SEHEMU YA 39/50
"Hawezi kumpenda randy na haiwezi tokea bossi sisi tunajua namna gani yakufanya".
" Anaonekana binti mwenye mawazo sana natamani nimuone kwa ukaribu zaidi kuliko hizi video zake mlizoniletea".
" Usijali boss kesho kutwa kuna mnada unapigwa wa kimataifa viongozi na matajiri mbalimbali watakuwepo hili kukamirisha jambo hilo".
" Naelewa nishapewa mualiko na president".
" Ndiyo mkuu serikali ina daiwa na hii ndiyo biashara pekee yenye hela kuliko madini". Jamaa huyo akazungumza na kumtizama boss wake
" Uuh kwa sasa nahitaji kupumzika hakikisheni huyo mwanamke mnampa kila kitu anachotaka".
" Sawa mkuu". Jamaa akaondoka na kumuacha boss wake.
Kwa sasa taifa lilikuwa katika deni kubwa la mikopo waliokopa viongozi waliopita mdarakani na kushindwa kulilipa mpka sasa nchi inadaiwa kiasi kikubwa cha pesa, njia pekee ilikuwa ni kuuza viungo vya binadamu, na bangi ili serikali iweze kupata pesa ya kulipia deni hilo linaloikumba taifa toka miaka mingi iliyopita, madini thamani yake ilikuwa imeshuka kwa sasa kwahiyo biashara haramu ndiyo iliyokuwa ikifanyika kwa wakati huu.
Gari aina ya hammer ikaja kutufata mimi pamoja na mke wangu diana huku ndani ya gari hiyo kukiwa na dereva pamoja na yule jamaa aliyekuwa ametupa maelezo yote kuhusu kumteke yule msichana wa raisi wa umoja wa mataifa Mr Malcom.
" fanyeni kazi kwa umakini mkishikwa hatuwezi wasaidia". Jamaa huyo akazungumza kwa msisitizo na kuzidi kutupa maelekezo yake na akatraki simu zetu alizotupa kutumia katika utekaji huo wa Tylat.
" TUMEFIKA". dereva akazungumza alionekana lafudhi yake ni mtu wa huko huko kwao, jamaa yule afungua mlango na tukashuka huku nikiwa makini zaidi kutizam eneo tulilopo lilikuwa eneo lenye giza totoro na vichaka vichaka pembezoni mwake kulikuwa na tank kubwa ambalo nilifanikiwa kuliona baada ya jamaa huyo kumulika kwa tochi, lilikuwa tank kubwa na lenye ngazi..
" ina maana uwanja upo porini au?". Nikauliza
" hapa ni town ila hili tank ndiyo lipo kidgo nje ya mji ko mtapita kwenye pipe zake kama mwendo wa dakika 30 mpka kufika kwenye chumba cha tylat".
" Duuh".
" Wakandarasi wa hili jengo mwanzo walihitaji kujenga ikulu ya raisi, ndiyo maana unaona njia kama hizi, mambo yalitokea yasiyoeleweka ndipo serikali ikahamua kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano na burudani za kusheherekea siku ya uhuru wa afrika ya kusini, na utawala wa Nelson mandela". Jamaa huyo akazungumza na kunikabadhi tochi huku akinionyesha ngazi za kupanda,
" Safari njema mtamkuta huyu mtu hapa hapa kazi ni lisaa limoja ma dakika 30". Akazungumza na kupiga simu huku akisema anahitaji kufatwa.
" Kwanini hii kazi msingefanya ninyi kama mmechora ramani yote hiyo".
" hahha tunahitaji uhakika zaidi maana historia yako tuanaijua". Jamaa akazungumza, nikamtizama diana na nikamuonea huruma kwani kipindi icho alikuwa tayari na ujauzito wangu. Nikasogea kwenye zile ngazi na kuzishika zilikuwa tayari zishaweka kutu kwa kukaa muda mrefu bila ya kupewa matunzo yeyote, nikazitingisha ila bado zilikuwa imara, nikaanza kupanda kuelekea juu ya tank hilo lilojengewa kwa zege ngumu ya sement,nikapanda kama sekunde 30 nikawa juu kabisa ya tank hilo na diana naye akafata nikampokea mkono na kumvuta, tukaona mfuniko mkubwa wa chuma ukiwa hauna kufuli kwenye nyororo zake, nikatoa zile nyororo na tukafungua, nikamulika kwa ndani na kushuhudia tu maji taka yakiwa yanaingia kwenye tank hilo ambalo halionekani kujaa leo wala kesho, maana ni matukio muhimu pekee ndiyo ukutanisha watu siyo mizunguko ya kila siku kusema kwamba litajaa. Nikashika ngazi na tukaanza kushuka chini huku panya na mende wakipita huko na huko, tukafika mpaka chini na kukanyaga maji taka ambayo kwa mbele tulijua lazima tukutane na kinyesi, tukaanza sikia harufu kali ya choo cha binadamu..Mwendo wetu ulikuwa ni wa haraka huku tukifata ile ramani kwenye simu, tuliendelea kutembea chini ya bomba ilo kubwa ambalo upokea maji taka toka kwenye bomba zengine,
" uuh" Nikatoa sauti baada ya kuona panya mkubwa ambaye sikuelewa humo anaishije na wenzake, tukafanikiwa kuona ngazi ambayo ndiyo inabomba linalotupereka mpaka juu ya kabisa na ndani ya choo ambacho ni cha kukaa na ndicho tutakachopitia, inawezekana walihitaji kujenga ikulu kweli, siku rais yakimkuta njia hiyo ndiyo iwe ya kumpitisha na inaonekana bado inatumika ata kwenye sherehe za uhuru kama kuna mambo mabaya yatatokea basi raisi au mtawala apitishwe eneo hilo kwa siri na kutoke kule kwenye vichaka, tukaanza kupanda ngazi huku harufu kali ilikiwa imeshatushika, tulitoa harufu ambayo hatukuhitaji ata kuzungumza,
" Baki hapa ". Nikazungumza na Diana huku nikimsisitiza abaki palepele kwenye nagzi akiwa amening'inia ili mimi nipande niende juu kabisa na kuingia ndani kwani tayari tushafika juu kabisa. nikasikilizia kama kuna mtu chooni ila kukawa kimya sasa nikafungua sehemu iliyokuwa imekatwa na hao wakandarasi kumpitisha mtu ilikuwa ya duara yenye mfuniko wa mviringo na ilikuwa ishaharibiwa nilitambua ni wale walotupa hii kazi ya kumteka huyu msichana, nikavuta pumzi na kuishusha kwani sasa naingia kwenye bomba la kinyesi na mkojo, nikaingia huku nikiwa na tochi, cha ajabu sikufanikiwa kuona hata funza wala chochote kile kikipita kwenda kwenye lile bomba.
" Hiki choo hakitumiki, ni mahususi kwa kumtorosha kiongozi wa serikali au mtu yeyote mkubwa". Nikawaza kwani bomba lake likikuwa jipya halina chochote, nikaanza panda ngazi taratibu kwenda juu ya choo icho, nikafanikiwa kuona tundu kubwa ambalo nikisukuma tu lile sinki la kukalia hili kujisaidia basi nakuwa tayari ndani, nikaweka tochi mdomoni na taratibu nikashika lile sinki kwa chini na kuanza kulisogeza taratibu mpaka uwazi mkubwa ukatokea, nilitambua sinki hilo lilikuwa limehalibiwa kwani ilikuwa ni rahisi sana alikutoa saut wakati ndani humo kuna vigae, nilijua walonipa kazi washafanya yao. Nikajinyanyua na kupanda juu sasa nikawa ndani ya choo icho, kilikuwa na mwanga za balbu ya umeme ko niliona kila kitu, nikasogea mlangoni na kuchungulia kupitia tundu la funguo, nikamuona tylat akiwa uchi anajiandaa nikajua kuwa hicho hakikuwa choo, nikamtizma jinsi anavyovaa nguo zake za show alikuwa uchi wa mnyama, ghafla nikamuona akikodoa macho upande niliopo mimi tena akakaza, huku akitizama kwa udadisi nikashtuka na kubaki nimeganda vile vile........
ITAENDELEAAAAAAAAA