Mchungaji wa Kinondoni kama hakufuata taratibu za kanisa katika kutoa mialiko ya aina hii anastahili adhabu kali lakini nafikiri si sahihi kurudisha pesa ya RA kwasababu yoyote ile.
Kweli dunia imekwisha!!!
Sasa hilo kanisa, au huyo binadamu (askofu, Sheik) ambaye ana uwezo wa kuchambua fedha haramu na halali yuko wapi wajameni...!!! Tuache hizi siasa kila mahali hadi makanisani.
Mtu ametoa kwa moyo wake... mwenye kujua za halali au sio za halali ni Mola wake... acheni siasa wajameni!!!!
Mi nafikiri kabla KKKT hawajoa kauli dhidi ya Rostam,ni vizuri wangeanza kusafisha kanisa kwa kutoa kauli dhidi ya mlezi wa KKKT dayosisi ya mashariki Mengi Benjamin kwa kuwatapeli wazungu mabilioni na kushirikiana na kaka yake Reginald mengi kuwafukuza nchini wazungu baada ya kuwatapeli,.KKKT ndio kanisa linaloongoza hapa nchini kuwa na wafuasi tena ndio walezi wa kanisa wanaongaza kwa kufanya biashara chafu,nani hamfahamu Kibo MAREALE, nana hawafaham mengi na mdogo wake, nani hafahamu kuwa katibu mkuu wa KKKT mstaafu Hamza Mwenegoa ni fisadi wa kupindukia "MKUKI MTAMU KWA NGURUWE KWA BINADAMU NI MCHUNGU'Mkuu Gembe, nakubaliana na wewe moja kwa moja! Kosa si la Rostam Aziz, kosa ni la uongozi wa Kanisa KKKT Kinondoni. Kwanini hawakutoa taarifa za mwaliko wa Rostam kwenye uongozi wa juu? Hapa ndipo kwenye tatizo, lakini Rostam kama Rostam yeye hana tatizo!
Haya maneno mawili ndiyo nilikuwa nayata sana,ni mojawapo ya yale yatakayo kuwamo katika walaka wangu kwenda kwao1.Mengi Benjamin kwa kuwatapeli wazungu mabilioni na kushirikiana na kaka yake Reginald mengi kuwafukuza nchini wazungu baada ya kuwatapeli
2.KKKT ndio kanisa linaloongoza hapa nchini kuwa na wafuasi tena ndio walezi wa kanisa wanaongaza kwa kufanya biashara chafu,nani hamfahamu Kibo MAREALE, nana hawafaham mengi na mdogo wake, nani hafahamu kuwa katibu mkuu wa KKKT mstaafu Hamza Mwenegoa ni fisadi wa kupindukia "MKUKI MTAMU KWA NGURUWE KWA BINADAMU NI MCHUNGU'
...........Huu ni wakati mgumu kwa Taifa letu sababu hatujui kwa 100% ni nani mzalendo wa kweli na nani ni adui. Hivyo juhudi zozote zinazofanywa na watu, vikundi au jumuiya pamoja na za kidini katika kulinda heshima ya Taifa letu ni vizuri tuzikaribishe.............
na El Je Ambaye Ni Muumini Mzuri Tu Au Alipoenda Israel Kuhiji Alisamehewa. (kama Anatoa Sadaka Kanisani)
mbona KKKT wapo kimya kuwakemea mafisadi waliomo ndani ya kanisa kama mlezi KKKT dayosisi ya mashariki Benjamin Mengi,na Kaka yake ambaye ni mfanyabiashaara maarufu Reginald Mengi walowatapeli wazungu na kuwafukuza nchini,au michango yao ni mikubwa kwa kanisa,jamani nani hawafahamu wafanyabiashara haramu wengi ni wana jumuia ya KKKT.nani hawafamu akina Kibo Mareale na biashara zao ,nani hafahamu kuwa katibu mkuu nsaafu kwa KKKT tz AMZA MWAENEGOA,alivyokuwa fisadi kiasi cha kukataliwa na akina CLEOPA MSUYA waziri mkuu msaafu,hata ALIPOGOMBEA UBUNGE NA KUSHINDA ALMASHAURI KUU YA CCM LIKAKATA JINA LAKE,
Nina wasiwasi na katibu mkuu wa sasa inawezekana Mengi kamweka mfukoni."Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni",kwa hili KKKT wamemuonea ROSTAM,kama binadamu kama ana makosa ilitakiwa aombewe ili arudi kundini,tujifunze kutoka kwa yesu na zakayo,
Viongozi wa dini msichanganye siasa na dini
La Rostam linafahamika,ila hili la wao kama kanisa leo kuona kwamba ndiyo wamekosea..walikuwa wapi ?Kurudisha pesa au kutorudisha hakubadilishi status ya Rostam Aziz. Fisadi ni fisadi tu. Kwanza kama ametoa hizo pesa kama mchango ni kwamba anarudisha tone la azoiba. Kama watarudisha ina maana kuwa wanamrudishia pesa mwizi, kama hawazitaki niafadhari wapelekewe yatima kwa sababu nao ni zao.
La Rostam linafahamika,ila hili la wao kama kanisa leo kuona kwamba ndiyo wamekosea..walikuwa wapi ?
Jamani pamoja na maneno mazuri yote watu mnanakili toka ktk vitabu vitakatifu.....lakini hatuwezi kuacha kukuemea uovu eti kwa sababu.....sijui nani alifanya nini huko nyuma.....
....haya maneno ya Mungu tunayoya-quote.........yanahitaji pia busara kuyatafsiri katika hali halisi ya matendo yetu ili tujenge jamii zilizo bora......
.............kwa hii taarifa iliyosababishwa na Rostam.............napenda kusema ni mlango MZURI wa kuanza kujirekebisha pale tunapokosea/tulipokosea/tutakapokosea.......
Nikweli Gembe nakuunga mkono kanisa lilikuwa wapi, au nalenyewe nifisadi!
Kinachotokea hapa ni kwamba sasa nyimbo za Injili zimepoteza lengo lake la asili la "uinjilishaji". Kwa sasa zimegeuka kuwa biashara. Hivyo kupatikana kwa fedha kupitia nyimbo hizi kunatangulizwa mbele na uinjilishaji unaachwa nyuma. Rostam Aziz ni tajiri wa Richmond, si alialikwa aweze kumwaga fedha? Mwashangaa nini? Je, angemwaga fedha yake bila kutoa 'neno'? Kanisani pale!!!.
Ndugu yao "Mmasai feki", Mmeru Lowassa alikuwa akimwaga Azania Front michango kwa mamilioni ya Richmond, alipowajibishwa alipokelewa Monduli kwa nderemo na bashasha wakiwamo viongozi wa KKKT (Askofu Laizer). Kwa nini mnashangaa kuwa VIP katika uzinduzi wa nyimbo za injili huko KKKT Kinondoni?
Eti mgeni kama huyo anafika kanisani bila viongozi kujua. Haya, lakini, fedha fedheha. KKKT jihadharini na mambo hayo.