Simbachawene aagiza kukamatwa kwa Askari 5 wa Uwanja wa JNIA kwa uhalifu wa kusafirisha binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameagiza kukamatwa kwa askari watano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutokana na kushiriki matukio ya kihalifu.

Agizo hilo linakuja siku chache baada ya kufukuzwa kazi kwa askari wanne wa jeshi hilo kutokana na ukiukwaji wa maadili ya Polisi kwa kushiriki matukio ya kiuhalifu ikiwamo kuomba rushwa na mwengine kuhujumu miundombinu ya umeme ya Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Waziri huyo ambaye anaendelea na ziara yake ya siku tatu kukagua shughuli mbalimbali za jeshi hilo, jana baada ya kutembelea Kikosi cha anga cha jeshi hilo, alifanya ziara JNIA ambako alitumia takribani saa moja kuzungumza na maofisa wa polisi uwanjani hapo na kisha kutembelea sehemu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Waziri Simbachawene alisema kuwa askari hao watano wameunda mtandao wao kwa ajili ya kusaidia usafirishaji wa vijana wa kike na kiume kwenda nchi za kiarabu kufanya kazi za ndani.

Alisema serikali imeshapiga marufuku usafirishwaji wa watanzania kwenda kufanya kazi za ndani kwenye nchi hizo na kuwa askari na maofisa uhamiaji nchi nzima wanalo jukumu la kuhakikisha hakuna mtu anayekwenda kufanya kazi za ndani kwenye nchi hizo.

Alibainisha kuwa askari hao wamekuwa wakishiriki kuhakikisha mawakala wanafanikiwa kusafirisha Watanzania kwenda katika nchi hizo.

Pia alisema askari hao wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaosafiri kutumia uwanja huo kwa kuwaomba fedha huku wakitishia kuwabambikia kesi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa za kiitelijensia ambazo waziri huyo alisema anazo, askari hao wamekuwa wakishirikiana na wabeba mizigo ya abiria uwanjani hapo.

Alisema wabeba mizigo hiyo wakifika kwenye eneo la magari ambapo kamera zimekuwa hazioneshi, askari hutokea na kutoa vitisho hivyo kwa wageni wakitaka kupewa fedha.

Alisema,"kwa taarifa nilizonazo na ambazo kwa muda wa mazungumzo yangu hapa uwanjani leo nimejiridhisha kuhusiana na uwepo wa matukio yasiyokuwa ya kiuungwana yanayoendelea mahala hapa, hivyo kwanza nimeagiza wakamatwe askari hao kwa mahojiano zaidi."

Pia Waziri huyo alisema kuwa utawekwa mfumo uwanjani hapo kuhakikisha kila anayetoka nje ya nchi anakaguliwa kwa ufanisi kwa kila hatua anatakiwa kukaguliwa kuliko hali ilivyo sasa ambapo askari anaweza kuamua nani wa kumkagua na nani asikaguliwe.

Alisema hali hiyo inashawishi mazingira ya rushwa . Alikemea polisi kuwawekwa muda mrefu abiria baada ya kuwakagua na kuwa askari atakayebainika kuendelea kufanya hivyo atachukuliwa hatua.

Waziri Simbachawene akiwa kwenye kikosi cha anga, alipata wasaha wa kuruka kwa helikopta kuzunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa takribani dakika 40 ambako mbali na kukipongeza kikosi hicho, alibainisha kuwa usalama kwa njia ya anga umeimarishwa na nchi ni salama.

Akiwa kwenye kikosi cha zimamoto mkoa wa Ilala, Waziri Simbachawene aliagiza Wakuu wa Polisi wa mikoa kutozungumzia masuala yahusuyo moto huku akiwataka askari wa kikosi hicho wanaopatikana kila mkoa kuwa wazungumzaji wakuu wa masuala hayo.

Alisema hiyo inatokana na utaalamu walionao askari wa zimamoto na kuwa kama wakitoa taarifa inakuwa na ufanisi na yenye utaalamu.

Alitaka uwepo ushirikiano mzuri kati ya Tanesco na Zimamoto hasa katika ukataji wa umeme kwa haraka pindi wakitakiwa kufanya hivyo na kikosi hicho.

Pia alikemea wanaopiga simu za kuhitaji msaada wa gari za kuzima moto lakini kunakuwa hakuna tukio la moto kwenye maeneo yao.

Akizungumzia kuhusu hali ya wakimbizi nchini, waziri alibainisha kuwa kwa sasa nchini kuna wakimbizi 275,000 na kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Wakimbizi(UNHCR) kuhusu njia bora ya kuwarejesha majumbani wakimbizi wenye kustahili kuondoka.
 
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Waziri Simbachawene alisema kuwa askari hao watano wameunda mtandao wao kwa ajili ya kusaidia usafirishaji wa vijana wa kike na kiume kwenda nchi za kiarabu kufanya kazi za ndani....
Bado sijamwelewa waziri wangu. Ina maana hao askari ndio wanatoa passports na viza kwa hao wasafiri, au?! Tuseme mtu kenda zake uhamiaji, kapata passport, kisha anaenda ubalozi, nako anapata viza. Kwahiyo mtu kama huyo akifika pale airport hao polisi walitakiwa kumrudisha kwa sababu anaonekana anaenda kwenye hizo nchi, au?!
 
Taasisi nzima ya polisi na usalama tanzania imeoza na kunuka mno, yaano askari polisi na uhamiaji wao wanajiona kuwa wako above the law na watakalo wanafanya kwa sababu wamevaa mkanda wenye bendera ya tanzania. kama kweli serkali inataka kusafisha taasisi hii basi ni lazima waanze katika vyuo vyao.

Maana huko ndiko askari anakofunzwa maadili ya polisi na inaonyesha hakuna mafunzo ya maadili na utendaji haki yanayofunzwa mbali ya watu kupelekwa mchakamchaka na kusulubiwa na ndio maana wakitoka na wao huona ni jambo la kawaida kuwaburuza wananchi.

Askari wengi mitaani hawafai kabisa kuwa walinda haki na sheria za wananchi, takriban wote wamejiunga na taasisi hii sio kwa mapenzi ya kazi bali kwa kuwa ni chaguo lao la mwisho kwa kutopata kazi nyengine.

By the way nadhani serikali pia inafaa kuangalia suali la askari wake kutokuwa fit kabisa! Askari tele wana vitumbo, askari unamuona njia anaburuza viatu, unahisi kabisa kama akitokea mwizi au mhalifu basi atashindwa kumfukuza kwa zaidi ya dakika tatu tu. Unakuta kuna askari wa kike wanene na vifua vilivyojaa kana kwamba wamebab matofali, yaani hata wakiinama tu unahisi wataanguka.
 
Nini Tafsiri ya walinzi wa amani kushiriki vitendo vya kihalifu ??
 
Bado sijamwelewa waziri wangu. Ina maana hao askari ndio wanatoa passports na viza kwa hao wasafiri, au?! Tuseme mtu kenda zake uhamiaji, kapata passport, kisha anaenda ubalozi, nako anapata viza. Kwahiyo mtu kama huyo akifika pale airport hao polisi walitakiwa kumdiswa kwa sababu anaonekana anaenda kwenye hizo nchi, au?!
Angalau wewe umetumia akili kuliko wengine wanaotumia chuki binafsi dhidi ya askari kusapoti usanii.
 
Siyo huko tu maaskari wenye maadili mabaya wako hata huku mitaani na Wana mitandao ya ovyo na wazi awafikie pia huku
Kipindi cha kampeni hizo Airport zimetumika kuwasumbua wapinzani sana kupitia hao hao Asikari ambao wamezoea kusumbua watu mno
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom