Simulizi Yenye Funzo la Maisha: "SINA CHAGUO"

Simulizi Yenye Funzo la Maisha: "SINA CHAGUO"

JJ FORMAR

Member
Joined
May 29, 2025
Posts
73
Reaction score
74
SINA CHAGUO
Simulizi tamu ya maisha, iliyosheheni visa na mikasa ya kuzisisimua hisia chanya za msomaji. Ukafumbuka macho uone, yazibuke masikio usikize kwa usahihi kila kilichotamkwa na kuzungumzwa na mwandishi kupitia wahisika bora waliochorwa kwa taswira za kuvutia.

Utavutiwa na mengi; yatakayouteka umakini wako, utamani kujua nini kiliendelea nje ya kile kilichoongelewa. Ni wazo la mwandishi kwamba ukajizatiti zaidi kunako maudhui mazuri yaliyofichwa ndani ya kila sentensi inayounda tungo tamu za simulizi hii.

Hakuna wazo hewa, kila aliyewaza alikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Aliyezungumza alilenga kufikisha kile kilichoujaza mtima wake. Macho hayana pazia, kuna anayeona kwa kukusudia mwingine akakusudiwa na alichokiona. Matendo ndiyo hutoa tafsiri halisi ya mtu.
✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️
Karibuni sana wapenzi wa simulizi. Leo naitambulisha kwenu simulizi hii tamu iendayo kwa jina la SINA CHAGUO. Mwandishi anakukaribisheni sana kutoa maoni, kwa wakati wote usomapo simulizi hii.

SEHEMU YA KWANZA.
(Hakika mimi sijui, Fungu jema kuchagua,)

Huenda kile nilichopitia enzi za utoto wangu ndicho kimeniumba na kunifanya niwe hivi nilivyo sasa. Mimi ni nani? Swali hili huzisumbua sana fikra zangu kila nikiutafakari uhusika wangu ndani ya simulizi ya dunia. Mala zote siachi kujiuliza chaguo lipi huwa ni zuri kwangu kupita yote, maana sijui kuchagua. Si kwamba sioni, hapana. Nimejaaliwa bahati ya kukutana navyo, jicho zuri la kuona na kuvitambua vilivyo vizuri. Huwa natamani sana kuvipata, lakini sina uhakika kama nimeshawahi kujutia kuvikosa. Kuna wakati huwa naafikiana na kile wakisemacho wengi juu yangu, “wewe si mtu wa kawaida, ni mtu wa ajabu sana; unayefurahia kupata au kukosa kile ukitakacho.” Wakati mwingine siafikiani nao, kwasababu huwa ninapatwa na hisia tofauti katika kukosa na kupata, ijapokuwa huwa ninalidhishwa na yote. Kipi sasa hunifurahisha zaidi? Swali hili ndilo limenisukuma kuyaandika haya machache, yamebeba mwanga utakaokuongoza, uone na kufahamu mengi juu yangu. Mwisho unishauri, NIMPENDE NANI, maana sijui kuchagua.
KARIBU
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏.

Tarehe tano ya mwezi wa sita, SALATOBA BUS, siti namba ishirini na tatu, saa 12:00 asubuhi. Niliyasoma maneno haya, nikayanena na kuyaimba ilimradi tu yanikae kichwani nisiyasahau nikiamini ile ilikuwa ni kalatasi tu ambayo ingeweza kupotea wakati wowote. Nilihakikisha nimeyakalili vema zaidi, nisiyasahau kama vile nilivyozisahau kanuni za mahesabu ya kukokotoa siku ya mtihani wangu wa kidato cha nne. Baada ya kuridhika na kile nilichokifanya, niliikunja kwa umakini kalatasi ile nikaitia ndani ya mfuko wa shati langu la kitenge nililolivalia, niliuamini sana mfuko huu kwakuwa haukuwa na rekodi mbaya ya kudondosha vitu vyangu. Hakuna lililokuwa mhimu kwangu kwa wakati huu; zaidi ya kuhakikisha usalama wa ile tiketi yangu ya basi. Nililazimika kwenda kituo cha mabasi kukata tiketi ili niwe na uhakika zaidi wa safari yangu niliyoitarajia siku tatu zijazo. Mda huu nilikuwa nikikatisha katikati ya vichaka vya msitu wa kipopo kwa mwendo wa harakaharaka sana; nikishindana na giza lililokaribia kuuteka uso wa dunia. Sikuwa na mzigo wowote zaidi ya begi dogo la mgongongoni, hivyo nilimudu vyema kutembea mwendokasi kwa namna ile niipendayo.

Japo nilibeba vitu viwili tu ndani ya begi langu, nilikuwa na uhakika usio na shaka kwamba ningepokelewa kwa shangwe na wadogo zangu mala nitakapofika nyumbani. Kwanza ulikuwa mfuko wa samaki pendwa aina ya mgebuka ambao ungelilazimisha tabasamu la mama yangu mzazi aliyewapenda sana samaki wale. Pili nilibeba pipi kadhaa za kijiti ambazo bila shaka zingenipatanisha vema na wadogo zangu, wasingesita kunisaidia kufua nguo zangu pale nitakapowaomba kufanya hivyo. Nilichagua kupitia njia hii ya mkato ili kuepuka gharama kubwa ya nauri ambayo ningelazimika kuitoa kama ningechukua usafiri wa kunifikisha nyumbani. Nilitembea mpaka pale nilipokaribia kijiji kwetu ndipo nikaanza kutimua mbio ili niwahi nyumbani. Siyo kwamba nilikuwa mshamba wa safari, hapana. Nilishawahi kusafiri mala nyingi tena safari ndefu ambazo zilinichosha na kunifanya nichukie kusafiri kwa wakati huo. Ule upekee wa safari ya awamu hii ndiyo ilikuwa siri ya shauku niliyokuwanayo. Safari hii imekuja kama matokeo ya wazo la mafanikio ya mda mrefu nililokuwa nalo...

Baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha nne ndipo nilianza kuionja radha halisi ya maisha. Wazazi wangu walifurahia sana kunipata nikiwa huru sasa, wakiamini ningewasaidia shughuli mbalimbali za nyumbani kabla ya kulejea tena shuleni. Kutokana na historia nzuri ya ufaulu niliyokuwa nayo, wazazi wangu, wanafunzi wenzangu, ndugu na wote walionijua; waliniamini sana linapokuja suala la masomo, wakaamini ningefaulu vizuri mtihani wangu. Imani yangu ilikuwa tofauti, nilitofautiana nao kwa kiwango kikubwa sana, nilikijua vema kile nilichokipanda hivyo sikuwa na matalajio makubwa. Imani yangu ilinisukuma kuanza kutafuta namna ya kutoka nyumbani, nitoweke kijijini mapema kabla matokeo hayajatoka kwani nilijua hakutokuwepo na maelewano tena. Mala kadhaa nilishawahi kumshuhudia mzee wangu akijigamba kwenye vijiwe vya kahawa kuhusu mimi, kwamba mwanae nilikuwa namba moja pale kijijini na hakuna mtoto wa yeyote angenizidi katika mtihani wa mwisho. Simlaumu kwa hilo, huenda ni kwasababu ya matokeo mazuri niliyoyapata katika mtihani wa kidato cha pili ndiyo maana aliniamini sana. Jambo ambalo wengi hawakulijua ni kwamba mambo yalishabadilika sana, ya jana yasingekuwa ya kesho. Ukweli huo niliujua mimi mwenyewe, ndiyo maana nilipambana sana, nikafanikiwa kuwashawishi wazazi wakaniruhusu kwenda kukaa kwa mjomba; zikiwa zimebakia wiki mbili tu kabla ya matokeo kutoka. Ruhusa hiyo ilikuwa zaidi ya fulsa kwangu, sikutaka kulaza damu hata kidogo. Niliondoka mbio pasipo hata kugeuka nyuma nikihofia kuiona aibu iliyoningojea.

Nilipokelewa vizuri sana. Mjomba na shangazi walinipongeza kwa kufanikiwa kuhitimu masomo yangu ya kidato cha nne, kisha wakanipatia rundo la ushauri kwamba nikishaenda kidato cha tano nihakikishe nasoma kwa bidii sana, nije kuisaidia familia yangu. Walinikumbusha kama nilikuwa mtoto wa kwanza; tena mwanaume, nikishafanikiwa itakuwa rahisi kuwawezesha wadogo zangu. Kusemakweli ushauri wao ulikuwa mzuri sana, niliupenda bure lakini bado sikuuzingatia. Sikuuzingatia kwa sababu sikuwa tena wa kuziishi ndoto zao. Nilibaki kujichekesha tu kama chizi, nikaitikia ahsante kwa ushauri mzuri, japo maneno hayo yalikuwa ya mdomoni tu. Moyoni niliumia, akili ikachemka maana sikuona utofauti wa hapa nilipo sasa na kule nilikotoka. Ilikuwa kama nimeruka maji nikakanyaga tope, nilihisi kinyaa lakini nikakaza; potelea mbali, bora lawama kuliko fedheha. Nilikuwa tayali inifike nusu shali kuliko shali kamili la kijijini kwetu, yaani kila mtu anicheke, si bora huku nisikojulikana. Nani angehangaika nami zaidi ya ndugu wachache tu walionijua? Siku zangu chache za kufurahia maisha ya utukufu kwa mjomba nilizitumia kuweka mambo sawa, nilielewa kwamba ule mda wa kula mema ya nchi ulikaribia kuisha. Nilianza kufanya kazi ndani ya karakana ya mjomba ya kutengeneza vyombo vya usafiri, pikipiki na gari chache zilizofika pale kijijini. Hiyo ndiyo fani pekee niliyoijua vema kwa kipindi hicho. Nikawa fundi gereji wa kujitolea.

Kudhalilika ni kubaya sana asikwambie mtu; maana hakuji peke yake, huambatana na jamaa zake ambao hukera sana. Dharau na kudharauliwa, fedheha na kufedheheka, masimango na kusimangwa, chuki na kuchukiwa, kejeli, kusemwa, kutukanwa, kununiwa na kukataliwa. Yote hayo niliyapitia kwa namna tofauti mpaka nikamkumbuka muumba wangu. Nikaanza kusali, kuhudhuria kanisani kwani ndiyo malezi niliyolelewa, yaani kumshirikisha Mungu wangu; magumu yangu.

Mpaka leo naamini ni Mungu alijibu maombi yangu kupitia njia ile ambayo ilinishangaza sana. Imani za kishirikina! acha ziwepo tu kwa sababu ziliniponya na mengi. Ilianza kama kauli ya mtu mmoja, mwisho ikasambaa, ukawa wimbo ulioimbwa na kijiji kizima kwa sauti nzuri zilizoyavutia masikio yangu kusikiliza. Atakuwa alilogwa huyu, siyo bure lazima kuna mchezo mchafu alifanyiwa na wenzake, yaani mtoto aliyekuwa namba moja kwa kila mtihani halafu leo hii afeli, lazima walimzungukia mbuyu. Imani hiyo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha ule uhusiano mzuri baina yangu na wazazi na ndugu zangu ambao ilifikia hatua wakaniona kama niliyewadhalilisha sana. Sasa kila mtu akawa ananihurumia, wengine wakidiriki hata kunipatia pole kwa yaliyonikuta, wakanishuri nimwachie Mungu kwani yeye ndiye hakimu wa kila mtu. Nilizipokea pole hizo, nami nikatoa za kwangu maana sikuwa gizani kama wao, niliijua siri ya maiti maana mimi ndiye nilikuwa muoshaji halisi. Licha ya yote hayo, bado baba yangu alikuwa mgumu sana, hakunikunjulia nafsi kama ilivyokuwa mwanzo. Ilinilazimu kukaa kijijini kwa miaka miwili, nikaijenga upya imani ya wazazi wangu kwa kuishi maisha ya kuwapendeza, maisha safi ambayo nadiliki kusema kwamba ndiyo yalikuwa maisha yangu bora sana. Zile tambo za baba yangu zikalejea tena, akaanza kujisifu kwamba mwanaye nilikuwa na tabia njema kuliko vijana wote pale kijijini. Hapo ndipo nilimshirikisha wazo langu la kurudi shule naye akaniunga mkono kwa zaidi ya asilimia miamoja. Kwa kutumia watu aliojuana nao alifanikiwa kunitafutia shule, mipango ya maandalizi ikakamilika. Sasa nipo najiandaa kwa safari, narudi shuleni kwa awamu nyingine nikiwa na kumbukumbu mbaya ya matokeo ya kidato cha nne. Naenda kuwa mwanafunzi wa chuo cha ufundi (VETA).

ITAENDELEA.
(Kila kitu kimeshakamilika, Simulizi ipo tayali. Ili kujua nini kiliendelea, tembelea uzi huu jioni ya kila siku kuanzia leo.)
 
(Uzuri siutambui, Ubaya kuung’amua,)

Narudi kusoma
 
TULIPOISHIA.
Kwa kutumia watu aliojuana nao alifanikiwa kunitafutia shule, mipango ya maandalizi ikakamilika. Sasa nipo najiandaa kwa safari, narudi shuleni kwa awamu nyingine nikiwa na kumbukumbu mbaya ya matokeo ya kidato cha nne. Naenda kuwa mwanafunzi wa chuo cha ufundi (VETA).

ENDELEA.
(Penye mbili sichagui, mwisho zikaniumbua,)

Kama wewe bado ni miongoni mwa watu ambao bado hawauamini uhalisia wa misemo ya wahenga, basi fanya ubadili imani yako; uamini sasa. Mwenzako nilishuhudia kweli na uhalisia uliojificha ndani ya kauli zao. Walisema usiku wa deni haukawii kukucha, ikawa hivyo kwangu. Niliona sekunde zikihesabu kwa kasi, halikadharika dakika na masaa vilikuwa mbio kuiwahisha ile siku niliyoisubiria kwa hamu sana, hatimaye ikafika. Saa kumi na mbili kamili juu ya alama ndipo safari ilianza. Pembeni yangu alikaa mwanamke ambaye sikuweza kumtambua haraka kama bado ni binti au mama mtu mzima, alikuwa ameuinamisha uso wake juu ya mkoba alioukumbatia kifuani mwake. Hakuitikia salamu yangu pale nilipomsalimia, nikaelewa huenda amelala au ni makusudi tu ameamua kunifanyia; kama zilivyo tabia za mabinti wengi wa mjini, sikujihangaisha nae tena. Nilikaa kwa kutulia katika siti yangu, nikamshukuru Mungu wangu kisha nikajiweka sawa kuanza kuifaidi ile raha ya safari yangu. Kwangu haikuwa safari ya kawaida tu, ya kutoka nyumbani kwenda chuo bali ilikuwa na maana kubwa zaidi ya hiyo. Ulikuwa mwanzo wa safari yangu ya maisha, kutoka kuishi maisha ya utegemezi nyumbani, sasa ninaenda kuyakabiri maisha ya kujitegemea kwa kiasi kikubwa. Kujua nitaishi vipi, nitakula nini, nitakunywa nini, nitalala wapi, yote hayo yangekuwa juu yangu. Kichwani niliwaza mambo mengi sana, kwanza kuhusu maisha yangu, mbili kuhusu namna nitakavyoishi huko niendako. Nilipanga nikaishi maisha safi yasiyo na shida yoyote. Pesa niliyokuwa nayo mfukoni ilinipa ujasiri mkubwa sana, nikaamini kila kitu kitakaa sawa. Mbali na yote hayo, bado moyoni nilikuwa na shauku. Shauku kuu ya kuishi maisha ambayo sikuwahi kuyafurahia vema hapo kabla. Maisha ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa sababu ya kufanya vibaya katika mtihani wangu wa kidato cha nne. Niliamini kwa wakati ule nilikosea sana; ndiyo maana yakanipata yote yaliyonipata. “Sasa ni wakati sahihi, ninaenda kuishi kwa uhuru. Nimeshakuwa mtu mzima,” nani angenisumbua? Hakika nilipania sana.....

Katikati ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani; ndipo safari ilipoishia. Abiria wote tuliokuwa ndani ya basi tukatakiwa kushuka, kila mmoja ashike uelekeo wake. Hapo ndipo niliweza kumtazama vema yule mwanamke aliyekaa pembeni yangu. Moyo ulinilaumu sana kwa ujinga nilioufanya, ukanishawishi kujutia kitendo cha kukaa kimya pasipo kumuaongelesha jirani yangu. Huenda ningekuwa muongeaji ningefanikiwa japo kuipata namba ya simu ya binti huyu aliyetokea kuzivutia sana hisia zangu. Alikuwa msichana mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo, umbo matata, rangi njeusi ya kukoleza, nywele ndefu na nyuma kabebelea mzigo wa…… “karibu sana kijana” Mawazo yangu yalikatishwa na sauti ya kiume ikinikaribisha ndani ya mji ule. Niligeuka na kumtazama, kisha nikamsalimia kwa adabu baada ya kumtambua. Alikuwa ndiye mwenyeji wangu niliyetambulishwa kwake na mzee wangu kipindi alipokuja kijijini kwetu kununua mazao. Nilimfahamu kwa jina moja tu la mzee Gelo, mfanya biashara maarufu wa mazao ya chakula kama vile mahindi, maharage na karanga. Biashara hiyo ndiyo ilimfikisha ndani ya kijiji chetu kinachosifika kwa uzalishaji wa karanga. Ilipomlazimu kutafuta mtandao wa wenyeji watakaomsaidia kuzunguka kijiji kizima na kukusanya mazao aliyoyahitaji, hapo ndipo akakutanishwa na mzee wangu aliyesifika kwa kazi yake ya udalali. Ukaribu wao ulikua na kuongezeka sana, mzee wangu alimuunganisha na wakulima wengi wa kijijini kwetu na vijiji jirani waliomuuzia mazao mengi kwa bei ndogo. Huenda aliamua kuja kunipokea yeye mwenyewe kama njia ya kuonesha kujali kwa mtoto wa rafiki yake aliyemsaidia kupata mazao ya bei ndogo toka kijijini; yaliyompatia faida kubwa baada ya kuyauza kwa bei kubwa mjini. Safari nyingine ikaanza kuelekea nyumbani kwa mwenyeji wangu, huko ndiko ningekaa kwa wakati wote wa kabla ya kuhamia chuoni.

Nyumba ya mzee Gelo ni kubwa sana, nyumba ya kisasa yenye kila kitu kinachohitajika kumfanya mtu kuishi maisha mazuri ya kifahari. Macho yangu yalivutiwa zaidi na mandhari safi yaliyokolezwa na mpangilio mzuri wa sebule dogo lililopambwa kwa maua mazuri. Kuta zake zilifichwa na mapazia yenye rangi ya kuvutia sana yalining’inizwa pande tatu za sebule ile; ukutani ilibandikwa runinga kubwa. Hapo nikaanza kuvuta picha ya nyumbani kwetu, nikalikumbuka sebule dogo lililopambwa kwa magazeti na picha za wachezaji maarufu wa mpira wa miguu na wanasiasa mashuhuri. Tabasamu la uchungu lilichanua usoni mwangu; nikakicheka kile nilichowahi kukiona bora kwa fikra hasi za kimasikini. “Bado nina kazi kubwa ya kufanya,” nilihitimisha kwa kuiambia hivyo nafsi yangu. Mzee Gelo aliniongoza mpaka ndani ya chumba cha kulala, akanitambulisha kuwa nitalala humo kwa muda wote nitakaokuwa hapo. Alinionesha maliwato yaliyokuwa chumba kidogo upande wa kushoto wa chumba changu, akanielekeza namna ya kuyatumia kisha akaniaga kwamba alikuwa arudi dukani kwake.

Dakika tano zilipita nikiwa bado nimesimama; nikitafakari hiki na kile kuhusu chumba kile. Kisha nikaanza kupanga vitu vichache vilivyokuwa ndani ya begi langu, nilijitahidi kuvipanga kwa umakini mkubwa ili nisiharibu mpangilio mzuri wa chumba kile. Mda huo masikio yangu yaliinasa kwa ufasaha sauti tamu ya kike ikibisha hodi nje ya mlango wa chumba chang. “Hodi! Hodi! Hodi kaka!” Nilijihisi msisimko fulani mwilini ulionipa ujasiri wa kuusogelea mlango, nikaufungua. Macho yangu yalikumbana na macho makali ya binti aliyesimama nje ya chumba changu, akinitazama kama vile anayenifananisha na mtu aliyewahi kumuona sehemu. “Karibu sana kaka mgeni, karibu chakula chako kiko tayari mezani,” aliongea harakaharaka maneno niliyoyasikia vema kisha akaondoka. Kitu pekee nilichoweza ni kupandisha na kushusha kichwa changu kama ishara ya kuitikia ukaribisho ule niliopewa, kisha nikamfata kule alikoelekea. Nisingeweza kujidanganya kubaki nyuma hata dakika moja kwani sikuwa nimeielewa vema ramani ya jumba lile kubwa, nilihofia kuchanganya maeneo au kupotea kabisa. Lakini pia sikutambua ni akina nani watakuwepo mezani kwa wakati huo ambao ningewapa taabu ya kunisubiria hali ya kuwa chakula kilikuwa tayali. Nilijionya kutofanya kosa lolote la kijinga ikiwa ndiyo kwanza nimefika ugenini nisikojulikana, nyumbani kwa mtu aliyeamua kunipokea licha ya kutokuwa ndugu yangu wa damu.

Hatua kama tano tu nyuma ya binti yule ndipo nilipokuwa, nilitembea kwa mwendokasi kidogo kujaribu kuendana na mwendo wa binti yule aliyetembea harakaharaka kama vile anakimbia au kukimbizwa. Nilimfata kila alikoenda, nikakatisha kila alikokatisha, mwisho nikajikuta ndani ya chumba chenye joto zaidi ya kule nilikotokea. “Jikoni” nililibaini hilo baada ya kuona mpangilio wa chumba kile, kulikuwa na vyombo vingi vya mapishi. Mwenyeji wangu alikuwa bize sana kupangapanga vyombo ndani ya kabati dogo la vyombo; sikua na uhakika kama ameniona hivyo nikajikohoza kidogo kutambulisha uwepo wangu eneo lile. Alishtuka sana baada ya kuniona, uwepo wangu ndani ya chumba kile ulimshangaza sana mpaka akaacha kufanya kile alichokuwa akikifanya. Akabaki kunitazama mimi niliyesimama wima kama mtu anayesubilia kupewa maelekezo fulani. Sikujua nini alichowaza juu yangu mpaka akanisogelea pale niliposimama, akanipatia kiti, eti nikae. Ningeanzaje kukaa eneo lile la jikoni, halafu nifanye nini? Hapo ndipo nililitambua kosa nililolifanya. Kitendo cha kumfata binti huyu pasipo kujua aendako, nikijiaminisha kwamba alikuwa akienda kule niendako; kilikuwa cha kijinga sana. “Nashukuru sana dada; hata hivyo siwezi kukaa hapa,” niliongea kisha nikatoka ndani ya chumba kile. Kichwani niliwaza mambo mengi yaliyonifanya kujiona bwege; niliyefanya vitu bila kutumia akili, nikaamua kurudi nilikotoka. Niliiona sebule ya nyumba ile, nikaingia nikiamini huko ndiko nilipaswa kwenda lakini sikuona kitu chochote kinachofanana na meza niliyoambiwa chai yangu iko tayari. Hali hiyo iliniudhi sana, hata hivyo sikuwa tayali kumfata tena binti yule, eti nikamuombe anielekeze ilipo meza ya chakula. “Kwanza sina njaa” wazo hili lilipigilia msumari uamuzi wangu kisha nikarudi chumbani kwangu. Baada ya kumaliza kuoga nilipanga kujipumzisha kidogo kupunguza uchovu wa safari; nikapitiwa na usingizi mazima.

Awamu hii ndipo niliamini mazingira huwa yana nafasi kubwa kuamua vipi uwe, nini ufanye na kwa wakati gani ufanye hivo. Kitendo cha kuupumzisha mwili katika mazingira mazuri ya chumba kile ilikuwa faida kubwa sana kwangu. Si kwa mwili wangu tu, bali hata akili na ubongo vyote viliifaidi faida ile, safari ikaendelea vizuri. Awamu hii mimi nikiwa ndiye dereva mwenyewe, siyo abiria tena kama ilivyokuwa mwanzo. Nilikuwa nimejipinda vyema nyuma ya usukani wa gari kali la kisasa, nikiliendesha kwa ujuzi na umahiri mkubwa sana. Pembeni yangu alikuwepo msichana mrembo kuliko wote niliowahi kuwaona maishani mwangu, yaani mke wangu au asali halisi wa moyo wangu. Mrembo huyu alikuwa akiuyumbisha mwili wake kwa mbwembwe; kufuatisha mapigo ya mziki mzuri uliotolewa na redio za gari langu, akionekana kuufurahia sana mziki huo.

Hongera sana mpenzi wangu, unajua bado siamini kabisa; hatimaye na sisi tumeweza kumiliki gari yetu wenyewe.” aliongea kwa sauti nyororo iliyozalisha ladha tamu masikioni mwangu.

Nilishakwambia mpenzi, lilikuwa suala la muda tu, na sisi tungefanikiwa. Kwani wao waweze wana nini, na sisi tushindwe tuna nini.” Nilijibu kwa kujiamini kisha nikakanyaga gia kuongeza mwendo wa gari. Maneno yangu yalimfurahisha sana, akanitazama kwa jicho la upole lililolegea kwa uchovu wa kusubiria kwa hamu kile lilichokitamani. Akaanza kujisogeza karibu yangu. Sasa nikawa nikilihisi kwa ukaribu lile joto lililozalishwa na mwili wake mtamu usiochosha kuuangalia.

Kwahiyo tunaelekea wapi mpenzi!” aliniuliza kwa sauti ya upole iliyoendana na pumzi zake zilizozalisha joto la ajabu usoni mwangu. Kitendo kile kilinipa raha sana, nikajihisi msisimko wa ajabu pale alipoupitisha mkono wake kifuani mwangu, akaanza kuzichezea ndevu zangu chache zilizochongwa kwa mfumo wa duara.

Tunaelekea kijijini kwetu.” Nilijibu kwa sauti nzito iliyoakisi raha niliyoihisi kwa wakati huo.

Weeeeee!!! Usitake kuniambia ndio unanipeleka kunitambulisha nyumbani kwa wazazi wako” aliongea kwa furaha huku akiuzidisha utundu mdogo aliokuwa akinifanyia. Awamu hii hakuishia tu kuchezea kifua na kidevu changu, mkono wake aliushusha eneo la nyeti zangu akaanza kukagua kama anayetafuta kitu kidogo alichokipoteza ndani ya msitu ule. Nilijihisi raha ya ajabu sana iliyousisimua mwili wangu, nikajikuta nikiyafumba macho yangu taratibu bila kupenda. Looooo!!! Nilichelewa sana kufumbua macho, sasa nilikabiliana uso kwa uso na roli la mafuta lililokuwa sentimita chache mbele yangu, Yalaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ngo! Ngo! Ngo! Ngo! Ngo! Ngo! Sauti ya kugongwa kwa mlango ndiyo ilinikurupusha toka kwenye ndoto mbaya iliyoulaghai ufahamu wangu.

Ngo! Ngo! Ngo! Mlango uliendelea kugongwa kwa nguvu, awamu hii mgongaji aliniita kwa jina langu. Niliamka haraka sana nikaenda kuufungua. “Karibu” niliongea baada ya kufungua mlango pasipo hata kumtambua vizuri mtu aliyekuwa nje. “Chakula kipo tayali, jiandae twende mezani,” niliufunga mlango baada ya kuisikia sauti hiyo. Bado nilikuwa na wenge la usingizi, kichwani nilichanganywa na kumbukumbu za ndoto nzuri yenye mwisho mbaya niliyoiota. “Hata hivyo ilikuwa nzuri,” nilijisemea wakati nikivaa nguo zangu. Dakika mbili baadae nilikuwa tayali. Wenge la usingizi limeshanitoka, sasa nilikuwa timamu.

ITAENDELEA
(Kila kitu kimeshakamilika, Simulizi ipo tayali. Ili kujua nini kiliendelea, tembelea uzi huu jioni ya kila siku kuanzia leo.)
 
TULIPOISHIA
Bado nilikuwa na wenge la usingizi, kichwani nilichanganywa na kumbukumbu za ndoto nzuri yenye mwisho mbaya niliyoiota. “Hata hivyo ilikuwa nzuri,” nilijisemea wakati nikivaa nguo zangu. Dakika mbili baadae nilikuwa tayali. Wenge la usingizi limeshanitoka, sasa nilikuwa timamu....

ENDELEA.
(Naepusha uadui, Kesho wakanibagua,)

Nikakumbuka vizuri kila kilichotokea. Baada ya kukumbuka kwamba nilitakiwa kwenda mezani nilishtuka sana, “mezani wapi?” kumbukumbu ya tukio la mchana ilinijia vema, nikakumbuka namna nilivyohangaika kupatafuta mezani bila mafanikio. Hapo swali likabaki moja kichwani, naeenda wapi? Haraka sana nilienda kuufungua mlango kumuangalia yule aliyeniita kama bado yupo au la! Alikuwepo, nilimuona binti yule aliyenikaribisha wakati wa mchana. Alikuwa amesimama kauegemeza mwili wake ukutani, bila shaka alinisubiria mimi. “Tayali?” aliniuliza baada ya kuniona nimesimama pale mlangoni. “Ndiyo” nilijibu kisha nikamuuliza kama watakua wamenisubiri sana. Akasema amelazimika kuja kuniita kwa mala ya pili baada ya kufanya hivyo kwa mala ya kwanza ikashindikana. Hapo nikaanza kumuelezea namna ilivyokuwa mpaka nikashindwa kufika mezani, “sikupajua mezani, ndiyo maana sikufika kwa wakati sahihi.” Hakunijibu chochote mpaka tulipoingia ndani ya sebule ile niliyoifahamu tokea mwanzo, mala hii kulikuwa na mabadiliko kwa kiasi kikubwa. Eneo la upana wa chumba kile ulikuwa umeongezeka mala tatu zaidi ya nilivyopaona mwanzoni, yale mapazia mazuri niliyoyaona mwanzoni hayakuwepo tena. Sasa kulikuwa kumebadilika sana, hata ile runinga kubwa iliyobandikwa ukutani haikuwepo tena. Mambo haya yalinishangaza sana. Nilipoangalia upande wa kulia mwa sebule ndipo nilipokiona kile ambacho sikukiona mda wote, “mezani” nilijisemea moyoni kisha nikasogea eneo lile baada ya kuelekezwa na binti aliyenifikisha hapo, yeye akaondoka.

Karibu sana Mhanuzi, na pole kwa safari ndefu,” nilikaribishwa na sauti tulivu ya mzee Gelo aliyeketi mezani; yeye na familia yake. Nilikaribia eneo lile; nikaketi juu ya kiti nilichooneshwa. Nikapata mlo wa pamoja na familia ya mzee Gelo. Ilikuwa familia ya baba, mama na watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike. Kwa wakati ule nyumbani walikuwepo wanafamilia watatu tu yaani mama, baba na kitindamimba wao, watoto wengine walikuwa na miji yao. Nilielezwa kuwa walikuwa wakiishi na wafanyakazi wawili wa ndani. Mama mwenye nyumba, yaani mke wa mzee Gelo alijitambulisha kwangu kwa jina la mama Eliza, kushoto kwake aliketi binti mdogo aliyetambulishwa kuwa ndiye Eliza mwenyewe. (Nasema mdogo si kwasababu alikuwa mtoto mdogo, ni kwasababu nilimuona kuwa na umri mdogo kwangu.) Niliyajua hayo baada ya maelezo marefu aliyoyatoa mzee Gelo akinitambulisha ndani ya familia yake. Hapo ndipo nilianza kupata picha kamili ya nyumba ile, japo kwa kiasi fulani sikuelewa mchanganuo wa watoto wa nyumba ile. “Vipi mama mwenye nyumba aitwe mama Eliza, halafu Eliza mwenyewe awe binti mdogo! kwahiyo huyu ndiye wadogo zake wameshaoa na kuolewa?” Nilijiuliza bila majibu. Usiku ule nililala nikiwa na furaha kubwa moyoni, si kwa sababu nimetambulishwa kwa wenyeji wa nyumba ile; ni kwasababu kesho nilikuwa ningefika chuoni.....

Mchana wa tarehe kumi ya mwezi wa sita ndipo nilifika kwa mala ya kwanza chuoni nilikopaswa kuanza masomo yangu. Niliongozana na mzee Gelo aliyesimama kama mlezi wangu katika mchakato wote wa kukamilisha usajili. Kwa kiasi fulani sikupendezwa na uwepo wake, ile namna alinisimamia kwa kila kitu iliniudhi. Yaani mimi mwanaume kuongozwa kila kitu na mzee, tena mbele ya umati wa vijana wengi wa rika langu? Roho iliniuma sana pale nilipowaona baadhi ya warembo wakikonyezana baada ya kushuhudia mzee Gelo akinilipia hela ya usajili; huenda walinichukulia kama mtoto wa mama, niliyedekezwa sana na wazazi wangu. “Mambo gani haya.” nilijisemea moyoni. Hata hivyo nisingeweza kuikataa sapoti kubwa aliyoionesha kwangu; alikamilisha kila kitu kwa hela yake ya mfukoni, mithili ya mzazi anayemhudumia mwanae. Taarifa ya kujaa kwa hosteli ilinifurahisha sana, nikajua isingewezekana tena mimi kuishi hosteli. Lazima ningepanga chumba mtaani, nikaishi yale maisha niliyokuwa nikiyaota; maisha ya uhuru wa kujiamulia nini nifanye na kwa wakati gani nifanye hivyo. Furaha yangu haikudumu kwa muda mrefu, mzee Gelo alilivalia njuga suala la mimi kukaa hosteli. Hakukubaliana nami nilipomueleza kuwa sikuwa na mpango wa kukaa hosteli, akidai kwamba ingenipunguzia gharama za maisha, ukizingatia mimi ni mgeni nisiyeijua mitaa ya jiji lile. Nilikubaliana naye kuepusha mabishano yasiyokuwa na lazima. Tokea utoto wangu sikuwa na mazoea ya kubishana na mzee wangu, hivyo nisingeweza kumbishia mzee Gelo ambaye kwa wakati huo alikuwa ni kama baba yangu. Nililidhia wazo lake la kukaa hosteli kwa wakati ule, moyoni nikapanga kuhamia mtaani mala tu nitakapokuwa mwenyeji wa mazingira. Baada ya mimi kukubali kukaa hosteli, changamoto ikabaki ni upatikanaji wa chumba maana kwa taarifa iliyokuwepo ni kwamba vyumba vyote vilishachukuliwa. Mzee Gelo hakuwa na wasiwasi na hilo, aliishia kutabasamu tu pale alipoangaliana na mwenyeji aliyetupokea. “Kufikia kesho kila kitu kitakuwa sawa,” ndilo jibu lililotolewa. Hapo nikaikumbuka misemo mbalimbali ya wahenga niliyokaririshwa kipindi nipo darasa la nne; Hakuna mkate mgumu mbele ya chai, pesa ni sabuni ya roho. Mpaka hapo nikawa nimekamilisha taratibu zote za usajili, ikapangwa kesho yake nije kuripoti mazima na kuanza mafunzo yangu.

Mimi huwa ni mpenzi wa filamu za mapambano hasa zile zinazohusisha mapambano baina ya wanajeshi waaminifu kwa taifa lao na magaidi waasi. Huwa napendezwa zaidi na matukio ya upande wa magaidi; vile wanavyotumia akili na mbinu kubwa kutekeleza matukia yao ya kigaidi mbele ya wanajeshi mahiri. “Yaani polisi wote hawa wanashindwa kumkamata jambazi,” sauti kubwa ilinitoka pasipo kutalajia kiasi kwamba nikageuza kichwa changu kuangalia kama kuna mtu yeyote atakuwa amenisikia. Mda huu nilikuwa nimejituliza mwenyewe sebuleni nyumbani kwa mzee Gelo; nikifuatilia filamu kali ya mapambano iliyorushwa moja kwa moja na chaneli ambayo sikulifahamu jina lake. Matukio ya filamu ile yalinifurahisha sana, nikajikuta nikichangia neno kama vile nilikuwa miongoni mwa wahusika. Sikuwa na kazi wala ratiba yoyote jioni ile, hivyo nilipotoka chuoni niliamua kukaa sebuleni ili nipitishe wakati kwa kuangalia filamu, kuepusha ule upweke niliouhisi kwa kukaa ndani ya jumba lile peke yangu pasipo uwepo wa mtu yeyote ambaye ningezungumza naye. Niliendelea kufurahia filamu yangu mpaka pale nilipohisi uwepo wa mtu nyuma yangu. Sikutaka kugeuka ili nimuangalie huyo aliyefika kimyakimya pasipo kunisalimia nikiamini angefanya hivyo, lakini haikuwa hivyo. Ilipita dakika moja kukiwa kimya, ndipo nikageuka halaka lakini sikumuona mtu yeyote. “Punguza wenge kwenye miji ya watu,” nilijisemea kimoyomoyo huku nikijipigapiga kichwa changu. Nilipoanza kuweka umakini kwenye matukio ya filamu niliuhisi tena ujio wa mtu, hapo nikageuka haraka kuangalia nani ananichezea michezo ya kitoto lakini sikuambulia chochote, hakukuwa na mtu. Jambo hilo lilinishangaza kidogo, nikawaza labda ni mwendelezo wa wenge langu. Mala hiyohiyo nilianza kuisikia sauti ya kicheko cha chinichini, teh! teh! teh! nikageuka lakini sikuona mtu. Hali hiyo ilinishangaza sana maana kila nikigeuka sikuona mtu yeyote, nikaanza kuwaza labda yatakuwa yale mauzauza yanayosimuliwa kuwepo ndani ya nyumba za matajiri. Kicheko kilijirudia tena teh! teh! teh! Hapo nikaamua kusimama kabisa ili nijue nini kinachoendelea, hofu ilishaanza kuninyemelea. Ile nasimama tu, nikamuona mtu aliyenifanyia yote hayo, nikatamani kumtia mabanzi lakini niliishia kumeza funda kubwa la mate kuipoza ile hasira niliyokuwanayo.

Hisia zangu zilikuwa sahihi, kulikuwa na uwepo wa mtu nyuma yangu. Tena siyo nyuma yangu labda niseme kisogoni mwangu. Nilichokosea ni kutoangalia kwa umakini, ndiyo maana sikuweza kumuona binti aliyejificha nyuma ya kochi nililolikalia. “Kumbe wewe ni muoga eeeeeh!” sikujibu kauli hii aliyoiongea kwa kujichekesha kama vile kahaba aliyepokea meseji ya muamala. “Karibu sana kaka Mhanuzi, jina langu ni Lizy mtoto wa mwisho wa mzee Gelo, vipi hujafurahi kukutana na mimi?” aliongea kauli ambayo nisingeijibu hata ingekuwa kufanya hivyo kunanipa mshahara. Kusemakweli sikumuelewa binti huyu, kwanza aliongea nami kwa sauti ya juu kama vile nilikuwa mbali naye. Mwanzoni aliongea kwa kujichekeshachekesha baadaye hali ya uso wake ikabadirika, alinuna na kuanza kuonesha chuki dhidi yangu. “Ok, kaka mgeni, mimi naondokaa! Nilikuja tu sebuleni mala moja baada ya kusikia sauti kubwa ya mziki inayoniumiza masikio yangu. Jitahidi kupunguza sauti, unatukera wenzio” Aliongea kisha akaondoka kwa mwendo wa madaha ya kike. Ule mtikisiko wa nyama za mapaja yake haukunivutia hata kidogo, sikuwa na hisia za ajabu kiasi cha kuvutiwa na makalio ya msichana asiye na heshima. “Ama kweli utajiri hauna adabu,” yaani mimi ndiye wa kufanyiwa vitu vya ajabu na kibinti kidogo tu ambacho kukiaangalia tu ninakipita zaidi ya miaka saba. Kilipaswa kunisalimia kwa adabu kwanza kabla ya kuongea ujinga wake, “eti, punguza sauti yako, unatukera wenzio” kwanini sasa kikapata muda wa kuniigizia michezo ya kitoto katikati ya sauti hiyo? Nilikasilishwa sana na kitendo kile, kiasi kwamba machozi yakaanza kunilengalenga machoni. Usinishangae, hivyo ndivyo nilivyo. Huo ndiyo udhaifu wangu. Huwa nina hasira za karibu sana. Kuna wakati huwa nakasilishwa na vitu ambavyo wenzangu huviona vidogo sana; visivyositahili kumkasilisha mtu. Niliituliza akili yangu kisha nikaendelea kuifurahia filamu yangu, hata hivyo nilipunguza sauti. Sikuhitaji kuwakera zaidi wenyeji wangu.

Niliutumia muda wa chakula cha usiku kutoa dukuduku langu la moyoni, nikashukuru kwa mapokezi mazuri niliyopewa na wenyeji wangu kisha nikawaaga. Nikawaeleza kuwa kesho yake asubuhi ningeondoka kuelekea chuoni ambako ningeishi kwa muda wote wa muhula wa kwanza wa masomo. Huenda kitu nilichokifanya hakikutalajiwa na mzee Gelo, alionesha kushangazwa na kile na safari yangu ya ghafla. Alipouliza kama nilikuwa na changamoto yeyote nilimwambia hapana. Hata kama ningekuwa na changamoto, nisingekubali kuieleza kutafuta kusaidiwa mbele ya binti yule aliyenikosea heshima. Japo hakulidhishwa na majibu niliyoyatoa lakini hakuongea chochote mbele ya familia yake, alinitazama tu kwa jicho liloonesha walakini. Mama Eliza alinitakia safari njema, akanitaka samahani kwakua ninaondoka kabla hatujaongea hata mala moja, alinieleza kwamba wakati huo alikuwa bize sana na shughuli za mahakamani. Hapo ndipo niliielewa sababu ya mwanamke huyu kutoonekana nyumbani mda wa mchana, kumbe ni hakimu wa mahakama ya wilaya. “Du! Mheshimiwa huyu” niliwaza. “Usiku mwema” niliisikia kwa taabu sauti hii iliyotoka kwa Eliza, aliongea kisha akanyanyuka na kutoweka eneo lile akionesha kuchukizwa na kilichoendelea. Kusema kweli sikupendezwa na tabia ya binti huyu, aliyeonekana kunichukia bila sababu yoyote. Labda hakupendezwa na uwepo wangu nyumbani kwao ndiyo maana hakujihangasisha na chochote kinachonihusu. Mda wote alikuwa bize, hata yale maongezi yaliyoendelea baina yangu na wazazi wake ni kama hakuyapenda. Alikuwa kimya, umakini wote aliuweka kwenye chakula alichokishambulia kwa utulivu mkubwa sana, pasipo hata kunyanyua kichwa chake. Niliamua kumpotezea kwa maana hii ndiyo ingekuwa mala ya mwisho kukaa na binti huyu mwenye gubu. “Haina noma, kesho naondoka, nakuachia jumba lako na wazazi wako.
ITAENDELEA
(Kila kitu kimeshakamilika, Simulizi ipo tayali. Ili kujua nini kiliendelea, tembelea uzi huu jioni ya kila siku kuanzia leo.)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom