Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Mkamap

Kwanza heading yako haijatulia kabisa imekaa kiushabiki na kama vile mtu anayefulahia mpasuko wa chadema.Kwa hali ya sasa wakati watu wengi wanaomba hilo lisitokee.

Mbowe, kufukuza watu kwenye chama ni jambo ambalo linafanywa na watu ambao hawana uvumilivu wa kisiasa. Ingekuwa kufuka watu ni jambo zuri sana basi ungeona historia ikikuambia hivyo. Tuna mifano hai kama zeller miller alikuwa democrat lakini alitoa speech kwenye convetion ya bush pai Joe amefanya hivyo lakini hawakufukuzwa uanachama. Kumfukuza mtu uanachama costyake ni kubwa kuliko kumuacha.

Solution hapa ni kujitahidi sana comcontain kwani akiwa nje bado atapata habari na atakuwa huru sana kuzisambaza kuliko sasa. halafu chama ambacho watu wake wote wanakubaliana 100 kwa 100 ni chama gani hicho Mafia tu nao wanakuwa na tofauti

Mbowe sisi sasa tumechoka na tunataka chama kiende mbele na kama utakuwa wewe ni kikwazo iitabidi tukutoe tu kumbuka kuwa ni rahisi kwa sasa kukutoa wewe kuliko hata kuwatoa vichaa. basi ni matamanio yangu kuwa utasikia kilio chetu na kujenga chama na pia kuwa siyo watu wote watakupenda lazima kuna wengine watakupenda wewe ma wengine zito hilo ni la kawaida kabisa. Kuna sehemu kuna mtu alikuwa amependwa na watu wengi lakini hakuwa raisi.

Mbowe sasa ni wakati wa kukipeleka chama kwenye ahtua nyingine na siyo kuanza kudeal na wanachama. mkicheza karata yenu vizuri wataondoka wenyewe na ilakuvukuza normal!

CHADEMA ni chama kizuri sana tatizo la chadema ni Mbowe , Mbowe ni tatizo kubwa chadema.
 
Mbowe kuwa na busara za ziada. Tafadhali jenga chama wakati huu ambao CCM ina mgogoro mkubwa. Wananchi wengi wa Tanzania wameanza kuiamini Chadema kuliko chama kingine cha siasa kilichoko upinzani. Acheni kufukuzana katika chama ila ongezeni Idadi ya wanachama wapya na kuweka misingi bora ya kuwapokea akina Samwel Sitta, Mwakyembe, Shelukindo, Selelii, John S.Marecelle n.k Hawa watatoka tu CCM baada ya Bunge kuvunjwa mwakani hivyo ni wakati wa Chadema sasa kuongeza kampeni za kupata wanachama wapya kwa kuangalia udhaifu wa serikali ya Kikwete katika mikataba ya Richmond, TRL, Meremeta n.k - Sitta ameshasema kuwa serikali haina mapya ---- (imeshindwa hoja ndo maana ripoti ya richmond haikujadiliwa). Please Mr. Chairman Mbowe soma majira na nyakati. Tatua mgogoro kwa amani
Nakuunga mkono kwa observation yako.Viongozi wa CHADEMA tafadhirini sana nyie na CUF mumeshawekwa kwenye target na Usalama wa Taifa(Disinformation Unit).Ni idara hii ndiyo inayofuel makundi CCM na kufikia uamuzi wa kwamba CCM wote wameshiriki ufisadi kama ilivyothibitishwa Mh Sofia Simba.
Kaeni macho taarifa nyingi zitapenyezwa kwa viongozi ili muvurugane ili watakaojimegua CCM wasipate pa kwenda.Vyombo vya habari na baadhi ya waandishi wamo wameshirikishwa kwenye jambo hili.Kutofautiana mawazo ni jambo la kawaida lakini kama kuna tofauti zifuate kanuni za vikao kama kupiga kura, ili kupata muafaka.Adui mkubwa katika kuendesha chama ni makundi ya siri ya kumjenga mtu na kumbomoa mwingine, hii ni siri ya mivutano mingi inayojitokeza kwenye vyama vyovyote.Kama mwanachama amepata taarifa ya kiongozi kurubuniwa ili akivuruge chama ni vizuri,huyo kiongozi apelekwe kwenye vikao vya kikatiba ahojiwe!
 
CHADEMA ni chama kizuri sana tatizo la chadema ni Mbowe , Mbowe ni tatizo kubwa chadema.
Vipi tena mkuu, tatizo lake ni nini? linafanana na matatizo ya kikwete, S.simba, RA,EL nakadhalika?
 
Vipi tena mkuu, tatizo lake ni nini? linafanana na matatizo ya kikwete, S.simba, RA,EL nakadhalika?

Huyu jamaa ana matatizo sana saizi hayawezi kuonekana sana kwa sababu hana madaraka ,lakini huyu jamaa kitu cha kwanza ni dikteta,kitu cha pili ni fisadi,kitu cha tatu anakitumia chama kama biashara,kitu cha nnen hana uwezo.............

Huyu jamaa kama CHADEMA mnaipenda mwangalieni kwa jicho la karibu.

Mbowe kawamtimua Kabouru na kumsingizia fisadi,kamtimua Chacha na kumpoteza kabisa ,kajaribi kumtimua Zitto lakini zitto kawa na roho ya chuma sasa anatumia njia ya nyuma.

Yoyote anayeonekana ni kikwazo ktk biashara yake na chadema kwake ni tatizo na hawezi kufanya na mtu kama huyo.

Kama akina Kikwete ni wabovu haina maana tupo hapa kutafuta mtu mwingine mbovu eti tukiwa na lengo la kusukuma gurudumu mbele.
 
Nakuunga mkono kwa observation yako.Viongozi wa CHADEMA tafadhirini sana nyie na CUF mumeshawekwa kwenye target na Usalama wa Taifa(Disinformation Unit).Ni idara hii ndiyo inayofuel makundi CCM na kufikia uamuzi wa kwamba CCM wote wameshiriki ufisadi kama ilivyothibitishwa Mh Sofia Simba.
Kaeni macho taarifa nyingi zitapenyezwa kwa viongozi ili muvurugane ili watakaojimegua CCM wasipate pa kwenda.Vyombo vya habari na baadhi ya waandishi wamo wameshirikishwa kwenye jambo hili.Kutofautiana mawazo ni jambo la kawaida lakini kama kuna tofauti zifuate kanuni za vikao kama kupiga kura, ili kupata muafaka.Adui mkubwa katika kuendesha chama ni makundi ya siri ya kumjenga mtu na kumbomoa mwingine, hii ni siri ya mivutano mingi inayojitokeza kwenye vyama vyovyote.Kama mwanachama amepata taarifa ya kiongozi kurubuniwa ili akivuruge chama ni vizuri,huyo kiongozi apelekwe kwenye vikao vya kikatiba ahojiwe!

Usalama wa taifa nafikiri hawajaitisha hicho kikao cha siri cha chadema, tatizo letu ni kujaribu kuiacha source ya tatizo na kukimbilia kusingizia wengine.

Na uhakika fulani mkubwa hata akina sitta wakitoka ccm hawatajiunga chadema maana hawa jamaa kuingia chadema watahatarisha masilahi ya Mbowe kitu ambacho Mbowe hatakubali.

Kama hawa jamaa wakijiondoa ccm kama wadanganyika tunavyofikiri bora waanzishe chama chao from the ground ama wakajiunge na chama kidogo kabisa kama pp maendeleo ama cha mtikila.
 
Mbowe hana akili hata kidogo na si mwanasiasa bali ni political enterpreneur, na kuongozwa na mtu kama huyo ni sawa kuongozwa na kipofu, kazi yake uadui na si kujenga umoja.
 
Tatizo la Mbowe ni elimu kiduchu inayopelekea kushindwa kwenda sambamba na ukuwaji wa chama. Ilipofika sasa Chadema Mbowe hawezi kuinendesha anakosa confidence. Kila wakati anaona watu wanataka kumng'oa hususan wasomi kina Zitto, Kitila et al.

Kwa ukubwa wa Chadema sasa asitegemee kupata watu wa yes sir, na wala asijidanganye kuwa mindhali baba mkwe yupo atakuwa ana kuja kum rescue kila wakati.

Umefika wakati kusema enough is enough, Mbowe mchango wako kufikisha chama hapo kilipo unatosha kutokana na uwezo wako kielimu umegota huwezi fanya zaidi ya hapo hata kamma dhamira yako ni nzuri tatizo ni shule ndogo. Kwa bahati mbaya kajaribu kwenda kusoma lakini kichwa chake ni cha nyoka hakibebi mzigo kafeli sasa karudi Bongo aakipeleka chama alijojo.
 
CCM wanarushiana vifurushi vya kinyesi hadharani na kupakana matope. Chadema nao unasema wanaudikteta wa hali ya juu wakiongozwa na ndugu Mbowe. CUF umesema Seif anapenda mno mafungu na kutumbukiziwa coins kama phone box.

Sasa ndugu Masatu, kama ushauri, ni uongozi wa chama kipi ulio bora ndani ya hili Taifa?!

Aaah Steve dont ask abt obvious!

Nevertheless check ur PM!
 
Una maana gani ?
Mie nafikir tuwe na mtazamo wa kujenga nchi yetu na si kuside na mtu kwa masilahi binafsi.

Hee! mkuu vipi tena?, mbona unakuja na maswali ya kipolisi, we unadhani mi nina maana gani?. Wewe si ume-copy na ku paste habari sasa wewe unahusikaje hapo mpaka unalipuka namna hiyo?.

Lazima tuwe tunachukulia hizi habari za magazetini sasa hivi katika skeptical view. 2005 tulisikia mengi sana. Ukiangalia michango karibu yote hapa ni reactionary biased against Mbowe badala yake tuwe-tuna"analyse", mimi Mbowe hanijui wala simjui zaidi ya kuwa yeye ni public figure kwa kuwa ni mwanasiasa. Sina maslahi yoyote binafsi zaidi ya kutaka Tanzania iwe na upinzani imara kwani ni nguzo ya kuwaamsha watawala wavivu wasiotaka kufikiri katika kuiendeleza nchi.
 
Mkuu ni mtazamo wangu wa kwamba saizi tuangalie masilahi ya taifa na si masilahi binafsi kama umekereka samahani na pole.

Pia nafikiri hakuna wa kuketi na kutunga habari japo mwandishi anaweza tia chumvi ili kunogesha habari lakini bado core inakuwa palepale.

Mbowe ni tatizo ktk chadema na ktk ukuuji wa demokrasia ,na pia tusijaribu kuwekeza kwa mtu utakuja juta mbeleni pia huo nao ni ushauri.
 
hii sasa hatari kama mifarakano imeanza kutokea tunakoelekea katika kipindi cha uchaguzi hii inaashiria nini??
 
Kama Mbowe hawezi kufanya kazi na Kafulila si aondoke yeye! maana Kafulila anaweza fanya kazi na Mbowe, kwa maana hiyo Mbowe ndio tatizo na si Kafulila
 
ohooo! CCM imeshaingiza mdudu wake ndani ya CHADEMA. Mbowe, umetumwa na MAFISADI WA ccm. Angalia unaotaka kuwafukuza, Kafulila na Mama zitto wote wanatoka kigoma, pia ni wazi kuwa ukimfukuza mama zitto automatic hata zitto hatakubaliana na uamuzi huo naye atakwenda, kinachobaki hapa una-prove rumours za ccm kwamba chadema ni chama cha kikabila (uchagga). Sasa unataka wtz tuamini kwamba kuna ukabila ndani yaq chadema?? Acha jazba, chadema sio mbowe, mbowe ni mwanachama wa chadema, tena usiharibu chama ambacho kwa sasa kinaonekana mbadala wa ccm
 
Usalama wa taifa nafikiri hawajaitisha hicho kikao cha siri cha chadema, tatizo letu ni kujaribu kuiacha source ya tatizo na kukimbilia kusingizia wengine.

Na uhakika fulani mkubwa hata akina sitta wakitoka ccm hawatajiunga chadema maana hawa jamaa kuingia chadema watahatarisha masilahi ya Mbowe kitu ambacho Mbowe hatakubali.

Kama hawa jamaa wakijiondoa ccm kama wadanganyika tunavyofikiri bora waanzishe chama chao from the ground ama wakajiunge na chama kidogo kabisa kama pp maendeleo ama cha mtikila.

Mbona argument zako zinaonekana kuelemea upande fulani? sina imani na wewe kabisa
 
Mimi sioni shida kuwajadili wanachama watakao onyesha utovu wa nidhamu au hata ambao wanahatarisha ustawi wa chama. Shida yangu ni njia zinazotumika kufanya hayo. Nilikuwa nafikri kama kuna uthibitisho kuwa Mama Zitto, Kafulila wanamatatizo chamani basi vikao halalali vya kichama viitishwe kuwajadili. Katika vikao hivyo watu wawe huru kutoa maoni ya kuafiki na kutoakuafiki. Mathalani Zitto ni Naibu Katibu Mkuu basi awepo kwenye hicho Kikao.

Kama Mh. Zitto anaamini kweli kwenye philosophy yake ya siasa za kupanga na sio za kuvizia basi naamini hawezi kumtetea mjumbe anayehatarisha uhai wa Chama kwasababu ni Mama Yake. Na Kama madai yatathibishwa na kuafikiwa na wajumbe wanaotosha kupitisha maamuzi kwa mujibu wa katiba, hata kama Zitto atakuwa tofauti nayo basi yatakuwa ni maamuzi ya Chama.

Nitamshangaa sana Mh. Zitto kama madai ya mwanachama mmoja kuvuruga chama kwa Makusudi yakathibitishwa na yeye akaendelea kumtetea bila hoja ya maana kwasababu ni "mama yake tu". Mh Mbowe atumie busara kama Mwenyekiti, matatizo ya chama hutatuliwa kwa vikao halali, hii mambo ya vikao vya siri siri vitamfikisha yeye, CHADEMA, na watanzania wote mahali pabaya sana ambako Mabere Marando na NCCR-Mageuzi walitufikisha watazanzania. Tumechoka jamani na hizi siasa za visasi na chuki, tunataka siasa za kukubali kukosolewa na kukosoana. Siasa za kukubali kuwajibika. Bahati mbaya sana Maendeleo ya nchi hayawezi kutenganishwa na siasa yake, kwa hiyo wansiasa mumeshika maisha ya watu, kwa hiyo mnapocheza Makida mkida kwenye siasa vyama Vyenu mjue mnachezea uhai wetu, mstakabli wa amani yetu, mnacheza na haki zetu.

Kaeeni chini muonyane kwa upole, wenye kuonywa na wapokee maonyo, khaaa!
 
Mbona argument zako zinaonekana kuelemea upande fulani? sina imani na wewe kabisa

Wewe kuwa usiwe na imani na mimi huo ni uhuru na demokrasia ya msingi kabisa ya kila mwanadamu na utashi wa kibanadamu.

Lakini na mimi nina uhuru wangu wa ku argue si kwa kuegemea upande fulani ili fulani awe na imani na mimi , ila ila mimi najaribu kutumia utashi wangu kuyaona mambo kwa njisi ninavyoyaona na si kwa njisi unavyoyaona kutokana na imani yako.

Sipo kuhubiri injili hapa ili nipate kumwaminisha mtu yoyote hapa , bali nafanya kuyasema ninayoona mema ambayo kwa namna ya pekee watu wengi wanajaribu kuyafumbia macho ama wanayaona ni sahihi ndio maana hawayasemi hii pia nikutokana na uelewa wao ,utashi na halikadharika mienendo yao ya kuzunguruka dunia.

Hivyo simwaliki yoyote mwenye imani yake bali na aalika wote wenye utashi na mtazamo huru.
 
Back
Top Bottom