SEE ME
CHAPTER THREE...
SEHEMU YA 16/50
(THE KEY)
Mkutano wa siri ulikuwa umewakutanisha viongozi wakubwa wa nchi pamoja na wafanyabiashara wakubwa haramu ndani ya nje ya nchi na ndani ya nchi ulikuwa mkutano wa watu 8 pekee uliofanyikia katika chumba cha siri, kilichojaa ulinzi wa kutosha kila kona nje na ndani ya chumba icho ambacho kilikuwa ndani ya jengo kubwa la kifahari, meza ilikuwa na maji ya kopo na glass ambapo kila mmoja wapo alikuwa na kopo la maji na glass moja huku wanne wakiwa wamekaa upande wa kulia na wanne wengine upande wa kushoto huku kiti kilichokuwa kipo mbele yao kilikuwa hakina mtu aliyekikalia. Kilikuwa kiti tupu na inaonekana mtu anayekaa hapo ndiye aliyekuwa akisubiliwa kwa hamu na kundi ilo la vigogo.
" Mheshimiwa anaingia" .Sauti ikasikika kwenye vipaza sauti vilivyokuwa vimefungwa ukutani,na vigogo wale wakasimama na kuinamisha vichwa vyao chini kumpa heshima mtu huyo aliyeingia, Uso wake ulikuwa Umefichwa na kinyago cha kutisha cha mwana sesele, akafika na kuketi kwenye kiti na wale wazee wengine wakaketi kwenye siti zao,
Mtu yule mwenye kinyago akawatizama kwa sekunde kadhaa kisha kutingisha kichwa chake ghafla taa ikazimwa ndani ya chumba icho kikawa giza na kufanya wale wazee 8 waanze kuongea kwa chini chini, ghafla TV kubwa ikawasha ukutani na kufanya mwanga ule wa tv ujae ndani ya chumba kile, wazee wote macho yao yakatizama kule kwenye Tv ambapo hapo awali hawakuiona tv hiyo, haikuwa tv kama walivyodhani kwani waligundua ni mwanga uliopiga ukutani na ukaonyesha picha ya mtu ambaye kila mtu alimfahamu, alikiwa ni rais wa tanzania kwa wakati huo.
" kila mtu mnamjua kiongozi huyo". Sauti nzito ikamtoka yule mtu mwenye kinyago cha kutisha, ilikuwa sauti iliyotengenezwa ili watu wale wasimjue ni nani? Wanazungumza naye.
" Ndiyo tunamfahamu".Wakamjibu
" Kila mmoja aseme malalamiko yake".
Mtu mwenye kinyago akazungumza hakuwa na muda wa kupoteza alitaka kila jambo lifanyike kwa haraka haraka.
" Nitaanza mimi mheshimiwa nashukuru kwa kutusikiliza ni miaka sasa imepita toka huyu kiongozi aliposhika madaraka ya serikali amebadirika ametugeuka wakati tulimpandisha ili kusaidia biashara zetu ziweze kukuua lakini katugeuka anasaidia na kujali maskini raia wa chini kuliko sisi, kwa sasa navyozungumza kazuia biashara yangu ya madini sipati wateja tena toka nje na migodi yangu baadhi kachukua akidai ya serikali anasema hakuna mtu anayemiliki aridhi maisha yangu yanaenda kuwa magumu kama akiendelea kuwepo maana nadaiwa na bank sasa million 600".
" Mwengine"
" Nashukuru sana mheshimiwa mimi biashara yangu ya unga kwa sasa haipo sokoni soko linazidi kuwa gumu zaidi fanya kitu mkuu nirudi katika biashara yangu"
Kila mmoja akawa anatoa malalamiko yake juu ya rais aliyeko madarakani kila mmoja hakupendezwa na utawala wake kwani uliwanyonya matajiri na kuwanufaisha maskini.
" Tumuue mkuu".Wote kwa pamoja wakazungumza huku wakipiga meza kuwa wamekubaliana kumuua rais
" Mnataka tumuue na huyu kama waziri mkuu aliyepita miaka 5 "
" ndiyo mkuu"
" Kumuua rais ni shilingi billoni 2 za kitanzania"
" Tupo tayari mkuu"
" Basi BLack mamba watafanya hiyo kazi". Mtu mwenye kinyago akazungumza na kuwatizama kisha akasimama na watu wale wakisimama na kuinama mpaka alipoondoka huku wakipanga siku ya kukutana kupanga tarehe watakayomuua..
*****
Tarehe waliyopanga kukutana ilipofika kila mmoja akaja sehemu ile ya siri na kuketi vile vile kama siku chache zilizoptia huku wakiambatana na sanduku lililojaa pesa taslimu bilioni 2, hakuna tajiri aliyempenda rais kwa wakati huo.
Mtu mwenye kinyago akaingia ndani ya chumba kile na wale watu wote wakasimama na kumpatia heshima yake mtu huyo ambaye hakuna aliyemtambua hata mmoja toka waanzishe kundi ilo la kutetea biashara zao ndani ya nchi, kundi la kunyonya raia na kuwanufaisha wao, kundi la kupanga nani awe rais wakuongoze wanavyotaka ili biashara zao ziende na kama ukiwageuka wanakupoteza kwenye uso wa dunia, hawa ndiyo wanaopanga viongozi wa serikali katika chama chao awe nane? rais wa nchi wanamuandaa toka zamani ndani ya kundi lao ili waje wamperekeshe wanavyotaka ni chama kilichoshika serikali miaka mingi ni chama tawala kinachopangilia kila kitu ndani ya nchi na walimuweka rais madarakani lakini kawageuka ni lazima WAMUUE. Sasa walikutana kwa ajili ya kutimiza hitaji lao. Walipata upinzani toka chama chengine lakini walikuwa na kila kitu,walikuwa washawekeza ndani ya nchi walikuwa tayari na kundi la black mamba ambalo mafuzo walipata toka JAPANI, walikuwa wakiteka watoto wadogi na kuwapereka japani, watoto ao walifundishwa kuua tu na baadhi walifundishwa zaidi kusoma vitabu wengine walikufa vitabu viliwakataa vilikuwa vitabu vya kukufanya wewe usiwe binadamu wa kawaida upotee na kutoonekana mbele za watu na kama usipofanikiwa kitabu kilikuwa KINAKUTESA MPAKA KUFA
" Raisi atakuwa na mkutano kesho kutwa dodoma nishamuandaa muuaji wangu atamuua na kumsambaratisha kwa shabaha moja tu". Akazungumza mtu mwenye kinyago na wazee wale wakapiga mokofi kwa furaha
" Ametaka yeye kufa hatuna kosa"
Mzee mmoja akazungumza nka kufanya wazee wengine wacheke kwa bashasha.
" nchi itakuwa chini ya makamu kwa muda mpaka pale tutakamteua mtu mwengine kugombea kiti cha urais"
" Mhh mheshimiwa katiba inasema makamu atashika nchi kwa muda au atakuwa raisi kabisa".
" hatuendeshwi na KATIBA nchi tunaendesha sisi". Mtu mwenye kinyago akazungumza
" wakimuua tukutane nimteue mgombea urais atakayegombea miaka miwili ijayo hii miaka miwili acheni makamu ashike kwanza nchi mpaka mwaka wa uchaguzi".
" Sawa mkuu"
Wakafunga mkutano wao na mtu yule mwenye kinyago mlinzi wake akachukua pesa na wakaondoka..
******* ******
DIANA akuhitaji kupokea amri nyengine toka kwa Don john alichokifanya ni kuandaa silaha zake kwenda kufanya tukio la mauji ya rais kisha kupewa visa na kusafiri kwenda japan kwa ajili ya kumalizia mafunzo
" Diana ukimaliza kazi utaenda japan utapishana na Randy yeye ndiye atakuwa anakuja"
" oooh Nitapishana naye nilitamani nimuone kama ameiva maana mnamsifiaga sana"
" Ukifanikiwa kumuua rais tutakuita lile jina ambalo ndiyo mtu hatari zaidi kwenye kundi la black mamba"
" ooh X"
" ndiyo ukifanya kazi vizuri tutakuita X na ndiyo utasoma vile vitabu rasmi".
" sawa mkuu." Diana akamjibu don john na kuondoka huku akiwa na furaha moyoni mwake, akapanda pikipiki yake na kuwahi eneo la tukio kwa ajili ya kumuondoa rais alifika eneo la tukio kabla ya masaa mawilo ambayo rais ndiyo atafika akapenya mpaka juu ya ghorofa ambapo toka juzi alishajua atakaa eneo gani kufanya kazi yake, akatengeneza bunduki yake na kuiweka standby akachukua darubini na kutizama sehemu ya mkutano zilikuwa mita za kutosha mita zaidi ya 1000 sawa na viwanja kumi vya mpira uvichukue uvipange pamoja ule umbali wake sasa ndiyo alikuwa amesimama juu ya ghorofa refu ambalo mtu wa chini hawezi ona juu ya ghorofa ina maana bunduki yake ilikuwa ina uwezo wa kulenga umbali mrefu zaidi..
" akitoka kwenye gari muue"
Akakumbuka maneno ya don john akatizama msafara wa magari meusi kama 9 yanayofanan pamoja na misafara ya vyombo vya polisi kama pikipiki na magari yao, gari ya tatu kati ya yale 9 ikafunguliwa na akashuka rais na watu wakaanza kupiga kelele za kumshangilia alijaza watu kibao katika uwanja mkubwa wa shule ya msingi
Akasogelea haraka bunduki yake ya masafa marefu akawa anatafuta kichwa cha rais kiko wapo akawa anazongwa zongwa na mlinzi wa rais ila akutaka kupoteza shabaha yake akajitahidi na mwisho Diana akakipata akapata paji la uso la rais na shabaha moja tu ikamshusha rais chini na kufanya watu waanze kukimbia ovyo huku walinza wa rais wakijaribu kuokoa maisha ya rais lakini haikuwezekana alifariki hapo hapo
Diana wakati anashuka na bastola yake akapishana na mtu wa usafi ambaye akamuona mwanamke huyo mwenye begi refu na mwenye uzuri wa kipekee alishangaa anatoka wapi kwa vile mtu wa usafi alikuwa na haraka zake hakutaka kufatilia zaidi ya kuendelea na mambo yake huku maswali mengi yakiwa kichwani mwake diana hakujua kuwa mtu huyo atakuwa shahidi wa sura yake ni bora angemuua kwani kitendo cha kumuacha hai kilifanya aende japani kwa shida zaidi maana sura yake ilichorwa baada ya maelezo ya mtu wa usafi diana ilibidi achonge sura ambayo anaitumia mpak sasa akijulikana kama X
*********
MR kala hukukubaliana na uteuzi wa mtu mwenye kinyago baada ya kumchagua mr solo kama mgombea urais miaka miwili ijayo moyo wake ulijua ni yeye kutokana na nafasi yake kubwa kuliko wenzake 7 akiwemo na mr solo
" Ndiyo maana nilifanya vizuri kurekodi toka hap awali" Mr kala akazungumza na kutoa kishikizo cha suti yake hakikuwa kishikizo cha kawaida lilikuwa ni jicho dogo la camera ambalo limeungwa kitaalamu na kurusha kila kitu kwenye kompyta yake nyumbani yani alirekodi kila tukio toka mpango wao wa kwanza wa kumuua rais
" mtu mwenye kinyago lazima anichague niwe rais nitamtisha mpaka akubali ata kama uso wake hauonekani dunia kwa sayansi imekuwa wakichuja sauti yake nzito atajulikana ni nani tu au wakiscan kinyago chake".
Akawaza na kutabasamu huku tamaa ikimuingia
" ngoja miaka miwili iishe kwanza ndiyo nilipue jipu kwa sasa acha makamu amalizie muda wake mr solo hawezi kuwa rais". Akawaza mr kala na kuhifadhi video zile zote kwenye memory kadi aliyoiweka ndani ya funguo yake yenye katundu ka siri kakuhifadhi memory kadi kule kwenye kushikia funguo, ilikuwa ni funguo ya chumba chake cha siri na ndipo alipohifadhi memory kwenye mshikio wa funguo ile ya kisasa zaidi
**********
SEE ME
SEHEMU YA 17/50
Mwaka wa uchaguzi ulipofika mr kala hakutaka kulaza damu akamtafuta mtu wa kinyago kupitia email wanapotumianaga jumbe zao kukutana mtu wa kinyago akashtuka baada ya kuona picha ya funguo huku kukiwa na video alipoplay mapigo yake ya moyo yakaenda kasi zaidi baada ya kuona siku wanayopanga kumuua rais mpaka siku wanayosheherekea kifo cha rais
" Unahitaji nini?" Akamtumia sms
" nahitaji kiti"
" wewe ni nani lazima uwe kigogo mmoja wapo"
" upo sahihii mr mask nahitaji kiti lasivyo naonyesha dunia hii video".
" uoni na wewe utakuwa hatarini"
" vipi nikisema mimi ni mpelelezi isitoshe sura yangu haionekeni wenzangu wote nawaona hahaha na wewe pia uso wako wa kinyago lakini sayansi imeendelea utajulikana".
Akatuma sms kwa email huku akitamba
" ooh nimekujua wewe ni Mr kala maana kwenye video huonekeni"
" hahah wewe mjanja sana kumbe"
" kwanini unakuwa msaliti"
" Nahitaji kuwa raisi huwezi mpa urais solo"
" usingefanya hivi mr kala ungeandika barua na ungesikilizwa"
" hapana wote walimuunga mkono mr solo"
" vipi ukiwa rais tukakuua na wewe".
Akatuma jumbe na mr kala akaingiwa na woga kwani kundi ilo ni kubwa mno
" Kwa vile nishawajua huwezi niua maana video yako nitawapa watu wangu wote wa siri nitawapa amri nitakapo kufa waisambaze" mr kala akatuma sms kupitia email na kuweka emoj ya kucheka
" Sawa nitakusikiliza". Mr kinyago au mr zengo akatuma sms na kutoka hewani uso wake ukajaa hasira na jazba kwani hapendwi kutishwa na mtoto mdogo.
Simu yake ikaita na akaichukua na kupokea kwani alikuwa ni don john
" Mkuu Amidu amefanikwa kupenya kwenye kundi la mgombea mwenza na wamemuamini kwa sasa anafanya kazi vyema na maselo".
" Kazi nzuri sana kafanya"
" ila kuna shida mkuu,"
" kapewa kazi ya kumteka juliana wiki ijayo ili mr solo aachie fomu ya kugombea".
" Mwambie amteke utamtuma Randy kwenda kumuokoa juliana "
" mmmh"
" anaweza peke yake nahitaji muuliza solo kama kweli yupo tayari kuwa rais inabidi amuue mgombea mwenzake nitamuuliza kama anautaka urais kweli amwage damu maana siwezi mfanya kwa rais bila ya yeye kumwaga damu".
" sawa mkuu"
" Watumie vigogo wote jumbe kuwa kuna video ya siri tulirekodiwa miaka iliyopita na mr kala na hipo ndani ya funguo yake ya siri".
" mkuu una maanisha nachokisema".
" ndiyo mpatie kazi Amidu yule mr kala hawezi shindana na mimi mr kala familia yake ipo nje ya jiji mwambie amidu haende hapo akaiteke ili apate funguo"
" sawa mkuu"..
SEE ME
ITAENDELEA
ENJOY.........
NAHISI UNAANZA KUNIPATA .......
MAONI YAKO MUHIMU......