SIKU KAMA YA LEO AYA HII NDO ILISHUKA AMBAYO INAUELEZEA UISLAM KWA MAPANA:
Maswahaba waliposikia aya hii walilia, kwa sababu walielewa kuwa utume ulikuwa karibu kukamilika.
﴿ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗا ﴾
“Leo nimekukamilishieni dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekuridhieni Uislamu uwe dini yenu.”
— Qur'an Suratul Maaida 5:3
NASAHA PANA YA AYA HII KWA MAISHA YA LEO
Bila neema ya dini, mimi na wewe tusingekuwa hapa.
Katika computer kulikuwa kuna windows 7, 8, 9, 10 na kila window inayokuja inakuwa updated haina virus, inakuwa imara zaidi, na dini ilikuja kidogo kidogo lakini kuanzia siku hii DINI tukatangaziwa kuwa imekamilika haina upungufu.
Allah ametuchagulia dini ya Uislamu kama mfumo wa maisha kwa maisha yetu yaliyobakia sisi na vizazi vyetu, dini ndiyo kodi ya maisha, dini ndiyo kila kitu kwenye maisha yetu.
Aya hii ni katika aya kubwa kabisa ndani ya Qur’an. Iliteremshwa siku ya Arafa wakati wa Hijja ya mwisho ya Mtume Muhammadﷺ.
Inaonesha kuwa Uislamu siyo dini ya muda, bali ni mfumo kamili wa maisha mpaka mwisho wa dunia.
1. Uislamu umekamilika — hatuhitaji kuongeza dini mpya.
Leo watu wengi wanataka:
dini inayofuata matamanio,
ibada zisizo na dalili,
“version mpya” ya Uislamu,
au kuchukua sehemu wanazozipenda tu.
Lakini aya hii inatukumbusha:
Hakuna anayemzidi Allah (S.W) hekima ya kuupanga mfumo wa maisha ya mwanadamu.
Dini imekamilika: kwenye ibada, biashara, ndoa, malezi, maadili, uchumi, uongozi,
hata namna ya kula na kuzungumza.
“Tatizo la zama hizi siyo kukosekana elimu pekee, bali ni watu kutaka kubadilisha dini iliyokwishakamilika.”
2. Ukamilifu wa dini hauko kwenye wingi wa teknolojia bali uongofu.
Leo tuna: simu kali, AI, internet, safari za haraka, elimu nyingi,
lakini bado:
huzuni imeongezeka, talaka zimeongezeka, stress imeongezeka, watoto hawana malezi, mioyo imechoka.
Kwa nini?
Kwa sababu maendeleo ya dunia bila uongofu wa Allah (S.W) hayaondoi upweke wa roho.
“Teknolojia inaweza kuunganisha simu, lakini Qur’an ndiyo huunganisha mioyo.”
Na watu tumeitupa Qur’an.
3. Neema kubwa si pesa — ni kuongozwa kwenye Uislamu.
Aya haisemi: “Nimekutimizieni mali.”
Bali:
“Nimekutimizieni neema yangu.”
Na neema kubwa kabisa ni: kuswali, kuijua Qur’an, kupenda Sunna, kuwa karibu na misikiti, kupewa tawba, kupewa moyo wa kutubu, kuwa nafikra juu ya Umma vipi upate hidaya.
“Watu wengi wanaishi na neema za dunia huku wakikosa neema ya kumjua Allah.”
“Dalili ya neema siyo kuwa na kila kitu unachotaka, bali moyo kuwa karibu na Mola wako.”
4. Aya hii inatufundisha kujivunia Uislamu.
Waislamu wengi leo wanaona aibu: kuvaa kiislamu, kusema Alhamdulillah, kushikamana na Sunna, kuonyesha dini hadharani.
Lakini Allah amesema: “Nimekuridhieni Uislamu.”
Ikiwa Allah ameridhia Uislamu kuwa dini yetu, kwanini sisi tuuone mzigo?
5. Uislamu ni mfumo wa maisha, si ibada za msikitini pekee.
Baadhi wanafikiri dini ni:
Ramadhan tu,
Ijumaa tu,
Eid tu.
Lakini aya hii inafundisha: Uislamu unahusika na:
biashara zako,
WhatsApp zako,
ndoa yako,
mavazi yako,
lugha yako,
marafiki zako,
hata muda wako wa faragha.
“Muislamu wa kweli haumwabudu Allah msikitini pekee, bali hata akiwa peke yake.”
6. Zama hizi zinahitaji kushikamana zaidi na Qur’an.
Kadri fitna zinavyoongezeka:
uzinifu, riba, muziki chafu, mitandao, kiburi, mashindano ya dunia kuhusu dunia, basi ndivyo tunavyohitaji kurejea kwenye dini iliyokamilika.
“Kila kizazi kinachoiweka Qur’an pembeni hulipa gharama kwa huzuni.”
Allah atuongoze , amin amin amin.
Dkt. Dhaakiriin
DOA ADMIN
+255713225702
+255685303727
DHIKRI ONLY ACADEMY DOA