Regina Mwalekwa wa Clouds FM alamba shavu BBC!

Regina Mwalekwa wa Clouds FM alamba shavu BBC!

kwa wanawake ndie mtangazaji wangu bora,na nampenda kumsikiliza anapokuwa anatangaza kipindi chochote.
kwa wanaume nampenda kumsikiliza samadu hassan wa star tv.....
 
Nilijiuliza alikosa nini mpaka akawa mtangazaji kwenye kijiredio ambacho haendani nacho. kila laher dada
 
Ivona kamuntu was star naye anafuata.kaza but I mama nyamwihura
 
ujue mnakurupuka sana,huyu wengine hatumjui anatangaza redio/tv gani,wa wapi huyu
 
hongera mwaya from radio tumaini - claus - bbc sio nchezo'
 
Ki booooo ndeeeee aende BBC akacheue pumba zake...
Ataenda kutuaibisha akae tu hapo

...mlamba viatu anandoto za ukuu wa wilaya ndo maana haachi kujipendekeza,hajui baba riz moko amebakiza wiki chache tu...
 
Mama unastahili kabisa hiyo nafasi. Kapeperushe bendera yetu vizuri na uelimishe dunia lugha yetu ya Kiswahili. Uendelee kusimamia haki na ukweli daima. Hongera wewe na familia yako Mungu awabariki sana.
 
Hongera zake ukifika UK mtengenezee njia na Kibooo...nde aje huko.

Hongera sana Regina tutakumic sana kanisani Peter Clavery Mbezi Louis, Kibonde hawezi kwenda BBC wewe huyu anafaa radio za 'Tandale' tu.
 
regina ntakukumbuka kama kiraka ukpewa kdocumentary kwenye sport extra pale utajapo majina ya wachezaj wa kfaransa bas katka tone yao.ukihamia italia katka tone yao tanx
 
Yaani hakuna watu wananikera kusikiliza kama hawa vijana ambao wanajiita "wanavipaji" vya utangazaji na mbaya zaidi hawana taaluma ila wanaishi kwa kudra za Mungu tu.Ebu angalia ubunifu na weledi alionao Regina Mwalekwa kwenye utangazaji na hata ubunifu wa vipindi vyenye maudhui ya kuelimisha na si kukaraisha msikilizaji.

Leo hii mpaka nawashangaa TCRA kwa kushindwa kuchukua hatua kwenye radio za hawa watu ambao wanajiita ni radio ya watu kama vile radio zingine ni za mapaka vile.

Kipindi cha mida ya saa fulani za asubuhi mpaka muda wa maakuli,yaani hiki kipindi mimi ningekuwa nina mamlaka huko TCRA ningekifungia kabisa.

Sikatai kuna maswala wanazungumzaga yanagusa jamii ndio,lakini sio kipindi ambacho unaweza sema kina caliber ya ushindani katika tuzo za kimataifa na ndio maana wanakosa hata tuzo za TASWA sijui zile!

Mimi sio mwandishi lakini nadhani hakuna ethic inayomtaka mwanahabari kuongea mambo ya ajabu katika radio ya umma nkimaanisha inayosikilizwa na watu wengi na wa rika mbalimbali..

Yani radio hyo ya Mikocheni yenye vijana wanaovaa milegezo ndio watangazaji ambao maneno machafu midomoni mwao ni kama sala kitu ambacho kilimtofautisha sana dada Regina na vijana hawa,lakini pia kwakuwa Regina alitambua kuwa radio ya vijana wanahitaji kufahamu lugha adhimu ya kiswahili aliamua kuwa na segment ya angalau neno moja kila siku ili vijana waelewe walau matumizi ya maneno.

Ila la kheri Regina na kama hao mabinti na vijana wanaosema "wanavipaji" watashindwa kujiendeleza kielimu wakiendelea kubweteka kwakuwa bosi anawapa vocha na wanajulikana na vijana basi Mungu awasaidie lakini wataishia hapa hapa na hawatakaa wapate exposure katika maeneo mengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom