2.Watuambie ni kwanini walimruhusu Askofu Dr. Laizer kumpokea Lowassa kule Arusha kwa mbwembwe nyingi na hawakumkea ili khali Mhe. Lowassa alikuwa na kashfa ya ufisadi.Kwanini wanamuonea Mchungaji huyu?Je Akofu Dr. Laizer alipewa baraka na Kanisa kufanya hivi?bila kunipa majibu haya huu niuonevu kwa mchungaji wa kanisa hilo na wengine.
Gembe, kwanza heshima mbele!
Pili kuhusu hii mada yako umechanganya mambo mengi sana, ambapo mengine yana majibu ya papo hapo na mengine ni kwa wale wenye kujua muundo na utendaji wa KKKT.
Kuhusu matukio ya "Askofu Laizer + Mh. Lowassa" na "Mch Massege + Mh. Rostam" yote yana sura ya kisiasa lakini yametokea katika mazingira tofauti.
Askofu Laizer alikuwa
mmojawapo wa waalikwa katika mkutano wa kumpokea Mh. Lowassa kule Monduli kwenye
uwanja wa mpira, wakati Mh. Rostam Aziz alikuwa
mwalikwa rasmi kwenye ibada iliyofanyikia
kanisani!
Sasa ukiangalia vizuri utaona tofauti hapo, kwanini KKKT imeweza kuingilia hili la Rostam, ni kwa sababu aliaalikwa kanisani (kama Mgeni rasmi) bila kufuata utaratibu wa KKKT, wakati Askofu Laizer alialikwa kama mtu binafsi na hata alipopewa nafasi ya kuongea kule Monduli aliongea kama mtu binafsi na si kama Askofu wa KKKT (ninayo hotuba aliyoongea naweza kukutumia).
Kila kanisa lina taratibu zake kuhusu mialiko ya watu (ususani wale mashuhuri) katika kushiriki ibada zake, na tena kwenye tendo kubwa kama lile ya uzinduzi wa CD ya kwaya. Utaratibu nijuavyo uko kama ifuatavyo.
Mchungaji Mkuu (KKKT Kinondoni) ---> Mkuu wa Jimbo (Kinondoni) ---> Katibu Mkuu wa KKKT (Dayosisi) ama Msaidizi wa Askofu Mkuu (Dayosisi). Katika hili la Rostam suala la mwaliko liliishia kwa pale pale KKKT Kinondoni halikwenda mbele kwa viongozi wa juu!! Kwa hiyo katika hili kuna walakini.