Ridhiwan anapewa escort; Kwanini?

Ridhiwan anapewa escort; Kwanini?

wanapewa ulinzi kutokana na threat level...escort ya magari matatu ni no no...mara nyingi wanapewa dereva na mlinzi na gari moja, huyo kikwete ana watoto nane sijui sasa kama wote wanapewa same treament si mzozo huo.

Kikwete ana watoto 22 acha urongo!
 
Mdogo wangu Rizwan anahitaji ulinzi kwani amejiexpose sana kwenye mambo mengi, siasa mpaka michezo. Mdogo wangu nafasi hizi huja mara moja katika maisha. Fata nyayo za husein Mwinyi, sasa soma, baba atakapoondoka madarakani awe na kitu cha kujivunia kama mzee Mwinyi, na Kigoma. Baba yetu ana wengi wa kumsaidia, wewe sasa jijenge. Unajua sikuhizi bila ya kuwa Dk ni matatizo matupu. Huu ni ushauri. mimi najua kwa nini inabidi uwe na ulinzi.
 
Huyo ndiyo mtoto wa kifalme wengine waliotangulia walikuwa hawana haki mungu awalani maana kesho tutaambia hata yule wa shule ya chekechea amesindikizwa hivyo.
 
Nijuavyo mimi watoto wa marais wengi tu duniani(wanaounda first family) hupewa ulinzi na ama polisi,jeshi,secret service ama chombo chochote kinachosimamia usalama wa viongozi kwa nchi husika(ikiwa ni pamoja na kuwa na motorcade yenye escort ya walinzi) so Ridhwan kama mmojawapo wa watoto wanaounda first family ulinzi ni stahili yake...
si ulinzi tu hata kuendesha nchi inapobidi
 
Kwani mtoto wa rais hadeserve usalama wa nchi? Nini maana ya kuwa first family? JF siku hizi imejaa watoto na watu wenye wivu tu. Kama mtoto wa rais anatakiwa apate ulinzi wa serikali ili kumlinda na hatari yeyote. Vilevile wanatengewa budget yao maalum kufanikisha usalama wao including gari za kuendeshwa, askari wa kuwalinda, security escort na kadhalika. Na hili lipo hata ulaya na marekani au mmesahau familia ya george Bush na watoto wake walivyokuwa wakiwasumbua usalama wa taifa wa marekani??
Hata Gamal Mubarak ni mwezi jana tu alikuwa akisindikizwa hivyo hivyo sasa yuko uhamishoni UK dunia ni mzunguruko..
 
ingetokea ukamuona anatembea kwa mguu kwenda uwanjani peke yake ungesemaje?
JK kamtosa mtoto wake au?

AAAAAAAH,...wamesha hangaikia kula nchi waacheni watafune wakichoka watuachie mifupa na sisi tutafune,...kula kwa zamu,nawa hurumia watoto ambao hawaja zaliwa hadi sasa watakuta nini cjui
 
Q1. Anaandaliwa kuzoea uongozi ili siku akishika nchi asibabaike, Mubarak pia alikuwa anamwandaa mwanae ila waandamanaji wamemwahi..,
Q2. Kamati itaundwa na RAIS kwa maagizo maalum ya kulipachika hilo ukizingatia wa tz hawasomi neno kwa neno.
Q3. Hili lilijibiwa na JK kwamba Urais ni wake na Familia yake.

Hoja hapa si Jk alisema nini.Katiba au sheria inaruhusu hili?Je wakati wa Nyerere,Mwinyi,au Mkapa kulikuwa na Urais wa familia?
 
Kwani mtoto wa rais hadeserve usalama wa nchi? Nini maana ya kuwa first family? JF siku hizi imejaa watoto na watu wenye wivu tu. Kama mtoto wa rais anatakiwa apate ulinzi wa serikali ili kumlinda na hatari yeyote. Vilevile wanatengewa budget yao maalum kufanikisha usalama wao including gari za kuendeshwa, askari wa kuwalinda, security escort na kadhalika. Na hili lipo hata ulaya na marekani au mmesahau familia ya george Bush na watoto wake walivyokuwa wakiwasumbua usalama wa taifa wa marekani??

ndio tatizo la jf nowadays!
 
Asante sana kwa kutujuza, maanake sisi ambao hatujui ni rahisi kukimbilia kulalamika kuliko kutaka kujua ukweli wa mambo. Nadhani familia ya mkuu kupewa ulinzi si kwetu au kwa Bush tu bali ni utaratibu wa dinia nzima, wale mnaojua zaidi mnaweza kutupa mifano zaidi ili kusaidia kuachana na chuki zinazotokana na uelewa wetu mdogo
 
ndio tatizo la jf nowadays!
Acha uongo memba wa JF wanazidi kuongezeka bcs JF ni jukwaa la kiukweli (hamna forum inayoisogelea hata kwa mbali), watu wanapotoa mawazo yao yakapingana na ya kwako usidai wivu unawasumbua.

Watu wanahaki ya kikatiba kuhoji matumizi ya hela zao. Labda ni kweli taarifa za kiinteligensia zililazimu msafara wa RZ 1.
Rz1 sio kama Hussein Mwinyi na wengine kwa sababu jamaa ameshawafitini watu kibao kwa mkulu hasa ndani ya CCM yaan akiondoka baba yake ndio atajua namna ya wanavyomchukia
 
Kwani mtoto wa rais hadeserve usalama wa nchi? Nini maana ya kuwa first family? JF siku hizi imejaa watoto na watu wenye wivu tu. Kama mtoto wa rais anatakiwa apate ulinzi wa serikali ili kumlinda na hatari yeyote. Vilevile wanatengewa budget yao maalum kufanikisha usalama wao including gari za kuendeshwa, askari wa kuwalinda, security escort na kadhalika. Na hili lipo hata ulaya na marekani au mmesahau familia ya george Bush na watoto wake walivyokuwa wakiwasumbua usalama wa taifa wa marekani??

...Hussein Mwinyi nae alipitia hatua hizi? Naomba kujulishwa.
 
Asante sana kwa kutujuza, maanake sisi ambao hatujui ni rahisi kukimbilia kulalamika kuliko kutaka kujua ukweli wa mambo. Nadhani familia ya mkuu kupewa ulinzi si kwetu au kwa Bush tu bali ni utaratibu wa dinia nzima, wale mnaojua zaidi mnaweza kutupa mifano zaidi ili kusaidia kuachana na chuki zinazotokana na uelewa wetu mdogo

Soma post zote utaelewa kwanini Rhizwan hastaili kupewa hizo huduma maalum. Au ndiyo kusema hata mtoto wa Rais akiwa ameolewa kule Magu inabidi tupeleke watu wa usalama kumlinda?

Watanzania sijui tuna matatizo gani? Tukiwa tunajadili mafao ya viongozi basi utasikia tunamlinganisha rais wa Tz na US lakini katika kujadili mafao ya raia utasikia tunasema US ni nchi tajiri hivyo uwezi kulinganisha huduma inazotoa kwa raia wake na zile za serikali yaTz kwa raia wake!.

Nasisitiza kama kweli, hiyo habari ni sahihi basi huo ni ufujaji wa mali za umma.

Lakini tulitegemea nini baada ya kumuona kijana akizunguka tanzania kumwombea baba kura?

Je akigombea Mzee Malecela (kwa mfano) 2015 tutamwona huyu mtoto akizunguka nchi nzima kuomba kura tena?

TAFAKARI!
 
Wakuu sijui ninyi mtazichukuliaje habari hizi, kwangu mimi naziona ni habari za kusikitisha. Habari kutoka chanzo cha habari cha kuaminika kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA), zinasema kuwa kijana, mtoto wa mkulu, Ridhiwan, kaonekana uwanjani hapo, ikisemwa kuwa ana safari yake binafsi, kwenda Dubai.

Nachelea kulia. Naomba nijikaze kiume, kijasiri ili niweze kulisema hili, naomba niwezeshwe, maana sasa nchi inakoelekezwa, aaaagh, basi wahenga na Mungu wanajua...KAPELEKWA UWANJA WA NDEGE NA ESCORT AKIWA KATIKA GARI YA IKULU, lenye ngao na polls mbili lakini HALIKUWA NA BENDERA. Mbele kulikuwa na gari ya escort ya king'ora na nyuma gari ya usalama, so the source said.

Kuna mengine tutayaongeza. Kuna kazi nafanya mara moja wakuu, just kuanzia hiyo. INASKITISHA JAMA, THIS IS EXTREMEEEEEEEEE

Assume the following:
  1. Habari hii ni sahihi
  2. Rizwan anastahili kupewa ulinzi kisheria za nchi
Je ni haki kutumia magari hayo matatu kwenye msafara wake?

Je siku nyingine wakimrusha kwa Helikopita itakuwa ni sahihi?

Inaingia akili kuwa usalama wa Rizwan unatishiwa kiasi hicho?

Huyu mtoa mada sioni kama angetueleza endapo angeona Rizwani akishuka katika gari ya Ikulu ampapo ndani yake kuna wanausalama kwasababu matumizi mabaya ya namna hiyo tumeyazoea. Nenda mashuleni utakuta STKs ndizo zinawapeleka watoto wa wakubwa shule!

REMEMBER
Wrong is wrong even if everybody does it and Right is right even if nobody does it!
 
Jamani hata kama wanastahili ulinzi, huu ulinzi ni kwa watoto watu wazima wenye miji yao? Ulinzi unakuwa kwa watoto ambao hawajafikia miaka 18. Hizo fedha zitabaki kweli kwa maraisi wetu waliojaaliwa uzazi?

Na mbona hatukuwahi kuona 'vituko' hivi kwa maraisi waliopita?
 
hii ndo tanzania zaidi ya uijuavyo, but ipo siku tu. na tutaanza na ridhwani...sijui mtakimbilia iran au Dubai familia nzima ...na jinsi mlivo wengi mtakoma
 
Mambo mengine ni siasa tu, mtoto wa Rais kupata escort ya watu wa usalama na magari ya Ikulu, bila nembo wala bendera ya baba yake (ambaye ni Rais) ni jambo la kawaida duniani kote. Ningeshangaa tu kama Ridhwan angetumia nembo za Ikulu kwa maana ya nembo ya Rais kupita barabarani lakini hili halina tatizo kwenye mambo ya ulinzi wa Rais na familia yake kokote duniani..
 
kwani hamjui kama ndie anayeendesha nchi? kikwete hana cha kusema mbele ya manae, kwa ufupi ridhwan ni associate president so lets find a way of dealing with it.
Hivi kuna mtu anajua namna ya kukwepa kulipa kodi, thats seems to be a solution to me, naumia sana jinsi kodi yangu nayoitokea jasho inavyotumika.:A S 20:
 
Kwani mtoto wa rais hadeserve usalama wa nchi? Nini maana ya kuwa first family? JF siku hizi imejaa watoto na watu wenye wivu tu. Kama mtoto wa rais anatakiwa apate ulinzi wa serikali ili kumlinda na hatari yeyote. Vilevile wanatengewa budget yao maalum kufanikisha usalama wao including gari za kuendeshwa, askari wa kuwalinda, security escort na kadhalika. Na hili lipo hata ulaya na marekani au mmesahau familia ya george Bush na watoto wake walivyokuwa wakiwasumbua usalama wa taifa wa marekani??

Mimi nashangaa! Hivi uzalendo ni mtoto wa rais kupanda daladala ua bajaj? Mambo haya yamekuwa yakitokea sehemu nyingi duniani, hata huko mnakodhani wameendelea. lakini mimi napata mashaka kuhusiana na ukweli wa story hiyo kwa sababu nimekutana naye mara kadhaa na sijawahi kuona akiendeshwa wala kusindikizwa. Tuache uzushi unaotokana na chuki binafsi jamani!
 
Back
Top Bottom