nimezisikia na nilikuwa najua kuwa kulikuwa na kikao kisicho rasmi kilichokaa Dodoma ila mpaka sasa sijapata barua yeyote, nasikia kuwa wanataka kunitimua uanachama, lakini ngoja tusubiri tuone wakinipatia barua kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Kafulila ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania Ubunge mwaka 2010 Kigoma Kusini

Kafulila pia aliwahi kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho, (Bavicha) katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa Agosti mwaka huu, lakini mshindi hakupatikana baada ya mpinzani wake, John Heche kupinga matokeo kwa madai kuwa kura 20 zilikuwa zimeongezeka.
Naye Danda Juju alisema taarifa hizo, amezisikia ingawa hana uhakika nazo na kusisitiza kuwa kwa kiasi fulani anaweza kuziamini kwa kuwa alikuwa na taarifa kuwa Mbowe anafanya kikao kisicho rasmi mkoani Dodoma. Mama mzazi wa Zitto, Shida Salum hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo.
 
Mwafrika;

Samahani tena samahani sana. Baada ya kukusoma nimeona upeo wako au namna ya kujadili mambo ni sawa na Mama Sophia Simba wa CCM. Nimetanguliza samahani kama nimekutafsiri visivyo.

Hapa kinachojadiliwa ni kuwa, Je Mbowe hawezi kukaa meza moja na wanaotofautiana naye kimtizamo na kumaliza tofauti hizo?. Kwanini vikao vya siri visivyo rasmi?. Laiti angeitisha kikao rasmi yoote haya yasingekuwapo.

Pia kwanini useme kuwa siwezi kufanya kazi na mtu?, Chadema sio kampuni ambayo lengo ni kutengeneza faida, hapa ni mitizamo tu mnakaa mezani mnayamaliza, tena ikibidi mnakaa ONE on ONE.

Hebu nakuomba tena fikiria OBJECTIVELY kwa manufaa ya TAIFA na si ya chama chenu.
 
Mwafrika akielezwa huwa mjuaji wa kila kitu, the best thing ni kuwa ameshakuwa marked na credibility yake ime slump down accordingly.

anatapatapa, hizi post atazijibu tu upende usipende

wait and see!
 
Uongozi wa CHADEMA needs to grow up.
  1. Mbowe anatakiwa kufahamu kuwa chama sio tena cha familia, ni cha wanachama wote na hakuna aliye bora kuliko mwingine.
  2. Kundi la Zitto nalo wanatakiwa kuelewa kuwa vurugu katika kugombea madaraka hazitakijenga chama. Wawe wawazi juu ya nia zao za kuchukua madaraka kwani ni haki yao lakini wasitumie mbinu ambazo zinazua migogoro ya chini chini.
 
Kuna taarifa ambazo zimetufikia muda si mrefu kuwa David Kafulila wa CHADEMA aidha kasimamishwa au kafukuzwa uanachama wa CHADEMA.

Nimejaribu kwa kila namna kuwasiliana na watu wa ndani katika chama hiki lakini simu hazipokelewi. Nimeongea na Zitto Kabwe ambaye pamoja na kutokujua kilichokuwa kinaendelea lakini ameonekana kushtushwa na taarifa hizi na kuomba wana-CHADEMA kutulia wakati huu na wasipaniki kwani suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Taarifa zaidi ni pale tutapopata kuongea na wakuu ndani ya CHADEMA.

-----
UPDATE
-----

Uteuzi wake ndo umetenguliwa na hajafukuzwa uanachama (kauli ya Kafulila)
 
Wacha tusubiri hapa, tokea jpili hapa JF kulikuwa na moshi unapepea inaweza ikawa moto tiyari umewaka.
 
Mbowe, Mbowe, Mbowe chama unakipeleka wapi sasa? Hebu jaribu kumuiga mwenzio JK wavumulie maadui zako/wapinzani wako na mpingane bila ya kupigana.

Fukuza fukuza haijengi inabomoa tu...
 
Mbowe, Mbowe, Mbowe chama unakipeleka wapi sasa? Hebu jaribu kumuiga mwenzio JK wavumulie maadui zako/wapinzani wako na mpingane bila ya kupigana.

Fukuza fukuza haijengi inabomoa tu...
Masatu,
JK ni mfano mbaya sana wa kuigwa. Ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi ndani ya CCM na sasa ndio wanaomwendesha.
 
Kumbe kweli imetokea?

Kama ni hivyo basi Mama yake Zitto na yeye anaondoka.

Kweli kuna haja ya kuanzisha chama na si kutegemea NGO za akina Mzee Mtei.
 
Back
Top Bottom