Riwaya: See Me (Nione)

Riwaya: See Me (Nione)

SEE ME

SEHEMU YA 40/50



Nikamtizama Tyalat nakumuona akitizama kule ambako mimi nipo ambapo nilikuwa nachungulia kupitia tundu la ufunguo wa mlango, akakaza macho na kuanza kuja kule nilipo mimi lakini ni kama alikuwa anashangaa kwa juu, yaani juu ya mlango, sasa nikakaa vizuri kwa ajali ya kumnasa ndege wangu huku nikiwa makini nisijetambulika nikatoa bastola yangu kiunoni na kuikoki vizuri ilitoa sauti ndogo maana ilikuwa ya kisasa zaidi na toleo jipya kwa ajili ya kazi kama hizo za siri, sasa nikamuona akitabasamu na kisha akageuka na kunipa mgongo, sikutaka kujiuliza mara mbili mbili kwa haraka nikabinya kitasa na kufungua mlango huo na nikamuona akishtuka na kutaka kugeuka ila tayari nilikuwa nishamkwida shingoni akawa anajaribu kujivuta vuta ila na kutaka kujinasaua ila mdomo wa bunduki nikaweka kichwani pake na akatulia tuli mithili ya maji ya mtungini,nikamkokota na kumuingiza ndani ya choo kile cha kisasa kisha na kifunga mlango, akaonekana kushangaa sana baada ya kuingia humo ndani, akaona shimo kubwa likiwa wazi ambalo ndipo nilipopita akataka kuzungumza kitu ila nikamuwahi kwa kumsonteshea kidole kuwa anyamaze na akatii huku akitetemeka, macho yake yalikuwa ya rangi ya Brown alikuwa mwembamba na mwenye nywele ndefu kama wazungu wengine sema yeye tu alikuwa na ngozi nyeusi yenye mvuto wa kuvutia kama wanawake wengine warembo wa afrika.
Nikamsonteshea bastola kuwa ashuke chini huku nikimulika kule chini na tochi, nikamuona akitetemeka huku akijitahidi kuficha maungo yake ya mwili maana alikuwa na chupi na sidiria kifuani, akatingisha kichwa kuwa hawezi kushuka ila nikamkazia macho na kukunja ndita kiasi kilichofanya mpaka aogope na taratibu akasogelea shimo lilo na kutanguliza mguu mpaka kwenye makanyigio ya ngazi, uso wake ulihisi kinyaa kila aliponitizama na yeye mwenyewe kuna muda alitaka kutapika, akaanza kwenda chini taratibu huku nikijitahidi kumulika mwanga wa tochi ili akanyage sehemu sahihi, akashuka mpaka umbali haliopo diana na nikaona diana akimvuta kwenda katika lile bomba la pili,
“ Madam”. Nikasikia sauti zikitoka kule upande wa pili kile chumba alichokuwepo tylat kwa umakini nikasikia sauti wakija kule nilipo kwa haraka nikajificha nyuma ya mlango na kuweka silaha yangu vizuri, nikasikia wakitembea kama kwa kunyata na kitasa cha mlango kikaguswa ili kufunguliwa, na ukafunguliwa mlango taratibu huku nikiona buti ya kike ikitangulia, kwa haraka nikajitokeza na kumbana mikono yake na kufanya bastola aloishika kuanguka chini niliweza kutambua ana bastola baada ya kuiona kupitia kivuli cha ukutani, alikuwa ni mwanamke wa kizungu, akafurukuta na kujitoa kwa nguvu kisha akarusha ngumi kwa haraka ila nikainama chini na ikapita na akaacha sehemu zake za mbavu wazi, sikufanya hajuza nikashusha ngumi kwenye ubavu wake wa kushoto ila ni kama nilipiga kitu kigumu mithili ya mgomba, akatabasamu na kuleta shambulizi lake la pili, nalo nikalikwepa na mara hii ngumi ya ubavu ikatua kisawa sawa na akagugumia kwa sauti ya kike yenye maumivu, kitu nilichogundua alikuwa anaacha sana mbavu zake wazi anaonekana hakuwa professional sana wa kupigana akatizama bastola yake iliyoko chini, lilikuwa kosa kwani tayari nilikwisha muangusha chini na kuanza kumfunga na mkanda wake ambaoa hajuhi ni saa ngapi nimeutoa kiunoni, akaanza kupiga kelele ila nikampiga kichwani na akazima, kisha nikafunga mlango na kumsogeza mlangoni, nikaanza sikia sauti za watu wakija, kwa haraka nikarudi kule kwenye lile shimo na kuanza kushuka haraka haraka kupitia zile ngazi, nikawa nasikia kwa mbali wakizungumza kizungu hiyo ni baada ya kufungua mlango ule uliochukua kama sekunde 30 kufunguka maana nililaza mwili wa yule mwanamke pale,
Nikafika kule chini na kuanza kukimbia kuelekea kule tulipotokea na kwa vile diana alikwisha tangulia na yule mwanamke sikuwa na kitu cha kupoteza zaidi ya kukimbia kutoka eneo lile, nikawakuta njiani wakimalizia kushuka bomba la mwisho ili kutoka na kupanda ngazi kwenda juu ya lile tank
“ Tuna sekunde kama 120 kufika kwenye zile ngazi ni kama dakika mbili au tatu”. Nikazungumza huku nikimtizama mwanamke yule ambaye tayari alikwisha tapika siku nyingi.
“ okay dear twende”. Diana akazungumza na tukaanza kwenda huki nikimkokota yule mwanamke au binti wa kizungu,
“ Ongeza mwendo kuna panya wanatoka huko tulipopotoka kwa fujo inaonekana wapo nyuma”. Nikazungumza na kuwatanguliza mbele diana na tylat na wakatembea haraka mpaka kwenye bomba ambalo lina ngazi ambazo zinatufikisha mpaka kule juu, akaanza kupanda diana kwa harka haraka kisha akafata yule binti wa kizungu mwenye asili ya kiiafrika yani mzungu mweusi, na yeye akapanda,kisha nikafata na mimi ile napanda tu na mwanga mkali wa tochi ukamulika pale nilipokuwa nikawasikia wakiteta kwa kizungu kuwa wapo huku.
Nikaongeza kasi na kupanda mpaka juu ya tank kisha kurudisha mfuniko ule wa chuma na kufunga na nyororo zake, milio ya risasi ikaanza kusikika na risasi zikawa zinapiga ndani ya ule mfuniko, nikashuka mpaka chini na tukaingia mpaka ndani ya gari ambalo yule dereva alikuwa akitusubiri,....
Alikuwa alishaliwasha ile naingia tu naye akaliondoa kwa kasi kutoka eneo lile ambalo tupo..
“ ooh sheet kuna gari linakuja”. Diana akazungumza nikageuka nyuma na kuona gari likija kwa kasi kutufata kule tulipo.
“ Mkague ana cheap”. Nikazungumza na diana akaanza kumkagua binti binti yule bila mafanikio yeyote.
“ Mtoe hereni zake”. Nikazungumza na diana akataka kufanya ivyo ila akashindwa baada ya mlio wa risasi kusikika na kuvunja kioo cha nyuma.
“ oooh shit”. Nikazungumza na kuona gari mara hii zikiwa mbili tena jamaa wale wakionekana hawana mchezo kabisa na sisi.
“ Ongeza mwendo”. Nikazungumza huku tukiwa tumeinama na mpenzi wangu chini na pia tumemuinamisha yule msanii chini ili asidhulike maana waokoaji wake walionekana hawana mchezo kabisa,
Milio ya risasi ikazidi kusikika na kutufanya tuwe makini zaidi maana kama ungeinua kichwa basi mwisho wako ungekuwa hapo, ghafla gari ikaanza kupepesuka hiyo ni baada ya gari moja kutugonga ubavuni mwa gari yetu, na kufanya dereva aanze kukosa mwelekeo vizuri wa barabara hiyo ambayo hipo kabisa nje ya mji na makazi ya watu ni machache, sasa zikawa gari mbili moja imetubana kulia nyengine kushoto, nikajikuta nikimtukama dereva wetu kimoyo moyo kwani aliishiwa ujuzi kabisa wa kufanya, jamaa wakaanza kuligonga kwa kupokezana.
“ kumteka huyu binti ni sawa na kumteka raisi wa umoja wa mataifa”. Nikazungumza baada ya kuona kazi imekuwa ngumu sasa nikagundua ndiyo maana wale jamaa walitutumia sisi, na siyo askari wao ili kulinda siri zao kama wakikamatwa, kwahiyo wakatutumia sisi maana siri zao hatuzijuhi ata tukishikwa.
Tukawa tunajigonga kwenye siti huku yule binti akiwa katikati yetu, nikaanza kuona gari ikizidi kujigonga na sisi wa ubavuni uwenda tungevunjika kabisa.
Dereva wetu akapigwa shaba ya kichwa na kuegemea usukani, kitendo kilichofanya miguu yake kufunga breki ya ghafla, na kichwa chake kutua kwenye usukani na kufanya honi ianze kulia tayari alikuwa amekwishafariki. Gari ikasimama katikati ya barabara, nikatoa bastolo na kutizama risasi zilikuwa kwa hesbu ya harka haraka kama 12 na hivi.
Wale jamaa wakashuka maana niliwasikia wakishuka baada ya milango ya magari yao kufunguliwa, nikamshika yule binti mkono kisha nikamtizama diana ambaye naye yupo kwenye hali mbaya, paji lake la uso lilikuwa likivuja damu.
“ Nakupenda sana randy”. Akazungumza na kunitizama
“ unataka kufanya nini?” Nikazungumza baada ya kumuona akishika kitasa cha mlango na kutaka kukifungua, nikachungulia na kuona wale jamaa wakizunguka lile gari letu tuliokuwemo huku wakinyata
“ Niache kwa sasa”.
“ Hapana”.
“ Fanya hivyo randy”. Akazungumza na kwa harka akafungua kitasa cha mlango na kutoka nje kisha kubamiza mlango kwa nguvu kiasi kwamba mpka ukajilock maana ulikuwa ushaharibika kwahiyo ukajilock, nikamuona akinyanyua mikono juu, kwa harka nikamgusa yule binti shingo kwenye mishipa yake ya fahamu na akazima, wakati wale wakimtizama diana nikatumia fursa hiyo kuwahi kusogea mpaka kule mbele alipo dereva, sikufanikiwa kukaa nilikuwa nimeinama kwa chini.. nikapangua gia kwa haraka na gari ikawaka huku nikimsukuma yule dereva kushoto na kumtoa kichwa chake kwenye usukani wale jamaa wakaanza kushambulia kule nilipo na risasi mbili zikanipata kwnye bega langu la kushoto ila tayari nilikuwa nishakanyaga mafuta, lilikuwa ni tukio la sekunde chache sana na la uhatari zaidi lenye kuondoa hata maisha yangu kupita sitemillor nikamuona diana akiwa kapiga magoti huku mikono yake ikiwa nyuma ya kichwa, wale jamaa wakambeba na wengine kupanda kwenye gari haraka, sikuwahi fika afrika kusini kwhiyo nikawa naendesha tu gari hiyo ambayo muda huo ilikuwa ikitoka moshi na muda wowote ule ingezimika au kulipuka, nikaona wale jamaa wakizidi kuja na gari zao kwa kasi ya ajabu, moyo wangu uliuma sana diana kwa kitendo kile alichokifanya, tukafika kwenye daraja kubwa ambalo chini yake kuna mto mkubwa ambao nina uhakika kuna mamba wa kutosha, lile gari likawa sasa linaenda kuzima, sikujishauri nikahama njia na gari lile kupiga kuta za daraja hilo na gari ikaanza kushuka chini kwa kasi huku nikijipiga piga na kupasuka pasuka kichwani, gari ikatumbukia mtoni.


SEE MEE
 
SEHEMU YA 41/50…..



Gari ikatumbukia mtoni na kuanza kushuka kwenda chini ya maji ambayo yalionekana yana kina kirefu mno, taa za gari zikaanza kuwaka na kuzima, huku mimi nikijitoa mguu ulokuwa umebana kwenye siti, nikawa najivuta huku pumzi nikiwa nimeibana maana maji yalikuwa yashajaa ndani ya gari, nikamuona yule binti akitapa tapa huku naye mguu akiwa anataka kuunasua uliposhika,nikafanikiwa kujitoa baada ya kunyanyua kwa nguvu ile sehemu ya kukalia, nikatoa mguu wangu na kwenda nyuma ya gari nikamtoa yule binti kisha nikataka kufungua mlango ila ukashindikana, nikachukua fire extinguisher na kupiga kile kioo cha nyuma ambacho tayari kulikuwa kishavunjika ila nilikiongezea ukubwa tu wa sisi kupita maana risasi ilikivunja vunja, kikawa kikubwa nikamshika mikono yule binti na kuanza kumvuta kutoka ndani ya gari, nikamuona akikata pumzi taratibu,nikajitahidi kuogelea kwa haraka kutoka eneo lile ambalo lina giza kubwa, nikajitahidi kumtoa mpaka nchi kavu, alikuwa tayari alikwisha zimia maana mapigo yake ya moyo yalidunda kwa kasi sana, nikamtoa macho maji tumboni, huku mara kadhaa nikimpulizia pumzi mdomoni mwake akashtuka na kunitizama huku akitapika maji na kuhema juu juu, nikatizama juu ya daraja sikuona kitu maana ukiwa chini huwezi ona chochote juu ni kutokana na ukubwa wa daraja hilo, yule binti akawa anatetemeka kwa baridi maana mpaka hapo alikuwa na chupi yake na sidiria pekee, nikamshika mkono wake na kumnyanyua kisha tukaanza kutembea kuelekea porini huku nikiwa sijuhi naelekea wapi.

“ We nani?”. Akaniuliza kwa kingereza huku akikata mkono wangu na ikaachana, alipata ujasiri wa ghafla.

“ Unataka nini kwangu?”. Akaniuliza kwa kingereza niliweza kuielewa lugha ya kingereza maana kila kitu nilisoma japani lugha ambayo sikuhisoma ni kiarabu pekee.

“ Naomba twende”. Nikazungumza kwa kingereza na nikamuona akitingisha kichwa kukataa, ghafla mchakacho kwenye majani ukasikika, nikamwambia atulie ila akatingisha kichwa kuwa hataki,

“ Nipo huku”. Akazungumza kwa sauti kwa lugha kingereza na kufanya kule kwenye majani kutulie, nikatizama kwa umakini kupita mwanga wa mbaramwezi nikafanikiwa kuona nyoka mkubwa akisogea kuja kule tulipo, na binti alikuwa ananitizamana na mimi huku joka ilo likiwa linakuja nyuma yake.

“ Ushawai ona nyoka mkubwa”?. Nikazungumza na kauli yangu ikamfanya kwa haraka anirukie juu na kunikumbatia kwa nguvu huku akijikunyata na kufurukuta furukuta, nikaanza rudi nyuma taratibu maana joka lile lilikuwa lina tutizama sasa, nikawa natizama kwa umakini huku nikirudi nyuma kwa umakini na binti yule kutokana na mwili wake kuwa mwepesi hakunipa uzito wowote ule,nikageuka kwa haraka na kuanza toka nduki huku nikiwa nimembana vizuri yule binti, na nyuma huku tukisikia michakacho ya majani kuonyesha joka lile linakuja.

“ Nikamate vizuri”. Nikazungumza huku nikiongeza kasi na kutoka eneo la majani,na kufata njia yenye vumbi vumbi lakini haikuwa ndefu sana kwani kwenye pori lile nyasi zilijaa na miti ya kutosha, sikutaka kugeuka nyuma kabisa zaidi ya kuongeza mbio, mlio wa risasi ukasikika na kufanya kwa haraka nibane kwenye mti.nikajificha bila ya kuona chochote kile wala kisikia michakacho ya majani,bega langu lilikuwa linazidi kutiririka damu za kutosha na jeraha kuzidi kuuma maana risasi mbili zilikuwa kwenye bega.nikamshusha yule binti ambaye alikuwa hataki kabisa kushuka nikaanza sikia sauti za kiarabu nikajua ni wale watu walonipa kazi wamekuja kunifata ila nikataka kupata uhakika zaidi, na inaonekana walimshambulia yule joka mkubwa, hakuwa joka mdogo .

“ Randy”. Nikaanza sikia wakiniita huku miale ya tochi ikimurika huku na kule, nikataka kujitokeza ila nikashindwa nikakumbuka kuwa sina Diana na kama nikijitokeza hawa jamaa watamchukua huyu binti na diana wangu sitompata kabisa na huenda nikampoteza kabisa

“ siwezi wapa”. Nikajisemea kimoyo moyo na kumshika yule binti mkono sasa kazi ikawa imebadirika ni kumrudisha mateka wangu kwa watu wake ili wanipe mke wnagu.

“ Tunajua umempata na unaye uko wapi?”. Sauti ya yule mtu mfupi ikasikika yule aliyenipokea na diana uwanja wa ndege. Nikajinyanyua taratibu na kumshika yule mwanamke mkono wake vizuri na tukaanza kutembea taratibu kutoka eneo hilo, huku nikijitahidi miale ya mwanga isitufikie.

“ nifate mimi nakurudisha”. Nikazungumza ili kufanya binti huyo awe pamoja na mimi,tukaendelea kutembea mwendo kama wa dakika 30 hivi, huku nikiwa nishaanza kuishiwa nguvu, kwa mbele tukaona kijiji kikubwa kilichojaa nyumba nyingi za nyasi na za udongo huku nyumba chache sana zikiwa za kisasa na zenye umeme.Mwili ukaanza kuishiwa nguvu nikaanza kupoteza nguvu ya kuona kwa mbali sana nikaona wanaume wawili wa kimasai wakiwa na mikuki mikononi na mishale, huku yule dada msanii akiwa amenikamata kwa nguvu huku akitetemeka kwani walituzunguka nikajikuta nazimia na giza zito kutua machoni mwangu…….

*************** *******************



SOMALIA


Mage hakutaka kusubiri mara mbilimbili akazidi kutembea kwa umakini mkubwa huku kila mara akitizama kulia na kushoto ili asiweze kukamatika kirahisi, akafanikiwa kufika mpaka kwenye yale mapipa makubwa ambayo uwa yanatolewa ndani ya kambi hiyo na kuperekwa kwenye boat au feli ambazo zinabeba mizigo hiyo na kuitoa na kuipereka sehemu asiyoijua hakuwa tayari kubaki hapo,akafika mpaka kwenye mapipa hayi na kufungua mfuniko mmoja, harufu kali ikamfanya afunge, ilikuwa ni mafuta ya petrol, akasogelea pipa la pili na kufungua lilikuwa na oil, akafungua na jengine na kukuta napo kuna mafuta,

“ uuh”. Akaguna kwani akiingia kwenye mafuta kwa kukosa hewa na harufu mbaya na pia mafuta ni sumu angekufa. Akafungua pipa jengine na kuona barafu akajishauri akashika shika zile barafu na roho ya kijasiri ikamwambia aingie katika barafu zile.

“ hapana”. Akaongea baada ya kuona gari ikija kubeba mizigo ile akatoka na kujibanza sehemu yenye giza kumbuka ni msichana aliyepitia mafunzo makubwa ya kijeshi, kwa haraka akatoka na kijiburuza chini na kuingia chini ya uvungu wa gari kisha akajificha, na kutulia tuli. Wale jamaa wakaanza kubeba mizigo ile na kuipakia kwanye gari walipomaliza wakafunga gari ile na wakarudi ndani ya gari, mage akajishikiria kwenye machuma ya gari lile kubwa huku akiwa makini asishike sehemu isiyokuwa sahihi, alipata maumivu makali ambayo hakuwahi kuyapata alihisi mpaka mimba yange changa uenda ingetoka, gari ikawashwa na kuanza kutoka eneo ilo.


******************
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom