SEE ME
SEHEMU YA 25/50
Season three
MISSION X
******** Mr zengo alitamani ashtuke toka usingizi na kukuta anachoambiwa na grace kuwa ni ndoto, na siyo kweli randy haiwezi kuwa mtoto wake moyo wake na akili yake havikutaka kusadiki maneno ya grace.
"Unanitania?". Mr zengo akazungumza na kumtizama grace anayelia kwa kwikwi, akamshika mabega yake na kumtizama machoni, wote walikuwa katika hali mbaya ya majonzi
" Inawezekanaje"?
" Siku nayojifungua mtoto kuna mtu alimchukua". Akazungumza na akalia.
" Nani?"
" Don john".
Mr zengo akashtuka na kuzidi kuchanganyikiwa
" Nieleze ukweli wote".
Grace sasa hakutaka kuweka mambo siri alihitaji kila kitu kiweze kujulikana kwani kateseka sana mtaani sasa alihitaji aseme ukweli wake wote ili atakapokufa asidaiwe kitu, alihitaji kusema kila jambo.
"Mke wako alinifatilia sana akitaka kuniua alipogundua na mimba Yako, alifanya kila njama lakini alifeli,".
"Siku nayojifungua mtu wako wa karibu alikuwepo na alinisaidia, mkeo alikuwa karibu na Mimi alifanikiwa kunifikia, akitaka kuniua na kunipoteza duniani, kabla sijawa ki mahusiano na wewe nilikuwa natembea na mtu wako wa karibu".
Akazungumza na kumeza fundo la mate na kufanya Mr zengo amtizame kwa umakini zaidi.
"Mkeo alinishikia bastola siku nayojifungua akitaka kupiga tumbo langu risasi ila nikashtukia yupo chini na damu zilikuwa zikimtoka kichwani, alikuwa kapigwa risasi ya kichwa na mtu wako wa karibu". Mr zengo akameza mate na kuzidi kuchanganyikiwa akili yake ikawa ishamjua huyo mtu wa karibu ila alihitaji kupata uhakika zaidi.
" Alimuua mke wako ili Mimi na mwanao tubaki salama, pia alikuwa akinipenda ndiyo Maana akafanya hivyo, nikipata uchungu na nikajifungua mtoto wa kiume, na don john ndiye aliyemuita Randy". Akazungumza na kulia kwa uchungu
" Alimchukua mtoto wangu akiwa mdogo na kuniacha na watu wake walionisaidia mpaka nikawa vizuri, nilimuhitaji mwanangu ila hakunipa alisema anahitaji apite mikononi mwako awe kama wewe na akifikisha miaka 10 atakutambulisha kwake, siku mnakamata watoto wa mtaani kuwapeleka japani ile usiku nilikuwepo na nilimuona randy kwenye lile kundi la watoto baada ya ya don john kunionyesha, alikuwa ni mwanangu kweli, sikumshika ata mikono yake wala miguu yake wala kichwa chake, lakini macho yake yalikuwa Yako kabisa kipindi kile ukiwa bado kijana siyo kama sasa".
Mr zengo majonzi yakazidi kumshika
" Umemuua mtoto wako don john Amenambia kila kitu".
Mr zengo akaanza kulia kwa uchungu moyo wake uliuma na kujiona mwenye hatia, alihisi amefanya dhambi kubwa ambayo Mungu haiwezi kumsamehe, akamkumbuka randy na kujikuta akizidi kulia kwa uchungu baada ya kukumbuka ile siku anayompa mateso makali na moyo wake ukawa unauma kwa mateso Yale hakujua kwanini alimuonea huruma randy sasa alitambua damu ni nzito kuliko togwa..
" Don john". Akawaza kichwani mwake, na taswira ya mary ikaja kichwani mwake akamkumbuka jinsi alivyokuwa anamtumikisha kingono mke watoto wake, tena kukiwa na mjukuu wake ndani, akajikuta akisimama na kuuma meno yake kwa hasira, sasa alihitaji kutubu dhambi zake, alihitaji kurudi kwa Mungu na kumsujudia, akitaka kupokea huruma toka kwa muumba.
Lakini moyoni mwake akawaza kuua mtu ndiyo alihitaji kumuua don john kabla ya yote..
Grace akazidi kulia na kuanza kukohoa akaziba mdomo wake na kukohoa huku akionekana kupata maumivu makali zaidi, mr zengo akatoa mikono ya grace kwenye kinywa akashtuka baada ya kuona mikono yake ikiwa imejaa damu..
" Nini hiki"?
" Nina cancer ya damu". Akazungumza kwa uchungu na kufanya Mr zengo ashtuke na kupata majonzi zaidi.
" Daktari kanambia nina wiki chache sana za kuishi". Akazungumza na Mr zengo kumkumbatia kwa nguvu.
" Nipereke mlipo mzika mwanangu au mlipomtupa nikaone ata mifupa yake au kama mbwa wako walikula nyama yake nipereke kwa huyo mbwa nimuone". Akazungumza na kufanya Mr zengo kulia kwa uchungu mpaka kamasi kumtoka.
" Hajafa". Mr zengo akazungumza. Grace akajitoa kifuani na kumtizama Mr zengo kwa mshangao
" Don john alisema kafa".
" Yupo gerezani". Mr zengo akazungumza.
" Mmh uongo".
" Niamini Mimi". Akazungumza kwa sauti ya chini zaidi.
" Nataka kumuona".
" Nitatuma watu wamtoe na kumfanyia upasuaji wa macho yake".
" Sawa".
***************
Moyo wake haukuwa na amani alihisi siku zake zimefikia tamati, kila akikaa alihisi kujutia juu ya makosa aliyoyafanya miaka mingi iliyopita, wivu, hasira na chuki vilitawala moyo wake Wakati ule wa zamani, hakutaka kumuona Mr zengo akiishi kwa furaha na mtoto aliyezaa grace mwanamke aliyempenda kupita maelezo, akitaka kumuweka mtoto yule mbali na baba yake na alifanikiwa kufanya hivyo, hakutaka kumuua Maana alitoka kwa Mwanamke ampendaye, sasa alijihisi hatia, moyo wake ukamwambia kwa sasa yupo sehemu hatari zaidi akakusanya pesa za kutosha zaidi ya dola millioni mia mbili, na picha zake muhimu akachukua visa na pasipoti za kisafiria alihitaji kwenda mbali nje ya nchi ulaya ilipo familia yake, ni Don john.
************
Siku ya sherehe ya jeradi ikafika na mage watu wakubwa mbali mbali walikuwepo na watu wa kawaida wapatao 30 na randy alikuwa ni mmoja wapo, kazi yake kubwa ilikuwa ni kukamata kuku wake,.
Sikutaka nijulikane nikaenda sehemu ya jikoni iliyokuwa ndani kabisa ya ukumbi huo mkubwa, nilimuhitaji kupata kofia na mavazi ya kipishi.
" Samahani njoo mara Moja" .nikazungumza na mpishi mmoja aliyenipita na kutaka kuingia jikoni, nikatizama kamera na kuona ikigeuka upande wa kulia na Mimi nilikuwa wa kushoto, alipofika nikambinya shingo yake kwa haraka na akazimia na nikamdaka asidondoke kama mzigo, nikamburuza na kumuingiza jikoni na bahati nzuri hapakuwa na kamera wala mpishi mwengine, nikamkokota na kumvua nguo zake za kipishi na kofia kisha nikamlaza chini ya meza kubwa ambayo juu ilikuwa na imekandiwa ngano na chini kulikuwa na Giza kwahiyo asingeweza kuonekana kirahisi, nikavaa mavazi yale na kutoka mule ndani ya jiko.
." Unafanya nini huku wenzako wanahudumia kule".
" Samahani ". Nikamjibu mzee mwenye suti aliyeniuliza baada ya Mimi kufungua mlango
" Wahi haraka we namba ngapi kwanza"?. Akaniuliza nikajikuta nikiropoka tu
" Nane".
" Sasa unafanya nini huku ulitakiwa kuwa kwa Mr zengo kule"
Akafoka na nikafurahi kimoyo moyo
" Samahani mkuu". Nikazungumza na kuondoka chapu huku mzee yule akiendelea na taratibu zake nikafika ukumbini na kumuona jeradi akiwa amesimama huku akiwa na Pete ya uchumba mkononi, hiyo siku ilikuwa ni ya kumvalisha Pete ya uchumba mage. Mage alikuwa amesimama na jeradi kapiga goti Moja chini, nikataka kuona kama mage atakubali ila nikamuona Mr zengo akinyanyuka toka kwenye kiti na kuondoka na akafatwa na mlinzi mmoja nikataka kumfata chapu kwani alikuwa anaenda chooni, mkono wangu ukashikwa na mikono milaini, na nikavutwa na kutolewa eneo ilo la mlangoni nililiokuwa nimesimama, ilikuwa ni mlango wa kuelekea jikoni kule... Mtu huyo akanibana ukutani na kufanya nishtuke kwani alikuwa ni X ( rose,Diana)
Je nini kitaendelea......
Usikoseeeeeee...
See me
Season three
Mission x
Maoni Yako muhimu................