hancy Abdon
Member
- May 24, 2026
- 78
- 58
SEHEMU YA KWANZA
AGE.............................18+
THE STORY MASTER
AUTHOR...................... Hancy A abdons
"Kuna mwanafunzi mgeni!".
Nikazungumza na kumtizama mtu aliyeniletea hiyo taarifa alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.
"Ndiyo mkuu".
akazungumza kwa uwoga baada ya mimi kusimama
juu ya meza niliyokalia huku mkononi nikiwa na kitabu cha mabara mbalimbali ambacho kilihusu mabara ya duniani siyo mabara the farmer akaanza kurudi nyuma huku midomo ikimtetemeka.
"Nishakukataza kuniita mkuu!".
Nikazungumza na kumshika shati yake shingoni nikamkamata vizuri shingo yake.
"Mwalimu anakuja."
sauti ikasikika nyuma yangu nikageuka na kumtazama Ray
"Kwahiyo"?.
Nikamjibu kisha nikamwachia yule kijana mdogo wa mwaka wa kwanza chuoni hapo akapepesuka kutaka kuanguka, mwili wake ulikuwa mdogo kama mnyoo.
"Mlete kule chini."
Nikazungumza na kuondoka ndani ya darasa hilo ambalo tulikuwa humo watu wanne pekee, Wenzangu watatu wakanifuata nyuma, na yule kijana akabaki amesimama huku ametupa mgongo; alikuwa bado anaogopa."Tabia yako bado hujaacha!" Sauti ya mwalimu ikanifanya nimtazame kwa dharau kwani nilikutana naye kwenye mlango. Alikuwa ni madam mwenye umbo kubwa; hips zake zilikuwa nene zilizoshiba mithili ya shape ya Kajala, yaani makalio ya Kajala halafu hips ya Mobetto, sura Mungu hakumjalia kivile. Nikanyanyua lips zangu huku nikimtazama kwa matamanio."Dominick unanitazamaje? Hili jambo naliripoti kwa mkuu wa chuo!" Madam akazungumza na kisha akasogea dirishani na kumwita yule kijana wa mwaka wa kwanza."Una roho mbaya, unatesa wenzako kisa kwenu mna hela, kisa baba yako ni Rais!" Akazungumza kwa uchungu ila sikujali nikapiga hatua kwenda napo kwenda.
"Na nyie mnaomfuata mwandike barua ya utovu wa nidhamu!".
Akazungumza na akaondoka na yule kijana mdogo kuelekea ofisini huku maumbo yake ya nyuma yakitingishika kama mfuko wa rambo wenye maji.
"Huyu madam mshenzi sana,"
Ray akazungumza. Nikatingisha kichwa na kuelekea darasani kwenye kipindi ambacho kilikuwa kinaanza muda mchache ujao, lilikuwa somo linalohusu mambo ya biashara na uchumi."Sitaki kelele!" Nikazungumza baada ya kuingia darasani na kukuta watu wakipiga kelele. Waliposikia sauti yangu wote wakatulia tuli, hata walioniona kabla sijazungumza walirudi kwenye siti zao. Nikaenda kwenye kiti changu kwa ajili ya kuketi, nikakunja ndita..
Baada ya kuona kalamu yangu ikiwa chini,
"Wewe ndiye uliyeangusha hii kalamu?". Nikamuuliza swali jirani yangu ambaye akanitazama kwa woga.
"Ni upepo," akanijibu.
"Na ukaiacha? Baadaye uje kule chini,". Nikazungumza na kuiokota."
"Husikii kupulizia marashi yako hayo?." Nikamuuliza swali msichana aliyekuwa pembeni yangu upande wa kulia. Marashi yake sikuyapenda toka siku ya kwanza nilipoyasikia.
"Mama hajanunua mengine," .Akanijibu na kuendelea kuandika kwenye kitabu chake kidogo mithili ya diary.Nikatazama katikati ya darasa na kumwona kijana niliyempiga juzi kipigo cha mbwa koko akiwa amelalia dawati. Nikatabasamu kwa furaha kwani napenda toka moyoni mwangu kuona mtu akiteseka, napenda kuona mtu akiwa na damu puani, mdomoni au popote pale.
Napenda kuona mtu akilia kwa maumivu makali huku akiniomba msamaha. Sipendi kuona mtu akifurahi au kutabasamu.Mwalimu wa somo la biashara akaingia darasani. Tukampatia heshima ambayo kila mwanafunzi anatoa kwa walimu au wakufunzi wake toka vidudu mpaka chuo kikuu. Alikuwa ni madam mwembamba mwenye umbo la Kisomali; alivutia kama twiga mbugani. Nikaacha kumkagua mwili wake baada ya kuanza kuzungumza."Jana sikumaliza kipindi, kwa hiyo nitafanya double!" Akazungumza na kufanya nitabasamu kwani huwa napenda kumwona kila muda.Ghafla darasa zima likalipuka kwa shangwe na furaha zilizoambatana na miluzi ya vijana wa kiume. Nikamtazama Ray na wenzake wawili ambao nao wakawa wananitazama, mimi.
Hatukujua kwa nini watu wale wanapiga kelele za kufurahi bila uwoga. Nikatazama mlangoni ambako watu wanatazama, nikamwona kijana wa kiume anaingia, mrefu mwenye umbo la misuli (mazoezi). Nikatabasamu baada ya macho yetu kugongana na yeye akatabasamu.
"Alex, Alex, Alex!" Watu wakaanza kutaja jina lake kama shujaa waliyemmiss kwa muda mrefu. Nikamtazama mkono wake nilioutegua (vunja) miezi mitatu iliyopita ulikuwa mzima, ulikuwa hujafungwa na P.O.P pia hata shingo yake ilikuwa nzima.
"Nitakuua, Dominick,"
Akazungumza kwa sauti nzito iliyofanya wanafunzi wote kutulia.
"Alex, maneno gani hayo?"
Madam akazungumza,Na kumtizama alex aliyenikazia macho, Nikasimama na kuelekea kule mbale ya darasa,alipo Alex, nikamtazama juu mpaka chini, mguu wake wa kulia niliouvunja miezi 2 iliyopita ulikuwa mzima.
Akatabasamu baada ya kuona namkagua.
"Baba yako amekupeleka India?" Nikazungumza na akatabasamu kwa kejeli.
"Nitahakikisha nakulaza miezi 6 kitandani!" .Akazungumza na kufanya watu wote kushangilia kwani hakunaaliyenipenda hata mmoja kutokana na tabia zangu mbaya za uonevu nilizokuwa nazo chuoni hapo. Kila mtu alionekana kumpenda Alex ambaye alikuwa ni head boy chuoni hapo na alikuwa mkarimu machoni mwa watu, alikuwa na roho safi na ndiyo mpinzani wangu mkubwa chuoni hapo yeye alikuwa mtoto wa Rais mstaafu, hakupenda tabia zangu ijapo kuwa mimi niliona niko sahihi.
"Demu wako nitambusu tena ili uje upambane na mimi!" Nikazungumza na kugeuka kumtazama Clara ambaye ni demu wa Alex, Clara akamtazama...
Alex huku machozi yakimlengalenga kwani nilimdhalilisha mbele za watu, nikaona hasira za Alex kifuani mwake zikipanda na kushuka kama mtu mwenye presha."Ukimshika tena Clara..." Alex akashindwa kumaliza kuongea, sauti ya mkuu wa chuo ikasikika."Njooni ofisini wazazi wenu wamekuja." Tukatazama dirishani na kumwona mkuu wa chuo akitutazama kwa macho makali, Alex akageuka na kuondoka nami nikafuata kwa nyuma na kundi la watu wachache wakaanza kunizomea, nikarudi kwa haraka darasani na wakatulia tuli.
"Ray, wakabili wote watakaonizomea.
""Sawa Domy," Ray akanijibu na nikaondoka bila ya kusikia sauti yoyote ile, nikaona msafara mkubwa wa magari ukiwa pembezoni mwa geti kuu, ofisi ilitazamana na geti kuu la chuo, ofisi ya mkuu wa chuo.
"Huyu mzee vipi?" Nikawaza na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa shule. Nikamwona baba akiwa amekaa upande wa kushoto huku Rais aliyepita madarakani mwaka uliopita naye akiwa ameketi upande huo huo wa kushoto na wanaume wawili waliovaa suti wakiwa nyuma ya mgongo wa baba. Nikamwona Alex akiwa katikati ya duara kubwa lililochorwa kwenye sakafu ambalo chuoni hapo tunaliita kikaango cha watukutu. Nikapiga hatua nami nikaingia kwenye lile duara, mkuu wa shule tukawa tunatazamana naye pamoja na wazazi wetu.
"Mnataka kuwa mabondia tumlete Tyson nchini?". Baba akazungumza huku akinitazama kwa macho makali ambayo kama angemtazama mtoto mdogo angelia na kulala usingizi fofofo. Nikatingisha kichwa kukataa alichozungumza.
"Mnataka kila siku mtuone hapa chuoni, hivi mnaleta picha gani nchini? Nashindwa kutatua changamoto za wananchi, tunashindwa kupanga mipango jinsi ya kuinua taifa letu toka uchumi wa kati mpaka wa juu, tena tuwaze na watu kama nyie wenye mapumbu!" Baba akazungumza kwa ukali zaidi huku akinikazia macho. Nikatizama pembeni.
"Alex, nitakuhamisha chuo." Rais aliyepita madarakani akazungumza.
"Baba haiwezekani, sitakubali!" Alex akazungumza kwa upole.
"Kwahiyo unataka ugomvi uendelee? Unataka mpaka wakuue au uue na wewe? Umelala hospitali miezi 3 hujitambui, mifupa imeteguliwa bado unataka nini?!" Baba Alex akafoka.
"Tupeni nafasi ya mwisho," nikazungumza na kuwatazama wote wawili.
Wakanitizama."Sababu ya kuonewa wenzako nini?" Baba akaniuliza, nikabaki nimetumbua macho.
"Mkuu hebu wachape viboko, inaonekana hamuwafundishi adabu."
Baba akazungumza na mkuu wa shule akasimama na kutoa heshima.
"Samahani mheshimiwa Rais na mstaafu, hawa tunawaonya sana na kuwaadhibu kwa kuwapa adhabu. Chuo chetu akiruhusu kuwatia fimbo wanafunzi wetu." Akazungumza.
"Nitamteua mtu mwengine." Baba akazungumza na kufanya mkuu wa shule ashtuke, akapiga simu hapo hapo.
"Nenda Form Six niletee fimbo za kutosha!"
"Zilete ofisini kwangu sasa hivi." Akazungumza na akakata simu.
"Hatuwezi lea ujinga kisa wazazi wenu wakubwa, mnafanya upuuzi chuoni!" Baba Alex akazungumza.
"Hawa wanatugombanisha, mitoto mjinga sana hii, mzee mwenzangu." Baba akakazia.Madam akaingia ofisini akiwa na mwanafunzi wa Form Six ambaye alikuwa kabeba fimbo za kutosha, mwanafunzi yule alipowaona wazazi wetu akashtuka sana, hakutegemea kama angeweza kuona watu kama hao.
"Shikamooni wakubwa," akazungumza kwa uchangamfu kuficha mshangao wake na uwoga, wakamuitikia wote kwa pamoja.
"Form Six?" Baba akamuuliza.
"Ndiyo kiongozi!" Akajibu.
"Sawa, sawa, kazana!" Baba akazungumza.
"Asante sana." Akaondoka huku uso wake na macho yake yalionyesha mshangao wa wazi kabisa.
ITAENDELEA.....