Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,109
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  Chadema sasa hali si shwari waendesha vikao vya siri kuwajadili wanachama

  Na Fidelis Butahe

  HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaonekana kuyumba baada ya Mwananchi kupata habari kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe juzi aliongoza kikao cha siri mjini Dodoma kilicholenga kuwajadili baadhi ya wanachama akiwemo mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum.

  Habari hizo kutoka ndani ya chama hicho, zilieleza kuwa waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Hemed Sabula, John Mrema, Erasto Tumbo, Benison Kigaila, Halima Mdee, Lucy Owenya na Anna Komu.

  Habari hizo zilifafanua kuwa Mbowe aliwasilisha ajenda ya kufukuzwa uanachama kwa afisa habari wa chama hicho, David Kafulila, mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Danda Juju ambaye ni afisa Mwandamizi kwa kuwa wanakichafua chama kwa kuchochea mgogoro kutokana na kuvujisha siri za chama kwenye vyombo vya habari.

  Habari hizo, zilieleza kwamba baada ya Mbowe kuwasilisha hoja yake, ilipingwa na wajumbe wa kikao hicho kwa maelezo kuwa, Zitto Kabwe hatakubaliana na jambo hilo na kusisitiza kuwa linaweza kukipasua chama, lakini katika majumuisho Mbowe alisisitiza kuwa hataweza kufanya kazi na Kafulila hivyo alisisitiza kuwa Kafulila apewe barua ya kufutwa uanachama.

  Kutokana na kusimamia uamuzi huo, ilidaiwa kuwa wajumbe wa mkutano huo walikubali kwa shingo upande umauzi huo.

  Baada ya tarifa hizo Mwananchi liliwatafuta wahusika ambao walikiri kuwepo kwa taarifa za kikao hicho na kusisitiza kuwa wanasubiri kuona kama watapatiwa barua za kufutwa uanachama au la.

  "Mimi hizo taarifa nimezisikia na nilikuwa najua kuwa kulikuwa na kikao kisicho rasmi kilichokaa Dodoma ila mpaka sasa sijapata barua yeyote, nasikia kuwa wanataka kunitimua uanachama, lakini ngoja tusubiri tuone wakinipatia barua kila kitu kitakuwa wazi," alisema Kafulila ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania Ubunge mwaka 2010 Kigoma Kusini

  Kafulila pia aliwahi kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho, (Bavicha) katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa Agosti mwaka huu, lakini mshindi hakupatikana baada ya mpinzani wake, John Heche kupinga matokeo kwa madai kuwa kura 20 zilikuwa zimeongezeka.

  Naye Danda Juju alisema taarifa hizo, amezisikia ingawa hana uhakika nazo na kusisitiza kuwa kwa kiasi fulani anaweza kuziamini kwa kuwa alikuwa na taarifa kuwa Mbowe anafanya kikao kisicho rasmi mkoani Dodoma. Mama mzazi wa Zitto, Shida Salum hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo.
   
 2. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452

 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Chadema mnaturudisha nyuma kama habari hizi zitakuwa za kweli...this is frustrated politics
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Fukuza fukuza haifai Mbowe kama kuna shida ongeeni kwa amani . Kutofautiana mawazo pia ni siasa sasa sijui kama kweli hao wachache wanaweza kuwakufuza hao watajwa uanachama
   
 5. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbowe kuwa na busara za ziada. Tafadhali jenga chama wakati huu ambao CCM ina mgogoro mkubwa. Wananchi wengi wa Tanzania wameanza kuiamini Chadema kuliko chama kingine cha siasa kilichoko upinzani. Acheni kufukuzana katika chama ila ongezeni Idadi ya wanachama wapya na kuweka misingi bora ya kuwapokea akina Samwel Sitta, Mwakyembe, Shelukindo, Selelii, John S.Marecelle n.k Hawa watatoka tu CCM baada ya Bunge kuvunjwa mwakani hivyo ni wakati wa Chadema sasa kuongeza kampeni za kupata wanachama wapya kwa kuangalia udhaifu wa serikali ya Kikwete katika mikataba ya Richmond, TRL, Meremeta n.k - Sitta ameshasema kuwa serikali haina mapya ---- (imeshindwa hoja ndo maana ripoti ya richmond haikujadiliwa). Please Mr. Chairman Mbowe soma majira na nyakati. Tatua mgogoro kwa amani
   
 6. N

  Nanu JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbowe, demokrasia ni kufanya kazi na wale ambao pia unawaona ni tatizo. Kama kuna vitu ambavyo haviendi sawa itisha kikao mkutane, msutane, na hapo mpeane mikono baada ya kukubaliana jinsi ya kwenda mbele. CCM wanajua wana matatizo sasa wanataka kuambukiza matatizo yao Chadema ili wanaCCM ambao wanataka kutoka wasitoke kwani hawaoni pakwenda kama Chadema nacho kinafukuta migogoro na ubabe. Please re-think, if you really want to take Chadema to new high heights.
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkamap

  Kwanza heading yako haijatulia kabisa imekaa kiushabiki na kama vile mtu anayefulahia mpasuko wa chadema.Kwa hali ya sasa wakati watu wengi wanaomba hilo lisitokee.

  Mbowe, kufukuza watu kwenye chama ni jambo ambalo linafanywa na watu ambao hawana uvumilivu wa kisiasa. Ingekuwa kufuka watu ni jambo zuri sana basi ungeona historia ikikuambia hivyo. Tuna mifano hai kama zeller miller alikuwa democrat lakini alitoa speech kwenye convetion ya bush pai Joe amefanya hivyo lakini hawakufukuzwa uanachama. Kumfukuza mtu uanachama costyake ni kubwa kuliko kumuacha.

  Solution hapa ni kujitahidi sana comcontain kwani akiwa nje bado atapata habari na atakuwa huru sana kuzisambaza kuliko sasa. halafu chama ambacho watu wake wote wanakubaliana 100 kwa 100 ni chama gani hicho Mafia tu nao wanakuwa na tofauti

  Mbowe sisi sasa tumechoka na tunataka chama kiende mbele na kama utakuwa wewe ni kikwazo iitabidi tukutoe tu kumbuka kuwa ni rahisi kwa sasa kukutoa wewe kuliko hata kuwatoa vichaa. basi ni matamanio yangu kuwa utasikia kilio chetu na kujenga chama na pia kuwa siyo watu wote watakupenda lazima kuna wengine watakupenda wewe ma wengine zito hilo ni la kawaida kabisa. Kuna sehemu kuna mtu alikuwa amependwa na watu wengi lakini hakuwa raisi.

  Mbowe sasa ni wakati wa kukipeleka chama kwenye ahtua nyingine na siyo kuanza kudeal na wanachama. mkicheza karata yenu vizuri wataondoka wenyewe na ilakuvukuza normal!
   
 8. O

  Orche Senior Member

  #8
  Nov 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wetu, kwa sababu wanataka kuendesha chama kama kampuni hivyo kutohitaji chalenge ndani ya chama. Pia wanatakiwa wawe waangalifu kwani CCM haiwezi kupenda chama chochote cha upinzani kikuwe ili kuwapa watanzania na wazito ndani ya CCM chama mbadala, watafanya kila njia kuidhoofisha. Hivyo naomba Mboe na timu yake wawe makini na maamuzi yao, na hasa kutokimbilia kufukuza. Naitakia CHADEMA utulive na maendeleo, watanganyika wamechoka.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhh.
  Mbowe is just a joke....
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,109
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  anacheza na maisha ya watu huyu...m nilifurahi nikijua ataondolewa na umwinyi wake heee walikuwa awamjui huyo ndio freeman
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Chama cha wakatoliki hicho.
   
 12. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I stand to be corrected but I think this is too cheap!
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  meaning what?
   
 14. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Waache na wao watoane macho kama wenzao wa CC em!! Majungu na kutoaminiana hakuko CC em tu jamani! Kujenga demokrasia si kazi ndogo!! Watanzania msihofu, tuko kwenye kipindi cha mpito.
   
 15. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Eeeh eti Zitto hatokubali na chama kinaweza kikapasuka????

  Wadau hii hofu ya Zitto inatoka wapi??? Kweli Zitto ni zaiddi ya Chadema??? Sikatai Zitto anaweza kuwa na influence ya kiasi fulani, lakini mnampa kichwa SANA!! Je imefikia mahala mama yake akivurunda aiadhibiwe na chama kisa Zitto atakasirika???

  Kwa staili hii, acha CCM iendelee kushika hatamu!!
   
 16. M

  Masatu JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbowe ni dikteta mkubwa, iweje aandae ajenda ya kufuta wanachama yeye mwenyekiti na sio katibu Dr Slaa? Iweje aseme siwezi kufanya kazi na Kafulila kwani chama ni kampuni yake binafsi?

  Tulijua haya yata surface. Sasa tusubiri Baba mkwe nae aje apigilie msumari wa mwisho.

  Huu woga wa Zitto unatokea wapi? au ndio kuogopa kivuli? Dhambi ya ubaguzi itaendelea kumla Mbowe na hatimae wakiisha "wabaya" wake atahamia kwa akina Slaa, Mnyika, Mdee etc
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Kama hizi habari ni za kweli ,basi Mbowe anamtafuta Zitto anamtaka zitto ajitoe mwenyewe chamani,hataki kumu face ana kwa ana anatumia njia za mzunguruko.

  Mbowe alisema maneno hayahaya hawezi fanya kazi na marehem chacha.
   
 18. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Yes. It's very cheap. Sorry to say.
   
 19. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Who said there will be oppositions in TZ? ccm will lead us forever!!
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  CCM wanarushiana vifurushi vya kinyesi hadharani na kupakana matope. Chadema nao unasema wanaudikteta wa hali ya juu wakiongozwa na ndugu Mbowe. CUF umesema Seif anapenda mno mafungu na kutumbukiziwa coins kama phone box.

  Sasa ndugu Masatu, kama ushauri, ni uongozi wa chama kipi ulio bora ndani ya hili Taifa?!
   
Loading...