Rostam aibukia kanisani!

Inajulikana kwamba Mtikila amekua akiishambulia na kuisakama CCM kwa muda mrefu.

-Mtikila amefungua kesi nyingi dhidi ya serikali ya CCM
-Mtikila amekua akiwashambulia viongozi wa CCM akiwamo Kikwete, Lowassa, Sumaye, Mkapa na hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

-Mtikila ndiye aliyeibua hoja ya ubaguzi wa rangi na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa kuwaita watu wenye asili ya Asia kuwa ni magabacholi
-Mtikila hakuwa na fedha na hana kipato, lakini sasa imebainika kwamba mfadhili wake mkuu ni Rostam Aziz, ambaye sasa anaanza kujivua gamba lake na kubaki na sura halisi

Rostam kama ameanza kumsema Mtikila na kuwageuka wanamtandao wenzake kwa kuwasema kwamba wanafanya ufisadi wa ngono hata wale ambao alikua akivinjari nao pale Sheraton/Royal Palm/Movernpick na baadaeye Kempisk na hata wale aliokua akikutana nao viwanja vya Dubai.

Hapo baadaye atawataja ama anawatisha kuwataja wale wote aliowafadhili katika chaguzi mbalimbali na hivyo hao CCM waliofadhiliwa na Rostam, wasijione wako salama kwani hapo baadaye akizidi kuchanganyikiwa atawataja wote hata wale wa juu kabisa wakiwamo wapinzani, waandishi wa habari, watendaji serikalini, wafanyabiashara na viongozi wa dini.

Kwa hiyo CCM wasichelewe, waanze sasa, wamhoji, maana sasa amechanyikiwa anaweweseka, atasemsa hata yasiyostahili, kama si hadharani atasema huko vichochoroni
 

Laiti Mtikila angelikuwa anamtetea Rostam hapo angehitajika kusema huko nyuma kakopeshwa pesa ngapi. Lakini kwasababu alikuwa anamshambulia, hakuna conflict of interest hapo.

Tena inabidi tumsifu Mtikila maana urafiki pamoja na kukopeshwa lakini bado alisimama na kuwa tayari kuhesabika akimshambulia Rostam.
 
Acheni maneno mengi,ushabiki wa kidini,n.k
Tanganyika inahitaji mabadiliko kwa vitendo,R.A na wenzake ni mafisadi hakuna ubishi.
Lazima tuwang'oe hawa mashetani haraka iwezekanavyo.
 

Huenda ikawa Mtikila alikuwa kwenye payroll ya CCM muda mrefu...sasa ukweli ndio unatokea
 
Mtikila ni mfano tu wa tabia za wapinzani Tanzania na vyama vyao feki.Anayewaamini hawa shauri yake.
Kama kuna mtu aliweka poni nyumba yake kwa sababu ya sera za "saa ya ukombozi ni sasa" basi ajue kajiingiza hasara.na wale wanaoweka poni nyumba zao kwa sera za kuvaa magwanda ya mgambo pia wanajiingiza hasara, siku yao ya kudharirishwa hadharani inakuja.
 

HATUMWAMINI MTU..TUNA AMINI HAKI NA SHERIA!

MTIKILA AMECHAGUWA HAYO...TUTAMSIKILIZA...NA BADALA YA WAZALENDO KUKAA PEMBENI NA KUSUBIRIA ccm WAINGILE...NADHANI WAKIWA WOTE PAMOJA ITAKUWA RAHISI KUSIMAMIA HOJA NA HATA KAMA MTIKILA ANA YAKE YA TOFAUTI...Basi ataumbuka.
 
wanachama na viongozi wa CCM wanaruhusiwa na ratiba ya chama kukutana na wanachama wa vyama vingine na kushirikiana nao katika kujenga taifa, sio kama CHADEMA.
 
Nakubaliana na Tina kabisa bila hata chembe ya maswali.

Hatua hiyo ya kwanza ifanywe na Mwenyekiti wao(ccm) ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Yeye pia katishwa na ndio maana hasemi kitu zaidi ya kusubiri Rostam mwenyewe amwandikie Hotuba ama amshauri kuhusu masuala ya Bashir na mengineyo kama vile kudai kuwa vita ya UFISADI SI YA WANANCHI DHIDI YA SERIKALI YA ccm BALI NI YA WAFANYA BIASHARA WA KIHINDI KIARABU NA WEUSI.

Na ndio maana akamuachia Rostama ayahamishie makampuni ya UFISADI KWA MANJI ILI IONEKANE KUWA NI UGOMVI KATI YA MENGI NA WAHINDI NA WAARABU WASILAMU!
 

na wale waliyoiweka rehan serikali yetu kwa wafanyabiashara?
 
Unafiki na ubadharuli hatimaye unakuwa na mwishowake na siku zote mwisho wake sio mzuri hata kidogo.
 

Huo hapo juu ndiyo ukweli. Laiti Kama wana CCM wangekuwa na tabia ya Mtikila hawa mafisadi wangeshashika adabu.
Keep up Mtikila. Hujakosea lolote. Siku nyingine akikupa pokea na umsute. Alidhani kakuhonga ili usimseme?
 
Hajakosea Mtikila. Kama Rostam alimpa pesa ili asimlipue alikosea maana Bwana huyu ahongeki. Keep up Mtikila.
 

Mkuu nakubakubaliana nawe, dhana hii ingeweza kukomesha takrima kirahisi sana. Kwakuwa Watanzania wengi wameshindwa kukataa takrima za mafisadi, ni bora wakapokea LAKINI wasikubali kununulika. Kula kwa A kura kwa B.
 
Utamsaidiaje Mtikila mtu ambaye aliwahi kumtukana hata muasisi wa CCM Mwalimu Nyerere? Hapa kuna jambo. Inaelekea kuna watu ambapo wako kwenye payroll ya fisadi RA wanachukua mabulungutu kila wakiwa na shida na wakati huo huo kujionyesha kwamba wanaisagia CCM na viongozi wake hasa kuhusiana na ufisadi.
 
Mtikila ni Mpuzzi ..Hata akisema neno lipi hatutamuelewa,alienda kuomba Pesa?unaenda kuomba pesa kwa adui yako...Kuna Upinzani kweli??Mie nakwambia tukianza kutaja Majina kwa wale waliopo kwenye Payroll za Rostam Mtashangaa

Ujumbe poa,tatizo hiyo Avatar!
 

Hapa nimeona kuna wanaosema Mtikila ni mbaya kwa sababu kapokea pesa zile toka kwa Rostam na vitu kama hivyo !

lakini Rostamu mwenyewe hajawahi kufikiria kwamba huwezi ukanunua kila mtu

tumeona akina Lowassa, chenge , baba chilingi, na wengine wengi wakirudi majimboni mwao na kujisafisha baada ya kuona mambo hayaendi vizuri.

kisha Edo Lowassa mwenyewe alishawahi kwenda huko KKKT kabla hata ya Rostam , unaona ! hapa ndipo mwanzo wa picha , yale mambo yaliyosemwa awali kwamba ukimwaga mboga ninamwaga ugali.

Kuna sinema moja inaitwa '' Mr Smith goes to Washington ''

humo kuna mchezo wote wa kupakazana mavi,na jinsi kila mtu anavyopigana kuupata mkate wake wa kila siku .

Nisingependa kusimulia kila kitu lakini sinema yenyewe it is very funny:

Jamaa alipata nafasi u senator katika lile jengo kwa kupitia mgongo wa baba yake, kijana mdogo tu kama mimi!

ila alipofika Washington kwenye senate akajifanya yeye anajua ingawa alikuwa hajui lolote lile.

Siasa ni mchezo mtamu sana kwa wanojua kuucheza.
 
Breaking News on ITV:

Mtikila anena: Kumfikisha Rostam kwenye vyombo vya sheria. Rostam aligushi stakabadhi. Mtikila anazo stakabashi halisi. There is no mention of a church. Nilikopa deni binafsi kwake, sio kanisa. Asitake kuficha aibu ya kugushi, kusingizia milioni tatu. Nitamlipa. Alinikopa mimi. Sio kanisa, na kanisa lenyewe lipi hilo (inaonyeshwa stakabadhi, yaani, ni kama Mtikila anavyosema... contribution to a church! .. which church?)

Haya, mambo ndio yameanza. Waliokuwepo kwenye mkutano walete habari. Tukae mkao wa kula... Tutaona mengi kabla 2008 haijaisha... ni wakati wa historia...
 
Breaking News on ITV:

Mtikila anena: Kumfikisha Rostam kwenye vyombo vya sheria. Rostam aligushi stakabadhi. Mtikila anazo stakabashi halisi. There is no mention of a church. Nilikopa deni binafsi kwake, sio kanisa. Asitake kuficha aibu ya kugushi, kusingizia milioni tatu. Nitamlipa. Alinikopa mimi. Sio kanisa, na kanisa lenyewe lipi hilo (inaonyeshwa stakabadhi, yaani, ni kama Mtikila anavyosema... contribution to a church! .. which church?)

Haya, mambo ndio yameanza. Waliokuwepo kwenye mkutano walete habari. Tukae mkao wa kula... Tutaona mengi kabla 2008 haijaisha... ni wakati wa historia...
 
Mtikila inabidi aelewe au akubali kuwa

1. Mtu unapopewa fadhila makali yako na objectivity inapungua, unakosa uhuru.

2. Mkopo ni fadhila.

3. Watu tunaweza kuamini kuwa hata kama alikuwa anampigia kelele Rostam inawezekana alikuwa anam blackmail ili asamehewe deni ikiwezekana hata "akopeshwe" tena hela ambazo hatalipa.

4.Amekuwa na hiki kitabia cha kula na mafisadi, hii sasa ni pattern na wala si mara ya kwanza. Ana nyumba Mikocheni B kule karibu na maghorofa ya Bima, alishindwa kurudisha mkopo TIB, wahindi wakainunua nyumba ile na kumrudishia ili asiwandame.Mtu kama huyu hafai.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…