Rostam aibukia kanisani!

Utamsaidiaje Mtikila mtu ambaye aliwahi kumtukana hata muasisi wa CCM Mwalimu Nyerere? Hapa kuna jambo. Inaelekea kuna watu ambapo wako kwenye payroll ya fisadi RA wanachukua mabulungutu kila wakiwa na shida na wakati huo huo kujionyesha kwamba wanaisagia CCM na viongozi wake hasa kuhusiana na ufisadi.

Ndio nilikufahamisheni Siasa za kupandiliana migongo sio siasa wala umahili.Na siasa za namna hii nyingi ni za staili ya encapsulation yani kutumia mgongo huo kujipatia umaarufu ama una owasakama wakupoze kwa vi m kadhaa.
 
Sasa kama Mtikila anaanguka kwa Tsh.3m tu ,Je ataweza kukataa vijisenti????
Suala la jina lake au la kanisa au la chama chake kwenye hiyo risiti bado ni issue nzito!..hapa tunaangalia movement of money kutoka kwa Rostam kwenda kwa Mtikila au Kanisa analoongoza Mtikila au chama ambacho mwenyekiti wake ni Mtikila period.!!!

Kwanza kabisa inabidi ajibu maswali yafuatayo:

-Kwa nini akakope au kuchukua mshiko kwa Rostam Aziz na si kwingineko tena kwa mtu ambaye anatuhumiwa kwa rushwa na ufisadi??

-Kwa nini alikaa kimya baada ya kukopa au kuchukua mshiko huo????

-Je mpaka sasa ameshachukua mikopo au mishiko mingine kutoka CCM au magabachori au mafisadi au viongozi wengine wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi?i???

-Terms na conditions za mikopo au mishiko hiyo ni zipi???

-Majina ya mashuhuda kwenye malipano hayo yapo???
 
Kama Mtikila anaitwa fisadi kwa kukopa au kupokea fedha kutoka kwa RA, je, wananchi waopokea fedha za mkopo kutokana na zile zinazoitwa mabilioni ya Muungwana nao tuwaite mafisadi kwa sababu Muungwana yumo katika list of shame?

Yeyote atakayepata bahati ya kupewa fedha na mafisadi azichukue na kuzitumia mradi tu kitendo cha kupokea fedha hizo hakimfanyi anyamaze kuwakemea mafisadi. Hizo fedha walizonazo mafisadi ni za wananchi wote na kwa maana hiyo wananchi wakizipata kwa kupewa wana haki ya kuzipokea na kuzitumia. Vinginevyo tutabaki kulalamika na kulia tu oooh Mafisadi, oooh Mafisadi, huku mafisadi hao wakiendelea kunenepa kwa kutunyonya damu yetu na jasho letu sisi wananchi tukiendelea kudhoofika na kupiga miayo tu kila siku!

Bravo Mtikila umeonyesha njia! Tukipata nafasi ya kuzipata fedha za mafisadi sharti tuzile. Ila tusikubali kuacha kuwakemea Mafisadi kwa ufisadi wao hata kama ni marafiki zetu.
 
Mtikila anena: Kumfikisha Rostam kwenye vyombo vya sheria. Rostam aligushi stakabadhi. Mtikila anazo stakabashi halisi. There is no mention of a church. Nilikopa deni binafsi kwake, sio kanisa. Asitake kuficha aibu ya kugushi, kusingizia milioni tatu. Nitamlipa. Alinikopa mimi. Sio kanisa, na kanisa lenyewe lipi hilo (inaonyeshwa stakabadhi, yaani, ni kama Mtikila anavyosema... contribution to a church! .. which church?)

1. Bunge lipitishe muswaada wa kuwachunguza hawa viongozi wawili, yaani Mbunge Rostam na kiongozi wa upinzani Mtikila, kuhusiana na kupeana kwao hizi hela, halafu pia sheria iangaliwe kama kuna sheria za TRA zimevunjwa hapa, kwa sababu je hela hizi zimelipiwa kodi kama sheria inavyosema?

2. Rostam sio benki au taasisi ya kukopa na kurudisha, huyu ni kiongozi wa taifa, tena rafiki wa karibu sana wa Rais wa Jamhuri yetu, sasa kweli badala ya kuwahimiza wananchi kwenda kukopa na kurudisha benki ili kuendeleza uchumi wa taifa letu, yeye anatoa hela kinyemela na kudai ni mkopo? Hivi kuna wananchi wangapi wa hali ya chini huyu Rostam amewahi kuwakopesha? Hiii ni rushwa hii kama nilivyosema majuzi kuwa CCM ina baadhi ya viongozi hufanya uhuni wao wenyewe na kujaribu kutafuta credit kwa mwenyekiti wa CCM, this is one of the things na viongozi niliokuwa ninasema.

3. Mtikila sasa anyamaze maana ukiweli uko wazi sasa kuwa na yeye ni fisadi tu kama Rostam, yaani unatukanaje hela ambazo na wewe pia umewahi kupewa na fisadi! This is a shame hata hao waandishi wa habari wangemfukuzilia mbali, huyu ni fisadi tu hana lolote, na ndio tabia yake hii, hata kule US aliwahi kukoipeshwa na mama mmoja dola karibu $ 1000 mpaka leo hajalipa wala kumpigia yule mama simu, huiyu ni fisadi ni afadhali anyamaze, ndio maana huyu fisadi anakuwa jeuri huyu!

Hakuna cha kughushi wala nini Mtikila nyamaza tu ukubali yaishe, huyu ni mnafiki na mfisadi, tena ni mtu hatari sana huyu Mtikila, baada ya kuongea huuu utumba ndio kabisaa ni fisadi huyu, sasa Rostam aombwe ili aseme ni viongozi gani amewahi kuwakopesha, ili muone aibu itakayotokea!

Mtikila sasa basi baba kumbe na wewe ni wale wale tu, sasa kaaa pembeni na hii vita vya mafisadi huviwezi! na usilete vitisho mbuzi hiyvo na wewe ni fisadi tu!
 
Sielewi anamaanisha nini kuwa alikopa kama mtu binafsi, yaani RA amekuwa benki au SACCOSS kwanini akakope pesa chafu na kuzisaidia kuwa pesa safi? hapo mch. amechemsha kwani tayari credibilty yake kama mpinzani na mwana harakati wa kufuta ufisadi imeingia doa.

Washauri wake mshaurini aombe msamaa kwa fisadi mwenzie waendelee kura pamoja pesa za nchi kwani na yeye ni fisadi vilevile kwa kusaidia fisadi kusafisha pesa chafu.

Tuambie ni wapi palipo na fedha safi! BOT, CRDB, au? Fedha za EPA zilizoibwa BOT, zililipwa vipi bila kupitia Bank unazosema ndiko Mtikila angekwenda kukopa? Je, una hakika gani kwamba fedha za huko Bank ndio safi hazihusiani na mafisadi? Bwana, ufisadi upo kila mahali na Mafasadi pia wapo kila mahali. La muhimu ni kupambana na ufisadi huku tukila na mafisadi lakini sisi wenyewe tukijiepusha kufanya vitendo vya kifisadi. Fedha waliyo nayo mafisadi ni yetu, hivyo tuna haki ya kuila tukiipata.

Badala ya kuwaachia mafisadi wale peke yao, ni vema tule nao maana ni fedha yetu. La msingi kama nilivyosema hapo juu, tujiepushe na vitendo vya kifisadi na tusinyamaze kuwasuta mafisadi hata kama tumepokea fedha kutoka kwao.
 
"Mtikila alipoulizwa zaidi, kwamba hata kama ni mkopo, vipi alikopa fedha kwa mtu ambaye amekuwa akimuita fisadi na mwenye kumiliki fedha chafu kwa kuwa pia alipinga Rostam kutoa fedha kwa KKKT, alijibu:
"Ni kana kwamba zile fedha si chafu ni za nchi yetu, ni za serikali yetu sema tu matumizi yake na amezipataje" Gazeti la Mwananchi.."



What a joke huyu mtu Mtikila is? Nilisema siku nyingi kuwa hawa ni wahuni na wamo kwenye payroll hawa yaani this is embarrassing!
 
Aibu iliyoje kwa Mtikila na upinzani!! kama kweli alichukua fedha au mshiko wowote kutoka kwa Rostam au kwa gabachori yoyote ni wazi kuwa njaa na kuendekeza umasikini inauwa upinzani nchini mwetu.
Tumekuwa tukisikia tuhuma hizi kuwa kuna wapinzani kadhaa huwa wanavuta mshiko kimya kimya kutoka CCM na kuharibu upinzani sasa hili liwe fundisho kwa wananchi kuhusu wapinzani!!..Nadhani kuna haja ya kuwa na wagombea binafsi kuliko kutegemea watu kama akina Mtikila na wengine kutuongoza katika mapambo dhidi ya umasikini na dhuluma za CCM...


Wembe.

Wewe wembe mkali ! haya ni mambo ya kutupiana lawama tu, huyo Rostam Aziz alikuwa wapi siku zote kutamka hayo?
miaka mingapi imepita leo ndio kaamua kusema, au kwa vile kaona kaelemewa mzigo hivyo kaona pa kuutupa.
 
Tuambie ni wapi palipo na fedha safi! BOT, CRDB, au? Fedha za EPA zilizoibwa BOT, zililipwa vipi bila kupitia Bank unazosema ndiko Mtikila angekwenda kukopa? Je, una hakika gani kwamba fedha za huko Bank ndio safi hazihusiani na mafisadi? Bwana, ufisadi upo kila mahali na Mafasadi pia wapo kila mahali. La muhimu ni kupambana na ufisadi huku tukila na mafisadi lakini sisi wenyewe tukijiepusha kufanya vitendo vya kifisadi. Fedha waliyo nayo mafisadi ni yetu, hivyo tuna haki ya kuila tukiipata.

Badala ya kuwaachia mafisadi wale peke yao, ni vema tule nao maana ni fedha yetu. La msingi kama nilivyosema hapo juu, tujiepushe na vitendo vya kifisadi na tusinyamaze kuwasuta mafisadi hata kama tumepokea fedha kutoka kwao.

Nyie watu WOTE MNAOMPONDA MTIKILA...MKIJIBU SWALI HATA MOJA TU LA HUYU "MTU WA MUNGU"

Basi na mimi nitakubaliana na nyie...!

Wembe...Unajuwa tuko pamoja na maswali yako hapo juu ni muhimu.

Hata hivyo wewe na wengineo naomba muyajibu maswali ya huyu mtu anayejiita kuwa ni wa Mungu.

Kwani maswali yake hayo ni ya msingi na ndiyo yaliyonifanya hata mimi nisimtupe Mtikila moja kwa moja.
 
Watu wanaopigia kelele milioni tatu za Mtikila na huku ni wazi NCHI IMEUZWA WANA LAO JAMBO!

HATUTAKI CHUKI BINAFSI!

Tunataka TOGETHERNESS!

Wapinzani wote mjiunge na Mtikila kwani COALITION YAO SI YA KIITIKADI BALI YA FREEDOM TOGETHER WITH LAW AND JUSTICE.

Na kama kuna matatizo...Myarekebishe mara baada ya kuungana na kuudai UHURU WETU!

Mtikila HAKIKISHA COALITION YENU INAKUWA KUBWA NA MUNGU ATAWASAIDIA!

Nilishawahi kuwaambia watu hapa JF kuwa kama wapinzani wasiporudi pamoja..Basi COALITION YA KINA MTIKILA ITACHUKUWA NCHI!

Nasema hivyo kwani hadi sasa ni wao wamekuwa wakifanya mambo POSITIVE NA HII NI LICHA YA KWAMBA WABUNGE WAMEROGWA HUKO BUNGENI NA HATA CHA KUSEMA HAWANA!

Kwa mantiki hiyo basi...Siwezi kumwita Mtikila FISADI IN LEAU OF ROSTAM NA ccm NA HUKU WAPINZANI WENYEWE WAKIWA HAWAJATULIA!

Hata kama walimkopa...Basi ni zamu ya wazalendo na wao kuchukuwa madaraka ya nchi yao ili magabochori nao waanze kutukopa wazalendo!

Yani nyie mmesahau kuwa hata hao MASIKINI HAPO BONGO kila siku wanapitia maduka ya wahindi na waarabu na kuomba hata ela ya kula?

Kuna muhindi ama mwarabu anayekufa njaa licha ya kwamba si wazawa!

PELEKENI UTUMWA WENU MBALI!

MTIKILA MBELE!

JF MBELE!

WAZALENDO MBELE!
 
  1. Hivi kwenye watu wote anaowajua Mtikila hakupata wa kumkopesha 3.0 million??
  2. Why Rostam?? Why 3.0 million not 500,000 or 100 million?
  3. Zilikuwa ni za nini na wakati yeye anapata ruzuku??
Huu sidhani kabisa kama ulikuwa ni mkopo.

Na Stakabadhi je? Ruzuku ni kwa ajili ya chama au Mtikila binafsi? Lakini mbona RA hajaongelea bahari za DP, hii habari ya ruzuku inaanzia wapi?

Chuki binafsi kwa Mtikila nini?
 
Mimi msimamo wangu ni ule ule! siku zote hizo Rostam alikuwa wapi kuanika uovu wa mtikila, ama ndio yale ya ukimwaga mboga nitamwaga ugali?

kama ni kukopa hayo ni mambo binafsi, lakini sio uchukue advantage sababu unataka uonekane wewe ni miongoni mwa watu.
 
Na Stakabadhi je? Ruzuku ni kwa ajili ya chama au Mtikila binafsi? Lakini mbona RA hajaongelea bahari za DP, hii habari ya ruzuku inaanzia wapi?

Assumption iwe basi kuwa alikopa kwa ajili ya matumizi binafsi, school fees n.k. Otherwise kama ni kwa harakati za DP, ruzuku aliyonayo inabidi atueleze ilikoishia.
 
wether Alikopa Before Or After Report Ya Dr Mwakyembe Still Does Not Justify What He Is Going To Say At The Travertine Hotel.ra Was A Known Fisadi Siku Nyingi Sasa Kama Yeye Kamjua Ra Juzi Baada Ya Hiyo Report Sasa That Is What He Will Have To Answer To The Tanzanians.

Mtikila Ndugu Yetu Ni Afadhali Angetuliza Ball Tu Kelele Zoooote Kumbe Anazunguka Nyuma Kuvuta ,ina Maana Kelele Zoye Za Mchgj Huwa Ni Gia Ya Kutafutia Pesa Ama Kweli Tz Bado Kupata Wanasiasa Wa Kweli
 
hivi Mtikila anapata ruzuku, si najua kuwa chama chake hakijasajiliwa rasmi na msajili wa serikali kama chama cha siasa ingawa kipo,au?

Maana nilifikiri wanaopata ruzuku ni wale wenye wabunge tu, au?
 
Wewe pundit! Je? unaweza ukatuthibitishia mtikila ni fisadi kiasi gani!

Umefuatilia issue ya Mtikila, TIB na wahindi? Nyumba yake ilivyopigwa mnada halafu akarudishiwa kinyemela na wahindi?

What more do you need?
 
Mtikila Ndugu Yetu Ni Afadhali Angetuliza Ball Tu Kelele Zoooote Kumbe Anazunguka Nyuma Kuvuta ,ina Maana Kelele Zoye Za Mchgj Huwa Ni Gia Ya Kutafutia Pesa Ama Kweli Tz Bado Kupata Wanasiasa Wa Kweli

Hawa wanaopiga kelele halafu ikifika jioni wanaenda kupokea kitu kidogo wako wengi. Inabidi sasa tutengeneze list. Naongezea jina la Mzee Cheyo aliyesaidia kupasisha deal ya IPTL.
 
Unajua desparate people huwa wanafanya deparate things, sasa saaa inakaribia wote watasemwa maana Rostam sasa yuko desparate,

Sasa hivi anahamisha kila mali yake kwenye mikono ya wengine na zingine anahamishia Dubai na South Africa, ninaamini kuwa sasa hivi anatembea na pasport mfukoni, angalau ametaja hata mmoja Mtikila, sio kina Balali kimyaa huyu Rostam atawataja wote huyu wallahi atawachafua kweli!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom