Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,261
- 18,261
Asante sana, japo naamini Sala au Funga bila matendo mema havifiki kwa Mungu pia (hiyo ni nyongeza kama hujaiona kwenye hadith)
Tunavyo sahau kuhimizana matendo mema kama nguzo muhimu ya kupokelewa sala (hata kipindi kisichokuwa cha mwezi mtukufu) ndio hapo unakuta watu wanasali ila washirikina, waasharati, mashoga, nk
Shukraan. Ni sawa.Waaleykum Salaam Warahamtullah Wabarakatuh,
Nakujibu kwa Niaba ya Ukthy Angel Nylon,
Muda wako wewe kwa kua upo Mwanza basi utafungua swaumu saa kumi na mbili na dakika hamsini na saba (18:57) na daku yako utakula saa kumi na moja na dakika thelathini na tisa (5:39) mpaka muda wa Salah ya fajri ukifika itakua mwisho wako,
Wengi hula saa saba hadi saa tisa wengine wanataka wapate muda wa kufanya ibada za usiku, wengine hawawezi kula alfajir, wengine hawawezi kuamka alfajiri,
Mola wetu Mlezi mwingi wa Rehema anatuambia katika Qur'an,
(….Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]
Na Allah anajua zaidi.
Shukrani kwa ukumbusho🙏🏽
"tofauti ya muumin na asiye muumin ni swala" unatekelezaje funga(amrisho la allah) ikiwa wewe si muumin?Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
"tofauti ya muumin na asiye muumin ni swala" unatekelezaje funga(amrisho la allah) ikiwa wewe si muumin?Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
Kweli kabisa , umeongea jambo la msingi sana kwani uzi wa kimasihara upo active mda wote watu wanashusha visa vyao vya uovu lakini kwenye mambo ya kheri sikuzote watu tuko nyuma labda sababu mambo ya dini yanahitaji elimu na umakini coz kuna hatari kubwa ya kupotosha umma kama mtu usipo elezea na kuwasilisha vyema(kielimu) kile unachokifikisha .Natamani hii thread ingekuwa active nyakati zote, sio ramadhani tu, ili tuendelee kumkumbushana.
Kwa sababu ukumbusho unawafaa waumini.
Lakini si haba tuendelee kunufaika nayo kadri inavyowezekana.
Unajua jf japo kuna majukwaa mengi lakini ni ngumu kukutana na ukumbusho wa masuala ya dini, na hata kwenye hilo jukwaa la dini mtu akinzisha thread ya hivyo, basi Uzi utavamiwa na inakuwa tafrani.
Lakini lillahi llhadu madhari tuna Uzi huu hasa katika mwezi mtukufu kama huu si haba.
Binafsi huu ni katika nyuzi zangu bora humu jf, huwa nafurahi kuona comments za ndugu zangu wakizungumzia masuala ya dini, na jinsi utulivu ulivyotamalaki.
نسأل الله السلامة و العافية
Tunamuomba Allah atupe salama na afya
[emoji23][emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] muumini wa kweli hufanya ibada bila kumbugudhi mtu wala kujionesha onesha hovyo kama ni mcha Mungu .
Hiyo ndo tabia yangu ukiniona utadhani ni mtu nisiyejua chochote kuhusu dini.
Samahani mpendwa, kwa mujibu wa riwaya zilizothibiti kisharia mwezi wa Ramadhani si katika miezi minne mitukufu, miezi mitukufu iliyotajwa ni Dhul-Qadah, Dhul-Hijjah, Muharram na Rajab, ambapo hiyo mitatu ya mwanzo imeongozana na mwezi Rajab peke yake ndo umejitenga. Utukufu wa mwezi wa Ramadhani ni katika lugha tu na ada za watu 'mazoea' kutokana na kuenea fadhila nyingi ndani yake. Kama utahitaji marejeo 'reference' nifahamishe. AhsanteMiezi mitukufu ipo minne.ramadhani ni mmoja wapo.
Na una heshima kubwa.ni chuo cha kutenda mema.mwezi wa toba,mwezi wa kuchuma kheri
Mungu ana huruma.na sisi ndo maana ndani ya mwezi wa ramadhani malipo ya kutenda mema ni zaidi.kuliko miezi mingine
Tukitoka hapo haturuhusiwi kutenda dhambi.miezi mingine
Amin In sha Allah kwa ummat muhamad S.A.W wote.Ramadhan maqbul