Sasa tutakuwa wajinga kama Rostam akiwekwa kwenye kundi la wanaolitakia mema taifa. Kanisa sio sehemu ya kutoa hukumu nadhani mahakama ni sehemu inayoweza kutoa hukumu. Mtazamo wa kanisa au mtazamo wa waumini wa dhehebu hilo na watanzania kuhusu Rostam siyo hukumu, ametufanya tumuone hivyo kutokana na vitendo vyake. .
Mkuu
Mbona mnakuwa waoga sana hukumu iko wapi?
Kusema ukweli, kwani Dowans na mdogo wake Richie walikuwa hawalipwi mamilioni ya pesa kila siku? Mangapi tunasikia kuhusu huyu bwana kwanini kama anazungumza asiende moja kwa moja kwenye point zinazohusu ufisadi wake badala yake anakuwa kama mzee wa masasi?
Si tumesikia Serikali ikisema kuwa ni Dowans na mdogo wake ni makampuni ya mfukoni?
Sasa nani alikuwa anakinga mkono kuchukua pesa?
Kama anajulikana nikisema aliyekuwa anakinga pesa ni FISADI si ni haki yangu?
Mimi nawapongeza KKKT kwa kutokumungunya maneno, mbona Mkuu Dr. Slaa, na waheshimiwa wabunge wanaotutakia maendeleo walisema moja kwa moja kuwa hawa ni mafisadi?
Tusiogope kusema ukweli pale ambapo unatakiwa katika kuokoa Taifa. Tusisubiri eti mahakama kwa sababu hakuna wa kuwapeleaka huko. Kwani ni wangapi ni mafisadi na hawajafikishwa mahakamani?
Mimi bado nitaendelea kutoa wito maana hata waziri Mkuu amesema kwamba hawatakurupuka kuwakamata, sasa kwa nini mafisadi wasipelekwe au wasijipeleke wenyewe mahakamani hili wakajisafishe huko?
Kwa nini wasumbue vichwa vya watu mara msikitini, mara makanisani, mara misibani nk, nafikiri sasa watavamia hata harusi.
Wito, serikali kama imeshindwa kuwafungulia mashitaka na kuwapeleka mahakamani basi iruhusu wananchi wahukumu wenyewe na kuchukua hatua za kinidhamu dhini ya mafisadi hii itatuondolea ghadhabu za kuwasikia wakitukejeli kila siku.