Story: The Worst Marriage

Story: The Worst Marriage

Status
Not open for further replies.

Chieffs

New Member
Joined
Aug 21, 2026
Posts
3
Reaction score
1
THE WORST MARRIAGE

SEHEMU YA 01

MWANDISHI:CHIEF

Siku zote asilimia tisini na nane ya wanawake au mabinti hutamani kuwa ifikapo miaka kadhaa, miaka ambayo inasemekana au kuonekana ni wakati sahihi wa mwanamke kuolewa basi wapate wenzi wa maisha yao na kuingia kwenye agano la ndoa.

Huku matumaini na matarajio ya ndoa yenye furaha na amani vikiwa vikubwa, na kuona kuwa wameweka heshima kubwa katika familia na jamii inayo wazunguka, lakini baadhi yao hufika kwenye ndoa na kukutana na hali ambayo hawakuitarajia.

Kila mtu kabla hajaolewa au kuoa huona ndoa ni kitu cha furaha sana kiasi ambacho anaona alie kwisha olewa/oa anafaidi sana tuseme kwa lugha ya vijana.

Bila kujua paa zinaficha mengi, ila laiti wange ona yaliyo ndani sidhani kama wangetamani hata kuisogelea, na nisinukuliwe vibaya tafadhali maana mtu anaweza hisi nasema ndoa ni mbaya.

No ndoa ni nzuri ndio maana Mungu aliiweka mara tu alivyo muumba mwanadamu hii inaama ni njema na pia nikitu cha agano zaidi, lakini pamoja na uzuri wa jambo hili kuna upande ambao ukiuona au kufika hutamani kukaa humo.

Ila kwakua tunapewa cheti kabla ya mtihani tunaingia tukijua mambo yanenda kuwa mazuri au tusema tunaenda kufaidi nacheka kama mazuri ila dah inatisha.

Msikilizaji/msomaji unaweza kuniita Evelyn Benard ni binti wa kitanzania nilie zaliwa Tanzania hii hii na kukulia humu, mimi bhana katika maisha yangu ya ubinti nilikuwa mmoja wa mabinti walio tamani sana kuwa na ndoa yenye furaha, baraka na kila aina ya jambo jema.

Na kwakua nilitamani kufikia huko nilijitunza na kumuomba Mungu sana, yes mi ni binti niliejawa na hofu ya Mungu maana toka nikiwa mdogo nimelelewa na kukulia mikononi mwa watu wenye kumcha Mungu.

Sina maana kwamba wazazi wangu ni wachungaji no, niwasharika wa kawaida sana katika kanisa ila niwatu walio jaliwa imani ya hali ya juu na kwa hiyo walitulea katika misingi bora ya imani.

Imani ambayo imekuwa mkombozi na salama katika maisha yetu, so katika makuzi yangu nilitamani sana siku moja nije kuishi ama kuolewa na mwanaume mwenye hofu ya Mungu na imani kama yangu.

Kwani niliamini kupata mwanaume ambae ana hofu ya Mungu kutanifanya niishi maisha ya ndoa kwa furaha na amani sana na nilihisi hivyo kwasababu niliona maisha ya wazazi wangu.

Watu hawa daima wamekuwa naupendo usio kifani, hivyo mara nyingi nilikuwa nikipiga goti na mwambia Mungu nipe mume kama baba yangu, yes nilimuomba hivyo tena kwa kumaanisha.

Na hata mara kadhaa nilimtamkia baba kuwa baba natamani ukifika wakati wangu Mungu anipe mume kama wewe, ila alikuwa ananikataza kwa kusema usiombe hivyo wala kutamani hivyo.

Bali muombe Mungu akupe mume wakwako alie kuandalia yeye nasi yule unae mtamani wewe, kwa tabasamu nilimwambia, "hapana acha niombe maana nikipata kama wewe nitakuwa na furaha kama alivyo mama.

Na hiyo ndio ndoto yangu", baba hakuwa na neno zaidi ya kuniangalia usoni kwa makini sana (nikama alikuwa anataka kuongea ila hakujua aongee nini).

Basi binti wawatu mie niliendelea kuishi na kufanya mambo yangu huku ombi la ndoa likiwa ombi la miaka yote, (nahisi kama Mungu angekuwa anachoka basi angenambia inatosha).

Maana toka napevuka hadi nakuwa binti mkubwa mwenye kujitambua haswa ombi langu lilikuwa lile lile sikubadilisha hata neno, na ili kuonesha au kuthamini maandiko na maagizo.

Nilihakikisha nautunza mwili wangu kwa kila hali, yes ni ngumu Sana kwa miaka ya leo binti kuingia kwenye ndoa akiwa bado na usichana wake ila mimi Evelyn niliweza.

Ninaposema niliweza sio story ama uongo, maana najua mtu anaweza kusema, yaani uolewe ukiwa bado hujaguswa haiwezekani labda utakuwa umeolewa ukiwa na miaka kumi naa huko.

Haiko hivyo my friend, nimeolewa na miaka 25 kamili na hapo nilikuwa tayari nimemaliza chuo, sasa wale wanaosema wanadada wanao soma chuo sijui ni malaya niwaambie si wote.

Mimi nimesoma chuo kwanzia mwaka wa kwanza hadi wa mwisho na sikuwahi, so haya mambo huwa ni chaguo japo kwangu nasema ni neema, maana kwa jinsi nilivyo umbwa, nimepewa muonekano ambao kila mwanaume lijali akiniona lazima atageuka.

Sio kwamba nina mzigo mkubwaaa no nina kishep changu kisicho chosha huku sura na rangi vikizidi kuupamba mwili na kufanya mvuto kuwa wajuu, kiufupi me mzuri tena sana.

Lakini pamoja na uzuri wangu wote nilifanikiwa kujitunza hadi kuja kumpata huyu Mr right wangu, nilimpataje tulifikaje kwenye agano la ndoa takatifu vuta kiti ukae tulianze safari kwa pamoja.

Kama ilivyo kawaida yangu kwa siku ya juma mosi niliamka asubuhi nikafanya usafi ndani na nje baada ya usafi nikachukua nguo na kufua na nilivyo maliza kufua nikaingia jikoni na kujiandalia chai.

Maana naishi mwenyewe, basi nilikunywa chai na baada ya chai nikaingia chumbani na kuwasiliana na baba yangu kipenzi ambapo nilitumia kama dakika 40.

Na baada ya maongezi marefu tuliagana nikaingia bafuni na kuoga kisha nikatoka na kuvaa nguo zangu nzuri nikachana nywele ambazo nilifumua usiku nikalala sijazichana.

So baada ya kuweka nywele vizuri na kuhakikisha kila kitu kiko safi nikachukua pochi na simu yangu kabla ya kutoka chumbani nikaomba ulinzi kwa Mungu maana barabarani kuna mengi hivyo kuomba ni muhimu.

Basi baada ya kuomba nikatoka na kwenda kupanda daladala moja kwa moja hadi sehemu ninayo sukaga, jamani hapa dar nina msusi mmoja tu, na asipo kuwepo huyo bora ni bane ila sio kusukwa na mtu mwingine (kichwa sio cha kushikwa na kila mtu, wanao jua wanajua/elewa).

So nilivyo fika nikafikia kuanza kusukwa maana nilitoa order toka jana yake (hii inaepusha kukaa sana) na nilivyo maliza kusukwa nikatoka na kwenda kufanya manunuzi ya vitu ninavyo hitaji.

Ambapo niliingia sokoni na baada ya kumaliza vitu vya sokoni nikaenda supermarket na huko ndiko nilipo kutana na huyo waubani wangu aka nyongo mkalia ini ama tuseme halal yangu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom